Kwa taarifa yako tu ni kwamba duru za chini chini zinasema kuwa huyo BM na Abood ni Mtu mmoja hivyo hiyo pongezi yako Kwao ni kama tu vile umempongeza Abood indirectly. Kuna mbinu moja ya Kimasoko ( Market Strategy ) ambayo ' wabobezi ' wa Masuala ya Biashara na Masoko watatusaidia kwani nimelisahau lile neno lake la ' Kitaaluma '. Ni kwamba kwa kawaida Mtu fulani anapokuwa anajua kuwa anakubalika mno na ameshajijengea jina kubwa na imani kwa Wateja wake mahala husika sasa ili kuweza kutopoteza Soko lake kwa ' Washindani ' wapya huamua kuanzisha ' vijikampuni ' vingine kadhaa ili ' Kuwazuga ' tu Watu lakini kumbe vyote ni vyake na faida itakayopatikana bado itabaki tu kuwa yake na ataendelea kutawala hiyo Biashara na hilo eneo.
Yapo Makampuni mengi sana makubwa na yaliyokwisha jizolea ' sifa ' kemkem hapa Tanzania na huko duniani ambapo na Wao walikuja na mbinu hii hii ila sisi ' Wateja ' tumezugwa tu kama siyo kufichwa na hatimaye Pesa / Fedha zetu zote mwisho wa siku tunampelekea tu ' Njemba ' moja na ' Utajiri ' wake unazidi kukua japo ameutawanya.
Hapana chezea ' Wafanyabiashara ' Mkuu kwani ni Wajanja na wana ' mbinu ' kali na za ' kutukuka ' kabisa.