Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 496
- 722
Hawa nao ni wale wale. Ukibahatika pita njia kama Moroko nwenge au daraja la Tanzanite unakuta kushoto bajaj kulia bajaj wote mwendo mmoja hawakupishi . Wanaboa sana kama vile njia ni yao tu. Au pita mtaa wa samora vile vinavyotoka feri mpaka stesheni ni kero tupu.Bodaboda hizi na sasa hivi naona bajaj zinachukua kasi
Hayo uliyoandika ni sahii kabisa ila in advanced level.BabaMorgan kwa picha ya haraka unaweza kuwatetea bodaboda na kuwalaumu wanaowalaumu bodaboda hasa kwenye hizi ajali za barabarani.. Lakini bodaboda ni pasua kichwa hasa japo sio wote
Tunacholaumu wengi wetu ni matokeo na sio chanzo ama asili ya tatizo
Maono kimo cha mbilikimo ya mamlaka ya kisiasa ndio asili kuu. Ili kupunguza kelele za ajira wakaamua kuruhusu biashara huria ya pikipiki kama aina ya usafiri wa haraka bila maandalizi ya kutosha na bila kujali viwango vya chombo husika
Mwendelezo wa tatizo ni pale kijana asiye na mafunzo kamili na sahihi kukabidhiwa chombo cha moto kwa ajili ya biashara ya kubeba binadamu
Huyu kijana hana mafunzo kamili na sahihi ya kuendesha chombo cha moto, sheria na kanuni za barabarani, usalama wake na wa wengine, elimu ya uchumi nk.. Na hii yote inasababishwa na uwezo wa kifedha,, mafunzo ya udereva yanahitaji hela na kijana hana
Rushwa na ufisadi
Ili kijana athibitishwe ni dereva na amefuzu mafunzo ya udereva na kufaulu anahitaji nyaraka zinazothibitisha hilo.!! Leseni.. Kuipata leseni kwa kufuata utaratibu wa kisheria kunachukua muda na ni gharama
Kupitia vishoka na watendaji wa mamlaka ya mapato na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wasiojali usalama wa raia na mali zao kijana anapata leseni chap kwa haraka na kwa bei poa
Kuna ukiukwaji mkubwa sana kwenye kupata leseni za udereva
Sasa kijana ana leseni na ana chombo cha moto anaanza biashara bila kufahamu walau kanuni moja tu ya kupita makutano ya barabara penye taa nyekundu
Majumuisho haya ya wanasiasa, watendaji wa serikali wasio waaminifu na vijana wasio na ajira matokeo yake ndio haya ya ajali zisizokoma, zinazoteketeza nguvu kazi ya taifa na kuleta uhujumu mkubwa wa uchumi kupitia vifaa tiba, vilema, uharibu wa vyombo na vifo
Sent using Jamii Forums mobile app
Wabongo nani ali waroga yani wako bussy ku record sijui hili iweje sasa mtu ana tumia nguvu kubwa a record tu asee
hilo nalo neno!Boda boda Kuna muda wanaforce sana njia ambazo sio salamaa, wakipita wanajiita wajanja ...wakigongwa wanatafuta huruma kwa jamii.
ukikatisha barabara kuu basi wewe unaekatisha iwe gari au bajaji au pikipiki uangalie pande zote na sio aliekuwa barabara kuu (STOP) mwingine akiona hakuna taa anaona kama ana haki.Alikuwa akikatisha barabara ya mwendokasi.
Boda boda wa DSM ndo kundi la wajinga zaidi bro , matrafiki wanatakiwa wawekeze nguvu Zaid Kwa hawa watu, usidhubutu kupanda boda katika any busiest road Dar es salaamLeo asubuhi pametokea ajali maeneo ya DIT iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki maarufu Bodaboda sina details za kutosha kuhusu madhara yaliyotokea kwa maana ya majeruhi au kama kuna kifo chochote lakini so far ni ajali mbaya maana time niliyokuwa napita basi la Mwendokasi lilikuwa linapigwa jeki na Pikipiki inatolewa chini ya uvungu mwa basi.
Kila mtu baada ya kuona mazingira yale alikuwa anatoa lawama kwa dereva bodaboda bila hata ya kuwa na picha halisi ya kile kilichotokea mpaka kusababisha ajali.
It's like ajali yoyote itakayohusisha bodaboda basi lawama zote atatupiwa bodaboda huu ni uonevu wa kiwango cha juu sio bodaboda wote hawaobey sheria za barabarani na sio kila dereva wa gari yupo perfect asilimia mia.
Tuheshimu Bodaboda nao ni Binadamu licha ya kuwa na mapungufu yao lakini still wana mema yao kama walivyo Binadamu wengine as long unajua kuendesha Pikipiki inabidi uwe mstari wa mbele kutetea bodaboda maana siku unaweza kuwa kwenye mizunguko yako ukapata mushikeli waka kuhukumu kama wanavyowahukumu bodaboda.
Unafaidika nini wakifa?? Wale ni ndugu, wazazi, watoto wa watu
Kuna siku dereva alikwepa bodaboda aliyejipachikaBoda huwa akili zao zinapita upepo muda mwingi, dereva huwezi ua watu 199 kumkwepa boda anaevuka mataa yakiwa yameruhusu upande wako nafikiri ndo ivo maana huwa wanafosi sana akikutana na dereva mstarabu uminya break ya gafla sasa abiria tuumie kwasabbu ya uzembe wa boda mmoja
Pale Zanzibar reassurance bodaboda hujikatizia tu wanavyotaka bila hata mataa kuwaruhusu.Sio DIT kabisa ni nyuma kidogo pale kwenye mataa ambapo kuna barabara ya kwenda Lumumba kama sijakosea.. Muda mwingine madereva wa mwendokasi wanadharau mataa.
Ningepewa nafasi ya kuishauri serikaliNamnukuu Godbless Lema..
"Boda boda ni Laana"
Na mimi naongezea kwamba, Uafrika hasa utanzania ni laana.
Kwa nchi zilizo endelea, First world countries, Bodaboda ni uchafu mjini.
Na si bodaboda tu, hata Bajaji ni takataka.
Zinachafua miji.
Kwahyo boda boda wana haki ya kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo kasi? Angalia ajali nyingi za boda lazima kuna tatizo mtu wa gari hawezi kuchomeka gari au kupenya kwenye foleniLeo asubuhi pametokea ajali maeneo ya DIT iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki maarufu Bodaboda sina details za kutosha kuhusu madhara yaliyotokea kwa maana ya majeruhi au kama kuna kifo chochote lakini so far ni ajali mbaya maana time niliyokuwa napita basi la Mwendokasi lilikuwa linapigwa jeki na Pikipiki inatolewa chini ya uvungu mwa basi.
Kila mtu baada ya kuona mazingira yale alikuwa anatoa lawama kwa dereva bodaboda bila hata ya kuwa na picha halisi ya kile kilichotokea mpaka kusababisha ajali.
It's like ajali yoyote itakayohusisha bodaboda basi lawama zote atatupiwa bodaboda huu ni uonevu wa kiwango cha juu sio bodaboda wote hawaobey sheria za barabarani na sio kila dereva wa gari yupo perfect asilimia mia.
Tuheshimu Bodaboda nao ni Binadamu licha ya kuwa na mapungufu yao lakini still wana mema yao kama walivyo Binadamu wengine as long unajua kuendesha Pikipiki inabidi uwe mstari wa mbele kutetea bodaboda maana siku unaweza kuwa kwenye mizunguko yako ukapata mushikeli waka kuhukumu kama wanavyowahukumu bodaboda.