Blood deal

Blood deal

BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 29

“okay , rudi nyuma ukate mkono wa kushoto , chumba cha kwanza “
“ahsante “,
alijihisi ushindi wa hali ya juu , alichokifanya ni kuingia uwani ,alibadili nguo kwa haraka sana , kisha alitoka kwa tahadhali sana , alinyosha moja kwa moja hadi mbele ya ofisi hiyo, akiwa na bastola pamoja na kisu ,kilichokuwa kiunoni , hakutaka kupoteza muda alifungua mlango, na kuingia ,macho yake yalipokelewa na zaidi ya watu wawili , waliokuwa wanazozana .
*****
Poul hakutaka kukubaliana na maneno ya MacDonald , aliona hafanyiwi haki , kwa jinsi alivyokuwa amewaka kwa hasira ilikuwa ni ngumu sana kumuelewesha ,
“ nyie mbona mnazozana ndani ya ofisi za watu ?,
Mtu aliyekuwa amesimama na bastola aliongea kwa lugha ya Kiswahili, akiwa anamtazama mmoja baada ya mwingine
“Poul nisa..mehe mwa..nangu …ni..nisam..ehe ta…”
“ funga kopo lako haraka , sihitaji ngojera zako hapa “,
mtu yule aliongea huku alivua kitambaa alichokuwa amejifunika usoni , lahaulla ! Alikuwa Ghati , alinyosha mkono wake sawasawa na uso wa David , mkono uliokuwa umeshikilia bastola , tayari kwa kumuua ,
“ sina muda wa kupoteza , rest in peace {pumzika kwa amani }paaaa!”
Maneno hayo aliyasindikiza kwa risasi , lakini risasi hiyo ilipiga talakilishi , mara baada ya mkono huo kupigwa teke na Omar ,
“ uyataka faya nini? This is our person , who send you?{ Huyu ni mtu wetu , nani kakutuma ?}, aliuliza Omar kwa Kiswahili kibovu , akiwa amemkamata vyema Ghati ,
“ hutakiwi kujua , ila tabua , mtu huyu hatakiwi kuishi , natekeleza agizo kutoka kwa boss “
“ boss! Who is your boss?[boss! Nani boss wako] ?”,
Poul naye aliyaingilia mazungumzo hayo , muda wote huo David alikuwa kimya ,kabisa ,moyoni aliomba miujiza itokee , ila kwa dalili zilizokuwepo mbele yake , ilikuwa ni ngumu sana kutokea hilo , mwili wote ulitweta kwa jasho , hakuwa akisikia hata maumivu ya kuchanwa kiganja chake , japo damu zilikuwa zikiendelea kutoka ,
“ binti usipousema ukweli utakufa “,
MacDonald aliongea huku akimuachia Poul na kumsogelea Ghati , alimkaba shingo yake kwa mkono wa kushoto , akiwa ameyatoa macho , mdomo wa bastola ukiwa usoni kwa Ghati,
“ semaaa”
“ sawa niachie “,
japo alikuwa amekabwa kwa nguvu lakini , hakudiriki kutetemeka , ilibidi asimulie nusu ya kisa , Poul kusikia jina la Vero , alijikuta akitoa chozi, picha na kumbukumbu zote zilirejea, alimkumbuka msichana huyo aliyekuwa akimlea vizuri , akimpeleka shule na kumfuata , akimchekesha pindi alipokwazika ,kila kitu kilirejea ndani ya akili yake .
“ Baba muachie , ni mtu mzuri sana “
“ kweli ?’
“ Ndiyo “
Ghati alipoachiwa alimfuata David , alimpiga ngumi ya kifua hali iliyopelekea kuinama kidogo , kwa jinsi alivyokuwa amenywea hata hakupata wazo la kuchukua bastola yake , alikuwa mdogo mithili ya pilitoni , kitu alichokuwa akikiwaza ni miujiza tu , alitamani kupiga kelele lakini hakuweza,
“ anatakiwa apelekwe sehemu nzuri kwa mahojiano zaidi “,
Ghati aliongea , huku akiwatazama wenzake , mawazo hayo yalionekana kufaa sana , ilibidi wampe somo la kujikaza pindi atakapotoka nje , na kama angeleta usumbufu kifo kilikuwa halali yake , hakuwa na ubishi alijikaza na kuanza kuongoza njia mbele akitanguliwa na Omar pamoja na Ghati aliyekuwa bado na mavazi yake yale yale mekundu , hakujali kama angeweza kushitukiwa , kisha alifuta Poul na nyuma kabisa alikuwa MacDonald ,
“ Linda nakuja “
“ sawa boss “,
msichana wa mapokezi alijibu huku akiwa amemkazia macho boss wake huyo , hakujua kipi kilikuwa kinaendelea , hadi wanatoka nje ya jengo hilo hakuna mtu aliye fahamu , japo walinzi toka shirika la Kk security walikuwa eneo hilo ,lakini hawakufahamu nini kilikuwa kikiendelea .
Baada ya kumuingiza ndani ya gari lake aina ya Prando hapo ndipo walipomfunga uso kwa kitambaa cheusi safari ya kuelekea Geita ndani ya pori la matete ilianza , Omar ndiye alikuwa dereva , aliendesha gari hadi kigongo feri ,kwa muongozo wa Ghati pamoja na Poul , akipitia barabara ya Shinyanga , walifuata utaratibu wote hapo kivukoni kisha waliendelea na safari yao .
Majira ya saa kumi jioni walikuwa ndani ya pori hilo ,walimshusha na kuanza kumvuta kuingia ndani zaidi ,
“unachotakiwa ni kuongea ukweli , ukifanya hivyo utakuwa umejiwekea uwezekano wa wewe kuendelea kuishi “,
Poul aliongea huku akimchanja chanja na ncha ya kisu chake , mgongoni, chanja chanja hiyo ilipelekea shati lake uchanika chanika , japo alikuwa akimuomba msamaha ,lakini Poul hakuwa na roho ya kutoa msamaha huo ,
“ mpe hii karatasi aandike sababu ya kuua”,
MacDonald aliongea huku akitoa kipande cha karatasi na kumpatia Poul ,naye alikifikisha moja kwa moja kwa David ,
“ andika ukweli wote , ukipindisha , kifo halali yako, pia orodhesha mali zote na unirithishe mimi “
“zote !”
“ Ndiyo ?”
“ Ha..ha..hapana mwanagu ,mie nitaishije lakini ?”
“ kwani mali zako? , Jasho la baba yangu ,ama hufahamu hilo paaaa!”
Aliongea kwa hasira , kitendo cha David kukataa kumrithisha mali ,kilimkera sana , ilibidi ampinge makofi ya usoni ili kumuweka sawa , makofi hayo hayakubadili nia ya David aliendelea kukataa tu ! Hapo ndipo msichana Ghati alipopandwa na hasira alimsukuma Poul na kumsogerea David ,
“ Omar nipatie huo mkasi , anaona tunacheka .“
Baada ya kupewa alianza kumbana kila sehemu ya mwili , muda mwingine alidriki kutoka na kiasi kidogo cha nyama , japo aliumia na kutoa machozi lakini msimamo ulikiuwa ule ule , mali hakutaka kuachia ,
“ sasa nakufanyia kitu mbaya , nakuoa meno bila ganzi “,
MacDonald aliongea kwa kichina , lugha ambayo ilikuwa ngeni kwa David na Ghati pekee yao , alimtoa Ghati na kumpiga ngumi moja tu iliyopelekea meno yake mawili ya mbele kutoka , yakiacha damu zikichuruzika ,
“ bado unagoma ?’
“ Naaaandikaaaa”,
aliongea kwa maumivu makali sana, ilibidi akubali , hali aliyokuwa nayo ilimtisha , tayari alishatambua nia ya watu hao , kukataa kwake kungepelekea hata kifo .
*****
“ Huu ndi…o.. ukw…eliiiiii, na..kuomba…usiniue …mwana..ngu”,
alizungumza kwa taabu sana ,kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia , Poul alishindwa kuvumilia pindi alipoyasoma maamdishi hayo ,ilikuwa kama katoneshwa donda alilia sana ,
“ ahsante , kwa ukweli wako ila tambua sitakuacha hai “
“ ha.pa..na .. nisa..mehe ..nai..acha ..fami..lia…yang..na..nani?”
“ Hahahaha! Ulipowaua wazazi wangu ulitegemea nitaishi na nani ?, Unastahili kufa, nitawasaidia mie “,
Poul hakutaka tena kuongea alianza kumchana chana kila sehemu ya mwili , jinsi alivyokuwa amevimba kwa hasira na uchungu ilikuwa ngumu mtu yeyote kumkataza , hakuishia kumchana chana tu, alianza kumkata kidole kimoja baada ya kingine , David alilia kama mtoto mdogo , maumivu aliyokuwa akiyasikia aliyafahamu mwenye ,
“ hadi unakufa nakukata kiungo kimoja baada ya kingine , jinsi unavyoumia na kuhangahika kwa maumivu makali na machungu tambua hata wao walihangaika vivyo , waliumia vivyo “ ,
aliongea huku akihamia vidole vya miguuni nako alikata kimoja baada ya kingine kwa kutumia kisu chake , muda wote huo wenzake walikuwa kimya wakikitazama kitendo hicho , hakuna aliyeweza kumuonea huruma David ,
“ sasa zamu ya kukata masikio , pua na mdomo “
“ boraaa un..iue..tu ..kuliko ..ku.ni..fa..ny..ia..hiviiiiiiiiiiiii”
“ hahahah !” Poul alicheka kwa dharau iliyochanganyikana na hasira , hakujali maneno yake alimkata sikio la kushoto na kuliweka pembeni , na la kushoto alifanya vivyo hivyo , alihakikisha kila kiungo amekitoa katika mwili huo ,
“ hebu mmalizie tuondoke “
“ sawa “ ,
papo hapo alimchoma kisu cha tumboni kama mara tatu , akichoma na kuchomoa , hakuna kilichosika zaidi ya kilio cha maumivu kisha David alipoteza maisha papo hapo ,
“ tunamzika ?”
“ Hana haja ya kuzikwa , baba yangu alilala barabarani usiku mzima akiwa amekufa , atakuwa chakula cha fisi , tuondokeni “.
Poul alihisi kutua kitu flani kizito ndani ya mwili wake , alijihisi mwepesi kabisa , kitu kilichokuwepo mbele yake ni kufikisha ujumbe huo kwa babu na bibi yake ambao sasa walikuwa wakiishi katika nyumba ya wazazi wake hapo Bugando . Walisafiri hadi mwanza jioni hiyo hiyo , majira ya saa nne usiku walikuwa kivuko cha kigongo feri , walisubili kwa muda wa dakika kumi na tano , ndipo feri hiyo ilifika , waliingiza gari lao ambalo lilikuwa la marehemu David , na baada ya dakika kumi na tano walikuwa upande wa pili , dakika arobaini na tano tayari walikuwa ndani ya jiji la mwanza ,
“ sasa mie nasepa “
“ wapi tena ?”
“ Kitwima hoteli , kesho asubuhi ya saa kumi na moja naingia Tarime “
“ hapana dada Ghati , naomba kesho twende sote nyumbani kwetu aghalau ukawaone wazee wangu ,nadhani watafurahi sana kukuona , na utanisaidia kuwaelewesha “
“ nini haraka , ila kwa kuwa umeongea wewe nitakuwa bega kwa bega nawe “ ,
yalikuwa maongezi kati Vero na Poul wakiwa nje ya mwanza hoteli usiku huo .Vero aliagana nao kisha akaondoka , kwa miadi ya kukutana siku ilifuata .
****

Hatimae David kauliwa na Poul (Mototo wa kaka yake)...

Ila nahisi Poul hatoishi kwa raha, misukosuko lazima itamuandama... Kuua siyo jambo dogo...

Cc: mahondaw
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimeshusha pumzi puuuuuuh!!! Baada ya kumaliza kusoma
 
Asante sana Madame. Hadithi nzuri, David kapata alichostahili
 
Duh imebidi niangalie km nimefunga vizuri mlango wangu,maana nimeingiwa na hofu huyu Poul asije akaingia na huku maana kukatana kiungo kimoja kimoja,vidole,masikio,pua mh inahitaji moyo dah ila kwa David bado adhabu ilikuwa haitoshi aisee maana unyama alioufanya ulikuwa wa kiwango cha Standard Gauge hivyo alistahilli kwanza kipigo cha mbwa koko.
Madame shukrani sana nimepata funzo inabidi tuwe makini sana na hawa madogo maana.
 
Duh imebidi niangalie km nimefunga vizuri mlango wangu,maana nimeingiwa na hofu huyu Poul asije akaingia na huku maana kukatana kiungo kimoja kimoja,vidole,masikio,pua mh inahitaji moyo dah ila kwa David bado adhabu ilikuwa haitoshi aisee maana unyama alioufanya ulikuwa wa kiwango cha Standard Gauge hivyo alistahilli kwanza kipigo cha mbwa koko.
Madame shukrani sana nimepata funzo inabidi tuwe makini sana na hawa madogo maana.
Hahahahaha asante kwa kushukuru bachelor sugu
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 30

“Khogoo! Khogoo!Khogooo!” ,
Ilikuwa ni sauti ya geti likigongwa , sauti hiyo haikufika mapema masikioni pa wakazi wa nyumba hiyo , kutokana na hali ya mvua ya rasha rasha ,iliyokuwa ikinyesha , asubuhi hiyo , wanaume watatu na mwanamke mmoja walikuwa wamesimama mbele ya geti hilo waliendelea kugonga bila kuchoka ,
“ bibi nasikia kuna mtu anagonga geti “
“ nenda kamtazame , yawezekana atakuwa shangazi yako , jana alisema anakuja “,
aliongea mwanamke aliyekuwa ameketi juu ya kitanda chake , huku mwili wake akiwa ameufunika kwa nguo nzito ili kulikabili baridi la siku hiyo , hakuwa na kawaida ya kuamka mapema, lakini siku hiyo alikuwa ameshaamka na tayari alikuwa ameshaoga , msichana wa kazi alipoelekea getini akiwa amejifunika na mwavuli kuzuia maji ya mvua yasiulowanishe mwili wake ,naye alitoka chumbani kwake akijikokota taratibu ,
“ kumbe uko huku babu “
“ ndiyo bibi , sikutaka kukuamsha ,harafu leo usiku nimeota ndoto mbaya sana “,
aliongea mzee Poul huku akijitengeneza vizuri , macho yake tu yaliashilia kile alichokiongea
“ babu umeota nini ?
Mke wake ambaye walizoeana kuitana babu na bibi, wakifatisha tabia za wajukuu zao , alimuuliza huku akiwa amemkazia macho yake madogo kiasi , ya kizee
“ nimeota mwanangu Emanuel akimpiga sana mdogo wake David , na hata amepelekea kumuua , sijui ndoto gani hiyo “
“mmmmh ! Unasema ?”,
Bibi alijikuta akiuliza swali hilo kana kwamba hakuwa amesikia kile kilicho zungumzwa , kabla mzee huyo hajazungumza , watu watano walisimama katikati ya sebule yake , Jesca ambaye ni msichana wa kazi aliwakaribisha kwa heshima,
“ shikamoo babu “,
Poul alimsalimia babu yake huku akinyosha mkono wake wa kulia , mzee huyo aliupokea kwa furaha , huku uso wake wa kizee ukiweka tabasamu na shangwa za kumuona mjuu wake huyo aliyekuwa kipenzi chake ,toka utoto ,
Umekuja lini ?Mume wangu ?” ,
Bibi yake naye alimuuliza , huku akinyanyuka kwenye kiti na kumfuata mjukuu huyo , alimkumbatia katika kifua chake , huku akitoa machozi ya furaha sana , japo ulikuwa muda mfupi tu toka wametengana , lakini kwake aliona kama miaka kumi iliyopita , baada ya salamu hizo , wote walikaa na utambulisho uliendelea ,muda ulipowadia , Poul aliwasimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea , hali iliyopelekea hata wao kushtuka sana na kushangaa , japo ilikuwa ngumu kuamini ,ila maneno yaliyokuwa yameandikwa kwenye karatasi yalizidi kuwaaminisha sana . Ilikuwa kama msiba ndani ya nyumba hiyo , wazee hao walimlilia mtoto wao Emanuel na mkwe wao Janiphar , huku wakiendelea kumtupia laana na lawama David , hawakusta kutoa shukurani za dhati kwa MacDonald aliyejitolea kwa moyo wake wa dhati na mapenzi ya kweli , ya kumtetea mjukuu wao hadi hapo , zaidi na zaidi walimshukuru pia Ghati na Vero kwa kazi waliyokuwa wameifanya , pia walimomba Ghati akirejea Tarime asiste kumsalimia sana msichana huyo na kumtaka afike nyumbani hapo , sasa walimchukulia kama mtoto wao wa kuzaa .
Taarifa hizo pia zilifika kwa shangazi yake Poul aliyekuwa Daktari wa Bugando kwa muda huo , aliumia sana , naye alimulaani kaka yake huyo mdogo , kwa kuwa alikuwa akizifahamu tabia zake toka wakiwa wadogo hakusta kumuamini Poul.
*****
“ Mwanao atakuja tu , naomba nipumzike tafadhali “,
aliongea Mohamed mara baada ya kufika Iran , akitokea China , mke wake alizidi kulalama japo alikuwaa ameshaambiwa ukweli wote na kuombwa amuache mtoto aendelea na maisha yake ,lakini hakukubaliana naye , alichotaka ni uwepo wa Joan nyumbani hapo , maisha yake bila binti huyo hayakuwa yamekamilika kabisa
“ sasa unategemea ningefanyaje ?’
“ wewe ulishindwa kumkamata kwa nguvu ?”
“ Wewe si unamjua MacDonald , yule mtambo , naomba tuwaache waendele na maisha yao , watoto wamependana basi “
“ huna akili Mohammed , nani akubali mwanangu awe na mtu mweusi tena kafiri “
“ wewe ulichanguliwa mume ?”
“ Hapana “
“basi muache Joan afanye mambo yake , cha msingi ni kuwashauri wasijihusishe na mapenzi katika umri mdogo , hilo linaweza pelekea kuharibu masomo yao “
, mwanaume huyo alijitahidi kumshauri mke wake , hadi alikubali , kilichokuwa kimebaki ni kuwaombea dua njema watoto hao , ambao hawakujua wako wapi , lakini waliamini wapo salama .
Wiki moja baadaye Poul na wenzake walisafiri hadi China walikaa nyumbani kwa MacDonald kwa muda wa siku tatu kisha walielekea Iran nyumbani kwao Joan , walipokelewa kwa furaha , hata wao walishangaa mapokezi hayo , siku hiyo wazazi hao, walitoa ruhsa kwa marafi hao na kuwasistizia zaidi kusoma , Joan alijihisi kunenepa kila kitu alikiona kipya ndani ya masikio yake , siku tano kulifanyika tafirija kubwa nyumbani hapo iliyohudhuliwa na idadi kubwa ya watu , tena wale walioheshimia ndani ya Iran na Oman , baada ya sherehe hiyo watoto hao walilejea China kwa ajili ya masomo yao , huku wakiwa na shangwe ndani ya mioyo yao.Siku hazikuganda hatimaye Poul alihitimu masomo yake yote ,hadi yale ya chuo na kulejea nyumbani kwao Tanzania kuziendeleza mali za baba yake ambazo kwa muda huo zilikuwa chini ya usimamizi wa shangazi yake na mke wa David ambaye hakuwa na roho mbaya kama ya mume wake , aliwashukuru kwa kusimamia vyema, mali hizo .
****
Ilikuwa ni harusi kubwa sana nchini Tanzania ambayo haijawahi kutokea , ni zaidi ya miezi miwili ndoa hiyo ilikuwa ikitangazwa katika vyombo mbalimabali vya habari , kila mtu alijihapiza kuhudhulia sherehe hiyo , ambayo ilikuwa ya kihistoria . Tarehe 03/02/2008, siku hiyo ilikuwa ikisubiliwa kwa hamu sana , mji wa mwanza ulikuwa umefurika idadi kubwa ya watu , japo ilikuwa siku ya mvua ya rasharasha, lakini watu hawakujali mvua hiyo , toka saa kumi na mbili asubuhi watu walijaa ndani uwanja wa furahisha kirumba, kungojea tukio hilo , hakuna kanisa ambalo lingeweza kutosha kuchukua idadi ya watu hao .
Majira ya saa nne asubuhi magari ya viogozi mbalimbali wa serikali yalianza kuingia ndani ya uwanja huo , siyo ya serikali pekee yake, bali hata ya watu mashuhuri nje ya Tanzania , saa moja mbele , zilisikika kelele na ndelemo toka kila kona ya uwanja huo , mwanamke mwenye asili ya kiarabu alikuwa ndani ya shela , akikokotwa na farasi mweupe toka uingereza , farasi huyo alipita katikati ya uwanja huo , hali iliyopelekea kila mtu kusimama na kushangilia , kabla hajafika mbele , bwana harusi alitokea , kitendo kilichozidi kuwashangaza watu hao ,ambao hawakufahamu ni muda gani alifika eneo hilo ,wazazi wa Joan pamoja na ndugu toka Iran na Oman hawakuwa nyuma kutoa tabasamu zao .
“ umependeza mpenzi “
“ ahsante , siamini kama leo naolewa na wewe”
“ amini “ ,
waliongea kwa furaha huku wakitembea kwenda mbele , mshereheshaji aliongea mawili matatu ,kisha Padri Nikodemu alifungisha ndoa hiyo , hali iliyopelekea shangwa za hali ya juu , wengi wao walitoa machozi ya furaha , mtu aliyekuwa akilia bila kunyamaza alikuwa shangazi yake Poul , kumbukumbu za ndoa ya kaka yake Emanuel zilikuwa zimelejea , alimuona Poul kama kaka yake kwa jinsi walivyofanana. Tukio hilo lilipokamilika watu walitawanyika wakisubili jioni kwenda ukumbini .
“ ujue siamini kama kweli nimekuoa “
“ kwanini?”
“ Misukosuko iliyokuwa mbele yetu ilikuwa inanitisha “
“kweli , ila yalishapita cha msingi tuangalie mbele , jana daima haitatusaidia “
“ umeongea la maana , eeeeh ! Hebu niambie utanizalia watoto wangapi ?”
“ Mmoja “, aliogea Joan huku akitabasamu .
“ acha masihala mie msukuma nataka watoto kumi , hujui natakiwa kutengeneza ukoo “
“ kumi , hawatoshi , nakuzalia kumi na tano , timu ya mpira , pamoja na viongozi wake “
“ hahahaha!”
Walicheka kwa furaha kisha walijifunika shuka gubi gubi , kuumalizia usiku huo , wakiwa ndani ya Goldcrest hotel , wakisubili siku inayofuata waelekee Marekani kwa ajili ya fungate lao.
MWISHO.
Inapendeza sana...


Cc: mahondaw
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 4

" masikini watoto wangu "
Hakika yalikuwa maumivu yasiyopimika ndani ya mioyo yao kuuawa kwa Emanuel na kupigwa kwa David kama walivyopata habari kutoka Afghanistan iliwaumiza sana, hakuna hata mmoja aliekuwa anaujua ukweli . Baada ya David kutekereza adhima yake aliamua nae ajiumize kiaina ili kuficha ukweli halisi ,kweli usiku huo huo aliiamua kujipiga risasi ya mguuni sehemu aliyona ingepona mapema, mikono nayo aliijeruhi achilia mbali usoni japo aliumia lakini hakujali roho ya dhuruma ilikuwa imemtawala kupita maelezo.
****
" bwana alitoa na bwana ametoa jina lake lihimidiwe, najua tunaumia sana kumpoteza mpendwa wetu ila kazi ya mola haina makosa, leo Safari ya mpendwa wetu Emanuel imeishia hapa nasi tumuombe mungu atusaidie kuishi maisha ya utakatifu hapa duniani, zaidi na zaidi tumuombe mungu ampumzishe pahali pema peponi ndugu yetu alietutangulia "
Yalikuwa ni maneno ya kuhuzunisha na kufariji kiasi flani kutoka kwa Padri Biruru ndani ya kiwanja cha kanisa kathoric bugando jijini mwanza, kutokana na idadi kubwa ya waombolezaji kufurika kanisani hapo misa ya mazishi ilifanyika nje ya kanisa ndani hakukufaa kabisa. Hakuna mtu alieshindwa kutoa machozi pindi alipoyatupia macho yake katika jeneza la Emanuel kipenzi cha watu mkoani hapo, mashirika mbalimbali nayo hayakuwa nyuma, vituo vya watoto yatima alivyokuwa akivisaidia navyo havikukosa kumsindikiza mpendwa wao.
" Mama Baba atakuja lini? "
"sass! ha..... "Janiphar alishindwa kujibu swali hilo kutoka kwa mwanae mdogo poul aliekuwa na miaka mitatu tu, swali hilo lilizidi kuumiza moyo wake, hakujua ajibu vipi ama aseme nini
" mama baba mbona haji? "
Poul alizidi kumsumbua mama yake aliekuwa hajiwezi kwa lolote na kila alipoyaruhusu macho yake kulitazama jeneza alipoteza fahamu.
Baada ya misa hiyo kumalizika safari za kuelekea makaburi ya Kangae wilaya ya Ilemela ilianza wakipitia barabara ya musoma, walipofika buzurunga walikata kushoto kuitafuta nyakato mecca, papo hapo kituo cha mecco walikata kushoto tena wakifuata barabara ya vumbi hadi makaburini, zoezi la kumhifadhi Emanuel halikuchukua muda mrefu hivyo Safari ya bwana Emanuel tajiri kijana ikawa imefika mwisho
" hakikisha unaitunza hiyo hati ya hoteli "
" sawa baba, ila vipi kuhusu hizo zingine? "
Msichsna wa kazi alimuuliza David ambaye hakuhuzuria maziko ya kaka yake kuanzia kanisani hadi makaburini akijifanya kuzimia kutokana na kulia sana hivyo ndugu hao waliamua kumuacha nyumbani, nusu saa baada ya kutoka nyumbani waombolezaji hao alizinduka na kuelekea chumbani kwa kaka yake alikoiba kila nyaraka za maana akiwa dakika za mwisho Vero msichana wa kazi alimfumania.
"zipo... zipooo kwani... vipi? "
Alishindwa kuongea vizuri baada ya kukaziwa macho makali na msichana huyo aliekuwa ameanza kumstukia muda mrefu hata kabla ya kifo cha boss wake ila hakuwa na uhakika hata kidogo.Hakutaka kukaaa tena chumbani humo alitoka akiwa anachechemea akielekea chumbani kwake
" huyu hanijui eeeh! ,nampa masaa 120".

" huyu hanijui nampa masaa 120"
David aliwaza maneno hayo huku akitembea kwa kuchechemea kutoka ndani ya chumba cha kaka yake, moyo wake ulijaa hasira isiyoelezeka hata kidogo aliona kila kitu kitaenda fyongo na siri yake ingetambulika na hilo hakutaka litokee hata kidogo.
" puuuuuuh! "
Alivuta pumzi ndefu baada ya kufika chumbani kwake alikojitupia kitandani kama mzigo puuu akiwa chali macho yake akiyaruhusu kutazama dali lilokuwa limenakishiwa kwa jipsamu rangi nyeupe ikiwa imepambwa vyema na maua ua. Dakika saba alitumia kufikiri ni kifo gani kingemfaa Vero tena kisicho na makelele ama maumivu
" hahaha! "
David aliachia cheko changa lenye maumivu ndani yake baada ya kupata jibu la kazi yake.
" Hail poison itamtosha huyu "
Hii ilikuwa ni sumu hatari sana yenye asili ya hewa hewa ambayo mtu ama kiumbe hai kikipewa sumu hii dakika tatu kinapoteza maisha huku akikiwa amebadirika rangi ya ngozi kuwa nyeusi, sumu hiyo aliipata nchini Austaria kwa gharama kubwa sana ndio aliona suruhisho tosha kutekeleza adhima yake aliyokuwa amekusuudia ya kumuangamiza Vero.
" atakoma" aliongae huku akinyanyuka kitandani hapo na kuliendea Begi lake dogo lililokuwa na sumu hiyo lakini kabla hajafanya chochote alipatata wazo la kurudisha nyaraka alizokuwa aneziiba chumbani kwa shemeji yake ,kweli alikubaliana na wazo hilo alinyanyuka haraka sana.
" sijui nimweleze Mama" Vero aliwaza akiwa bado amesimama ndani ya chumba cha boss wake mkononi akiwa bado ameshikilia hati ya hoteli aliyokuwa amepewa na David baba mdogo wake, kilichomshitua ni kufunguliwa kwa mlago tena kwa kasi ya ajabu haraka aliigeuza shingo yake na kukutana na David akiwa ameshika karatasi tano
" unafanya nini "
" aaaaah!, ba... baba.. nina... "
Vero ama Veronica alishindwa kuongea baada ya kukaziwa macho makali na Baba yake huyo Mdogo aliekuwa bado asimama katikati ya mlango
" pishaaa"
Aliongea huku akianza kutembea kuliendea kabati, Vero hakutaka kuendelea kubaki hapo aliondoka na ile hati hadi chumbani kwake na kuificha ndani ya begi lake dogo la nguo aina ya Omega rangi ya ugoro lililokuwa sakafuni bila kuwekewa kitu chochote chini .
" kazi ipo hapa daaa sijui tutasalimika huyu ni nyoka tena koboko daaa!. yawezekana hata Baba alimuua huyu "
Kwa kuwa Vero alikuwa Binti aliejitambua na kujaliwa uelewa mkubwa alianza kumstukia David na kupanga mikakati ya kupambana nae bila kujua kama mwenzake alikuwa mafia na jambazi mkubwa.
" kesho nakiondoa duniani kijinga sana "
Aliwaza huku akiondoka chumbani humo kwa Mara ya pili.
*****
Kesho nakiondosha duniani kijinga sana "
Aliongea huku akiondoka chumbani humo kwa Mara ya pili.
Baada ya lisaa limoja kuondoka waombolezaji walilejea kutoka makaburini hivyo David aliendelea kujiuguza tena.
Kesho yake kikao cha familia kilichukua nafasi na pendekezo lililopatikana Janiphar ataendelea kuwa msimamizi mkubwa wa mali zote akisaidizana na David, kwa kuwa hakuna na shaka nae yeyote akuwa na budi kumkataa na ukizingatia walikuwa wakifanya kazi nae muda mrefu hata kabla ya kifo cha mmewe.
"afadhali mambo yangu yameanza kwenda vyema sasa"
" kiaje David? " Eric miongoni mwa marafiki zake waliokuwa hawafanyi kazi zaidi ya kutegemea kodi kutoka kwenye nyumba zao za uridhi zikizokuwa mtaaa wa uhuru mkabara na mount meru university
" si kuhusu yule demu? " David alisema huku akichukua kipande cha nyama choma ndani ya sahani wakiwa Kumalija Hoteli iliyoko nyegezi stendi usiku huo
"aaah!,sikia huwezi kukiua kibinti kizuri kama kile bila kukila kwanza, tukiteke kikiwa kinaenda sokoni tukakibake kwanza harafu ndo tukiue "
" kile hakifai kichafu "
"mie naugwadu mtu wangu nipe nipunguze mafuta mwilini "
" basi poa kesho jiandae, "
Japo zilikuwa siku mbili tu baada ya kuzikwa kwa Emanuel David alikuwa tayari ameanza kunywa pombe, hakuwa na huruma hata chembe na mbaya zaidi alikuwa akianza kumuwinda Vero ambaye nae alikuwa amedhamilia kupambana nae.

kikao kati ya David na Eric kilivunjwa baada ya wao kwa wao kuanza kutoleana maneno ya kashifa usiku huo, hakiri ya David ilikuwa ikifanya kazi zaidi ya computer, vyovyote vile aliamini lazima Erick angemsaliti na hilo huwa hakubaliani nalo hata siku moja
" lest in peace Erick ( pumzika kwa amani Erick) "
David alizungumza maneno hayo huku akiwa anatoa machozi ya hasira iliyochanganyikana na uchungu, mkononi alishika bastola yake aina ya Berreta isiyo na sauti, aliibusu huku akiendelea kuiomba ifanye kazi yake sahihi,japo Erick hakuepo lakini tayari alishapanga kumuua usiku huo huo. Aliwasha gari na kuondoka hotelini hapo akiwa na hasira zisizo elezeka safari yake iliishia mtaa wa uhuru nyuma ya Wande hoteli hapo ndipo Erick alikuwa akiishi zaidi ya dakika 180 alikuwa eneo hilo akiwa anaendelea kuvuta sigara aina ya ESM ndani ya gari la kaka yake.
" safi sana " aliongea peke yake mara baada ya kumuona Erick akija eneo hilo, papo hapo aliichomoa bastola yake iliyokuwa kiunoni , aliikagua kama ilikuwa na risasi, alitabasamu mara baada ya kukutana na risasi tatu alimulenga Erick kichwani ,risasi moja tu ilikimaliza kichwa chake kisha aliondoka eneo hilo bila mtu yeyote kuona hiyo ilisababishwa na hali ya mvua usiku huo. Hakuwa na hofu yeyote dhidi ya vyombo vya dola, zaidi ya viogozi wakubwa walikuwa marafiki zake, pia heshima ya marehemu kaka yake aliitumia kufanyia uovu na uozo uliopindukia.
******
"lete bia hapa wewe kahaba! "
Erick aliongea kwa Sauti ya kilevi iliyochanganyikana na ukali kiasi,
"mshikaji punguza maneno machafu"
" wewe acha kuongea pumba hawa ni mamalaya tu yanat **** ,kila siku "
Erick aliendelea kuporomosha maneno makali dhidi ya wasichana wale hasa hasa akina Dada waliokuwa wamebarikiwa ama kujaliwa makalio makubwa ,hakujali maneno yake kwamba yalikuwa mwiba kwa wengine, yeye aliona kila muhudumu ndani ya kumalija hoteli alikuwa malaya.
Story inanikumbusha kwetu rock city, naona raha kuisoma, nikiisoma hiyo mitaa najiona niko home kabisa
 
Thank you kwa hadithi nzuri ambayo imenirudisha home kabisa, home sweet home.....Mwanza.
Dave umevuna ulichopanda.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom