Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 43,158
- 51,511
Hata walete mapya kiasi gani siwezi acha kupanda abood kisa BM ni jipya.BM anaweza kuwa na magari mapya lakini hana wateja kama ilivyo kwa abood
BM anafanya vizuri Moro - Arusha kuliko Moro - Dar
Hata walete mapya kiasi gani siwezi acha kupanda abood kisa BM ni jipya.BM anaweza kuwa na magari mapya lakini hana wateja kama ilivyo kwa abood
Unalosema mkuu ni sawa,huyu mchaga Blasto Makundi(BM) alianza na magari mabovu sana Isuzu journey na Coaster zilikuwa zinatoka Turiani kuja Moro mjini nakumbuka hivyo ilikuwa mwaka 2007 akanunua basi mbili kubwa ndio zikaanza kuja Dar Turiani.Ni mtu aliyeanza na biashara hii chini sana.Uzuri jamaa alikuwa anaishi Japan kwa muda mrefu,Turiani kule ndiko makazi yake na biashara zake zilipo.Mwaarabu na mchaga wapi na wapi? BM hawezi kuwa boya kihivyo...Nimfanya biashara na yeye siku nyingi...Kama wameungana hapo sijui lakini siyo eti ni substitute
sijawah ona basi lakubeba watu mia na kitu mkuu
Bado Abood yuko juu. BM mabasi yake kwa sasa ni chakavu.Kwanza naomba nikiri wazi kuwa sina uhusiano wowote na mabasi tajwa mimi ni msafiri tu wa kawaida.
Kiukweli Abood Bus alianza kubweteka na kufanya vile anavyojisikia bila ya kuzingatia mteja anataka nini.
Miaka ya 2000 mwanzoni mpinzani mkubwa wa Abood Bus kwa ruti ya Dsm mpaka Moro alikuwa ni Hood.
Hood alifanya soko la Abood kuwa gumu pale alipoleta Marcopolo Torino na mfumo mpya wa basi kuwa na dereva tu bila ya kondakta.
Wakati huo Abood bado akiendelea na yale mabasi yake ya zamani zile scania engine ipo nyuma (mimi sio mtaalam wa model za magari).
Hii ilipelekea basi nyingi za hood ziwe njiani yaani basi linatoka dsm kwenda Moro likifika chalinze tayari lishajaa abiria wanaolisubiri pale msamvu Moro wards nalo Dsm.
Kuona hali inakuwa tete Abood ikampasa kuvunja kibubu chake nae akazama Africa Kusini akatuletea Marcopolo Andare Class.
Kiukweli basi hizi kwa wakati huo zilikuwa zipo kileleni kwa kila kitu na hii ikapelekea kuvuruga soko la hood na kuzipoteza kabisa.
Kinachomsaidia hood gari zake ametawanya Tanzania tofaut na Abood ruti zake zinahesabika.
Baada ya kushinda soko akaanza kujisahau maana akawa wakati mwingine analeta yale mabasi yake ya zamani mwanae.
Nakumbuka niliwahi kukata tiketi pale ubungo kuingia ndani tunaletewa basi sio bahati tulikuwa na ushirikiano tuligoma ndipo likaletwa lile tulilokatia tiketi.
Kwa takribani muda kidogo alijitokeza AL saedy akashindwa kuleta changamoto kwa Abood tatizo la AL saedy gari yake ni kama daladala.
Akaja Gombe Expedition nae hakufanya lolote.
Ndipo BM akamwaga zile youtong zake za mwanzo kwa fund. Na cha kupendeza zaidi akawa anatoa dizaini yote ya mabasi ya kisasa kuanzia youtong, higher mpaka zhongtong na vioo tinted ndani ac(ingawa inawashwa pale stendi ila mkitoka tu wanazima).
Sasa naona Abood nae anatoa youtong za ukweli tatizo lake kubwa zinanyata balaa
Hivyo uwepo wa BM Coach umeleta changamoto kwa Abood Bus.
Anayo hadi Zhongtonghuyu bwana anataja taja tu aina za magari ya kichina niwazi hayajui kabisa BM COACH ana yutong tupu
BM= BLASTO MAKUNDIAnaitwa Makundi
Yako poa sanaBado haya mabasi ya BM Coach yapo vizuri au ilikuwa nguvu ya soda?
Nina safari ya Moro hivi karibuni so ushauri unapendelewa!
Ndio masharti ya mgangaAbood kuna dereva mmoja mjinga eti akiwa na basi ya kwanza kutoka Morogoro HARUHUSIWI na tajiri kusimama katika vituo husika abiria WACHIMBE DAWA, hivi ni kweli ? Swali kwako mmiliki
Yule Wa CrdbNijuavyo mimi BM ni mabasi ya mswahili (mchaga wa kilimanjaro)
Abood bado wapo moto mzee baba. Bado wanaongoza huko Moro kwenye huduma za mabasi.. Labda kwingineko sijui..Abood zilipendwa
Siyo huyo.. Anaitwa Makundi.Yule Wa Crdb
SawaSiyo huyo.. Anaitwa Makundi.
New Force nao usiwasahau lakini...Abood bado wapo moto mzee baba. Bado wanaongoza huko Moro kwenye huduma za mabasi.. Labda kwingineko sijui..
Hao Wanawapa Tabu Sana Maana Bus Nyingi Sana WanazoNew Force nao usiwasahau lakini...
Waluguru lazima wapande aboodAbood bado wapo moto mzee baba. Bado wanaongoza huko Moro kwenye huduma za mabasi.. Labda kwingineko sijui..
Yap niliwahi kwenda hadi kwake, wale watoto wake walimzingua dogo wangu! Nikalianzisha.Nijuavyo mimi BM ni mabasi ya mswahili (mchaga wa kilimanjaro)