BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.
SEHEMU YA 20
“ mmmmh! “ Aliguna kwanza , mguno uliyokuwa umechanganyikana na uchungu , wasiwasi na hata hasira dhidi ya mpigaji huyo,
“ atanikoma mjinga sana “,
alijisemea ndani ya nafsi yake huku akibonyeza sehemu ya kupokelea , kisha aliupeleka mkono huo sikioni .
“ kwanza samahani sa……….”
“ Homayoun ,kama huwezi kazi sema , humuwezi kukaa kimya muda wote huo , hamjui kipi kilichonipata ?”
Aliongea David kwa hasira ,huku uso wake ukikunja ndita , povu nalo mdomoni lilitoka , mfano wa povu la bia ndani ya birauli ,
“ unatakiwa utusikilize ,sio kulalamika , ok fine kama unaona tunazembea basi fanya wewe , na kuanzia sasa mie usinishirikishe katika mambo yako sawa?”
Homayoun nae alijikuta akipandisha hasira , hakujali kama David alikuwa boss wake , matatizo aliyokuwa nayo aliyafahamu yeye!
“ Usifike huko , ta…tafadhali! Bado nakuhitaji zaidi ya unavyofikiria, nakuomba sana , sana “
“ kwanza kabla ya yote ,vijana wako wote toka Tanzania wameuawa , pili ninavyoongea nawe uwezekano wa kumkamata kijana huyo ni mudogo sana , anasaidiwa na MacDonald tajiri wa nguvu zote, anatumia mitandao mirefu , na ana mbinu nyingi za kivita , naomba tuachane nae “
“ hujui unachokizungumza , wewe mwarabu koko, mjinga sana , kwa lipi atuzidi ?
“ Humfahamu ndo maana, ila ukweli ndio huo ,sawa kila kitakachoendelea nitakujuza sawa? “
“ poa”
Aliitikia kwa unyonge , siku zote hakutaka moyo wake upate karaha yeyote , jinsi alivyomjua Poul uhakika wa kumuacha hai haukuwepo,
“ siku nikimfahamu aliyemuua baba yangu nahakikisha namchoma kisu cha tumbo “
“kwanini Poul?”
David alihoji huku akimkazia macho kijana huyo ,
“amenifanya nikawa yatima, amenitesa vya kutosha , na mbaya zaidi ameniliza kwa muda mrefu , wallah ba mdogo namuua acha nikue “
“mmmh!” David aliishia kuguna tu, mara baada ya kuyakumbuka mazungumzoa kati yake na kijana huyo ,miaka kadhaa iliyopita , alihisi kuchanganyikiwa ,muda mwingine alijilaumu kuumuacha hai muda wote huo .
“ lakini nashindwaje ?”
Aliendelea kujiuliza mawazo yenye mfumo wa swali ,lakini hakupata jibu sahihi , zaidi ya kuongeza mawazo .
Hadi anafika nyumbani kwake majira ya saa sita usiku ,hakuwa amepata jibu lolote , zaidi ya kuendelea kuchanganyikiwa , hakutaka kuongea na mtu , kujitupa kitandani tena bila kuoga ,mkewe alipouliza hakupata jibu sahihi zaidi ya maeno makali tena yenye kuudhi sana .Saa kumi na mbili asubuhi alidamka na kuelekea bafuni alitoka bila kuongea na mtu yeyote ,zaidi ya salamu tu , hali hiyo ilimkwaza sana mkewe , hakujua kipi kilimsibu mumewe , kwanza hakuwa nyumbani hapo usiku mzima na mchana yake , bila taarifa yeyote ,na mbaya zaidi simu alizima zote , pili karudi bila kuzungumza chochote zaidi ya maneno ya karaha ,vyote hivyo vilimchanganya sana mwanamke huyo ,lakini hakuwa na cha kufanya .
“Kaka maji yamefika shingoni ukisikia aibu ,sasa ndio hiyo yaja ujue “
“kiaje David ?”
Deus alihoji huku akikigeuza kiti chake cha kuzunguka , na kumtazama David, aliyeonekana mnyonge kupita maelezo,uso wake tu ulionyesha hali hiyo ,achilia mbali midomo kukauka ,mithili ya mgonjwa wa maralia !
“Dogo anachosha kichwa changu ,kaka sipati usingizi , na mbaya zaidi nimetoka kwa babu a……….”
“ safi sana ,mtumie babu amuagamize , kwanini unachelewa ?”
David hakujibu mapema swali hilo ,zaidi ya kukaa kimya kama dakika tatu ,kisha alinyanyua shingo na kumtazama Deus kwa macho ya kukata tamaa,
“Babu kafariki “,
“nini? Na…nani kakwambia wewe ?”
Deus aliuliza kwa mshangao wa hali ya juu ,hakutaka kuyaamini maneno ya David kirahisi hivyo ,kifo cha mzee huyo kilikuwa pigo hata kwake ,
“hebu niambie kinaga ubaga ,”
aliongea huku akiwa katika hali hiyo hiyo , ilibidi David amsimlie kila kitu ,bila kuficha hata tone la mambo yote ,
“ ndiyo hivyo ,hapa nilipo sijielewi ,sina moja wala mbili ,nimechanganyikiwa kaka “
“ sikia kuna rafiki yangu toka Somalia atapambana nae najua lazima atamkamata tu “
“kweli? ,Maana mtu mwenyewe mtambo ,tena mtambo kweli kweli! Nimafia wa kimataifa tena aliyebobea , China nzima inamuogopa ,sijui kama tutamkamata ,hapa mie naona niuze kila kitu nisepe Tanzania hainifai kaka “
“ha ha ha ha ! Kaka maji ukiyavulia nguo shariti uyaoge , cha msingi hapa ni kutafuta njia nyingine si kukimbia ,na tambua kukimbia tatizo si kulitatua ,bali ni kujiongezea matatizo mengine ,umo ndani ya blood deal cha muhimu ni kukaa humo humo , “
“kweli ila kuna mengine yanakuwa magumu Deus “
“nisikilize mie , nimeanza kuona jua kabla yako, Masoud namuaminia sana hashindwi ,kama aliweza kulipua chuo kikuu cha Gharisa huko Kenya na kufanya matukio mengi na makubwa sana duniani , atamshindwa huyo sijui Donaldmac wako huyo? “
Deus aliongea kwa kujiamini kupita maelezo , kwa jinsi alivyomuamini Masoud ,kumkamata MacDonal kilikuwa ni kitendo kidogo sana na chepesi kwake .
“nakutegemea sana kaka “
“ondoa wasiwasi ,tena namtafuta sasa hivi “ ,
papo hapo Deus aliwasha tarakilishi yake ndogo ya menzani na kuanza kumtafuta Masoud ,bahati ilikuwa yake alimkuta akiwa mtandaoni , walianza kuwasiliana , Deus alimuomba afike mara moja Tanzania , kwakuwa masoud alikuwa kipesa zaidi hakukataa wito huo ,na aliahidi siku mbili angekuwa Tanzania .
****
Joan aliendelea kuwa kimya ndani ya basi hilo, bila kuongea na mtu yeyote ,akili yake yote ilikuwa ikiwaza jinsi ya kumpata Poul , China aliifahamu tena sana ,ila hakufahamu wapi alikokuwa Poul ,
“nitafanya nini ?’
Alianza tena kuwaza , muda mwingine alijikuta akiongea kwa sauti ,hali iliyopelekea hata kijana aliyekuwa amekaa pembeni yake kumsikia .
“Dada mambo? ,Naitwa Sharifu , mwanafunzi wa Nanjing Normal University,mwaka wa kwanza , nachukua e……..”
“eeeeeh! Sijakuuliza ,tafadhali “
Joan hakutaka kusikiliza ngojera za kijana huyo , aliyeonekana muongeaji sana , naye kuona hivyo ilibidi atulie na kuendelea kufanya mambo yake ,hadi basi hilo linaingia mjini Beijing mtaa wa Yaojiayuan ,katikati ya jiji hilo ,majira ya saa saba mchana saa za huko ,hakuna aliethubutu kuongea na mwenzake . Alitoka nje ya kituo hicho na kuelekea usawa uliokuwa umepaki kebu.
“ nipeleke Yi” Joan aliongea kwa kichina ,
“ sawa keti “,
safari ya kuelekea mjini Yi ilianza , mita chache kutoka kituoni hapo , Joan alishangaa kuona picha yake ikiwa imebadikwa kila pahali ikiwa na ujumbe wa kumtafuta ,si ukutani ama kwenye miti ,alishtuka sana , mshtuko huo ulimfanya hata dereva nae kushtuka ndipo alipmtazama vyema Joan .
“ unafanana sana na binti anayetafutwa “
“ pacha wangu ,hapa nilipo na elekea huko kutoa matangazo , sijui tutampata ?
“ kweli? Sio wewe ?
“ Pacha wangu , mbona mbishi lakini !“
“ basi yaishe “
Bwana Dong hakutaka kuyaamini maneno ya binti huyo hata kidogo , roho yake ilimweleza kuwa huyo ndiye , hakutaka kupoteza bahati hiyo , ahadi ya zawadi iliyokuwa imetolewa na baba yake , aliitamani sana ,kiasi hicho cha pesa kingesaidia kuyabadiri maisha yake kwa kiasi kikubwa , na hata kazi ya udereva kebu angeuacha ,
“siwezi lazima nimpeleke kituo cha polisi ,siwezi nikawa mjinga kiasi hicho ,yaani napiga teke gunia la pesa ? Ha ha ha ha ! Nitakuwa mjinga tena namba moja duniani ,yawezekana hii ni moja ya bahati yangu “,
Bwana Dong aliwaza peke yake , huku akiwaza kituo kipi angempeleka binti huyo , kwa upande wa Joan alihisi mambo kuanza kubadirika , hakutaka kurudi mikononi mwa wazazi wake akiwa bado hajafanikiwa kumpata Poul , haraka kama mbio za swala alianza kutafuta mbinu za kutoroka kabla ya kufika mjini Yi , akiwa bado hajafanikiwa kupata jawabu sahihi alishangaa , dereva huyo akikata njia ya kuelekea kituo cha polisi , hapo ndipo taa nyekundu iliwaka ndani ya kichwa chake .
“Binti nisubili hapa nakuja “,
Bwana Dong aliongea huku akifungua mlango wa kebu hiyo na kutoka mbio ,
“ sawa “,
Alijibu kwa haraka sana , huku akijitengeneza tengeneza . Dakika tatu bwana Dong alilejea huku akiwa ameambatana na askari watatu , mmoja wa kiume na wengine wa kike , jinsi walivyokuwa wakitembea kwa kasi , huku wakiongea ilionekana walikuwa na hasira sana .
“ Sasa yuko wapi ?”
Askari wa kike ,mnene kupita wote alihoji huku akimtazama ,bwana Dong , aliyekuwa bado haamini kama kweli Joan hakuwemo ndani ya gari hilo dogo ,
“ ongea , acha kutumbua macho , mtu mzima kama wew unadriki kudanganya jeshi la polisi? Unaifahamu kweli sheria ?”
“ kweli nimekuja naye “ ,
alijitetea ,lakini hakuna aliyedriki kumuamini,
“ basi acha ukae kwanza ndani ,nadhani akili yako itakaa sawa ,“
papo hapo askari hao walimkamata bwana Dong na kurudi nae ndani ya kituo cha polisi , akilia kama mtoto mdogo ,kitu kilichomuumiza zaidi ni hali ya mkewe aliyekuwa amelazwa hospitali kwa ajili ya uzazi. Na mbaya zaidi hakuwa na mtu wa kumsaidia zaidi ya yeye mwenyewe.
****
Hakuna kitu kilichowaumiza wazazi hao kama kuondokewa kwa mtoto wao wa pekee , uwepo wa Joan maishani mwao ulitosha kabisa kuyafurahia maisha hayo ya utajiri wa kupindukia,walimpenda sana binti huyo wapekee ,na hawakuwa tayari kumpoteza kwa namna yeyote ile , walikuwa tayari kupoteza pesa zote lakini si kumpoteza Joan . Alikuwa wa thamani sana kupita maelezo ,
“ namhitaji mwanangu Mohammed , wewe ndiye chanzo cha yeye kuondoka “ ,
mama yake Joan alisema huku akilia kilio cha uchungu , mapenzi aliyokuwa nayo kwa binti yake huyo aliyajua mwenyewe ,
“ mama Joan huu si muda wa kulalamikiana ,cha muhimu ni kutafuta njia mbadala ya kumpata , sio kulia “