BM Coach mmeleta changamoto kwa Abood Bus Dar mpaka Moro

BM Coach mmeleta changamoto kwa Abood Bus Dar mpaka Moro

Kwa taarifa yako tu ni kwamba duru za chini chini zinasema kuwa huyo BM na Abood ni Mtu mmoja hivyo hiyo pongezi yako Kwao ni kama tu vile umempongeza Abood indirectly. Kuna mbinu moja ya Kimasoko ( Market Strategy ) ambayo ' wabobezi ' wa Masuala ya Biashara na Masoko watatusaidia kwani nimelisahau lile neno lake la ' Kitaaluma '. Ni kwamba kwa kawaida Mtu fulani anapokuwa anajua kuwa anakubalika mno na ameshajijengea jina kubwa na imani kwa Wateja wake mahala husika sasa ili kuweza kutopoteza Soko lake kwa ' Washindani ' wapya huamua kuanzisha ' vijikampuni ' vingine kadhaa ili ' Kuwazuga ' tu Watu lakini kumbe vyote ni vyake na faida itakayopatikana bado itabaki tu kuwa yake na ataendelea kutawala hiyo Biashara na hilo eneo.

Yapo Makampuni mengi sana makubwa na yaliyokwisha jizolea ' sifa ' kemkem hapa Tanzania na huko duniani ambapo na Wao walikuja na mbinu hii hii ila sisi ' Wateja ' tumezugwa tu kama siyo kufichwa na hatimaye Pesa / Fedha zetu zote mwisho wa siku tunampelekea tu ' Njemba ' moja na ' Utajiri ' wake unazidi kukua japo ameutawanya.

Hapana chezea ' Wafanyabiashara ' Mkuu kwani ni Wajanja na wana ' mbinu ' kali na za ' kutukuka ' kabisa.
Acha uongo Mkuu, Huyu BM mimi namjua vizuri sana, ninaposema namjua namaanisha namjua, sitaki kuelezea sana ila kwa kifupi BM ni mchagga, na hiyo BM ni kifupi cha Majina yake! Sema kingine ila kwa hili Kwamba Mzee Abood ndio BM SIO KWELI na haitokua kweli.
 
Hapo na kataa kabsa yaan alsaedy sasa hv magr yake abood na bm hawaon ndan fulu kiyoyoz na usb magar yote unachaj simu sio kama ilivyo kwa hayo mengne yapo machache yenye sehemu ya kuchajia lakn alsaedy uhakika asilimia mia moja
Hukuelewa mkuu, ni hivi nikisema gari zake kama daladala namaanisha kuwa inasimama vituo vingi NJIANI Sasa kwa safari kama zile ni kuchoshana tu, kawaida gari ikitokea UT kwenda Moro haisimami mpaka kibaha, ikitoka hapo ni mpaka choline, lakini AL SAEDY sio kwanza mtatoka na mikwara pale terminal then mkifika ubungo kimara anaweka kituo mbezi anasimama tena si kwa dakika moja mnaweza toboa hata dakika tano na kwa gari dakika tano ni nyingi unavuta umbali mrefu
 
Mimi wa Air Tanzania napita tu,,,,,
Nasubiria SGR ya umeme
 
New force ni zuri sema wajitahidi kwa ndani kuwe na accessory za kutoshaaa
 
Kwanza naomba nikiri wazi kuwa sina uhusiano wowote na mabasi tajwa mimi ni msafiri tu wa kawaida.
Kiukweli Abood Bus alianza kubweteka na kufanya vile anavyojisikia bila ya kuzingatia mteja anataka nini.
Miaka ya 2000 mwanzoni mpinzani mkubwa wa Abood Bus kwa ruti ya Dsm mpaka Moro alikuwa ni Hood.
Hood alifanya soko la Abood kuwa gumu pale alipoleta Marcopolo Torino na mfumo mpya wa basi kuwa na dereva tu bila ya kondakta.
Wakati huo Abood bado akiendelea na yale mabasi yake ya zamani zile scania engine ipo nyuma (mimi sio mtaalam wa model za magari).
Hii ilipelekea basi nyingi za hood ziwe njiani yaani basi linatoka dsm kwenda Moro likifika chalinze tayari lishajaa abiria wanaolisubiri pale msamvu Moro wards nalo Dsm.
Kuona hali inakuwa tete Abood ikampasa kuvunja kibubu chake nae akazama Africa Kusini akatuletea Marcopolo Andare Class.
Kiukweli basi hizi kwa wakati huo zilikuwa zipo kileleni kwa kila kitu na hii ikapelekea kuvuruga soko la hood na kuzipoteza kabisa.
Kinachomsaidia hood gari zake ametawanya Tanzania tofaut na Abood ruti zake zinahesabika.
Baada ya kushinda soko akaanza kujisahau maana akawa wakati mwingine analeta yale mabasi yake ya zamani mwanae.
Nakumbuka niliwahi kukata tiketi pale ubungo kuingia ndani tunaletewa basi sio bahati tulikuwa na ushirikiano tuligoma ndipo likaletwa lile tulilokatia tiketi.
Kwa takribani muda kidogo alijitokeza AL saedy akashindwa kuleta changamoto kwa Abood tatizo la AL saedy gari yake ni kama daladala.
Akaja Gombe Expedition nae hakufanya lolote.
Ndipo BM akamwaga zile youtong zake za mwanzo kwa fund. Na cha kupendeza zaidi akawa anatoa dizaini yote ya mabasi ya kisasa kuanzia youtong, higher mpaka zhongtong na vioo tinted ndani ac(ingawa inawashwa pale stendi ila mkitoka tu wanazima).
Sasa naona Abood nae anatoa youtong za ukweli tatizo lake kubwa zinanyata balaa
Hivyo uwepo wa BM Coach umeleta changamoto kwa Abood Bus.
Nani mwenye nauli ndogo kati ya hao wote maana huyo ndio atakuwa tunayemuhutaji sisi.
 
Kwa taarifa yako tu ni kwamba duru za chini chini zinasema kuwa huyo BM na Abood ni Mtu mmoja hivyo hiyo pongezi yako Kwao ni kama tu vile umempongeza Abood indirectly. Kuna mbinu moja ya Kimasoko ( Market Strategy ) ambayo ' wabobezi ' wa Masuala ya Biashara na Masoko watatusaidia kwani nimelisahau lile neno lake la ' Kitaaluma '. Ni kwamba kwa kawaida Mtu fulani anapokuwa anajua kuwa anakubalika mno na ameshajijengea jina kubwa na imani kwa Wateja wake mahala husika sasa ili kuweza kutopoteza Soko lake kwa ' Washindani ' wapya huamua kuanzisha ' vijikampuni ' vingine kadhaa ili ' Kuwazuga ' tu Watu lakini kumbe vyote ni vyake na faida itakayopatikana bado itabaki tu kuwa yake na ataendelea kutawala hiyo Biashara na hilo eneo.

Yapo Makampuni mengi sana makubwa na yaliyokwisha jizolea ' sifa ' kemkem hapa Tanzania na huko duniani ambapo na Wao walikuja na mbinu hii hii ila sisi ' Wateja ' tumezugwa tu kama siyo kufichwa na hatimaye Pesa / Fedha zetu zote mwisho wa siku tunampelekea tu ' Njemba ' moja na ' Utajiri ' wake unazidi kukua japo ameutawanya.

Hapana chezea ' Wafanyabiashara ' Mkuu kwani ni Wajanja na wana ' mbinu ' kali na za ' kutukuka ' kabisa.
Mwaarabu na mchaga wapi na wapi? BM hawezi kuwa boya kihivyo...Nimfanya biashara na yeye siku nyingi...Kama wameungana hapo sijui lakini siyo eti ni substitute
 
Kudadadeki.....tusubiri tu makafara ya umwagaji damu mwaka huu ama siku za karibuni.....hawa jamaa wa biashara za mabasi si watu wa kuwachukulia poa, ni wapuuzi sana na hawajali maisha ya wenzao. Mtasikia tu basi lao moja limepinduka tena kwenye barabara isiyo na kasoro yeyote na watu mia na kitu wamepoteza maisha hapo hapo na tajiri kutajirika Zaidi. Anaanza na basi moja, baada ya ajali ananunua mengine 10 kwa mpigo.
sijawah ona basi lakubeba watu mia na kitu mkuu
 
Nani mwenye nauli ndogo kati ya hao wote maana huyo ndio atakuwa tunayemuhutaji sisi.
Mkuu kwa safari ya dar mpaka Moro Abood anatoza elfu saba BM elfu saba sijajua kwa AL SAEDY lakini pia zipo za elfu sita akina Islam lakini bado abiria hawapati, BM anakimbizana na Abood
 
Back
Top Bottom