Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,190
- 34,526
- Thread starter
- #61
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.
SEHEMU YA 24
MacDonald alisema , huku akipiga hatua kumfuata Masoud ,kabla hajamfikia alishangaa kumuona akiruka sarakasi kisha alitua kifuani kwake ,kidogo MacDonald aanguke ,lakini alijiwahi na kunyanyuka , alirudi nyuma kama nusu mita na aliporudi alirudi kama mwendo wa umeme , na kutua kifuani kwa Masoud , moja kwa moja aliangukia mtaloni ,
“ sitaki kukuua kirahisi hivi ,naomba nikuonyeshe kazi kwanza , “
jinsi alivyokuwa na hasira alianza kumshambulia kwa kila aina ya pigo , japo naye alijaribu kujibu lakini alijikuta akizidiwa nguvu .
“ Nielezeni nani aliyewatuma ?
Aliwauliza wote , mara baada ya kuwakusanya sehemu moja , kwa jinsi Omar alivyojiweka ilikuwa ngumu sana mwenzake kumtambua , siri hiyo ilikuwa yake na MacDonald,
“ hakuna mtu “
“ kweli ?”
“ Ndiyo , “
Masoud alijibu kwa nyodo , hakutaka kumnyenyekea mwanaume mwenzake , alikuwa radhi kufa kuliko kuongea , japo alipigwa kipigo cha mbwa lakini hakudhubutu kuongea chochote , hadi anapoteza maisha hakuweza kumtaja David .
“ Sasa tuonaondo kwenda Tanzania mida hii , Hassan naomba ukamtupie ndani ya pipa huyu boya ,pia na yule demu muunganishe humo humo ,usisahau kuja na Poul “
Hassan alitekeleza hayo ,dakika saba alilejea akiwa na Poul aliyekuwa akilia ,kilio cha hasira , hakuja kwanini ,baba yake mdogo alikuwa akiendelea kumfuatilia , wakiwa bado wanajadili namna ya kusafiri walisikia sauti ya nyayo za mtu akitembea wote walishtuka, hakuna aliyeweza kumfahamu mtu huyo.
Joan alihakikisha anafuatilia kila nyendo za wanaume hao , aliamini kufanya vile kungemrahisishia kumpata Poul, japo alijua ni watu hatari , lakini hakutaka kukata tamaa, alikuwa radhi kuyapoteza maisha yake lakini ampate Poul , hata chai hakutaka kunywa tena , alibaki amesimama eneo hilo macho yake akimkangua mmoja baada ya mwingine , muda mwingine alitamani kuongea nao ,lakini alijikuta akipata woga , alipoona wameelekea chumbani kwao aliwafuatilia kwa nyuma ,hadi alipohakikisha anakifahamu chumba cha wanaume hao ,
“ naomba chai “ ,
alipiga simu sehemu husika
“ sawa “ ,
dakika tano mlango wa chumba chake uligongwa , kwa kuwa ulikuwa wazi hakuhangaika kunyanyuka alichofanya ni kumuomba muhudumu huyo kuingia mara moja .
“ sijui unaweza kunisaidia kitu dada ?”
“Kitu! Gani ?’
“ Aaaah ! Kuna wanaume wawili wapo chumba namba 453, naomba wakitoka unijuze “
“ hiyo siyo kazi yetu , siye tupo kwa ajili ya kuwahudumia ninnyi, na siyo kuchunga ka…”
“ dada usipende kuongea sana , kwani bei gani ?”
Joan aliongea, huku akiwa amemtazama machoni msichana huyo, aliyekuwa amestajabishwa na maneno ya msichana huyo mdogo , hakujua ujasiri huo kaliutoa wapi, kiumri kalikuwa kadogo sana , hata hakakustahili kuwa kaongeaji kiasi hicho ,
“ unaweza ukanipa kiasi gani labda ?”
Aliongea kwa nyodo za hali ya juu ,msichana huyo wa kichina , macho yake tu yaliashiria umaringo wa hali ya juu ,lakini hilo Joan hakulijali ,alichojali yeye ni kufanyiwa kazi yake , alijifunika vizuri sura yake ,kisha alichuku kipochi chake kidogo na kufungua , alitao idadi nyingi za noti na kuzitupia miguuni mwa msichana huyo ,aliyeyatoa macho yake mithili ya mwizi aliyekamatwa ,kwa picha ya haraka –haraka zilikuwa ni pesa nyingi sana,
“ okay nakuhakikishia ushindi “
“ fanya kweli , “
“poa “.
Alitoka akiwa haamini ,kama kitoto kile kingeweza kuwa na pesa zote hizo , hata alipozihesabu ilikuwa mishara yake ya miezi mitatu , na ili kuzifanyia kazi pesa hizo alikuwa makini kupita maelezo , usiku wa saa moja alimpatia taarifa ya kuondoka kwa wanaume hao ndani ya hoteli hiyo ,alitoka haraka sana na kuanza kuwafuatilia kila walikopita alikuwa nyuma yao , hadi wanaikaribia ngome ya MacDonald . Alitembea kwa tahadhali sana huku akiwa amejificha ficha , hakutaka kukurupuka sana alichofanya ni kutulia kwanza nje ,sehemu aliyoiona inamfaa zaidi , akiwa bado amesimama eneo hilo ghafla walitokea wanaume wawili mmoja alifanania na baba yake ,japo kulikuwa na giza ,lakini aliweza kumtambu vyema , alihisi moyo kumpasuka, alitembea taratibu kuelekea usawa uliokuwa na giza zaidi ,akawa anasikiliza kile kilichokuwa kikiendelea .
“ kweli umemuona akielekea huku?”Alimuuliza kwa lugha ya kichina ,
“ ndiyo , tena alikuwa anawafuatilia wanaume wawili “
“ unauhakika na ulisemalo ?”
“ Mjomba mie ndiye Shayyu , sikosei kazi yangu ,nimezaliwa China ,na nimekulia China, kila kitu nakifanya kwa akili , binti yako yuko hapa hapa, wewe nitoe changu ,handasi zinazidi “
, kijana aliyekuwa amejitolea kumsaidia baba yake Joan toka alipoingia ndani ya mji huo , mara nyingi kazi zake alizifanyia ndani ya hoteli , kwani aliamini humo ndimo watu hujificha , japo hakuwa na uhakika na binti huyo alipomuona kwa mara ya kwanza akitoka ndani ya hoteli , lakini alijiaminisha kuwa ndiye! Kweli alipatia, Mohammed hakuyaamini maneno ya kijana huyo ,mara moja kutokana na muonekano wake wa uteja teja ,lakini alijikuta akiyaamini japo kwa asilimia ndogo sana , ilibidi amtoe kiasi kidogo cha pesa na kuahidi kumuongeza kiasi kilichobaki mara baada ya kufanikisha zoezi yake .
Alianza kutembea taratibu kuingia ndani ya ngome hiyo ,iliyokuwa ikiyatisha macho yake , hatua chache aliuona mwili wa Run Snake ukiwa umetapakaa damu ,hapo ndipo alipoamua kuwa makini , alitoa sirasha yake ndani ya suruali na kuishika mkononi , jinsi alivyokuwa akinyanta ilionyesha alipitia mazoezi flaani ,baada ya kutembea umbali wa hatua kadhaa alisikia mabishano , kidogo alitulia kusikliza ,akiwa bado haja kaa vizuri masikio yake alipokea milio mitatu ya risasi , kisha kikasikika kilio cha mtu na baadaye kimya kikatawala , mara moja hakufahamu kikilichokuwa kiendelea ,
“ Kweli mwanangu yumo humu ?”
Alijiuliza peke yake , akiwa bado amesimama eneo hilo kwa tahadhali ya hali ya juu , dakiaka tano alisikia tena mazungumzo ,hapo ndipo alipoamu kutembea kwa kuvuruta miguu yake , aliona afanye hivyo ili kuwapa nafasi watu hao kumsikia yeye , ghafla taa zilizimwa ,alishituka sana ,macho yake yakapokelewa na giza tororo , akiwa bado hajapata jawabu la mazingira hayo ,kwa mbali aliona kivuli mfano wa mtu kikija eneo hilo , hakutaka kukimbia alichokifanya ni kupiga hatua kukifuata .
“ mikono juu “
Alitoa amri ambayo haikutekelezwa na kiumbe hicho ,zaidi kilizidi kusogea eneo alilokuwa amesimama,
“ukileta ubishi naku,,,,,,,,,,,,,”
“nawe nyosha mikono juu “
Mohammed alijikuta akikatishwa sentensi yake ,na pande la mtu , mara moja hakuweza kumfahamu mtu huyo ila baada ya taa kuwaka alijikuta akitetemeka mwili mzima , hakuamini kama siku hiyo angeweza kuangukia mikononi mwa MacDonald , alimfahamu toka zamani , hakuweza kufanya chochote zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa ,
“ unatafuta nini hapa ?”
“ Na…namf…uata mwanagu “
“ mwanao?”
MacDonald aliuliza kwa mshangao , hakujua ni mtoto yupi aliyekuwa anatafutwa ,wakati alikuwa na Poul tu ndani ya nyumba hiyo ,
“ nimetokea Iran … nimeambiwa mwanangu yumo humu tafadhali nipe mwanagu “.
Alizidi kujitete ,huku mikono yake akiwa ameikunyanta kwa mbele ,kwa jinsi alivyoonekana, usingeweza kuamini kama alikuwa mtu mkubwa, na aliye heshimika ndani na nje ya Iran ,
“ anaitwa nani ?”
“Joannnnnnn!”
Sauti nyororo na yenye utoto ndani yake ilipenya vyema ndani ya ngoma za masikio ya watu hao , wote walibaki wakistajabu , msichana aliyekuwa amejifunika mwili mzima alisimama mbele yao .
“ Joan mwanagu um……….”
“kimya !Unatafuta nini hapa binti ?”
MacDonald aliuliza huku akimfuata msichana huyo aliyekuwa umbali kidogo , Joan aliamua kujificha mara baada ya kumuona MacDonald akimfuata baba yake , ambaye alikuwa amempa mgongo mwanaume huyo . Ila baada ya kumuona baba yake akitaka kuingia matatizo aliamua kujitokeza angalau aweze kujaribu kuyaokoa maisha ya mzee wake .
“Hassan kamata hao na ufunge kamba ,wapeleke gerezani “,
alitoa amri na ilitekelezwa mara moja , lakini wakiwa wanaelekea huku Poul aliweza kumuona Joan ,
“Joannnn!!!!
”Aliita kwa sauti ya juu sana iliyopelekea kila mmoja wao kumshangaa , hakuishia kuita tu bali alianza kupiga hatua ya kumfuata eneo alilokuwa amesimama
“ unamfahamu huyu mwanangu ?”
Mac Donald alimuuliza Poul mara baada ya kufika eneo hilo ,
“ ndiyo , ni rafikiyangu sana ,tafadhali naomba umuachie nipo chini ya miguu yako “,
alizungumza ,huku akipiga magoti ,uso wake tu uliashilia ukweli wa hali ya juu , japo aliufahamu uadui kati yake na baba wa binti huyo, lakini hakujali ,alichojali ni kumtetea Joan ,tayari alishamngundua MacDonald hakuwa Mtu wa msamaha kwa kiumbe yeyeto anayedriki kuivaimia ngome yake .
Upande wa Mohammed alikuwa kimya kabisa , hakujua kama angeweza kutoka salama ndani ya ngome hiyo , yeye na MacDonald walikuwa maadui wa muda mrefu sana ,toka enzi za kutekwa kwa Poul miaka kadhaa iliyopita , na mara baada ya kumgundua mtu huyo aliamua kutomsaidia David zaidi ya kutoa pesa tu ! Alifanya hivyo kwa sababu David alikuwa akimuuzia madawa ya kulevya nchini kwake .
“ okay sasa unataka nikusaidieje ?”
“ nakuomba usimuue muache aende salama ,tambua tuna safari kwa leo usiku ?
“ haina shida ,ila hawataondoka hapa hadi siye tufike Tanzania “
kusikia Tanzania Mohammed alichanganyikiwa tayari alishangundua kipi kinaenda kutokea , alijihapiza kama atapata mwanya kidogo atoe taarifa kwa David .
“ Tunaenda sote Poul “
“hapana , huwezi ukaondoka kwenda huko , unatakiwa urudi nyumbani haraka iwezekanavyo “
“ sirudi , nipo tayari kuyapoteza maisha yangu ,kuliko kurudi mikononi mwenu , hamfai kabisa ,nishangundua ub….”
“shiiiiii!”
Joan alikatizwa na Poul ,hakutaka mzozano , alichotaka yeye ni kwenda Tanzania mara moja , hasira aliyokuwa nayo dhidi ya David aliifahamu mwenyewe , alitamani kumuua kwa mkono wake , haraka iwezekanvyo . MacDonald hakutaka kupoteza muda alimchukua Mohammed na kumfungia ndani ya chumba, Joan alimpa nafasi ya kuongea na Poul , kila mtu alitoa machozi ya furaha , Poul alimshukuru sana Joan kwa moyo wake huo wa kujitolea kwa ajili yake , japo hakutoa pesa ,ama kitu chochote ,lakini kitendo cha yeye kusafiri hadi China ilikuwa ni moja ya upendo wa hali ya juu sana .
****