KERO Bus la BM mnazingua sana. Parcel zinapotea na wateja wanaachwa vituoni

KERO Bus la BM mnazingua sana. Parcel zinapotea na wateja wanaachwa vituoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,047
Reaction score
1,474
BM ni mojawapo ya mabasi ambayo imewekeza na kuingia kwenye usafiri na usafirishaji wa parcel kwa nguvu sana. Wana mabasi mengi sana route ya DAR-ARUSHA.

Wasafiri wa kanda hizo wanapenda luxury sana, ukipeleka bus lako ngwarngwara huwezi pata abiria. Wao kulipa TZS 87,000 kwa 2 X 1 seat sio tatizo. Shida inaanza pale ambapo kampuni imekubalika na mnapata wateja wengi na tender parcel za kufa mtu maanaza kuzingua.

Baadhi ya abiria wameshaanza kutoa lawama za kupotea kwa parcel, kuachwa kwenye vituo vyao walipopanga kupanda bus, kupitishwa vituo vya kushukia, kukataa kushusha kwenye baadhi ya vituo, very poor customer care and handling customers complains na mengine mengi.

Hata kama wakubwa wa serikalini wamewekeza shares zao huko ya kuwafnya kuwa na mabasi mengi lakini wao sio wateja wenu wa kuwafanya muwe na kiburi.

Akina TILISHO, ESTER, HOPE BUS, ASANTE RABI, EXTRA LUXURY, KIDIA, wanakungalieni tu na aabiri wana multiple option., mkijisahau tu kazi mnayo.

BM msione kama nyie ndo wababe wa ROAD hata kama mna mabasi mengi, wapo wengi walikuja wakapotea kama barafu. Wapo wapi HOOD BUS LIMITED, NGORIKA, SCANDNAVIA, ISLAM, n.k

Akina KILIMANJARO nao walianza kama wewe sahivi wanachechemea kibishi bishi

TEMBO AKISIFIWA SANA...............................................................................................
 
Back
Top Bottom