Boda boda kila siku watu wanapata ajali Dar

Boda boda kila siku watu wanapata ajali Dar

Haya yote lawama ziende kwa serikali ya CCM kwa kushindwa kuwatengenezea vijana ajira za uhakika na kueleweka, wameua viwanda Kila mahali pa nchi hii. Hivi unadhani vijana wanapenda kukimbiza upepo?? Ni basi tu wanajikuta hawana option
 
Dr. Charles Sokile ni mtu mwema sana.

Uchungaji ni kazi yake tu nyingine...
Kwenye upande wa Development he played a huge role...

Taifa limepoteza, OPM wamepoteza.

Lala salama Dr.
MTU WA STRATEGIC PLANNING AND DEVELOPMENT , mtu anasaidia kila kona kwa maarifa yake, leo anlala kwa ajali za vijana wanaokunywa viroba na kuruhusiwa kutamba barabaranni.
 
Hawa jamaa nakiri wengi wao wako rafu na wazembe sana barabarani, wanachomekea bila kuangalia, wengine wamelewa kabisa na hawajali sheria za barabarani

ila kuna muda wanagongwa na wapo sehemu sahihi hasa na malori. Kama kuna yule binti bodaboda wa mbagala aliyegongwa Buguruni Chama akitoka kupeleka abiria Mbezi. Binti alikuwa njia sahihi, pia ana leseni yake halali, fuso moja likakatiza uhai wake.

Madereva wa malori hasa mafuso wana tabia za ajabu mno, unaweza kusema ni boda wasiyo na leseni ambao wamepewa hayo magari waendeshe. Kuna mahali wakiona ni pikipiki tu wanadharau na hawafuati sheria wakijua boda ataepuka. Kama boda naye kawaza mwenye lori atasimama kutii sheria basi ni kifo chake.

Mfano unakuta boda ipo moto barabarani, fuso linaingia toka barabara ya pembeni, badala aangalie umakini na aingie kama ameruhusiwa na aliyepo barabarani. Akiona ni pikipiki hajali anakanyaga tu kuingia akijua atampisha, eti wanasema udereva wa kujihami bosa anatakiwa ajihami. Ikotokea boda hesabu zake si kusimama na anampigia honi kumwashiria asiingie bado wanapeleka.

Wapo wengi wanakufa kwa uzembe wa madeeva wa malori ila kwakuwa kati yao kuna kundi la wasiyofuata sheria. Basi nao wanaonekana ni walevi tu. Hizo bandari kavu na ujio wa malori, roho za watu zitamalizwa vya kutosha sababu yanasababisha msongamano na kupelejea uchomekeaji wa bodaboda na bajaji ili watu wawahi​
 
Dr. Charles Sokile ni mtu mwema sana.

Uchungaji ni kazi yake tu nyingine...
Kwenye upande wa Development he played a huge role...

Taifa limepoteza, OPM wamepoteza.

Lala salama Dr.
Doctor Charles ,alikuwa amepakiwq na bodaboda,au walimgonga akiwa njiani?Poleni sana,ndugu na jamaa.
 
Kama una gari mjini haijachubuliwa na Baja basi wewe umeweka ngao.
Yaani sijui tufanyeje.
Mtihani huu,anakuchunia gari na hana cha kukulipa..tumeondowa Hiyace tumeruhusu bajaji sasa tunaanza wapi wachingiaji wa ccm ndio waingizaji wa hizi takataka.
 
MTU WA STRATEGIC PLANNING AND DEVELOPMENT , mtu anasaidia kila kona kwa maarifa yake, leo anlala kwa ajali za vijana wanaokunywa viroba na kuruhusiwa kutamba barabaranni.
Mkuu ilikuaje mtu mzito namna hiyo kutumia usafiri wa boda boda ,alikosa hata ka starlet ka mkopo
 
Ikiwa hii dunia,hakuna mungu na hatujui tutokapo,hata kuwahi kufa si jambo baya
Kuwahi kufa inaweza kuwa si jambo baya kama umeamua hivyo mwenyewe.

Lakini mtu ambaye hajatimiza ndoto zake, hajafanya mengi anayktaka kufanya, hataki kuwahi kufa, kuwahi kufa ni jambo baya.
 
Back
Top Bottom