Tatizo kubwa la ajali za barabarani zinazohusisha pikipiki(boda) katika jiji la Dar es Salaam

damiro

New Member
Aug 16, 2022
4
3
Andiko langu linahusu tatizo sugu la ajali za barabarani zinazohusisha pikipiki (boda) katika jiji la Dar es salaam linavyoleta madhala makubwa kwa jamii.

Dar es salaam ni jiji kubwa linaloongoza kwa kua na watu wengi shughuli nyingi za kimaendeleo, kibiashara na hufanyika nyakati zote usiku kwa mchana, matumizi ya vyombo vingi vya moto imekua moja huduma mhimu katika jiji hili ili kuwezesha shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kufika maeno ya kazi.

Moja ya usafili maarufu sana unaotumiwa na wakazi wengi ni usafili wa pikipiki (boda) ni usafili ambao mtu hupanda pale anapohitaji afike mahali husika kwa kuwahi na kwa halaka zaidi au kwa wepesi zaidi kwa maana ya kuepuka foleni au pasipokua na usumbufu wowote au kwa kukosa usafili wa mabasi hasa usiku

Lakini usafili huu unaonekana kua na dosali au kasoro kubwa kwani umekua chanzo cha ajali nyingi za barabarani na kusababisha madhala makubwa kwa watumiaji na jamii husika hali hii inapelekea jiji la Dar es salaam kuongoza kwa kua na ajali nyingi za barabarani zinazohusishwa na pikipiki(boda) tofauti na majiji au mikoa mingine.

Vyanzo au visababishi vya ajali.
Hizi ni moja kati ya vyonzo vikubwa vya ajali.
  • Mwendo kasi
  • Utumiaji wa vilevi wakati wa kuendesha chombo cha moto
  • Kukosa umakini wakati wa endeshaji
  • Kutokuzingatia sheria na alama za usalama barabarani
  • Ubovu wa chombo au barabara.
Taarifa fupi ya hospital
Taarifa fupi ya huspitali za mkoa za rufaa zinazopatikana katika jiji la Dar es salaam AMANA, TEMEKE na MWANANYAMALA, zinaonyesha ukubwa wa tatizo hili kwa robo mwaka ya mwisho tangu mwezi wa nne, tano na sita kwa kua na wagonjwa wengi waliowapokea wa ajali zilizohusishwa na pikipiki(boda) katika hospitali hizo, waliopewa matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani, waliopewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa mhimbili na Mloganzila, vifo vilivyotokea eneo la ajali na vifo vilivyo tokea hospital.

Hospital ya mkoa ya rufaa ya Temeke.
Kati ya wagonjwa wote wa ajali waliopokelewa hapo asilimia 88% walikua wagonjwa wa ajali zilizohusisha pikipiki na vyombo vingine vya moto,
  1. Waliotibiwa na kuruhusiwa kuludi nyumbani ni asilimia 26%.
  2. Waliotibiwa na kupewa rufaa kwa matibabu zaidi katika hospital ya Taifa mhimbili na Mloganzila ni asilimia 52%.
  3. Vifo vilivyotokea eneo la ajali au njiani akiwa analetwa hospital ni asilimia 7%.
  4. Vifo vilitokea hospitalini ni asilimia 3%.
Hospital ya mkoa ya rufaa Mwananyamala.
Kati ya wagonjwa wa ajali waliopokelewa ndani ya hiyo miez mitatu asilimia 89% walikua wagonjwa waliopata ajali zilizohusisha pikipiki na vyombo vingine vya moto.
  1. Waliotibiwa na kuruhusiwa waludi nyumbani walikua asilimia 23%.
  2. Waliotibiwa na kupewa rufaa kwenda hospital ya Taifa Mhimbili na Mloganzila 57%
  3. Vifo eneo la ajali au njiani wakipelekwa hospital ni asilimia 5%.
  4. Vifo vilivyotokea hospital ni asilimia 4%.
Hospitali ya rufaa ya Amana.
Kati ya wagonjwa wa ajali waliopokelewa asilimia 85% walikua wagonjwa wa ajali zinazohusishwa na pikipiki (boda) na vyombo vingine vya moto.
  1. Waliopata matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani ni asilimia 27%
  2. Waliopata matibabu na kupewa rufaa kwenda hospital ya Taifa mhimbili na Mloganzila ni asilimia 47%
  3. Vifo eneo la ajali au njiani wakiwa wanapelekwa hospital ni asilimia 8%
  4. Vifo vilivyotokea hospital ni asilimia 3%.
Kwa ufafanuzi huu wa taarifa hii fupi tunapata kuona ukubwa wa tatizo hili kwani linaleta madhala makubwa kwa watumiaji wa usafili wa pikipiki na jamii kwa ujumla kwa kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu, namba kubwa ya taarifa inaonyesha wagonjwa wengi wanapewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Mhimbili na Mloganzila, waliopata huduma hospital husika na vifo pia.

Bado hakuna tathimini na taarifa kutoka kwenye kila hospital za wilaya, zahanati na vituo vya afya wanakoanzia wagonjwa wengi kabla hawajafika hospitali ya mkoa ya rufaa pia hatuna taarifa husika kutoka hospital ya Taifa mhimbili( MOI)na Mloganzila ambako wagonjwa wengi wanapewa rufaa kwani ni dhahili kwamba wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospitali ya TAIFA tatizo lake ni kubwa zaidi kwa maana ya majeraha kua makubwa sana na hivyo yanahitaji matibabu ya uangalizi zaidi.

MAKUNDI YANAYONGOZA ZAIDI KUPATA AJALI ZINAZOHUSISHA PIKIPIKI(BODA) NA VYOMBO VINGINE VYA MOTO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM. (WAHANGA WAKUBWA)
Haya ni makundi yanayochangia ajali nyingi za barabarani zinazohusisha pikipiki (boda) na vyombo vingine vya moto kwa jiji la Dar es salaam kwa maana ya wahanga wakubwa.
1) Watumiaji wa usafili wa pikipiki (boda) dereva na abilia.
2) Watumiaji wa usafili wa pikipiki nyakati za usiku hasa wanaokwenda maeneo ya starehe na kuludi mwishoni mwa wiki ijumaa, jumamosi na jumapili.
3) Wanaofanya mazoezi alfajili sana hasa siku za mwisho mwa wiki kwa maana ijumaa, jumamosi na jumapili.
4) Watembea kwa miguu hasa maeneo ya vivuko vya punda milia.

Muda hatarishi zaidi.
Kutokana na taarifa za hospitali huu ndio mda hatarishi zaidi ajali nyingi mbaya hutokea sana,
1. Mwishoni mwa wiki ijumaa, jumamosi na jumaapili nyakati za usiku kwani watu wengi hutoka na kwenda sehemu za starehe na usafili unaotumika sana ni pikipiki, pia watumiaji wa barabara nyakati za usiku mwishoni mwa wiki wengi wanakua wametumia vilevi hivyo hupelekea kusababisha ajali mbaya.
2. nyakati za alfajili hasa mwishoni mwa wiki ijumaa jumamosi na jumapili, hii kwa wale wanaofanya mazoezi pasipo kubeba alama au kutokua kwenye vikundi vya watu wengi, mazingla ya barabara husika pia watumiaji wengi wa barabara nyakati za usiku na alfajili wametumia vilevi hivyo kua chanzo cha ajali.

MADHARA YA AJALI
Madhala makubwa yamoja kwa moja ya ajali ni;
Kifo
Ulemavu wa kudumu
Kupelekea kupata magonjwa mengine kama matatizo ya akili, kupooza na menine mengi ya kijamii na kiuchumi pia.

USHAURI WANGU.
Ushauli wangu utajikita katika maeneo mawili ;
  • Kwanza ni kwa serikali na Mamlaka husika.
  • Pili ni kwa jamii kwa ujuma.
Ushauri kwa Serikali na Mamlaka husika,
1
.Kotoa elimu ya kutosha namna kuepuka ajali, taarifa kuhusiana na ukubwa wa tatizo hili na njia za kuepuka pia.
2. Kuendelea kuboresha huduma za afya kwa kuweka miundo mbinu, vifaa na wataaramu katika hospitali za mikoa za rufaa kuwezesha huduma za kibingwa za upasuaji wa mifupa zinapatikana hapo, hii itafanya watu wengi kupata huduma hospitali husika na kuondoa msongamano wa wagonjwa wengi wanaopewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Mhimbili na Mloganzila.

Ushauri wangu kwa jamii kwa ujumla.
Hii ntajikita zaidi kwenye makundi yaliyohatalini zaidi au wahanga,
Nashauli jamii tuendelee kuchukua tahadhali mda wowote na mahali popote tuwapo barabarani na tutumiapo vyombo vya usafili kwani ni vigumu kujua wakati gani ajali itatokea lakini madhala yake ni makubwa zaidi.
Kwa dereva pikipiki(boda), Acha kutumia vilevi, kua makini mda wote unapoendesha, epuka mwendo kasi uwapo barabarani zingatia pia sheria za za barabarani.

Kwa abilia, Mchunguze mwendesha pikipiki kwa haraka kabla hujapanda epuka kupanda kama ukiona viashilia vifuatavyo, halufu ya pombe, kama ana muonekano wa watumiaji wa madawa ya kulevya, kama ni wale wakuvaa visendo upande wakiwa wanaendesha, mpe tahadhali kua usalama ni mhimu zaidi kuliko mwendo kasi, vyote hivi vitakuhakikishia usalama wa safali yako uendako.

Chukua tahadhali unapokwenda sehehu za starehe na kuludi nyumbani kwa usafili wa pikipiki au bajabji hasa mwishoni mwa wiki,
Ajali nyingi mbaya zinatokea mwishoni mwa wiki ijumaa jumamosi na jumapili wahanga wakiwa wanaenda au wanatoka sehemu za starehe nyakati za usiku wakitumia usafili wa pikipiki au bajaji wengi wakiwa wametumia vilevi, wamepanda pikipiki moja watu wengi (mshikaki).

Kuchukua tahadhali kwa wale wanaofanya mazoezi alfajili,
Zingatia barabara unayofanyia mazoezi sio hatali kwa ajali, kua na alama au vaa nguo zinazofanya uonekane kwa wepesi zaidi (refrecter), kua kwenye kikundi muwe wengi, kuwa makini zaidi uwapo barabarani,unapohisi uchovu ni tembea au pumuzika kuliko kupoteza muelekeo ukiwa barabarani.

Ushauri wangu wa mwisho kwa jamii tuhamasike kuwa na bima za Afya hata ya 40,000/ tu itasaidia kufanikisha matibabu, ajali hatabiliki na wala haijulukani wengi wamepatwa na maswahiba hayo ikapelekea kukosa matibabu kwa wakati kwa kukosa malipo au galama za matibabu uchunguzi au vipimo na vifaa tiba hasa waendeshaji wa pikipiki,
 
Kama nawaona wabrashi viatu wakitamani Mh. Kinana atengue kauli yake iliyotupa afueni kweli kweli 😂😂.
 
kwakweli bodaboda wengi hawajitambui,wao huona kama sheria za barabarani haziwahusu
msimamo wangu kabla sijapanda boda namuangalia kuanzia kuonekano wake ikiwa ni pamoja na mavazi na pikipiki kama iko shwari yaani unakuta mbuzi kavaa mayebo et naye ni boda
 
Pia wajitahidi kuvaa mavazi ya kujikinga.

Yanasaidiaga likitokea la kutokea samtaimu.

Kwa imani za kisukuma tunaamini Mungu akikubariki anakupa akili. Na maarifa yanakuja kwa kujifunza kile kizuri MasalaKulangwa(AkiliKufunzwa)

HATA SULEIMAN alibarikiwa kwa kuoewa maarifa akayatumia akawa mwenye heri duniani.

Maarifa yapo dunianii watu walishafanya tafiti wanajua miguu, kichwa, na mikono inaumizwaga maeneo haya wakaweka vi ngao. So tutumie hivyo vitu.
20230119_190213.jpg

Ole wao wanaoyakataaa maarifa maana hata Mungu hafagilii hao watu. Mungu atusaidie sana
Chukua tahadhali
 
Pia wajitahidi kuvaa mavazi ya kujikinga.

Yanasaidiaga likitokea la kutokea samtaimu.

Kwa imani za kisukuma tunaamini Mungu akikubariki anakupa akili. Na maarifa yanakuja kwa kujifunza kile kizuri MasalaKulangwa(AkiliKufunzwa)

HATA SULEIMAN alibarikiwa kwa kuoewa maarifa akayatumia akawa mwenye heri duniani.

Maarifa yapo dunianii watu walishafanya tafiti wanajua miguu, kichwa, na mikono inaumizwaga maeneo haya wakaweka vi ngao. So tutumie hivyo vitu.
View attachment 2487918
Ole wao wanaoyakataaa maarifa maana hata Mungu hafagilii hao watu. Mungu atusaidie sana
Mzee ivo vitu ni shingap?
 
Mimi nina mwaka wa kumi na mbili na naendesha pikipiki na niliyonao ni ya 5kumiliki,niliwahi kupata ajari ndogondogo2 ya kwanza kuna gari ilinigonga ,sema alinilipa uzembe ulikuwa wake ,ya pili niligongwa na bodabda ingine alinivaa kwa nyuma,alikuwa kwenye mwendo kasi,niliposimama ghafla baada ya gari ya mbele yangu kusimama akanivaa,nikamwambia vipi akasema kosa la mwenye gari ya mbele,nikamwambia kivipi,akasema amesimama ghafla,nikamwambia mbona mi alikuwa mbele yangu sikumgonga ila we umenigonga mimi,akanisukuma dah,basi nikachuka mchanga alikonyaga ,nikaenda malizana nae(barabarani huku siyo kila unaemuona ni mtu kuweni na heshima,)aliumwa sana mtu yule alilazwa miezi 6 na nilienda hospital ili anione ajue kuwa mimi ni hatari siezi ogopa binaadamu
 
Hizi ajali za pikipiki ni hatari sana.
Tujitahidi sana kuepuka bodaboda. Tupande kama kuna ulazima. Huyo mleta mada amelisema vizuri ila tatizo ni kubwa zaidi.
Elimu kwa ndugu na jamaa zangu kila siku huwa ni kwamba panga muda wako vizuri, usipande bodaboda.
 
Ushauli~ushauri
tahadhali~tahadhari
Abilia~abiria
Tabili~tabiri
Halufu~harufu
Hatalini-hatarini
Usafili-usafiri
Alfajili-alfajiri
Galama-gharama
Halaka-haraka
Dosali-dosari

Hizi bima za 40,000 zinakuaje mkuu embu tuelezee kidogo
 
Back
Top Bottom