BM Coach mmeleta changamoto kwa Abood Bus Dar mpaka Moro

BM Coach mmeleta changamoto kwa Abood Bus Dar mpaka Moro

Kwa taarifa yako tu ni kwamba duru za chini chini zinasema kuwa huyo BM na Abood ni Mtu mmoja hivyo hiyo pongezi yako Kwao ni kama tu vile umempongeza Abood indirectly. Kuna mbinu moja ya Kimasoko ( Market Strategy ) ambayo ' wabobezi ' wa Masuala ya Biashara na Masoko watatusaidia kwani nimelisahau lile neno lake la ' Kitaaluma '. Ni kwamba kwa kawaida Mtu fulani anapokuwa anajua kuwa anakubalika mno na ameshajijengea jina kubwa na imani kwa Wateja wake mahala husika sasa ili kuweza kutopoteza Soko lake kwa ' Washindani ' wapya huamua kuanzisha ' vijikampuni ' vingine kadhaa ili ' Kuwazuga ' tu Watu lakini kumbe vyote ni vyake na faida itakayopatikana bado itabaki tu kuwa yake na ataendelea kutawala hiyo Biashara na hilo eneo.

Yapo Makampuni mengi sana makubwa na yaliyokwisha jizolea ' sifa ' kemkem hapa Tanzania na huko duniani ambapo na Wao walikuja na mbinu hii hii ila sisi ' Wateja ' tumezugwa tu kama siyo kufichwa na hatimaye Pesa / Fedha zetu zote mwisho wa siku tunampelekea tu ' Njemba ' moja na ' Utajiri ' wake unazidi kukua japo ameutawanya.

Hapana chezea ' Wafanyabiashara ' Mkuu kwani ni Wajanja na wana ' mbinu ' kali na za ' kutukuka ' kabisa.
Acha kudanganya watu! BM ni Bestow Makundi, hivyo ni kampuni mbili tofauti na wamiliki tofauti,
 
IMG_20181213_200557_950.jpg
 
Kwanza naomba nikiri wazi kuwa sina uhusiano wowote na mabasi tajwa mimi ni msafiri tu wa kawaida.
Kiukweli Abood Bus alianza kubweteka na kufanya vile anavyojisikia bila ya kuzingatia mteja anataka nini.
Miaka ya 2000 mwanzoni mpinzani mkubwa wa Abood Bus kwa ruti ya Dsm mpaka Moro alikuwa ni Hood.
Hood alifanya soko la Abood kuwa gumu pale alipoleta Marcopolo Torino na mfumo mpya wa basi kuwa na dereva tu bila ya kondakta.
Wakati huo Abood bado akiendelea na yale mabasi yake ya zamani zile scania engine ipo nyuma (mimi sio mtaalam wa model za magari).
Hii ilipelekea basi nyingi za hood ziwe njiani yaani basi linatoka dsm kwenda Moro likifika chalinze tayari lishajaa abiria wanaolisubiri pale msamvu Moro wards nalo Dsm.
Kuona hali inakuwa tete Abood ikampasa kuvunja kibubu chake nae akazama Africa Kusini akatuletea Marcopolo Andare Class.
Kiukweli basi hizi kwa wakati huo zilikuwa zipo kileleni kwa kila kitu na hii ikapelekea kuvuruga soko la hood na kuzipoteza kabisa.
Kinachomsaidia hood gari zake ametawanya Tanzania tofaut na Abood ruti zake zinahesabika.
Baada ya kushinda soko akaanza kujisahau maana akawa wakati mwingine analeta yale mabasi yake ya zamani mwanae.
Nakumbuka niliwahi kukata tiketi pale ubungo kuingia ndani tunaletewa basi sio bahati tulikuwa na ushirikiano tuligoma ndipo likaletwa lile tulilokatia tiketi.
Kwa takribani muda kidogo alijitokeza AL saedy akashindwa kuleta changamoto kwa Abood tatizo la AL saedy gari yake ni kama daladala.
Akaja Gombe Expedition nae hakufanya lolote.
Ndipo BM akamwaga zile youtong zake za mwanzo kwa fund. Na cha kupendeza zaidi akawa anatoa dizaini yote ya mabasi ya kisasa kuanzia youtong, higher mpaka zhongtong na vioo tinted ndani ac(ingawa inawashwa pale stendi ila mkitoka tu wanazima).
Sasa naona Abood nae anatoa youtong za ukweli tatizo lake kubwa zinanyata balaa
Hivyo uwepo wa BM Coach umeleta changamoto kwa Abood Bus.
Mkuu kiukweli uko sahihi,Mimi nimepanda basi zote,About,BM,Al saedy,new force.
Nilipopanda BM na kuona wako,tofauti na wengine,kiukweli mkuu sipandi hayo magari mengine.
Kitakacho nitoa BM ni ujio was train ya umeme itakapoanza kutoa huduma kwa ajili ya muda.
 
Mleta mada tambua Bm sio wa leo toka dar moro nauli 800 yupo japo kipindi hiyo watu walikua awayapendi mabasi yote kuanzia abood hood watu walikua wanaenda magomeni mapipa unakamata coaster ndio ilika habari ya mjini kama unavyoona sasa ukipanda coaster unachelewa zamani coaster ilikua fast enzi za kina TOP STORY.LICO PELLO bm ndio makundi alikua anapeleka dcm tuliani kwa hiyo anajua ubunifu
 
Kwa taarifa yako tu ni kwamba duru za chini chini zinasema kuwa huyo BM na Abood ni Mtu mmoja hivyo hiyo pongezi yako Kwao ni kama tu vile umempongeza Abood indirectly. Kuna mbinu moja ya Kimasoko ( Market Strategy ) ambayo ' wabobezi ' wa Masuala ya Biashara na Masoko watatusaidia kwani nimelisahau lile neno lake la ' Kitaaluma '. Ni kwamba kwa kawaida Mtu fulani anapokuwa anajua kuwa anakubalika mno na ameshajijengea jina kubwa na imani kwa Wateja wake mahala husika sasa ili kuweza kutopoteza Soko lake kwa ' Washindani ' wapya huamua kuanzisha ' vijikampuni ' vingine kadhaa ili ' Kuwazuga ' tu Watu lakini kumbe vyote ni vyake na faida itakayopatikana bado itabaki tu kuwa yake na ataendelea kutawala hiyo Biashara na hilo eneo.

Yapo Makampuni mengi sana makubwa na yaliyokwisha jizolea ' sifa ' kemkem hapa Tanzania na huko duniani ambapo na Wao walikuja na mbinu hii hii ila sisi ' Wateja ' tumezugwa tu kama siyo kufichwa na hatimaye Pesa / Fedha zetu zote mwisho wa siku tunampelekea tu ' Njemba ' moja na ' Utajiri ' wake unazidi kukua japo ameutawanya.

Hapana chezea ' Wafanyabiashara ' Mkuu kwani ni Wajanja na wana ' mbinu ' kali na za ' kutukuka ' kabisa.
Psychological marketing
 
Back
Top Bottom