Blood deal

Blood deal

Uchu na uroho wa mali ni mbaya sana...

Na dhambi ya kuua ni mbaya sana... ukianza kuua kila utakayekutana nae utamuona mbaya wako au anajua maovu yako, utaendelea kuua hutokaa kuishi kwa amani...

Ndicho kinachomtoea David...


Cc: mahondaw
Hahaha tusubiri tuone ntapost keshooo inshallah
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 7

"khoook!Khoook!"
Sauti ya kugongwa kwa dirisha la gari lake ndio iliyomshtua David, hakuwa na haraka sana maana alijua ni Salama tu ,kweli mawazo yake hayakukosea alimfungulia mlango.
"niambie mme wa mie "
Salama alizungumza huku akimbusu David mdomo, nae hakuwa nyuma alimpokea kwa mikono miwili
"leo kula pesa yangu kadri unavyojua, jichetue ujuavyo linga mtoto wa kike" David alizungumza hayo baada ya wote kuachiana, hakutaka kukaa sana ndani ya gari,walishuka na kuingia ndani ya Club hiyo, ambayo ni maarufu na ni pendwa kwa wakazi wa mji wa mwanza.
Saa kumi na moja alfajili ndipo walipotoka ndani ya club hiyo, David alimpitisha Salama nyumbani kwao kisha alielekea kwake!,Kwa kuwa ilikuwa jumapili, hakuwa na haja ya kuamka mapema sana, alilala hadi saa sita mchana, kisha alielekea nyumbani kwa marehemu kaka yake, kichwani akiwa na lengo la kupata picha ya Poul kwa njia yeyote.
"waaooooo Baba shikamooo "
"mar -haba hujambo mzee wetu "
David alijibu salamu hiyo huku akimnyanyua kutoka chini na kumpakata, kisha alianza kuelekea ndani.
"Safi sana umekwisha! " Alijikuta akiwaza maneno hayo huku macho yake yakimtazama mtoto Poul aliekuwa amejawa na tabasamu usoni mwake, laiti angefahamu huyo alikuwa adui yake namba moja duniani, asigedhubutu kumsogelea,
"Mama yuko wapi? "
"Kalala "
"aaaah!, Kamwambie nimekuja "
"sawa "
Poul aliondoka eneo hilo akikimbia kuelekea ndani, huku nyuma, David akimtazama kwa uchu kana kwamba alikuwa akitamani kumtafuna mbichi mbichi!. Akiwa katika lundo la mawazo Janiphar shemeji yake alitokea sebuleni hapo.
"nakuona mke mwema "
"shemu huuishiwi na maneno " Janiphar aliongea huku akikaa na kumpakata mwanae.
"Unajua nataka nikuridhi, hahahaha! "
David alichomeka utani hali iliyopelekea wote kucheka kwa furaha, ili asijulikane adhima yake, alishinda hapo siku nzima huku tayari akiwa amefanikiwa kuchukua picha ya Poul, kupitia simu yake ya mkononi.Safari yake ilianzia studio iliyopo karibu kabisa na sheli ya moili raundi abauti ya mwalimu Nyerere, mkakabala na benki ya stabick.
"Babu kila kitu kipo tayari, na nimeituma kabisa ipokee kesho katika basi la Zuberi "
David aliongea baada ya kukamilisha zoezi la uchapishaji wa picha hiyo, kisha alielekea hofisi za mabasi yaliyokuwa yakienda kigoma, mtaa wa natta barabara ya Igoma.
"Sawa babu kesho kutwa utaona jibu, si tayari na majina yake umeyaandika kama nilivyokueleza? "
"Ndio! "
"Tegemea ushindi, mjukuu wangu "
"nitafurahi sana babu! "
"Lazima ufurahi "
"hahahaha! "
David alimalizia kwa cheko, kubwa na lenye ushindi mkubwa ndani yake, siku hiyo hakutaka kwenda kokote, kutokana na uchovu wa jana aliamua kwenda nyumbani kwake moja kwa moja bila kumpitia msichana yeyote.
******
"Mama leo siendi shule "
Kwanini Poul? "
Mama yake alimuuliza huku akiendelea kunyosha nguo za shule za mwanae, asubuhi ya jumanne.
"sitaki tu nimemkubuka Baba, harafu hutaki kuniambia baba yuko wapi? "
"Puuuuh!,
Mama yake alishusha pumzi ndefu, kisha aliichomoa pasi kwenye soketi na kumsogelea mtoto wake ,aliekuwa amelala chali macho yakimtazama Mama yake.
"Nikweli mwanangu, naomba uende shule ukirudi tu nitakuelezea kuhusu Baba atarudi lini, sawa Baba? "
Japo Janiphar alizungumza maneno hayo, huku akitoa tabasamu, tabasamu hilo lilikuwa la bandia tu , moyoni aliumia alihisi moyo ukivuja damu, lakini hakutakiwa kumuonesha picha hiyo mwanae.
"Kweli Mama na utanipeleka? "
"Ndio, ni.... nit.. akupe.... leka "
Alijikuta akishindwa kuongea vizuri, baada ya kukabwa na kitu kizito kooni.
"Naenda kuoga mwenyewe leo "
Poul alizungumza huku akitupa pembeni shuka, alivua pensi na kujifunga taulo la Baba yake , vitendo vyote hivyo mama yake alikuwa akivitazama tu, ila kilichomuhuzunisha zaidi ni kitendo cha mwanae kujifunga taulo la mmewe, chozi jembamba lilianza kutiririka na kulowanisha kope zake.
"Masomo mema baba "
"haya Mama, nikirudi unaniambia sawa? "
Mtoto Poul aliongea, maneno hayo huku akimbusu mama yake mkononi, kisha alipanda ndani ya school bus, safari ya kuelekea Alliance international school ilianza. Hadi bus hilo linapotea machoni mwake Janiphar alikuwa bado ameganda eneo hilo akiyatafakari maneno ya mwanae!, Taratibu alianza kuondoka eneo hilo kwa unyonge usioelezekea, hofu kubwa ikaanza kuushambulia moyo wake, mawazo mabaya kwa mwanae yakaanza kupita ndani ya kichwa chake.
"Kunanini? "
"Kwani vipi Mama? "
Janiphar alijikuta akishtuka ,baada ya kuulizwa swali hilo na Mama mkwe wake ambaye alikuwa bado nyumbani hapo pamoja na baadhi ya ndugu wengine. Alibaki ameduwaa asijue cha kuongea, hata hakujua amefikaje sebuleni hapo, alichokuwa akikikumbuka ni uwepo wa yeye barabarani, sasa ndani humo ameingiaje?, nani aliemfungulia geti?.
Kutokana na mawazo mengi kumzidia alijikuta akitembea bila kujua.
"Tuambie mama tatizo nini? "
Mama mkwe aliendelea kumdadisi baada ya kumuona amebadirika ghafla,
"hata sijui nasikia moyo ukiniuma sana "
"Pole sana mama punguza mawazo mwanangu "
Mkwe wake alisema hayo huku akimkalisha chini.
"Griiiiiii! Griii"
Mlio wa simu ya Janiphar ndio uliowashtua wote , haraka bila kuchelewa aliichukua kutoka juu ya meza, alimwangalia mpigaji, lahaullaa! Alihisi moyo ukichomoka ndani ya kifua chake, baada ya kukuta jina la dereva wa poul, hakuweza kuipokea simu hiyo kutokana na mikono kutetemeka, moyo ukienda mbio, taarifa za habari mbaya zilianza kujitengeneza ndani ya hakiri yake, iliita hadi ilikatika yenyewe.
"Mama mbona hujapokea si... ?"
Hakumalizia , mara simu iliita tena, mama mkwe ilibidi aichukue na kubofya kitufe cha kupokelea, kisha aliiweka sikioni.
"Halo! "
"Kuna tatizo limeji.... "
Hakuweza kumalizia alikatishwa
"nini? "
"Ndio, tumepata ajari hapa Natta, mtoto wenu ame.... "
"mamamamamamama weeeee Poul mwanang... "
Mama mkwe alishindwa hata kusikiliza vizuri, alijikuta akilia kwa sauti ya juu, hali hiyo ilipelekea kila mtu kuacha kile alichokuwa akikifanya, kelele za vilio zianza kusikika ndani ya nyumba hiyo, kila mtu alijua Poul amefariki, Mama yake tayari alikuwa ameshazimia ,alijuta kumlazimisha mwanae kwenda shule, laiti angemsikiliza yote hayo yasingetokea.
Ilibidi dereva wa familia hiyo aliekuwa akifahamika kwa jina la Dominic, atoke nje akiwa na simu ya boss wake, ndani hapakufa tena, alitafuta namba za Dereva huyo katika kitabu cha namba, huku akitetemeka alitafuta jina hilo na kupiga kabla ya kuweka sikioni.
"Niambie mwanangu Poul amekufa?"
Domi aliuliza huku naye akilengwa lengwa na machozi, miguu ikikosa nguvu,
"hajafa ila yupo hospitali ya Aghakhan hali yake mbaya sana, katika wote yeye ndie alieumia sana"
Dereva aliongea huku akitetemeka kupita maelezo,
"daaaah! Ilikuwaje mwanangu? "
"Hata sijui lori lilitokea wapi?, nimeingia freshi barabara ya Igoma, ghafla lori lilitoea ubavuni na kunigonga kwa nyuma hali iliyopelekea bus letu kuanguka, huku Poul akikandamizwa na kiti kifuani ."
Alitoa Maelezo hayo kisha alikata simu.
"Jamani Poul hajafa yuko Aghakhan, twendeni "
Hakuna alietaka kubaki nyumbani hapo, kwa masada wa ndugu Janiphar alisaidiwa kutembea, kuelekea kule gari lilikuwa limepakiwa.
Kweli walifanikiwa kumkuta Poul akiwa katika hali mbaya sana, mwili wake karibia wote ulijaa madonda, jinsi alivyokuwa akitisha haikuwa rahisi, kuamini kama alikuwa mzima,
Ilibidi wakae kidogo kusubili majibu ya daktari, nusu saa waliweza kuonana nae, aliwapa matumaini ya mwanao kupona japo alikuwa ameumia sana kifuani , kisha wengine waliondoka wakimuacha Mama yake na Bibi yake kumuangalia.
*****
Kazi ya kutengeneza ajari ya kiini macho haikuwa ngumu sana kwa mzee Songoro, baada ya kuipokea picha hiyo majira ya saa mbili usiku, hakutaka kulala , aliichukua na kuitumbukiza ndani ya dawa nyeusi, huku akizunguka zunguka eneo hilo, mkononi alishika usinga mweusi, dakika tano aliitoka na kuiweka ndani ya ungo uliokuwa umejaa kila aina ya dawa, alileta kioo kilichokuwa kimevikwa kitambaa chekundu na cheupe nacho alikitumbukiza ndani ya ungo huo, alichukua dawa iliyokuwa na asili ya kimiminika, kidogo alimimina ndani ya kiganja chake na kukipakaza kioo hicho kwa juu huku chini yake akiwa amekandamiza picha ya Poul, vitendo hivyo viliambatana na maneno aliyokuwa akiyatamka kumuita Poul.
Dakika saba, sura ya mtoto Poul ilitokea juu ya uso wa kioo, hapo hapo aliachia tabasamu, alichukua dawa nyeupe na kuipaka sura hiyo, dawa hiyo ilimsaidia kuyatambua majina yote ya koo mbili ,kwa Mama na kwa baba, akiwa katika zoezi hilo ghafla yalitokea majina yote, hivyo akawa ameimchoma kisu kikali picha ya Poul sehemu ya kifua.
Baada ya zoezi hilo alichukua, ile picha na kuifunga ndani ya karatasi kisha aliweka tena, juu ya kioo na kuanza kuongea maneno yake, mara juu ya kioo ilianza kuonekana school bus ya akina Poul, hapo hapo alianza kutengeza ajari ,kwanza alitengeneza eneo sahihi la ajari itakapotokea, akimpiga upofu dereva, baadae alichomeka lori feki litakalo ingonga gari la shule. Hakutaka kulala aliondoka kigoma usiku huo hadi jijini mwanza akiwa ndani ya umbo la bundi, safari yake ilianzia Natta alipopawagia, kisha alienda kuliwangia school bus na hata kiti alichota mtoto Poul kukaa alikiwangia, akiuchochochea moyo wake kukaa pale pale.
"nimemaliza subili matokea kesho! "
"Kweli mzee? "
David aliuliza kwa shauku ya hali ya juu, hakuamini kama kazi hiyo ingekuwa rahisi kiasi hicho . Furaha ilizidi kuongezeka kadri muda ulivyokuwa ukiyoyoma, hakuweza kupata usingizi mapema hadi jongoo wa kwanza kuwika alikuwa macho , saa kumi na nusu ndipo alipopitiwa na usingizi, alikuja kushituka jua likiwa limechomoza.
"acha nimpigie Baba simu, najua ataniambia tu "aliwaza hayo huku akiiangalia saa iliyokuwa ikionesha saa mbili na nusu asubuhi.
"Shikamo Baba "
David alisalimia baada ya simu kupokelewa, sauti yake tu ilionesha hali mbaya
"vipi mzee mbona unaongea kinyonge hivyo? "
David aliuliza swali hilo ma kusudi ila tayari alikuwa ameshaanza kuhisi jambo.
"Poul amepata ajali hali yake mbaya sana, kaumia kifuani ya... "
Mzee huyo alishindwa kuongea vizuri, maumivu ya kuondokewa kwa mwanae yalikuwa bado yakiisumbua hakiri yake, leo tena mjukuu wa pekee alieridhi jina lake nae amepata tatizo kubwa, na linaweza kupelekea kupoteza maisha yake! Kweli alikuwa na haki ya kulia.
"Pole sana Baba je yuko wapi kwa sasa?".
Aliuliza David huku akiwa amechanganyikiwa, hakupendezwa na taarifa hizo, alichotaka yeye ni kusikia taarifa ya kifo si majeruhi.
"nitaenda kuongea na daktari "
Aliwaza hayo huku akinyanyuka kitandani.

David atakuja kufa kifo kibaya sana...

Dhambi anazojibebesha ni kubwa sana...

Kashaua mtoto wa kaka yake tayari kwa ulozi...

Cc: mahondaw
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 9.

Ilikotoka......

Mpango wa hatari Kati ya Dk. Eddyson na David umesukwa tena kwa lengo la kmuangamiza Janiphar kwa kumuchoma damu yenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi , kabla ya kutoka ndani ya Aghakhan, huku poul nae akiwa bado ndani ya hati hati ya kuchomwa sindano ya sumu, je nini kitatokea?.

SONGA NAYO.

DK Eddyson alianza kutembea taratibu kuingia hofisini kwake, mkononi alishika koti lake la kazi, alionekana mtu mwenye mawazo sana, kweli hakiri yake ilikuwa imevurugwa kupita maelezo, nafsi mbili zilizidi kushindana , moja ikipinga shauri hilo, ila nyingine ilizidi kumtia nguvu, ikimtamanisha maisha mazuri.
"puuuuuuuuuh! ".
Alishusha pumzi ndefu, akiwa ameegemeza mikono yake juu ya meza, akiwa amesimama, hakujua achague lipi kati ya kutekeleza ama kukataa.
"my Jesus (Yesu wangu), lakini kanuni na taratibu za udktari hazi r..... " alishindwa kuyaendeleza mawazo yake, baada ya kukatishwa na ujumbe mfupi uliongia katika simu yake. Ukitoa sauti ya juu sana.
Haraka sana aliitoa simu hiyo ndani ya mfuko wa shati, alienda moja kwa moja upande wa meseji, ili kujua ujumbe huo ulitoka wapi,
"mmmmmh "aliguna baada ya kuona Meseji hiyo, akiwa haamini hata kidogo, kitendo cha kupokea laki tisa kutoka kwa David, kama moja ya malipo kilimtisha na kumshangaza sana, alibaki ameduwaa huku akiwa ameitumbulia macho simu yake.
"duuu! Mtihani kweli, huu je nimchome? Aaah! Potelea mbali dhambi ngapi nimefanya?, pesa kwanza maisha yangu "
Dk. Eddyson alijikuta akidhamiria kufanya kazi aliyotumwa na David, na kilichomchanganya zaidi ni zile laki tisa, tayari zilikuwa zimeshapata kazi, jioni hiyo hiyo alipanga kupita bar kidogo, kama ishara ya kujipongeza! Kwa kazi ndogo iliyokuwa mbele.
******
Baada ya David kumrudisha Dk. Eddyson kazini kwake, yeye alielekea moja kwa moja Nyakato National majanini, huko kulikuwa na moja ya nyumba aliyokuwa ameijenga marehemu kaka yake, bila kumshirikisha mkewe zaidi ya kumshirikisha mdogo wake David,hata hati za nyumba alikuwa nazo David. Kama ujuavyo wanaume huwa hawana utaratibu wa kuwashirikisha wake zao baadhi ya mali, wakiamini mwanamke hatakiwi kutambua kila kitu anachokifanya mwanaume, hivyo hata Emanuel hakuwahi kumshirikisha mkewe baadhi ya mali, ikiwemo nyumba hiyo, iliyokuwa bado haijakamilika vyema,
"nitampa hii hii itamtosha ,ila akinizingua namuondoa duniani! "
David aliongea huku akiuma meno kwa hasira, safari yake iliishia hapo alishuka na kuikangua ,baada ya zoezi hilo aliondoka akipitia ATM alikotoa kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili, laki tisa alimrushia ,Dk. Eddyson na zilizobaki alimtumia shemeji yake.Akimpumbaza.
"Umeiona picha ya nyumba? "
"Ndio!, Tena nzuri sana, tajarajia ushindi ndani ya siku tano, ama tatu"
"mimi nimeshamaliza ,kazi imebaki kwako, unatakiwa ufanye sio ombi tena, tambua kuanzia sasa upo ndani ya Blood deal, nikimanisha mpango wa damu, maana kile unachokwenda kukifanya lazima damu imwagike ndo mpango wako ufanikishe, kuwa makini, nakupenda sana "
David aliongea kwa msistizo sana, akimanisha alichokizungumza, daima hakuwa mtu wa kukata tamaa, ama kughairi, hakuwa na tabia hiyo , lazima afanye alichokiamu hata kama kingehatarisha maisha yake, ilikuwa ni lazima. Alikata simu na kuuma kidole gumba cha mkono, huku akiwaza kupita maelezo, dakika tano alipata wazo la kumtafuta Deus rafiki yake mkubwa.
"Acha nimtafute Deus "
Hapo hapo alichukua simu yake na kulitafuta jina la Deus, dakika moja alilipata , alibonyeza kitufe cha kijani kisha aliweka sikioni, sekunde mbili simu ilianza kuita .
"Dogo Safari hii umeamua sio masihara ".
Deus aliongea baada ya kupokea simu
"hasira niliyonayo hata nikikupunguzia, huna pa kuiweka kaka "
"safi sana, huo ndio uanaume, mwanaume lazima awe shujaa , mwenye kujitoa tena kwa viungo vyote, na ikiwezekana hata kupoteza maisha yake, babu alinieleza kila kitu "
Eeeeh! Kaka lazima nimalizie ,kama damu tayari nimeshamwanga, na mpango utimie "
"hahahahaha! "
Deus alicheka kwa furaha sana, hali iliyopelekea hata David kuunganisha cheko hilo. Kisha alielekea hofisini kwake bila kujua tena habari za Poul zaidi ya kusikia taarifa za kifo kutoka hospitali hiyo , muda mwingine alidriki hata kusali akimuombea mtoto Poul afe.
******
Siku tano baada ya ajari, Poul aliruhusiwa kutoka ndani ya chumba cha wagonjwa mahuti huti, baada ya hali yake kutengamana, kwa asilimia sabini lakini alikuwa bado akilalamika kifua kilikuwa bado kikimsumbua sana, kwa upande wa Dk. Atanasi alikuwa makini sana kuhakikisha Poul anakuwa nafu kama si kupona kabisa ndani ya muda mfupi tu! Kila baada ya masaa matatu ilikuwa lazima apite kitandani hapo, ukaribu huo na umakini huo ndio uliochangia mtoto Poul kupata nafu kwa asilimia kubwa.
"Mama "Poul alimuita Mama yake kwa sauti ya chini yenye maumivu ndani yake ,dakika moja Janiphar alibaki kimya bila kuitika akimtazama mwanae, hakuamini kama kijana wake angeweza kutoa kauri, picha ya ufu aliyokuwa nayo ndani ya chumba cha wagonjwa mahuti huti ilikuwa bado ikimsumbua.
"Abee Baba "
Alitika kwa unyonge huku akimtazama machoni, hakika alikuwa na huruma sana na maumivu makubwa ndani ya mtima wake , muda mwingine alitamani mmewe angekuepo.
"niambie kuhusu baba ,siku ile ulikataa ndo maana niliumia "
"hapana, sikukataa mwanangu "
"haya Mama , baba yuko wapi? "
Poul aliuliza huku akimtazama Mama yake usoni, macho yenye usiriazi na kile alichokiuliza, hakujali maumivu aliyokuwa akiyapata pindi alipozungumza, yeye alihitaji kufahamu wapi Baba aliko, tayari moyo na masikio yake vilichoka kusikia taarifa za Baba kuja kesho.
"Pona kwanza mwanangu "
"hapana mama ,niambie natakaaa"
Poul alizungumza huku akianza kulia, Mama yake hakutaka hali hiyo itokee, kulia huko kungezidi kuongeza maumivu ndani ya kifua chake, ilibidi ambembeleze akimuahidi kumueleza ukweli wote, japo aliamini kufanya vile kungezidi kumuumiza hata yeye mwenyewe.
"Baba hayupo mwanangu "alianza Kuongea, bila kumtazama mwanae, maumivu aliyokuwa akiyapata pindi asimuliapo habari hiyo ilikuwa siri yake na mungu wake
"atakuja lini? "
"Haji mwanangu "
"kwanini Mama, inamana hatupendi tena? Kumbe Baba mbaya akinidanganya ataniletea baskeli ha... "
"shiiii! Sio hivyo Poul "
"kumbe? "
"Baba amefariki mwanangu "
"amefariki? Ndo kwenda wapi? "
Poul alikuwa na maswali kama mtu mzima, hata mama yake alimshangaa kupita maelezo , umri wake haukuendana na maswali hayo.
"kufariki ni kuondoka duniani, hatakuja tena kutuona, hawezi kuja mwanangu, huna Baba tena, mpende Baba mdogo David, huyo ndie aliebaki pamoja na anti Agnesi, Babu na Bibi, sawa mwanangu "ilibidi Janiphar ajikaze .
"Amefarikiiiiii, haji aaaaaah! "
Poul alishindwa kuvumila alianza kulia sana, neno kutomuona Baba yake tena lilimuumiza sana, haikuwa kazi rahisi kumtuliza, alipotulia alipitikiza kusinzia kabisa.
Janiphar alinyanyuka na kuelekea bafuni, alioga na kurejea, alijilaza pembeni ya mwanae aliekuwa bado amesinzia, akiwa ndani ya mawazo nae alijikuta akipitiwa usingizi, hiyo ndo ikawa nafasi ya Dk. Eddyson kutekele kazi yake, aliyokuwa ameipanga kwa muda mrefu, kila kitu kilikuwa tayari, damu yenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilikuwa imeshaandaliwa siku moja nyuma, tena ikiwa ndani ya chupa. Siku hiyo hakutoka hospitalini hapo, mara baada ya kugundua uwepo wa Poul ndani ya vyumba vya kawaida , kila hatu iliyokuwa ikitendeka alihakikisha anaifatilia.
Baada ya kumuona Janiphar amepitiwa na usingizi alinyanyuka haraka sana akiwa na bomba mbili zenye damu hiyo pamoja na kichupa kidogo kilichokuwa na dawa ya usingizi, ndani ya koti lake, alitazama huku na huko kuhakikisha usalama wake, alipogundua hakuna akiemuona alinyata kuingia ndani ya chumba cha Poul na Mama yake ,taratibu akiurudisha mlango, kisha akitoa kichupa cha dawa ya usingizi , aliitikisa na alipohakikisha imekaa sawa alimpulizia Janiphar kidogo sana, maana ilikuwa Kali sana kisha alitoa bomba la damu iliyokuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kumchoma nayo Janiphar kupitia ndani ya mshipa mkubwa wa mkono wake wa kushoto , huku akiwa amefumba macho, kiwa anamalizia kuchomoa sindano ya pili mara mlango ulifunguliwa, alihisi haja kubwa ikizichafua nguo zake, mwili wote ulianza kutetemeka asijue la kufanya.

Dk. Eddyson hakujua afanye kipi? Moja kwa moja alijua ni Dk. Atanasi, haraka bila kuchelewa alizirushia bomba za sindano ndani kabisa ya shati lake , lililokuwa limechomekwa ndani ya suruali, kisha likafungwa kwa mkanda, kwa muonekano huo isingekuwa rahisi mtu yeyote kufahamu kilichokuwa kikiendelea.
"Khook! Khoook! ".
Alikohoa kikoozi kikavu, ili kumshitua mtu aliekuwa bado akiusukuma mlango
"vipi Mama? "
Dk. Eddyson aliuliza, mara baada kuufungua na kukutana macho kwa macho na mama mkwe wa Janiphar, kiasi alihisi, mwili wake ukipoa, mapigo ya moyo yaliyokuwa yanaenda kwa kasi, sasa yalipungua, picha ya kufumaniwa iliondoka hakirini mwake.
"Aaaah!, Nilikuja kumuaga mie nataka kuondoka! "
"OK, sawa ila kalala, sijui utafanyanje? "Dk Eddyson alizungumza huku macho yake makubwa kiasi , yalikuwa makini kumtazama mwanamke huyo, kujua kama aligundua ama la.
"Basi nisimchoshe, kesho nayo siku nitakuja kuwatazama "
"haya mama ".
Kwa pamoja walitoka ndani ya chumba hicho, wakimuacha Poul na Mama yake wakiwa ndani ya usingizi,
"haloo boss mambo tayari"
"kweli? "
"Ndio sasa nikutanie, keshaisha huyo, na nzuri zaidi nimemchoma chupa moja kabisa "
Dk. Eddyson aliongea huku akicheka cheka, furaha aliyokuwa nayo, ndani ya moyo wake aliifahamu mwenyewe.
"daaah!, safi sana, cha muhimu tunza siri hiyo milele "
"kutunza siri, ni moja ya sheria ya udaktari, kwa hilo ondoa wazo "
"basi sawa, naomba nikutakie usiku mwema, kesho tukutane Nyakato nikumalize kabisa "
"haya ".
Dk. Eddyson alikata simu na kubaki amesimama, moyo wake ulijaa furaha, hakuamini kama zoezi hilo lingekamilika salama, hakutaka tena kukaa neno hilo ,alianza kujiandaa kuelekea kwake, moyoni akiwa na amani sasa. Usiku mzima ulikuwa wa furuha kupita maelezo, hadi kunapambazukua alikuwa na tabasamu tu, hali hiyo ilimshangaza hata mke wake, lakini hakuweza kumuuliza .

Nahisi Dk. Eddyson kipindi anarudisha sindano na chupa haraka haraka kwenye shati lake, nae atakua amechomwa na hizo sindano zenye virusi vya ukimwi...

Natamani sana iwe hivyo...

Jenipher mke wa marehemu Emanuel ndiyo kashaambukizwa ukimwi kwa kuchomwa sindano makusudi... inasikitisha sana...


Cc: mahondaw
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 10.

Dk. Eddyson alikata simu na kubaki amesimama, moyo wake ulijaa furaha, hakuamini kama zoezi hilo lingekamilika salama, hakutaka tena kukaa neno hilo ,alianza kujiandaa kuelekea kwake, moyoni akiwa na amani sasa. Usiku mzima ulikuwa wa furuha kupita maelezo, hadi kunapambazukua alikuwa na tabasamu tu, hali hiyo ilimshangaza hata mke wake, lakini hakuweza kumuuliza .
Safari ya kwanza, asubuhi hiyo ilikuwa ni kuelekea Nyakato national majanini, huko alikutana na David, aliekuwa amemsubili muda mrefu.
"Nakupa nyumba hii, ila hati sitakupatia leo, utazipata baada ya kifo cha Janiphar, hapo ndipo nitakapoamini, na kuanzia muda huu, umeshakuwa rafiki kwangu na ndani ya Blood deal, hutakiwi kukataa kufanya chochote, ukienda nje ya utaratibu, kichwa chako kitakuwa chakula cha hii "
David alizungumza huku, akitoa bastola ndani ya suruali yake, wote wakiwa ndani ya gari lake, alianza kuipangusa pangusa, akiwa ameitumbulia macho, upande wa Dk. Eddyson, hali haikuwa nzuri, kulikuwa na nafsi iliyoanza kumbeza na kumsunta, muda mwingine alijuta kukutana na David, kukubali kufanya kazi yake, alidhani mambo yatakuwa rahisi sana! Masikini Dk Eddyson alianza kutetemeka, bila mwenyewe kutegemea.
"Sasa unatetemeka nini? Mbona unakuwa kama mwanamke! Daima mwanaume huishi popote, hufanya lolote, na tambua mwanajeshi hachagui adui wa kumshambulia hata mtoto mdogo anaweza kushambuliwa akiwa upande wa adui, wewe mwanaume kaza mjomba " alizungumza maneno hayo David akiwa anakipiga piga kifua cha Dk Eddyson, kilichokuwa kidogo na cha kawaida sana .
"Lakini makubaliano yetu hayakuwa hivyo? "Alizungumza kwa unyonge, muda mwingine alitamani kuitoa damu yenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi ndani ya mwili wa Janiphar, lakini haikuwezeka, tayari maji yalikuwa yamemwangika ndani ya bahari, na ni ngumu sana kuyachota yaleyale, lazima utoke na mengine, majuto ambaye ni mjukuu tayari ,alikuwa rafiki yake kuanzia dakika hiyo.
"hahaha Dk Eddyson!! Hahahaha! Unanifurahisha kweli baadala ufu....."
David alicheka kwa furaha, huku akiongea, aliyakata maneno yake, baada ya kuchukua mzinga wa konyangi, aliutikisa tikisa kama dakika moja, huku macho yake yakiendelea kumtathimini Dk. Eddyson ,aliekuwa mnyonge kupita maelezo ,
"puuuuh! Sikiliza bwana mkubwa, siku zote ahadi huvunjwa kutokana na sababu za kila mmoja, hujawahi kuona penzi la watu waliokuwa wakipendana sana, na kila mtu akiwatamani lakini mwisho wa siku wanaachana? Na hata wakikutana hawasemeshani? "
"kweli "
"sasa Kama ni kweli!, Je mimi nitakuachaje, na tayari umeshafahamu kila kitu changu, ukitaka nikuache labda nikuue "
"nini? "Dk. Eddyson alipayuka kupita maelezo,
"ndio lazima ufe, ndipo utakuwa huru la sivyo karibu ndani ya Blood deal, kuna swali?"
"ha.... hap... aaana "
Alijikuta akishindwa kujibu vyema, zaidi ya kuendelea kutetemeka, ile furaha ya asubuhi aliyoamka nayo ilotoweka ghafla.
"Basi kama hakuna, karibu kwako, unaweza ukarudi kuishi hapa kuanzia leo, fanya usafi, tutazidi kuwasiliana, unaweza kuondoka chukua pikipiki wahi hofisini "
David alimkabidhi noti tatu za elfu tano tano mpya, Kama nauli.
*****
Usiku mzima hakuna alieshituka, zaidi ya kujigeuza geuza, saa kumi na mbili, Poul alikuwa wa kwanza kuamka, aliyafuta macho yake ili kuiondoa hali ya usingizi singizi, kisha alinyanyuka na kuketi, hakutaka kumuamsha mama yake, muda huo, alichofanya alishuka taratibu hadi chini alikoanza kufanya mazoezi kama Dk. Atanasi alivyokuwa amemweleza,
"Mama nataka kuoga "
Poul alimuongelesha Mama yake, huku mikono yake ikimtikisa tikisa, dakika mbili alishituka akiwa mchovu mchovu sana,
"shikimoo Mama "
Mar- haba ,umeamka salama? "
"Ndio mama, wewe je? "
"Salama ila nahisi, mwili mchovu, na mkono unauma hapa "aliongea huku akipashika shika eneo lililokuwa likimuuma, hakujua ni kipi kilimpata zaidi ya kuhisi uchovu tu, hakuta kulala tena, alimchukua mwanae na kumpeleka bafuni alimsafisha, kisha nae alijisafisha, baada ya kumrudisha chumbani huko,dakika kumi wasalimiaji waliingia, hata kabla hawajakaa Dk. Atanasi alifka chumbani humo kumjulia hali rafiki yake Poul, aliwaomba wampishe kidogo na baada ya vipimo aliondoka, akiahidi kurudi mchana huku akiwapa matumaini ya kuondoka siku chache.
Ilikuwa jumatano asubuhi Janiphar alikuwa akijiandaa kuelekea kazini, baada ya wao kuruhusiwa kutoka hospitali siku tano nyuma, hakuwa na furaha hata kidogo, kutokana na upweke uliokuwa ukimsumbua, siku zote alizoea kuondoka na mmewe ,tena wakiwa wanacheka kwa furaha,
"mpenzi nilikuzoea sana, sikujua kama siku moja utaniacha peke yangu, nilijua tutaishi milele ndani ya vicheko na tabasamu zisizo na kikomo, leo umeondoka na kuniachia mtoto, leo umeondoka na kuniachia lawama na hata uaduni, laiti ningekuwa na uwezo ningekufuata, nit...... "Janiphar alishindwa kuongea, alijikuta akilia sana huku akiwa ameikumbatia picha ya mmewe, siku wakifunga ndoa, miaka mitatu nyuma, hakiri yake, moyo wake vyote vilishindwa kuzoea kabisa, kila siku kwake kilikuwa kilio,tena kibichi, muda mwingine alidhani ni ndoto, ama yuko Safari na siku moja angelejea, lakini haikuwa hivyo, Emanuel alikuwa ameshafariki! Na asingeonekana tena ndani ya uso wa dunia.
Taratibu aliitoa picha hiyo kifunia kwake, aliibusu, kisha aliirudisha ndani ya kabati lake la nguo, hakutaka tena kuiona kwa muda huo,
"bwana nipe uvumilivu "papo hapo alichukua funguo za gari lake aina ya BMW ,mkoba mkono wa kushoto na kutoka chumbani humo, aliwaga ndugu waliokuwepo kisha aliondoka, bila kuyafuta machozi yaliyokuwa yamesambaza sambaza powder yake.
Kila mtu alifurahi kumuona, neno Pole ndilo aliloshinda nalo masikioni mwake, siku hiyo alishinda mnyonge sana, lakini kadri siku zilivyozidi kusonga alijikuta akianza kuzoea zoea na kusahau ,ndani ya miezi mitatu alikuwa keshazoea, kule kulia lia kulipungua kiasi, tabasamu likaanza tena kuonekana usoni mwake, ngozi nayo ikaanza kukujuka na kurudi katika muonekano wake, wa kawaida.
Mwezi wa sita alianza kuugua ugua hovyo hovyo, muda mwingine alihisi ni maralia hivyo alinunua dawa, ama aliongea na Dk. Atanasi aliemshauri cha kufanya, lakini hakupona akawa mtu wa homa homa baada ya muda mfupi, hali ilivyozidi kuendelea ilibidi aende Aghakhan kuchukua vipimo.
"Janiphar Emanuel! "
" Abeee Dk "
Akiitika Janiphar huku akinyanyuka na kuelekea chumba alichokuwa Dk Larry, raia wa Hindia
"karibu Janiphar "Dk. Larry aliongea kiswali chenye rafudhi ya kihindi hindi huku akimtazama machoni ,
"ahsante "
Kimya kilitawala huku Dk. Larry akikagua kagua karatasi zake,
"Dk. niambie vipi namaralia sugu nini ? "
Aliuliza Janiphar baada ya kuona kimya kimetawala muda mrefu.
Dk Larry hakutaka kuongea chochote zaidi ya kumtazama kama dakika tatu, kisha aliachia kikohozi kikavu kutengezeza koo lake,
"Janiphar "alianza kwa kuita, kisha akiendelea
"majibu yako utapata, ondoa wasiwasi, hebu niambie mmeo alikufa kwa ugonjwa gani? "
"aaaah! Aliuawa nchini Afghanistan, kwa ufupi hakufa kwa ugonjwa wowote "
"sawa, na kabla ya kifo chake, aliwahi kuugua ugua kitu chochote?"
"mmmmmh! Hapana, mme wangu hakuwa na tabia ya kuugua hovyo hovyo, kwani vipi? "
"hakuna tatizo, nilikuwa nataka kujua tu, je wew hukuwa ukiugua chochote? "
"hapo nyuma hapana!, ila miezi mitano ama sita baada ya mme wangu kufariki, mwili wangu ulianza kuumwa umwa hovyo, mwanzo nilijua mawazo, lakini hali iliendelea endelea tu "
"ok sawa, samahani kwa swali hili, sina nia mbaya, je baada ya kufiwa uliwahi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwingine? ".Safari hii Janiphar alishituka, hakujua kwanini Daktari huyo alikuwa na maswali, mengi kiasi hicho!.
"Hapana sijawahi, na siko tayari kwa muda huu, nampenda mme wangu sana, je nimeonekana na Ukimwi? "
"mmmmmh! Janiphar ondoa wasiwasi, bado tunashughulikia vipimo, na hatuwezi tukakueleza, kuwa umeambukizwa ila njoo baada ya miezi mitatu tutajua zaidi "
Maneno ya Dk. Larry alimchanganya sana Janiphar, hakutaka kuendelea kukaa tena ,chumbani humo alitoka mbio mbio hadi ndani ya gari lake, safari ya kuelekea mwananchi hospital ilianza, njia nzima alikuwa akitoa machozi, hakujua alifikaje hapo, alipaki gari lake mbele ya jengo la zamani la Tanesco,alishuka haraka, huku akikimbia kukifuata kijia cha kuingia soko la makoroboi, lakini hakufika huko ,alikunja mkono wa kushoto na kuingia ndani ya hospitali hiyo iliyojificha ficha, kwa mtu mgeni jiji la mwanza ni vigumu sana kuifahamu.
"Agines ninaukimwi! "Janiphar aliongea bila hata kukaa, Wifi yake Agines aliekuwa daktari mpya ndani ya hospitali hiyo alimshangaa, haikuwa kawaida ya Janiphar kwenda pale bila kumtarifu.
"nani kakueleza wifi? "Agnesi aliuliza kwa upole, huku akiacha kumuhudumia mgonjwa aliekuwemo ndani,
"nimetoka Aghakhan dakika hii nimeelezwa, ninaukimwi wifiiii, na nani kaniambukizaaaa"Janiphar alishindwa kuongea vizuri, zaidi ya kulia, alikiona kifo kikimkabili muda si mrefu , kifua nacho kilichemka kupita maelezo .
"Mamy tulia Kwanza, acha nimalizie kumuhudumia huyu nije tujue zaidi " Agnes alizungumza hayo, huku akimalizia kumuhudumia mgonjwa wake, dakika kumi alianza kuongea na wifi yake ,Janiphar alianza kumuelezea kila kitu, huku akitia huruma,
"acha tuchukue kipimo ".
Papo hapo alichukua damu kutoka kwa Janiphar, na kuipeleka sehemu husika, dakika mbili alilejea kuongea na wifi yake, akimtia moyo, kidogo Janiphar akianza kufarijika, wakiwa wamezama ndani ya mazungumzo, majibu ya Janiphar yaliletwa na kukabidhiwa Dk. Agines ambaye ni wifi yake kabisa, kabla hajafanya chochote Janiphar alimnyakua na kuyasoma, papo hapo alidondoka chini kama mzigo puuuu, na kupasuka kichwa upande wa kisogoni, Agines alibaki amepigwa bubuwazi, hakujua afanye nini, zaidi ya sekunde arobani na tano alikuwa hajielewi ,alikuja kushituka baada ya kuona damu nyingi zikiipamba taizi, kelele akizozipiga zilichangia kujaza watu, dakika saba ndizo zilizotumika kumsaidia Janiphar aliekuwa akihema kwa mbali sana ,huku akiwa amepoteza fahamu , huduma ya kwanza ilitolewa ,kabla ya kwenda Bugando hospitali kwa uchunguzi zaidi.
Machozi na kamasi nyepesi nyepesi hazikukatika machoni, na puani kwa Agines pindi alipogundua majibu ya wifi yake, yaliyokuwa yakionesha maambukizi ya virusi vya ukimwi, hakujua muda gani walifika Bugando, wakiwa bado getini Janiphar alipandisha kifua juu, macho yakiwa yametoka, huku mdomo ukiachama na alipokuja kushusha kifua tayari alikuwa amefariki, kila mtu ndani ya ambulance hiyo hakuamini hasa hasa wifi yake, alieona kama maigizo flani lakini ukweli ndo ulikuwa huo.

What? Kirahisi hivyo?

Janiphar kazimika kirahisi hivyo?


Cc: mahondaw
 
BLOOD DEAL, 11.
NA Teddy
Cont : 0655 202 285.

Ilikotoka....

Hali ya Janiphar imeanza kubadirika, baada ya miezi mitano kutokea kifo cha mme wake, hali hiyo inamchanganya sana anaamua kwenda kuchukua vipimo, ndani ya hospitali ya Aghakhan, majibu yanayotolewa na Dk. Larry yanaichanganya hakiri yake, anatoka ndani ya hospitali hiyo kwa kasi ya ajabu, Safari yake inaishia ndani ya mwananchi hospital, nako mambo yanakuwa magumu, japo wifi yake Agnesi anajitahidi kumshauri, Wakiwa ndani ya mazungumzo majibu yake yanaletwa, katka hali ya kushangaza na kushtua, Janiphar anamkwapua Dk. Agnes karatasi hiyo, nguvu zinamuishia, anaona giza na ghafla nanadondoka chini, na kupasuka kichwa papo hapo, harakati za kuokoa maisha yake zinachukuliwa, wanamkimbiza Bugando, lakini wakiwa getini Janiphar anafariki, kitendo kinachomchanganya kila mtu, je nini kitatokea?.

SONGA NAYO.

Agines alihisi nguvu zikimuishia mwili mzima, alitetemeka bila kujua na hata mwili wake ulianza kuota vipele vya baridi ,hakuamini kama kweli wifi yake kipenzi na wa pekee alikuwa amefariki!Tena mbele ya macho yake! Zaidi ya dakika moja alibaki ameganda asijue la kufanya, kulia alishindwa, kila kitu hakuweza kufanya. Kilichokuja kumshtua ni hatua ya madaktari toka mwananchi na Bugando walipoanza kuyarudisha macho pamoja na mdomo.
"Mama Poul? "
Agines alimuita huku akimlalia kifua, machozi yalianza kuchora barabara katika mashavu yake, aliona ni mkosi uliokithili,
"hata mwaka hujapita wote wanafariki? Na wifi kautoa wapi ukimwi? "Yalikuwa ni mawazo yenye mfumo wa maswali , yakipita ndani ya kichwa chake.
Mwili wa Janiphar ulitolewa ndani ya ambulance hiyo, na kulazwa juu ya kitanda kilichokuwa na matairi mawili mawili, mbele na nyuma, huku ukiwa umefunikwa,kuanzia kichwani hadi miguuni. Safari ya kuelekea chumba cha daktari kwa uchunguzi zaidi ilianza, huku Agines akiwa ameushilia,
"Naomba ufanye uchunguzi Dokta siamini kama kweli wifi amefariki? "
Aliongea Agines huku akitoa machozi
"kuwa na subila binti, kaa kwanza hapo nje "
"hapana naomba nikae humu humu, nami ni daktari "aliongea huku akitoa kitambulisho ,Dk George hakuwa na jinsi , ilibidi afanye kazi hiyo, akiwa amesimamiwa, dakika tatu alikinyanyua kichwa chake na kumtazama, uso wake ukivaa vazi la huzuni.
"Amekufa? "
"Ndio! "
"Ooooosh!" Alitoa neno hilo huku akikaa juu ya kiti kilichokuwemo chumbani humo, alihisi kichwa kizito kupita maelezo, macho yalianza kuona giza, huku mapigo ya moyo yakienda kasi ,lakini alijikaza sana.
"OK Dokta "
Dk. Agines alitoka chumbani humo, mbio, alitoka hadi nje ya geti, alichukua pikipiki iliyimpeleka nyumbani kwa kaka yake, mita chache kutoka hapo.
"Ma... maaaa wifiii ,wifi amefa.... " Dk. Agines alianza kupiga kelele, pindi alipoukanyanga uwanja wa nyumba hiyo, ile ahadi ya kujikaza kwanza ilitoweka ghafla, sauti yake hiyo ilipelekea mama yake kutoka mbio.
"nini? "
Aliongea Mama yake, huku akinyanyuka , alihisi kama kisu cha moto kikiuchoma moyo wake, hakutaka kusikia habari mbaya ,masikio yake yameshachoka.
"Agi niambie, kunanini? "
"Mamaaa, wifiii kafarikiiiiii! "Aliongea huku akitoa kilio cha hali ya juu, hali hiyo ilisababisha mji huo kujaa watu, na kutanda kwa vilio kila kona, hakuna alieweza kumsaidia mwenzake, hakuna aliamini kama Janiphar nae alikuwa amefariki! Na asigeweza kuja tena, maswali yalikuwa mengi kwa kila mtu, wengi wao walijiuliza kafa kwa kitu gani? Wakati asubuhi alikuwa mzima kabisa ! Ilibidi wamtulize Dk. Agines ili aweze kuwaeleza nini hasa kilipelekea kifo cha Janiphar? Japo haikuwa kazi rahisi kumtuliza, lakini walifanikiwa kwa kiasi kidogo.
"Ukimwi "
"Nini!!!!!!!!!!!! "watu wote walishangaa kwa pamoja, Hakuna alieweza kuamini kama kweli, Mama Poul alifariki kwa ukimwi.
"Puuuuuuh! "Alishusha pumzi ndefu, kisha aliyafuta machozi, alianza kuwaeleza kila kitu, japo ilikuwa ngumu kwa kila mtu kuamini,ilibidi waamini maneno hayo, kati ya watu waliokuwa wameumizwa sana na msiba huo ni mtoto Poul, alilia kupita maelezo, maneno aliyowahi kuambiwa na Mama yake miezi saba nyuma yalimuumiza sana, sasa alikuwa akifahamu nini maana ya kufariki, alijua Mama yake nae hatakuja tena,
"kama Baba aliondoka na hakurudi, itawezekanaje Mama arudi? Amekufa sina Mama mimi msinidanganye niacheniii" Poul alitoa maneno hayo huku akilia, kilio kisichoeleweka ni muda gani kingekoma, hakuyaamini maneno ya bibi yake aliona ni uongo mtupu, mtu aliekufa , alikufa tu, na asingerudi tena, iweje bibi yake amdanganye? Mama atarudi! Poul alitia huruma sana , kila aliemtazama alishindwa kujizuia kutoa chozi, maneno yake yalikuwa miiba miyoni mwao.
*****
Hakuna siku iliyokuwa njema masikioni mwa David kama siku hiyo! Alijiona mshindi kupita maelezo, kila sekunde alitoa tabasamu
"Kaka mambo tayari"
"Unasema? "
"Kaondoka mchana huu, kuanzia dakika hii, mie boss hapa mjini "David aliongea kwa kujingamba, habari ya kifo cha Janiphar, ilikuwa njema sana masikioni mwake, furaha aliyokuwa nayo hakika haikuelezeka, mara baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kwa baba yake, alibadirika sana, alijiona mwili mwepesi si mfano, papo hapo alitoa agizo kwa wafannya kazi wote wagawiwe soda, walishangaa! Sana .
"Hogerea sana sasa umekomaa, na Dk. Utampatia nini? "
"Nitamkabidhi rasimi nyumba yake, na kumtumia katika mambo yetu, mara baada ya kumpika vyema "
"hilo nalo neno jema "
"tena anatufaa sana "
"kweli "
"sasa acha nikazuge msibani, jioni tutaonana "
"kwanini tusiambatane wote, kusherekea ushindi leo ni kunywa kwenda mbele "
"kweli Deus, nakuja kukupitia "
David alikata simu, na kushusha pumzi ndefu ya ushindi, aliitazama hofisi hiyo, bila kuamini kama kweli ilikuwa yake, hakuwa na adui tena wa kuisumbua hakiri yake, mtoto Poul alimuona kama mkia wa ngo'mbe, kuukunja na kuurushia mdomoni haikuwa kazi ngumu.
"Daaaa! Nimemaliza "
aliongea Peke yake huku akinyanyuka na kutoka hofisini kwake , hakujali macho makali ya wafanyakazi wake na Marehemu Janiphar, waliokuwa wakilia sana, kwake aliona maigizo tu!
"muda wa kufunga hofisi ni ule ule, na kesho ,kazi Kama kawaida "
David alitoa maagizo hayo kwa mhasibu wake, Dada huyo hakuamini, kile kilichozungumzwa, alibaki ameshangaa.
"Umenielewa? "
"Ha.... hapanaa,lakini mwenyekiti amefar...... "
"shiiiii! Toa ngojera hapa, yule kaenda na tumbo lake, maisha yake yameishia hapo hapo, tukikaa kumuabudu, madeni yatalipwaje?, Msharaha wako!, muda mwingine uwe unatumia hakiri ".
David alizungumza kama hana hakiri, hakujali kabisa kifo cha Shemeji yake, makelele yake yalipelekea , wafanyakazi wote kuzunguka eneo hilo, wakiwa wamevimba sura.
"Boss tunataka kwenda msibani "
"nani kafa? "
"Mama Poul? "Kijana aliekuwa akijiamini Kupita maelezo alijibu, bila wasiwasi,
"hakuna cha msiba hapa, tazemeni kazi ,ndicho kilichowaleta hapa, si vilio, ok anaetaka kwenda aende, ila atambue kuanzia dakika hii hahesabiki mfanyakazi wa hapa ". Wafanyakazi wote walinyanyuka na kutoka, kama kukosa kazi, walikuwa tayari, David hakuamini macho yake, alibaki amesimama katika ya mlango, bila kujielewa.

Macho ya David hayakuamini hata kidogo, aliona kama mawenge, taa ya hatari ikawaka kichwani kwake , tayari alikuwa ameshagundua udhaifu wake, kwa wafanyakazi wake. Hivyo alihitaji hakiri ya ziada kurudisha hali ya kawaida, na si kesho ama masaa kadhaa, ilitakiwa afaye papo hapo! Kuondoka kwa wafanyakazi wote kulionesha picha ya mambo yake ambayo sasa yanaweza kuharibika kwa muda mchache, hilo David hakutaka litokee, na ili kurudisha hali ya kawaida ilitakiwa atumie hakiri ya ziada.
"Mossee "
"Naam boss "
"hebu njoo mara moja "David aliongea huku akitembea taratibu kumfuata kijana huyo, alionekana ndie kihelele
"nikimtuliza huyu wote, watakuwa nziiii! " David aliwaza, akiendelea kumfuata Moses .
"Sasa Mosse kuwatania tu mnaondoka? "Aliongea huku, uso wake akiupamba kwa tabasamu la bandia, ilihali moyo haukuwa radhi kabisa .
"Unajua tunashindwa kukuelewa kabisa boss, hofisi yetu imepoteza mtu wa muhimu sana, aliekuwa akitegemewa na kila mtu, mji wote umezizima iweje wew ukatae sie tusiende? Picha gani tutaionesha? Binafsi niko radhi kupoteza kazi, ila si kumterekeza Janiphar! Mama huyu ameondoka ingali anahitajika, upole wake, na huruma yake kwetu,siku zote leo iwe hivi? Hatukuelewi watu wanahisi yawezekana umehusika! Hiyo siyo roho mbaya bali ni mbaya roho, hatuwezi kumfanyia hivi, hatuko nae kimwili ila kwa imani tuko nae kiroho tunaenda kumhani kwaheri "
"hap.... apanaaa! Aaah! Mosse, punguza jazba, tuongee kama wanaume, muda ule nilikuwa sijielewi, si unajua pombe "
David aliongea taratibu, tena kwa aibu ,ule ukali wake , siku hiyo ulikwama, lakini hakutaka kukubali kushindwa alitakiwa apambane hadi mwisho wake.
"Pombe? Pombe na msiba aaaaah! "
Kijana Mosse alishangaa kupita maelezo , hadi mishipa ya kichwa ilimsimama, macho ameyatoa kupita maelezo, hakudhamiria kusikia maneno kama hayo.
"Usinishangae Mosse, nimawazo ndo yanayopelekea kufanya vile, kifo cha shemeji yangu kimeniumiza sana, na ili kuondoa mawazo ilibidi nifanye tafadhali nisameheni "ilibidi ajishushe ili mambo yaende sawa
"poa acha tuwahi, hayo yamepita "
"chukueni gari za hofisi mtumie "
Toka uhai wa Emanuel, hakutaka wafanyakazi wake wasumbuke kwa usafiri, hivyo alinunua magari mawili kwa ajiri ya usafiri, asubuhi na jioni, pia usafiri huo ulirahisisha kazi yake kwenda alivyotaka, wakati muafaka, hakukuwa na visingizio vya usafiri mgumu.
"Sawa tutatumia "
Alijibu Mosse huku akianza kuondoka taratibu eneo hilo, David aliyauma meno yake kwa hasira, huku akiikandamiza aridhi, kwa kiatu chake upande wa mbele
"Sitakiwi kuonesha dhamila yangu muda huu ,acha nigonje muda utimie " aliongea huku akiingia ndani ya gari lake Safari ya kumpitia Deus ilianza, akiwa njiani alijikuta akikumbuka mambo mengi sana ya nyuma.
*******
"Emma mbona mdogo wako habadiriki? "
"Baba hata mie sijui, tuendelee kumkanya tu nadhani ataacha "Emanuel aliongea huku akiacha kulima, alimtazama Baba yake aliekuwa amechakaa kupita maelezo, hali ngumu ya maisha hakika ilikithiri ndani ya familia hiyo, aliyauma meno kwa uchungu, hakuyapenda maisha hayo ya kuchekwa kila siku, umasikini wao ulionekana kama matangazo ya biashara kwa watu.
Toka Emmanuel ajitambue hakuwahi ona uafadhari wa maisha, kila siku kwao ilikuwa afadhali ya jana , kulala njaa kwao kilikuwa kitu cha kawaida! Kuchekwa kisa masikini nalo lilikuwa jambo la kawaida .
"Lakini vipi masomo yako? "Baba yake alimkatisha mawazo hayo mwanae, japo alishatambua kipi kilikuwa kikimuumiza kijana huyo hakutaka kumuacha aendelee.
"Aaaah! Nashukuru Baba yanaendelea vizuri, na baada ya mwezi huu kutakuwa na mtihani "
"soma sana Baba, Sote tunakutegemea ujue, tumekupa nafasi hii wewe, na ukituangusha hukumu utaibeba mwenyewe, ona mimi na Mama yako kutwa tunashinda shamba, kulima kwa ajiri yako , wadogo zako hawasomi, nguvu zetu zote tumeziwekeza kwako, kama tulivyokueleza ukifanikisha tafadhali usiwasahau ndugu zako "

ITAENDELEA
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 12

Toka Emmanuel ajitambue hakuwahi ona uafadhari wa maisha, kila siku kwao ilikuwa afadhali ya jana , kulala njaa kwao kilikuwa kitu cha kawaida! Kuchekwa kisa masikini nalo lilikuwa jambo la kawaida .
"Lakini vipi masomo yako? "Baba yake alimkatisha mawazo hayo mwanae, japo alishatambua kipi kilikuwa kikimuumiza kijana huyo hakutaka kumuacha aendelee.
"Aaaah! Nashukuru Baba yanaendelea vizuri, na baada ya mwezi huu kutakuwa na mtihani "
"soma sana Baba, Sote tunakutegemea ujue, tumekupa nafasi hii wewe, na ukituangusha hukumu utaibeba mwenyewe, ona mimi na Mama yako kutwa tunashinda shamba, kulima kwa ajiri yako , wadogo zako hawasomi, nguvu zetu zote tumeziwekeza kwako, kama tulivyokueleza ukifanikisha tafadhali usiwasahau ndugu zako "
Aliongea mzee Poul kwa uchungu sana, japo alikuwa na imani kwa mwanae, ila kama mzazi wajibu wa kumshauri ilikuwa lazima, alijua vyema ujana ulivyo, hivyo bila kumsistiza kila muda kungechangia matokeo mabaya.
Kutokana na hali ngumu ya maisha kuikabili familia hiyo, iliamua kumteua kijana mkubwa Emanuel kupewa nafasi ya kusoma huku wadogo zake, David na Agines wakinyimwa nafasi hiyo ya kuendelea na masomo ya secondary kwa muda mfupi, huku wao wakijikita katika kilimo ili kumsomesha ndugu yao.
Baada ya kufaulu kwenda chuo kikuu bahati nzuri alipata mkopo uliomuwezesha kuanza kumsomesha mdogo wake David aliekuwa amepoteza miaka mitatu bila kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza, kukaa huko nyumbani kwa muda mrefu huku akishurutishwa kulima kwa ajiri ya ndugu yake, alijikuta akijenga chuki dhidi ya Emanuel, pamoja na wazazi wake, mara nyingine alidhamiria kumshawishi na Dada yake kufuata njia zake lakini haikuwa rahisi, kwani Agines hakuwa na roho kama yake, alikuwa msikivu kupita maelezo, imani kwa Emanuel haikupungua na aliamini siku moja angeedelea na masomo tu! Mara baada ya kaka yake kufanikiwa.
"sikia wewe asali wa mzee , usidhani nitakufarahia na kukuchekea, umenikalisha miaka mitatu nyumbani, eti leo unajipendekeza kunisomesha, mimi ningekuwa mbali sana ujue, tunashinda sham..... "
"David mdogo wangu chuki ya nini? "
Emanuel aliongea kwa upole sana, hakuamini hata siku moja angeweza kusikia maneno makali kutoka kwa mdogo wake huyo, aliwapenda wadogo zake, aliwadhamini kupita maelezo, bila wao yeye asingeweza kufika hapo alipo! Kila siku alizungumza na moyo wake, akiusihi kutobadirika, alijua ana deni na moja ya kutatua deni hilo ni kulipa, hivyo moyo ulitakiwa utobadirika kabisa.
"wewe unaona chuki? Eeeh! Ok poa mimi ndo fomu One, tena niko na dogo, wakati nisingeshindishwa shamba ningekuwa kidato cha nne, zee zima kidato cha kwanza, wewe unafurahia mie kuitwa babu wa darasa? ".
David alizungumza kwa hasira sana, hakutaka kusikia ngojera kutoka kwa kaka yake, aliona ni uonevu na hakusitahili kulima kisa asome ndugu yake! Hivyo alianza kujenga chuki na kiapo cha kumkomesha!, japo hakujua angemkomesha kwa njia gani ila tayari alishahapa!
"David elimu haina mwisho, na usipende kuishi kwa ajiri ya flani! Mipango ya familia yetu, usifananishe na familia ya flani, sie masikini, kijiji chote kinatufahamu kisa umasikini! Sasa utakaposikiliza flani kasema hivi utapotea nakwambia "
"wewe toa ushambani Robert hapa, nani kakueleza nahitaji mashairi? Fala nini? "
David alimalizia kwa kumtukana kaka yake, kisha alitoka chumbani kwao, hawakujua alikwenda wapi, hadi kunapambazuka. Emanuel aliumia sana ila hakutaka kuonesha maunivi hayo kwa wazazi wake ila alijiwekea nadhiri ya kumsaidia kwa hali na mali ndugu yake huyo.
Kweli mara baada ya kufanikiwa hakutaka kuwatupa ndugu zake , alimchukua David na kumpeleka kusomea nchini Kenya ,akiamini atabadirika, lakini haikuwa hivyo David aliendelea kutunza hasira yake hadi alipomaliza masomo yake, japo kaka yake alimjengea nyumba, gari alimununulia na kuwa nae ndani ya biashara zake, akiamini ndugu yake huyo keshabadirika kumbe haikuwa hivyo! David alimchekea machoni tu, lakini moyo wake ulivaa vazi la kisasi!.
Miaka mitatu baadae Emanuel alioa ,lakini hakuweka siri kwa mkewe , aliyeyapokea maneno hayo kwa furaha akimwahidi kutomuangusha.Hivyo Janiphar akawa amewapenda Sana ndugu wa mme na kuwashika mkono, akiwapa maneno ya ushindi, hakusita kumkanya mmewe pindi alipoona anawakwanza watu waliompa maisha, hakika Janiphar alikuwa miongoni mwa wanawake wa kuigwa.
Ushirikiano wao uliendelea kuzaa matunda, walijikuta matajiri sana ndani ya mji wa mwanza, na hata Simiyu, umasikini uliokuwa umewatoboa kwa muda mrefu uribaki hadithi, masikini waliochekwa na kuzaraurika sasa waliheshimika, hata wao hawakuamini kama wangefikia hatua hiyo. Japo Emanuel alichekwa na kuzomewa kisa mtoto wa masikini, lakini hakuwa na moyo wa malipizi, alisamehe na kusahau, na ili kuonesha msamaha huo ndipo alipoanzisha utaratibu wa kusaidia masikini, siku zote aliumia sana pindi alipowaona masikini wakidharaurika.
David hakuta kumsamee kabisa, hasira yake ilizidi kuongezeka pindi akipoona ndugu yake akizidi kufanikiwa, hivyo alianza kupanga mikakati kumuangamiza ilianza upya, Deus aliekuwa rafiki wa Emanuel ndie aliezidi kuchochea hasira ya David, kwanza alipandikiza chuki kwa Emanuel akidai kuzurumiwa, wakati yeye ndie alimzurumu pesa baada ya kuagizwa magari nchini Japan ,hapo ndipo mikakati ilipoanza ya kumuangamiza Emanuel, Deus alianza kumuingiza ndani ya ujambazi hadi alipokomaa, na kuwa mafia wa kimataifa .
****
"puuuuh! David alishusha pumzi ndefu, hakutaka kujiraumu kwa chochote, alijiona yuko sahihi kabisa, mara baada kufika hofisini kwa Deus alimpitia na safari ya kuelekea msibani ilianza njia nzima walicheka na kufurahi .

Kadri muda ulivyozidi kusonga mbele, watu walizidi kuongezeka sana, sauti na vilio vilizidi kutanda eneo lote la nyumba hiyo. Akina Mama ndio waliokuwa wakitoa sauti za vilio kwa hali ya juu, hakuna alieshindwa kutoa chozi pindi walipomtaza mtoto Poul.
"Nyamaza mwanangu Mama atarudi kesho, nitamfuata sawa? "
Poul hakumjibu mwanamke huyo aliekuwa akimbembeleza, hakujua aseme kipi ili hali kila kitu alikielewa, neno kifo halikuwa geni kwake, aliufahamu ukweli wote, japo kilikuwa kitoto kidogo sana, lakini kilijariwa hakiri ya kunasa mamba na kuyahifadhi.
"Unti niambie Mama yuko wapi? "
Poul aliongea huku akiyafuta machozi, hakutaka tena kulia , sasa alitaka kusikia ukweli wote
"Poul Mama amefariki, alidondoka chini "
Dk. Agines alijikaza na kuongea, alishindwa kuelewa kwanini Poul amebadirika ghafla, alivimba sura kwa hasira, aliacha ghafla kulia ,macho makubwa kiasi ya kiume yalimtazama shangazi yake.
"Sawa nimesikia ukisema Ukimwi, je nini?"
Dk . Agines alishtuka kusikia neno hilo, taratibu alinyanyuka na kukuketi, sio yeye tu alieshangazwa na swali la Poul, hata baadhi ya akinamama waliokuwa wameketi kando yao nao walistajabishwa, mining,ono ya chini chini ilianza kuchukua nafasi, huku wakimtazama Poul.
"Njoo huku " Dk. Agines aliongea huku akinyanyuka kuelekea chumbani, japo hakujua kipi angeenda kukiongea, tayari alishaanza kuhisi kitu japo hakukifahamu kwa muda huo.
"Unataka kufahamu kuhusu Ukimwi?"
"Ndio, ulisema Mama yangu ameuawa na Ukimwi ndo nani huyo nimfuate na kisu? "
Mtoto Poul alizungumza, huku akiwa ameuma meno, macho makavu kupita maelezo,
"mmmh! Sio mtu, bali ni ugonjwa, je ukimfahamu mtu huyo utamfanya nini? "
"Nae atafariki, na hawezi kuja tena hapa, Mama alinieleza, Baba alifariki haji, na Mama haji, nae nikimfahamu haji, atafariki "
"Aaaah! "Dk .Agines alishusha pumzi ya mshangao ,hakujua aseme nini? Alibaki akimtazama mtoto huyo,
"niambie "
"Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini, ndo maana yake, na unasababishwa na kirusi ama kidudu kinachoitwa kirusi cha ukimwi, sasa unapopata kirusi hicho kin...."
"unakipataje? "
"kunajia nyingi, mojawapo ni kuongezwa damu, kwa kuchomwa sindano n..... "
"nini? " Poul alishangaa kusikia neno hilo, hakiri yake ilikumbuka kitu, japo ni muda mrefu sana ulikuwa umepita, lakini mawenge mawenge yalikuwa bado yanakitembelea kichwa chake.
"Kwani vipi? "
"Hapana! "Papo hapo alianza kulia, alihisi kitu kibaya dhidi ya Mama yake, kile kitendo cha Mama yake kuchomwa sindano alikikumbuka, japo alikuwa katika hali ya usingizi singizi lakini kwa mbali aliweza kuona Dk Eddyson akishika mkono wa Mama yake, na hakujua kipi kiliendelea maana nae dawa zilimfikia japo kwa mbali sana, hakujua afanye nini? Sura ya Dk. Eddyson haikuwemo kichwani mwake , hata hospitali nayo hakuikumbuka.Lakini hisia zake zikimtuma kitu, hakika Poul alilia sana.
Siku iliyofuata ndugu wote walikuwa wameshafika, na kilichokuwa kikijadiliwa ni mazishi tu. Jibu lilipatikana siku hiyo hiyo na taarifa zilipokelewa vizuri na serikali ya mtaa, usiku huo huo. Kesho yake mwili wa Janiphar ulifuatwa hospitali ya Bugando na jioni ya saa kumi alizikwa ndani ya makaburi ya Kangae huko Buswelu nje kidogo ya jiji la mwanza, akiachiana mita chache na mmewe Emanuel. Poul alililia hadi alifikia hatu ya kupoteza fahamu, neno Mama umeniacha nitaishi na nani, lilikuwa mswaki mdomoni, alimlilia Mama yake bila mfano, hakujua atamuona wapi? Lakini hakuwa na jinsi ilibidi aupokee ukweli huo, kwa mikono yake miwili.
Kesho yake kikao cha ndugu kilichukua nafasi yake, karibia ndugu wote walimkabidhi jukumu la kumlea na kumsomesha Poul, Baba yake mdogo David ,hakuna aliejua siri iliyokuwa imejificha nyuma ya pazia, pia alitakiwa kuziendeleza mali za Kaka yake na baada ,yote hayo aliyapokea kwa mikono miwili .
Maisha yaliendelea David akawa ameazimia kumsomesha Poul, hakuwa na roho mbaya kama mwanzo, alianza kumpenda sana, baada ya kuona maendeleo mazuri ya kijana huyo , miaka mitatu baadae alimpeleka nchini China baada ya kushauri na Deus, hawakuwa na wasiwasi tena na mtoto huyo, kwa umri wake na siri waliokuwa wameifanya tangu mwanzo hadi miaka hiyo bila mtu kugundua, ingekuwa ngumu sana kwake kuelewa, mali zote alizibadiri na kuwa zake, japo kikao kiliazimia ziandikwe kwa jina la Poul! .
*****
ITAENDELEA
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 13

Maisha yaliendelea David akawa ameazimia kumsomesha Poul, hakuwa na roho mbaya kama mwanzo, alianza kumpenda sana, baada ya kuona maendeleo mazuri ya kijana huyo , miaka mitatu baadae alimpeleka nchini China baada ya kushauri na Deus, hawakuwa na wasiwasi tena na mtoto huyo, kwa umri wake na siri waliokuwa wameifanya tangu mwanzo hadi miaka hiyo bila mtu kugundua, ingekuwa ngumu sana kwake kuelewa, mali zote alizibadiri na kuwa zake, japo kikao kiliazimia ziandikwe kwa jina la Poul! .
*****
Mohammed Imran alikuwa mwarabu na tajiri mkubwa sana nchini Iran aliishi kusini mwa mji kerman.Alizaliwa katika familia ya kitajiri kupita maelezo, Baba yake mzee Imran Said alimiliki visima vya mafuta zaidi ya elfu kumi duniani kote, alimiliki bandari pamoja na meli zaidi ya laki moja, ambazo zilikuwa zikifanya kazi ndani na nje ya Iran.
Hakuwa na utajiri huo huo pia pesa zingine alizipatia kwa njia ya uuzaji madawa ya kulevya ,ambayo aliyafanya kwa siri sana, muda mwingine serikali ya nchi hiyo ilidiriki kuomba msaada kwake. Akiwa na miaka arobaini na nane mzee huyo aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa sikukuu ya Idd Mubarak akiwa na baadhi ya marafiki zake.
Mzee huyo akawa ameacha watoto wawili Mohammed na Rahma ambaye alikuwa mtoto wa miaka miwili tu, huku kaka yake Mohammed akiwa na miaka kumi na tano, kuuawa kwa mzee Imran Said kulimfanya mkewe Aziza kuanza kutoka nje akisimamia mali za mmewe, miaka mitatu baadae aliamua kumuingiza ndani ya biashara kijana wake huyo. Mohammed aliendelea kuindeleza mali ya mzee wake hadi alipofikia umri wa miaka thelathini na moja ndipo alipoamua kumuoa binti Salma toka Oman.
Baada ya miaka miwili ya ndoa walibahatika kupata mtoto mmoja tu Joan, kwa bahati mbaya bi Salma alitolewa kizazi baada ya kuonekana kwa dalili za kansa ya kizazi, hivyo familia hiyo ikawa na binti mmoja tu!.
Joan alilelewa katika mazingira ya kitajiri sana, toka akiwa na siku moja tayari alikuwa akimiliki kiasi cha dolla million moja benki, hakuweza kupelekwa kilinki daktari alikuwa akimfuata! Nyumbani mtu aliehitaji kumuona mtoto huyo alitakiwa atume barua kwanza! Hadi anafikisha umri wa miaka miwili hakuwahi kuliona jua, kasiri la baba yake lilimfanya asionekane pahali popote.
Utundu wake wa utoto ulizidi kuongeza furaha ndani ya familia hiyo, kila kifaa cha kuchezea alikipata! Baada ya mwaka mmoja na nusu Joan alitafutiwa mwalimu wa kumfundisha hapo hapo nyumbani . Uelewa wake ulizidi kuwafurahisha wazazi hao, hadi anatimiza miaka mitatu mtoto Joan alikuwa na uwezo wa kusoma vyema lugha ya kingereza achilia mbali kiarabu,
"natafuta mwalimu toka Marekani kwa ajiri ya Joan " mzee Mohammed aliongea mara baada ya kutoka kuswali swala ya jioni, akiwa na mkewe Salma
"Mwalimu? "aliuliza Salma kwa kiarabu
"ndio! Sitaki binti yangu asomee nje, nitamfungulia shule yake hapo hapo nyumbani "
"Haaaaa! Mtume! Hapana utamharibu kabisa inatakiwa ajichanganye na watoto wenzie "
"Joan tumemlea kwa maadili na misingi ya dini, nahofia kupoteza imani yake "
"hapana naamini hakuna kitakachotokea, tutamtafutia shule nzuri sana hapa Iran "
"basi sawa, tena nitaanza kulifuatilia suara hilo kesho, nataka asome sana "
"kweli ".
Huo ndio uamzi uliopatikana ,kesho yake mzazi wake alianza kufatilia shule na baada ya wiki moja Joan alianza kusoma ndani ya shule ya kimataifa Saquafa international School, akiwa chekechea.
Alisoma hapo hadi darasa la tatu, na kuhamishiwa nchini China ,mji kuu wa Beijing. Changchun ilikuwa ni shule nzuri sana nchini humo, ikiwa katikati ya mji mkuu wa China Beijing.Changchun ilisifika duniani kote, idadi ya watoto waliokuwa wakisoma hapo walikuwa wachina, warabu walikuwa wachache sana ,huku waafrika wakiwa watatu tu mmoja toka Afrika kusini, Nigeria na Tanzania .
Shule hiyo ilikuwa ikifundisha karibia lugha zote duniani,
"nice boy never seen before ( mvulana mzuri, sijawahi kumuona hapo nyuma)"
"Who? (yupi?) " Joan alimuuliza rafiki yake Nasra, wote wakitokea Iran
"yule alieketi nyuma ya chungyoung, black eyes (mwenye macho meusi) "
"ooooooh! "
Joan alishindwa kuongea chochote, zaidi ya kumtazama tu kwa macho ya wizi, toka azaliwe hakuwahi kumuona binadamu mwenye ngozi nyeusi, hivyo alitumia muda mrefu kumtazama kijana huyo, pindi walipogonganisha macho Joan aliinamisha uso wake, hadi masomo ya asubuhi yanakatika Joan hakuwa ameambulia chochote.
"Nisindikize dukani Joan "
"nahisi tumbo linauma siendi "
"real?(kweli?) ha ha ha ha! Sio tumbo sema unataka kuongea na.... " Nasra aliongea huku akicheka, hakumuamini rafiki yake, maana alimtambua sana.
"Nasra sitaki ujinga bhana "
"hilooooo! Mie najua, lakini.... "Nasra hakumalizia sentesi yake alitoka nje, akimuacha Joan na yule kijana aliekuwa anaonekana mgeni ndani ya shule hiyo.
Alibaki amekaa juu ya kiti chake, huku akimpiga jicho la wizi kijana huyo, dakika mbili alimuona akilia, papo hapo alinyanyuka na kumfuata
"Hey should i sit a while with you (naweza kukaa karibu yako) " aliongea baada ya kufika eneo hilo
"nooo! Just go, no body like me! It time to think my parents ( hapana! Ondoka, hakuna anaenipenda, ni muda wa kuwafikiria wazazi wangu)".
Aliongea kijana huyo huku akiendelea kulia, kilio chake cha kwikwi kilimfanya hata Joan kuanza kulia, huruma dhidi ya kijana huyo iliutesa moyo wake, japo alikuwa mtoto wa miaka nane tu, lakini alijikuta akiumizwa na kijana huyo,
Taratibu aliuzungusha mkono wake begani kwa kijana huyo huku akimpapasa, akimsihi kunyamaza.
"naitwa Joan Mohammed "
"Poul Emanuel" akijibu kijana yule bila kumtazama Joan.
"naomba niwe rafiki yako?"
"Noo! I don't want a friend until i.....
(Hapana! Sihitaji rafiki hadi ni....) "Poul alishindwa kuongea baada ya kuzidisha kilio, papo hapo alinyanyuka na kuanza kukimbia akitoka nje ya darasa hilo, akimuacha Joan
.
Yalikuwa ni zaidi ya maumivu ndani ya mtima wa Joan, hakuamini kama Poul angeweza kuondoka eneo hilo, bila kumsikiliza, japo alikuwa binti mdogo sana, lakini tayari roho ya kupenda ilianza kuiteka hakiri yake! Hakujua hali hiyo ilitoka wapi? Sura ya kijana huyo mwafrika tayari ilikuwa imeubomoa moyo wake mchanga!
"Ooooosh! " Joan alitamka neno hilo huku akisimama, uso wake ulijawa huzuni, lile tabasamu la mwanzo liliyeyuka mithili ya barafu, moyo nao ulianza kuona aibu, angemweleza nini Nasra.
Hakutaka kubaki ndani ya darasa hilo, alitoka mbio hadi nje, aliangaza kulia na kushoto, lakini hakumuona Poul wala kusikia harufu yake.Taratibu alianza kutembea kinyonge huku akilia! Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwa Joan, kulia kisa Poul! Hata yeye aliushangaa moyo wake.
"Joan!!!!!! "
Sauti ya kuitwa ndio iliyoyatibua mawazo yake, aliigeuza Shingo taratibu, huku akiendelea kutoa machozi bila yeye kujielewa . Hakutaka kuitika pindi alipogonganisha macho na Nasra akiwa na Sindy raia wa Nigeria .
"Kwanini unalia? "
Sindy alimuuliza baada ya kumfuata
"that little boy , break my heat ( yule kijana mdogo, kauvunja moyo wangu) "
"who? (yupi)? "
"a black like you, aaaah! I mean new one ( yule mweusi kama wewe, aaah! Namanisha yule mgeni) "
"ooooh! From Tanzania? (oooooh! Anaetoka Tanzania? )"
"that one (huyo huyo) "
Joan alijikuta akiongea bila woga, siku zote alikuwa mtu wa kutoficha kitu,
"nimemuona pale chini ya bebea akilia "
Hata kabla Sindy hajamalizia kuongea Joan alitoka mbio.
Miguu yake ilikoma kukimbia baada ya kumuona Poul amejiinamia, kwa mwendo wa kunyata alianza kumfuata Poul .
"Nisamehe " aliongea huku akiketi pembeni yake
"wewe tena? "
Poul aliongea kwa hasira na kwa sauti ya juu, yenye kutisha, hakutaka kumuona msichana huyo ndani ya mboni zake, hakiri yake haikuwa tayari kuzungumza na mtu.
"Nisamehe kama nimekukwaza kaka " Alizungumza kwa kichina , huku akizidi kumsogelea, macho yake hayakuacha kutoa machozi, ile ngozi yake ya kiarabu ilizidi kuiva zaidi.
"Nimesema toka,"
"naweza kukusaidi tafadhali "
"wewe? "
"Ndio! "
"Walete wazazi Wang "
Joan aliposikia hivyo, ashtuka kidogo, hakujua kwanini Poul aliongea maneno makali kiasi kile, alichokifanya alimrukia na kumbana kifuani kwake huku akimtazama machoni, wote wakitoa machozi , dakika tatu Joan alimuachia na kumuomba akae.
"Naweza nikafahamu kinachokuliza?"
Joan alimuuliza Poul, pindi na yeye alipokaa kando yake,
" Baba yangu na Mama yangu, wote walifariki tarehe kama ya leo,miaka mitano iliyopita, nipo naadhimisha siku hiyo kwa kulia "
"kufariki? "
"Ndio!, kuondoka duniani milele, hawawezi kuja tena, nafikiri kumuua Ukimwi, yeye ndie aliemua Mama "
"pole sana ".
Japo Joan hakuelewa chochote ilibidi akubali tu, papo hapo alianza kumshawishi Poul awe rafiki yake, kutokana na uongeaji wake Poul alijikuta akikubali kuwa rafiki wa Joan hali iliyozidisha furaha ndani ya moyo wake .
"Keho Mama anakuja tutakwenda sote mkoani Anhui "
Alisema Joan huku akimnyanyua Poul chini.
*****
Huangcun ni kijiji kidogo ambacho Kipo ndani ya mji mdogo wa Yi, kusini magharibi kwa mteremko wa mlima Huangcun mkoani Anhui.Mkoa huu unasifika kuwa na vivutio vizuri sana nchini China, wakazi wengi wa nchi hiyo hupenda kuutembelea mji huu, vivutio hivyo pia huwafanya hata watengenezaji wa filamu kufika eneo hilo, umejaliwa madaraja manne yenye hadhi ya juu, milima pamoja na mabonde pia yanapelekea ongezeko la watu.

ITAENDELEA
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 14

Huangcun ni kijiji kidogo ambacho Kipo ndani ya mji mdogo wa Yi, kusini magharibi kwa mteremko wa mlima Huangcun mkoani Anhui.Mkoa huu unasifika kuwa na vivutio vizuri sana nchini China, wakazi wengi wa nchi hiyo hupenda kuutembelea mji huu, vivutio hivyo pia huwafanya hata watengenezaji wa filamu kufika eneo hilo, umejaliwa madaraja manne yenye hadhi ya juu, milima pamoja na mabonde pia yanapelekea ongezeko la watu.
Vivutio vyote hivyo pia hupelekea vyuo na shule mbali mbali kutembelea eneo hilo, kwa lengo la kujifunza,Chungchang ni mojawapo wa shule zinazopenda kupeleka watoto eneo hilo, majira ya joto. Majira hayo huwa ni mazuri sana kwa wazazi wa Joan ambao hupenda kutembelea eneo hilo, wakiwa na binti yao, siku za mwisho wa Wiki na jumatatu humrudisha shuleni, utaratibu huo ulimfanya Joan kukalili siku hizo, hivyo alidhamilia kuondoka na Poul pindi mama yake bi Salma angeweza kufika eneo hilo kesho yake.
Siku hiyo alidamka mapema sana, safari ya kwanza ni kumkumbusha Poul mazungumzo yao ya jana, bahati nzuri alimkuta keshajiandaa akimsubili yeye,
"waooo! Uko tayari? "
"Ndio "
"basi nipe dakika saba nakuja"
Alisema Joan huku akianza kuondoka chumbani kwa Poul kwa mwendo wa haraka, alipitiliza moja kwa moja bafuni ,kisha alilejea na kuvaa, dakika kumi ndizo alizotumia, alitoka akiwa na kibegi mgogoni, huku kamera ndogo akiwa ameining'iniza shingoni, alimpitia Poul safari ya kuelekea getini kumsubili Mama yake ilianza.
Wakiwa wamezama ndani ya mazungumzo gari aina ya Escudo rangi nyeusi ilifunga break, kisha vioo vilifunguliwa, sura ya mwanamke wa kiarabu ilitokeza hali iliyopelekea Joan kutabasamu, alinyanyuka kuliendea gari hilo.
"shikamoo Mama "
"Mar -haba "alitikia mwanamke huyo huku macho yake yakiwa yamemtazama Poul ,roho yake ilimuuma sana kumuona binti yake akiwa amekaa na kijana huyo.
Nani yule? "alimuuliza Joan huku akimsonta Poul, hali iliyopelekea Poul kushituka
"rafiki yangu kipenzi "
"mtu mweusi? "
"Ndio! Nampenda ,na... nataka twende nae Anhui Mama".
Japo mazungumzo hayo yalifanyika kwa lugha ya kiarabu, ambayo Poul alikuwa haielewi vyema, lakini hakiri yake ilianza kufikiri jambo.
"OK mwambie aje twende "
Salma aliongea huku akiachia tabasamu la kubandika, haraka sana alitoa picha iliyokuwa ndani ya mkoba na kuitazama, kisha aliachia tabasamu. Yote hayo yalifanyika bila Joan kuona chochote.
"Kijana yuko hapa, labda mshindwe ninyi " ulikuwa ujumbe mfupi uliotumwa kwa nja ya mesengi
"kweli? "
"Ndio, nilijua uongo "
Basi jiandae namleta.
*****
Hakiri ya David ilikuwa makini sana, kila jambo alilifanya kwa uangalifu kupita maelezo, tayari alimejimilikisha mali zote. Kitu kilichokuwa kimebaki ni kumuangamiza Poul mara moja, lakini hakutaka jambo hilo litokee mapema sana, hivyo anaamua kumpenda kama mwanae na ili kuonesha upendo huo kwa ndugu wote, anaamua kumpeleka China.
Wote wanamuamini hakuna aliekuwa akifahamu lengo lake, baada ya miezi miwili ya Poul kuwa China anatuma watu wakamue, vijana wa kwanza wanajikuta wanakamatwa, anamua kumshilikisha rafiki yake mkubwa Mohammad na muuza madawa mwenzi, wote wanakubaliani.
Wanapanga kumtumia Joan kama chambo, na bahati nzuri wanawakuta wakiwa pamoja, hali inayopelekea ushindi mkubwa kwa David aliekuwa amejificha ndani ya mji mdogo wa Anhui akisubilia Poul aletwe.

Escudo ilizidi kuongeza mwendo, bila hata kusimama popote, hasira alizokuwa nazo mwanamke huyo hazikuelezeka, hakutamani kumuona kabisa Poul akiwa hai! Maumivu aliyokuwa nayo aliyajua mwenyewe, kitu kilichozidi kumuumiza sana ni kitendo cha binti yake Joan kuwa na ukaribu na kijana huyo, kwake lilikuwa ni kosa, tena kosa kubwa sana kwa binti wa kiarabu kushikamana na kijana mweusi!
"kafiri! Kafiriiii! Hafai ha.... "
Aliongea maneno hayo ndani ya moyo wake huku, mkono wake wa kushoto ukipiga piga usukani, aliyauma meno kwa hasira hali iliyopelekea mishipa yake ya shingo kusimama, juba alilokuwa amevaa lilijikuta likianza kulowa kwa jasho, hakika Salma alikuwa katika hali mbaya.
"Mama mbona leo tunapitia huku? "
"Njia hii ni ya mkato "Alijibu Salma bila kugeuza shingo, macho yake yalikuwa makini sana na barabara. Umakini aliokuwa nao aliufahamu mwenyewe, japo alikuwa akiendesha kwa kasi sana.Muda wote huo Poul alikuwa kimya sana, hakujua kwanini alikuwa hivyo! Roho yake ilikuwa ikisita sita, furuha ya mwanzo nayo iliyeyuka mithili ya barafu ndani ya maji moto.
"Kuna hatari mbele yako, ondoka ondoka"ilikuwa ni kama sauti kizungumza ndani ya moyo wake, mwili nao ulianza kupata hali ya woga,
"Jo.. .Joan nataka kushukaaaaaa! "
Alizungumza kwa hali ya woga huku akimtazama msichana huyo mdogo aliekuwa akitabasamu, tabasamu hali iliyopelekea vishimo vyake vya mashavuni kutokezea na kumfanya kuzidi kupendeza sana.
"Kwanini lakini?"
"Sijui ila nataka tu!"Safari hii Poul alisema huku akitafuna vidole vyake baada ya kugonganisha macho yake na Mama Joan kupitia kioo kilichokuwemo ndani ya gari.
"Anhui ni sehemu nzuri sana utaipenda Poul "
"Kweli naomba nishuke, zungumza na Mama!"
"Mie sipendi bhana "
Joan alizungumza kwa Madeko , huku kichwa chake akikilaza mapajani kwa Poul ,mazungumzo hayo na vitendo hivyo vyote vilifanyika bila woga dhidi ya mama Joan , aliekuwa mkimya kwa muda mrefu. Wakiwa wamezama ndani ya mazungumzo, ghafla gari lao lilipitwa na kigari kidogo kwa kasi ya ajabu, hali hiyo haikumsumbua Salma, alizidi kukanyanga mwendo huku akiwa amebakiza kilomita kadhaa kufika eneo hilo la bonde walilokuwa wamekubaliani, ghafla alishangaa ile gari iliyompita ikirudi kwa kasi sana manusuru imugonge.
"mfyyyyyy!"aliachia msonyo mrefu uliowashtua hata watoto wale ,mita chache mbele kile kigari kilitokea tena kwa nyuma, kilimpita kisha kilienda kuziba njia, hali iliyopelekea salma kuanza kupiga honi zisizokuwa na idadi, hakuna alieshuka ndani ya gari hilo, hasira zilanza kumshambulia kwa haraka sana alishuka ndani ya gari hilo na kuanza kupiga hatua, kabla hajalifikia vijana saba wenye siraha , walotokea ndani ya vichaka.
Nusuru Salma ajikojolee kwa woga
"yuko wapi mtoto? "mmoja wa wale vijana aliuliza huku akipiga hatua kumfuata, sura ikiwa imelamba sumu,
"mtoto? "
"mtoto ulienda kumteka shule!"
"Sina" Salma alijibu kwa nyodo, bila kufahamu kama alikuwa akicheza na watu hatari.
"oyaaa, hebu nendeni mkamkague huko "alieonekana kama kiongozi, alitoa amri, hiyo na vijana wake walitekeleza.
"Noooooo! Msimchukue taf.... " Joan alianza kupiga kelele, baada ya kuona Poul amechukuliwa kwa nguvu, hakujua ni akinanani hao, lakini tayari walikuwa wameshamtoa ndani ya gari hilo, wakiacha wameivunja vunja na kamera dogo iliyokuwa ikichukua kila kitu, kitendo kile kilifanya mawasiliano kati ya David na Salma kupotea,
"mnanipeleka wapi? "
"Nyamaza!, ".
Papo hapo waliondoka nae kwa kasi ile ile, bila kuongea chochote, japo Poul alikuwa akilia sana lakini hakuna aliejari kilio chake ,kwao kilionekana kama nyimbo za taarabu za bi kidude. Muda mwingine aliwapiga na vigumi vyake vya kitoto, lakini hakuna aliemjibu chochote, hakuna aliempiga.
"vipi ameelekea wapi?"
"Kaondoka kaelekea kule kule "
"basi saw hakikisheni mnatoka eneo hilo haraka iwezekanavyo "
"poa "
Yalikuwa ni maongezi Kati ya wale vijana na waliomteka Poul, Safari yao ilishia ndani ya kijimgahawa kidogo sana , walimshusha Poul na kuanza kumsukuma kuingia ndani.
"Sikiliza mtoto mzuri "Mwanaume mnene kupita wote pale alianza kuongea kwa kichina, huku mkononi akiwa ameshikilia kileo, sura yake ilitisha sana kila pahali palikuwa na kovu, dhahili alionekana mtu wa hatari sana, lakini kilichomshangaza Poul ni ile sauti yake ya kipole kitu ambacho kilikuwa tofauti na muonekano wake, maneno hayo yalimfanya Poul kuacha kulia.
"Sipendi uteseke mwanangu nakupenda sawa"
"hapana!!!!!!....Hunipendiiii, hunipendi niacheeeeeeniiiiiii "Poul alisema huku akianza kuondoka eneo hilo kwa kukimbia, mbio zake hazikuzaa matunda alijikuta akiangukia mikononi mwa vijana wale waliomrudisha pale pale ,huku akiendelea kupiga kelele za kuomba aachwe,
Unaenda wapi Baba?"
"Niachee niende shule "
Poul alisema huku akiwa bado anaendelea kulia, kilio kisichokuwa na kikomo, kelele zake zilizidi kuwashangaza watu wengi sana, lakini hakuna alimjari.
"Shirafu mpelekeni shule na chukueni na barua hii hakikisheni mnaifikisha pahali husika "mtu yule mneno aliongea hayo huku akiwakabidhi bahasha hiyo.
*******
Mac Donald alikuwa jambazi mkubwa sana ndani ya china, alizaliwa mwaka 1977 nchini Afghanistan katika familia ya watoto kumi na moja yeye akiwa mtoto nje ya ndoa, Baba yake mzee Amir alimpa msichana wa kazi ujauzito huo siku moja baada ya kuzidiwa pombe , papo hapo ujauzito wa Suleiman ulipatikana, japo Mama yake alipata maumivu makali sana, hata muda mwingine aliweza kupiga kelele za kuomba msaada lakini hazikuzaa matunda, kutokana na uwezo wa nyumba hiyo kutoruhusu kupitisha sauti.
Miezi miwili Estar toka nchini Uganda alianza kujihisi ndivyo sivyo, ndipo alipomueleza mzee Amiri aliyelipokea jambo hilo kwa furaha, hakutaka akae hapo alimtafutia chumba, hadi alipojifungua mtoto wa kiume .
Baada ya miezi sita alirudishwa nyumbani kwao kwa kutekwa na kulambishwa madawa ya kulevya huku akimuacha mwanae Suleiman. Siku hiyo hiyo Suleiman alipelekwa nyumbani kwa Baba yake, maisha ya kulelewa na Mama wa kambo yakaanza rasimi katika umri huo! Familia nzima haikumpenda kutokana na muonekano wake, alikuwa mweusi Kama mama yake, huku akichukua nywele na sura kwa baba yake. Suleiman hakuweza kuendelea na masomo yake, mara baada ya kuzidiwa na mateso, alichofanya aliondoka nyumbani hapo na kukimbilia mitaani akiwa na umri wa miaka mitano tu! Maisha ya mtaaani ndio yaliyoanza kumtegeneza upya kwanza alianza kuwa mdokozi na mkorofi sana, ndani ya miaka kumi na mbili Suleiman alichukuliwa na kudi la Mr Donald lililokuwa likijihusisha na uuazaji wa madawa ya Kulevya, aliishi hapo kwa muda wa miaka saba, huku akiwa kashazoea kazi hiyo , baadae aliamua kuligeuka na kumuua Mr Donald ndipo alipoamua kujiita Mac Donald, uwezo wake wa kutumia siraha za moto ulikuwa tishio kubwa sana kwa makundi mengine, muda mwingine aliweza kupambana na serikali ya nchi hiyo.

ITAENDELEA.
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 15

Baba yake, maisha ya kulelewa na Mama wa kambo yakaanza rasimi katika umri huo! Familia nzima haikumpenda kutokana na muonekano wake, alikuwa mweusi Kama mama yake, huku akichukua nywele na sura kwa baba yake. Suleiman hakuweza kuendelea na masomo yake, mara baada ya kuzidiwa na mateso, alichofanya aliondoka nyumbani hapo na kukimbilia mitaani akiwa na umri wa miaka mitano tu! Maisha ya mtaaani ndio yaliyoanza kumtegeneza upya kwanza alianza kuwa mdokozi na mkorofi sana, ndani ya miaka kumi na mbili Suleiman alichukuliwa na kudi la Mr Donald lililokuwa likijihusisha na uuazaji wa madawa ya Kulevya, aliishi hapo kwa muda wa miaka saba, huku akiwa kashazoea kazi hiyo , baadae aliamua kuligeuka na kumuua Mr Donald ndipo alipoamua kujiita Mac Donald, uwezo wake wa kutumia siraha za moto ulikuwa tishio kubwa sana kwa makundi mengine, muda mwingine aliweza kupambana na serikali ya nchi hiyo.
Akiwa na miaka thelathini aliamua kuhamia China ndani ya kijijini cha Anhui mji wa Yi kusini magharibi mwa nchi hiyo, huko alijenga nyumba chini ya aridhi bila mtu yeyote kujua, pia ndani ya himaya yake hiyo aliweka kamera kila pahali, kamera hizo zilikuwa na uwezo wa kunasa maongezi yote ya mji huo ,na kuona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, juu ya nyumba hiyo alitengeneza vijimgahawa na hata hoteli.
Siku moja akiwa ndani ya chumba chake, akifatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea aliweza kuona mipango na maongezi ya David na Mohammed, kwanza alipuuzia lakini baadae alijikuta akivutiwa nao, papo hapo akinyanyuka na kuisogelea television ndogo, iliyokuwa imeunganishwa na mitambo yake. Mac Donald alijikuta akiumia sana kusikia mipago yao ya kutaka kumuangamiza Poul, japo alikuwa hamfahamu na hajui kosa lipi alilifanya mtoto huyo, lakini alijikuta akiingiwa na roho ya huruma, siku zote za ukatili na ujambazi wake hakuwa na tabia ya kuangamiza watoto wadogo, na ili umkosee basi angamiza mdogo!
Alihisi mwili ukitetemeka sana, na kilichomumiza ni kitendo cha wao kukabidhiana picha, papo hapo aliwatuma vijana wake kumkomboa Poul haraka iwezekanavyo, akijikuta akimpenda kupita maelezo.
Baada ya kutekeleza jambo hilo ndipo alipoamua kuandika barua ya kuitaka shule hiyo kutomruhusu Poul kutoka nje, hata kama ingefungwa, alijifanya yeye ndie mzazi wake.
*******
Ilikuwa ni taarifa mbaya sana masikioni mwa David, alihisi mwili ukiwaka moto,kutokana na hasira, hakupenda kumuona Poul akiishi! Maswali mengi yalianza kukigonga kichwa chake,
"nani alienisaliti? "
"Sasa nani? Sote tulikuwepo hapa, na tulikuwa tukifatilia kila kitu ,wewe mwenyewe umeona jinsi mke wangu alivyotekwa na madubwana hao"
Mohammed alizungumza huku akiwa anazunguka zunguka huku na huku, ndani ya jumba hilo, hakika kila mtu alikuwa amechanganyikiwa kupita maelezo, kitendo cha kutekwa kwa Poul muda mfupi na kukatwa kwa masiliano yao kiliumiza sana hakili zao.
"Najua cha kufanya David "
"Kipi? "David aliuliza huku akimtazama machoni Mohammed
"hatutakiwi kukurupuka kwa sasa , yawezekana serikali inakufatilia "
"serikali ipi? "
"Ya China "
"mmmh! Sina uhakika "
"kwanza keti hapa " David alipiga hatu kukiendea kiti kidogo kilochokuemo ndani ya chumba hicho.
"Rafiki, usitumie nguvu, unachotakiwa kutumia hakiri, unaona hii, basi iruhusu ikutatulie hili " aliongea huku akigonga ngonga kichwa chake kwa kidole cha katikati ,cha mkono wake wa kulia, huku macho yakiwa yamemtazama David
"fuuuuuuuh! "Alishusha pumzi ndefu zilizoashilia kuchoka kabisa, siku zote alijua amebakiza kazi rahisi sana kumbe haikuwa hivyo,
"OK nitamtumia hata babu nadhani hatashindwa "
"babu gani? "
"Mganga wa kienyeji "
"Aaaah! Hapa wapo wengi sana, kuna mzee crugchany, yupo hapa "
"basi twende "
Hawakutaka kupoteza muda, walinyanyuka na kuanza Safari hiyo.
Crugchany alikuwa mzee wa miaka sitini, aliishi ndani ya mji wa Yi. Umahili wake katika matumizi ya nguvu za giza ulimfanya aogopekwe kila pahali alipofahamika, hakuna alichokishindwa iwe biashara alikuwa na uwezo wa kuiharibu endapo angependa, ajali za kugushi ndo usiulize, dawa zake nyingi zilikuwa za kutumia nyoka, ama nzi !
Crungchany alikuwa na wake wawili huku mke mkubwa alimuweka kafara pamoja na mtoto wake mkubwa, kutokana na uwezo mkubwa mji wake hawakukauka watu , sio wachina pekee bali hata nchi jirani nazo ziliingiza raia wake kwa mchina huyo.

Hakuna alieweza kuongea na mwenzake, kila mtu alikuwa akiwaza yake , hakiri ya David ilizidi kufanya kazi zaidi na uwezo wake ,muda mwingine alihisi kuwa tahira , alitamani hata wapae na wafike haraka ,lakini haikuwa hivyo, zaidi ya masaa mawili walikuwa njiani.
"Habari za saa hivi!"
"Njema"
"sijui tumemkuta mzee ?"
Mohammed aliuliza huku akichuchumaa karibu na kijana alieonekana mgonjwa wa muda mrefu sana.
"Ha.. Ha... Hayu.. pooo"
Alijibu kwa taabu kutokana na kubana kwa taya zake,
"oooofuuuuu! "David aliachia pumzi ya kuchoka kabisa, aliona kila kitu kilikuwa kimeharibika,
"mbona mkosi kiasi hiki? "
"Si mkosi, rafiki "
"Ila? "
"Changamoto tu, ndogo ndogo, hakuna haja ya kulalamika sana, turudi kwanza kambini, tukatulize hakiri " alisema Mohammed bila wasiwasi wowote, kwake kilionekana kitendo kidogo sana na chepesi bila kijua kama David alikuwa akiumia kiasi gani.
"Poa ila acha niende kwanza shuleni kwao "David alisema huku akianza kuondoka eneo hilo, alihisi miguu inakosa nguvu kutokana hali aliyokuwa nayo.
"Huna haja ya kupaniki David, mzee atarudi "
"nafahamu hilo, lakini nani alieamua kumteka? "
"tutamfahamu tu, ondoa wasiwasi? "Mohammed alisema huku akiendelea kuendesha gari kwa fujo sana, hadi wanafika getini majira ya ya saa kumi na moja, saa za huku hakuna aliemsema na mwenzake .
Walishuka na kuliendea geti, baada ya salamu na mlinzi waliruhusiwa kuingia ndani ya shule hiyo.
"babaaaaaa! Walinichukuaaa huko, watu wanene, babaaaa ni.. nipeleke kwa Bibi " Poul alizungumza mara baada ya kumuona Baba yake mdogo David, aliekuwa akikanyanga ngazi za kuingia ndani ya chumba cha mkuu wa shule, toka arudishwe shuleni hapo hakutaka kuondoka hofisini humo, hofu ilikuwa inaushambulia moyo wake.
Japo Poul alizungumza kwa furaha pindi alipomuona mzazi wake huyo, lakini upande wa David ilikuwa tofauti kabisa, alitamani kumshambulia kwa ngumi themanini za mbavu, japo alimtazama kwa uso wenye tabasamu lakini haikuwa hivyo, juu alijionesha mwema ila ndani alikuwa mbaya sana. Alimshika mkono na kukiendea kiti kilichokuwa mbele ya meza kubwa, aliketi na kutazamanana macho kwa macho na mkuu wa shule, hiyo raia wa kijerumani.
"kwanza Pole sana bwana David" alianza kusema, huku mikono yake ikiendelea kupanga panga vitabu mezani hapo
"nishapoa, vipi ni akinani walidhamilia kumuangamiza kijana huyu? "
"Hatufahamu, ila tunamshikilia Bi Salma Mohammed, raia wa Iran "
"huyo ndio alietaka kumuangamiza mwanangu? " David akijifanya kushangaa sana ,ingali kila kitu alikifahamu na mbaya zaidi Salma alikuwa tayari nje ,
"ila usihofu tutakuwa makini sana "
"nitashukru sana "
Baada ya mazungumzo hayo mafupi David alianga na kuondoka, huku akiwa ameumia sana, siku iliyofuata alianza kufatilia usafiri wa kurudi Tanzania, kwa mambo yaliyomkuta hakutaka tena kuendelea kubaki ndani ya nchi hiyo.
Hadi inakatika miaka saba David hakutaka tena kurudi China kumfuatilia Poul, zaidi ya kutuma pesa kwa ajili ya masomo, upande wa Mac Donald nae hakuwa nyuma kuhakikisha kijana huyo anakuwa salama, salimini, muda mwingine alituma vijana kumtembelea shuleni hapo.
"nitakukumbuka sana Poul "
"mie pia, Joan ila kama nikifauru kwenda kidato cha kwanza tutaenda shule moja "Poul alizungumza huku, akiendelea kusafisha begi lake ,kwa ajili ya safari tarajiwa, japo kila mtu alikuwa na furaha sana kuhitimu masomo ya awali kabla ya kuendelea na ya sekondari, lakini ilikuwa tofauti kwa vijana hao, walizoeana kupita maelezo, walipendana na kushirikiana kwa hali na mali na kila mwanafunzi ndani ya shule hiyo alitamani urafiki wao.
"Unajua nini J! "
"Sijui! Joan alijibu huku akiwa ameendelea kusimama na kujiegemeza kwenye nguzo ya kitanda cha Poul ,sura yake ikipambwa kwa tabasamu,
"Nak... u.... pen..... malizia "
"ha ha ha ha! Comedian boy "Joan aliishia kucheka sana, wakiwa wamenogewa na mazungumzo, kengele ilikongongwa, hivyo wanafunzi wote, waliohitimu walianza kusogea eneo husika kwa ajili ya taarifa muhimu.
Walimu waliwahukuru kisha, walitakiwa wapande basi kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege wa Jinjiang Inna capital Airport ulioko ndani ya wilaya ya Tianzhuzhen Shunyi mjini Beijing .
Wahitimu wote walipiga kelele za shangwe, lakini si Poul wala Joan walionekana wanyonge kupita maelezo, hawakuta kutegana kabisa, kila mtu alianza kutoa chozi, lakini halikusaidia ilikuwa lazima wategane tu! Hadi wanafika ndani ya uwanja huo kilio kilikuwa bado kinaendelea ,,walishuka ndani ya basi hilo wakiwa bado wanyonge, dakika saba walielekea chumba cha kukaguliwa kabla ya kuingia ndani ya ndege zao.
Hapo ndipo huzuni zilipongezeka, zaidi , Joan alimkumbatia Poul kama dakika tano kisha alimuachia na kuanza kuondoka. Hakutaka kumtazama tena, ilikuwa lazima aondoke haraka kuiendea ndege iliyokuwa ikielekea Iran. Hakika ilikuwa siku ya huzuni sana kwao.
Ndege kubwa kutoka shirika la ndege duniani Cathay Pacific la wingereza. Ilionekana ikihangaika kutua ndani ya uwanja wa ndege wa kenya, na baada ya hapo abiria waliokuwa wakielekea Tanzania walibadirisha, kutoka shirika la ndege la kenya (kQ) Kenya Airways ,iliyowaleta moja kwa moja Tanzania.
"Baba hivi Baba yangu alifariki lini? " Poul alimuuliza swali hilo Baba Mdogo wake David usiku wa siku aliyofikia mara baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku.
"Swali ngani hilo? "
"Baba Rebecca, mtoto anataka kufahamu, haki yake kwanini umuzuie "mkewe aliyaingilia mazungumzo hayo
"kama unafahamu muelezee " David alisema maneno hayo huku akinyanyuka na kuondoka sebuleni hapo, hakutaka kabisa kusikia maneno ya Poul
"Pole Poul, Baba alifariki miaka kumi na moja iliyopita ukiwa na miaka mitatu, na mwaka huo huo Mama yako nae alifariki "
"daaa!, Hivi anti nani aliemuua Baba?"
"mmmmmmh! Hapo sielewi mwanangu, ila niliwahi sikia kuwa ni wafanyabiashara wenzie "
"unawafahamu? "
"Hapana! Jaribu kuongea na Baba yako atakueleza "
"ahsante sana anti "
"ondoa hofu, nakupenda kama mwanangu "
Waliendelea kuongea mengi, hasa hasa Poul alimsimulia masaibu aliyoyapata China, upweke wa kukosa wazazi na dhamira yake ya kumtafuta mbaya wake, kwa udi na uvumba! Nayo pia aliigusia ,miezi minne ilikatika huku Poul akiendelea kuchunguza kisa kilichowaua wazazi wake, lakini hakuweza kufanikiwa, ndipo alipoamua kuelekea nchini China kwa masomo ya kidato cha kwanza.
*****
ITAENDELEA
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 16

Waliendelea kuongea mengi, hasa hasa Poul alimsimulia masaibu aliyoyapata China, upweke wa kukosa wazazi na dhamira yake ya kumtafuta mbaya wake, kwa udi na uvumba! Nayo pia aliigusia ,miezi minne ilikatika huku Poul akiendelea kuchunguza kisa kilichowaua wazazi wake, lakini hakuweza kufanikiwa, ndipo alipoamua kuelekea nchini China kwa masomo ya kidato cha kwanza.
*****
"Haiwezekani hadi dakika hii kiumbe huyu aendelee kuwa hai, hamjui ni hatari sana kwangu? "
David aliongea kwa jazba, huku akizungunguka zunguka ndani ya ukumbi wa Tilapia hotel, jijini mwanza, dhahili alionesha kuchanganyikiwa kabisa, maswali na udadisi wa Poul ulianza kumtisha kupita maelezo.
"Boss.. la... lakini ulidai tusimuulie Tanzania, tugoje akifika kenya nd....."
"kenge mkubwa wewe! Hivi unaweza kujitetea kwa ushenzi kiasi hicho? "
"Tusame...... "
"sasa sikieni nawapa masaa 120 , muwe mmemaliza sawa? " David alisema huku mikono yake miwili ikiwa imeshikilia meza kubwa, hali iliyopelekea mgongo wake kuinama kidogo, uso nao ulibadirika na kuiva mithili ya nyanya mkomao! Maneno aliyokuwa akizungumza hayakuwa na utani hata kidogo, Safari hii alikuwa radhi hata kupoteza maisha, lakini si kumuona kijana Poul aliekuwa na miaka kumi na tano sasa, akindelee kuishi! Kumuacha hai lilikuwa kosa kubwa sana kwake, na lingechangia kuhatarisha maisha yake, kudharaulika mbele ya jamii iliyokuwa ikimzunguka, kuindoa heshima kubwa aliyokuwa amejijengea, aibu kubwa kwa mke wake pamoja na mabinti zake wawili.
"Tutafanya hivyo!!!!!! "vijana saba akiwemo na Dk. Eddyson waliitikia kwa pamoja, kisha kikao hicho kifupi kikavunjwa, vijana wale walianza kuwasiliana na wenzao wa Afghanistan,Iran na China, ujumbe huo ulipokelewa kwa shangwe kila pande na walijihakikishia ushindi ndani ya masaa kumi na saba tu! Taarifa zilipomfikia David alifurahi sana, hata kazi zake zilianza kwenda bara-bara.
Usiku huo huo wa saa tano na dakika arabaini na nane, vijana wote walikuwa ndani ya ndege wakielekea China, hawakutaka kupoteza muda mara baada ya kushuka ndani ya uwanja wa Jingiag Inna Capital Airport, baada ya masaa kadhaa walichukua tax iliyowapeleka ndani ya hoteli ya The westin Beijing Chaoyang ,iliyopo katikati ya mji wa Beijing, huko walikuta wenzao tisa wakiwasubili kwa hamu, kikao kidogo cha dakika ishirini na tano kilichukua nafasi yake
"nimepata tetesi leo wanasherehe ya kuwakaribisha wao "
"kweli? "
"ndio! " mwingine aliitikia huku akivuta sigara kupandisha muzuka wa kazi ,
"itakuwa njema sana tutamteka hapo hapo "
"ndo mpango "
wote walitawanyika kuiendea shule hiyo, walisimamisha gari zao kando kabisa na njia ya treni ya umeme , vijana saba walishuka na kuanza kutembea kuelekea usawa wa shule hiyo, kwa kuwa kulikuwa na sherehe ndani ya shule hiyo, ulinzi haukuimarishwa zaidi, hali iliyopelekea vijana hao kuingia kwa urahisi shuleni humo.
"Pisiiiiiiiiii! " jambazi aliekuwa amevalia suti nadhifu alimuita mmoja wa wanafunzi waliokuwa wameketi nyuma kabisa.
"mambo"
"poa! "
"naitwa David Baba mdogo wa Poul yule mwafrika ,nataka nionane nae "
"ooooooh! Unamtaka pacha mwarabu wa Miss Joan? "
"Haswaa! "
"Dakika tatu "
Mwanafunzi huyo aliondoka eneo hilo, na kuelekea mbele, dakika chache alilejea akiwa ameambatana na Poul.
"Mzee anakuitahiji hapo nje "
Hata kabla Poul hajafika vizuri, kijana huyo alimuongelesha ili kumtoa wasiwasi, huku uso wake akiupamba kwa tabasamu nadhifu
"kweli? "
"ndio tuondoke "
"mmmmh! Ujue sikufahamu " Poul alisita kidogo,
"aaaah! Poul, sina nia mbaya, ok kwanini nimeamua kukuita wew na nikawaacha wengine, mie ni mmoja wa mfanyakazi wa Baba yako mwanza "
"aaah! Sawa twende nataka niwahi speache "
Walianza kuondoka kwa mwendo wa haraka sana, huku jambazi huyo akichekelea ushindi huo, hatua chache kutoka ndani ya shule hiyo ghafla ilitokea helkopita iliyoanza kuwashambulia vijana wale, kilikuwa ni kitendo cha kushtukiza na cha haraka sana, hakuna aliekubali kushindwa, walishambuliana huku Poul akianza kukimbia kuelekea ilikokuwa njia ya treni, kimbia hiyo haikumfikisha mbali alijikuta akinasa ndani ya njia hiyo ya treni mara baada ya kuzuiwa na gari hilo lililokuwa likija kwa kasi ya ajabu.


Alihisi mwili wote ukitetemeka kupita maelezo, video iliyokuwa ikionekana ndani ya runinga yake ndogo, iliyokuwa imebandikwa ukutani, ilizidi kumchanganya kupita maelezo, ilikuwa ni lazima afanye kitu tena cha haraka sana! La sivyo maisha ya Poul yangekuwa matatani. Mazungumzo ya vijana wale yalizidi kukibabua kichwa chake, MacDonald alinyanyuka kitandani hapo kwa haraka mithili ya mwendo wa umeme, miguu yake ilisimama mbele na kabati kubwa, aliunyosha mkono wake wa kulia na kuzungusha funguo kuelekea kushoto, ilitoa sauti ya paaa!,sauti iliyoashiria kufunguka funguo hiyo ndogo iliyokuwa imening 'inia pahali hapo.
Alinyosha mkono wake na kutoka na bastola yake aina ya revolver, aipeleka mdomoni na kuibusu, kisha akaiomba
"Rafiki mwema naomba ukamsaidie mtumishi wako "
aliutoa mkono huo, huku akiachia tabasamu hafifu na lenye hasira, aliikangua na kukuta kila kitu kipo sawa, aliushasha mkono wake hadi ubavuni na kuichomeka ndani ya suruali yake, kisha alitoa na zingine tatu, tofauti na hizo.
Akili yake ikamtuma kuyapeleka macho yake ,katika saa yake ya mkononi aina ya quartz, alishituka sana alipongudua kulikuwa na dakika kumi na tano tu mbele! Kuendekea kukaa pale kungeongeza matatizo mengine, pia hakutaka kutuma mtu yeyote ilikuwa lazima aende mwenyewe, kundi la Taliban halikuwa la kutumia vijana wake, alitoka ndani ya chumba hicho kwa mwendo wa haraka sana.
"Hassan!!! "aliita huku akifungua mlango wa stoo, dakika moja Hassan raia wa Iran na mwanajeshi alieasi alisimama mlangoni hapo kishujaa,
"mwambie snake Run awashe helkopita, nawe ondoka na siraha hizi "
"sawa mkuu, "Hassan alitekeleza maagizo hayo, mara moja, alichanganya miguu yake kama mwehu, hata kabla hajafika tayari snake Run alimdaka na kumpoke, kisha alikimbilia usawa kulikokuwa na helkopita hiyo, tayari kichwa chake kilikuwa kimegundua kitu flani, hakutaka maelekezo aliiwasha na kuiweka tayari, sekunde hamsini alimuona MacDonald akija mbio, huku uso ukiwa umejaa sumu, shingoni alining'iniza kiona mbali chake.
"Tuna dakika kumi na mbili tu, je tutafika Beijing? "
"Ndio mkuu! "
Alijibu Snake Run kwa sauti ya kukwaruza kwaruza, huku akiitoa aridhini helkopita hiyo, kutoka mjini Yi hadi Beijing ulikuwa mwendo mrefu kiasi, kwa dakika kumi na mbili ilikuwa kama kichekesho! Lakini MacDonald na vijana wake walitaka kutumia dakika hizo.
"Maulana! Eeeh mwenyezi mungu nisaidie "
Alizungumza maneno hayo, mara baada ya kukitoa kiona mbali (darubini) machoni mwake
"vipi? "
"Kijana anazungumza nao! "Alijibu kwa woga sana, alihisi kuwa tahira kabisa, moyo ulichemka kwa maumivu, huku mapigo ya moyo nayo yakiongezeka kugonga.
"snake naomba uendeshe kwa kasi ya mwisho, kama kufa nianze mie kisha kijana afuatie, lakini si kuona yeye akifariki, tayari na... na.... nao... onaaa.... wanaanza kutokaaaa..... ndani ya shule "
"sawa! "
Alijibu huku akiongeza mwendo, hakika kama ingeweza kutokea hitirafu yeyote, hata mifupa yao isingeonekana! Mwendo wa helkopita hiyo ulitisha, ilikuwa lazima wamkomboe Poul kwa gharama yeyote ile! Japo ilikuwa ikikimbia kwa kasi lakini haikuweza kutoa sauti, hilo lilichangia wao kufikia eneo hilo bila kugundulika.
"Ofuuuuuuu! Punguza kidogo, natakiwa nifanye shambulizi la kushtukiza "
"sawa! "
MacDonald alijifunga kamba ngumu kiunoni kisha alifunga katika moja ya chuma, na kujitupa nje, alitambaaa hadi upande wa nyuma, huku kifaa cha masiliano kikiwa masikioni mwake, sekunde sabini na tatu ndizo walizochelewa lakini waliweza kumuona Poul akiwa na yule kijana wakielekea katika moja ya gari, papo hapo Hassan alitupa bomu juu ya gari walioyokuwa wakimpeleka Poul, hali iliyosababisha vijana wale kushtuka na kuanza kuishambulia helkopita hiyo iliyokuwa ikizikwepa risasi hizo, Poul kuona vile alichanganyikiwa, alichofanya alianza kukimbia akielekea usawa wa njia ya treini lakini alijijuta akinasa. Huku gari moshi hilo likija kwa kasi ya ajabu.
*******
"Boooooooo!!!!!!! "sauti ya gari hilo ilizidi kuongezeka kila sekunde ikimuomba Poul atoke barabarani, lakini haikuwezekana, tayari miguu yake ilikataa kupiga hatua, hangaika hiyo ilipenyeza machoni kwa MacDonald, bila kupoteza muda alijiachia kutoka juu ya helkopita hiyo Kama ndege, na kushuka chini huku miguu yake akiwa ameitandaza, hakufika chini alimpiga teke la nguvu Poul lililomfanya anasuke eneo hilo kiurahisi sana na kuanguka umbali wa mita tano, kisha nae aliruka sarakasi za hewani hadi eneo hilo. Lilikuwa ni tukio la kushangaza sana! Na gumu kutokea, abiria walioshuhudia tukio hilo walibaki wakistajabu, kwani ilikuwa ni sekunde sitini tu Poul angesagwa sangwa na gari hilo, lililokuwa likija kwa kasi ya ajabu.
"Saidiaaa! "
MacDonald alipiga kelele, huku akiendelea kushambuliana na vijana hao hatari, waliokuwa wamempiga risasi mbili za paja na mkono wake wa kushoto, lakini hilo halikuchangia yeye kutulia, Snake aliipeleka helkopita hiyo eneo hilo na kumbemba poul aliekuwa amepoteza fahamu, lakini kabla hajamuingiza ndani ya helkopita hiyo alishangaa kuiona ikiwaka moto ,hapo ndipo hasira za MacDonald zilipozidi kupamba, aliyauma meno yake kwa hasira kisha alianza kutembea kuwafuata, bila kuogopa mvua ya risasi iliyokuwa ikinyesha, kwa mikono yake miwili alianza kurusha mabomu kila sehemu,hali iliyosababisha moto kutanda kila eneo hilo, vijana wale walianza kukimbia na baadhi yao walikuwa wameshapoteza maisha, Katika kimbia hiyo Dk. Eddyson alijikuta akiangukia mkononi mwa Mac Donald baada ya kupigwa risasi ya bega na mguuni.
"Paaaa! Paaaaaaa! "
Makofi mawili ya nguvu alitua juu ya pua yake, hali iliyopelekea damu kuanza kumtoka,
"kenge wa mayai wewe "
Alimtukana kwa lugha ya kiarabu ,huku akimvuta kichwa chini, kuelekea kwenye gari walilokuwa wakitumia vijana hao ,dakika tatu walitoka eneo hilo mara baada ya kusikia ving'ora vya magari ya polisi.
"Snake kimbiza gari hadi wangyan, "
"sawa "
Ilibidi atumie akili ya ziada kuwakwepa polisi wale, Hassan nae aliendelea kumsaidia Poul, huku MacDonald akimsurubu Dk. Eddyson bila kujali kelele zake za maumivu.
Wangyan kilikuwa ni kipori kidogo ila kilisifika uwepo wa wanyama wakali, lakini MacDonald hakujali hilo, mita saba walishuka na kulitelekeza gari hilo kisha walianza kutembea kuingia ndani ya kipori hicho, huku Hassan akiwa amembeba begani Poul, na snake Run akiwa anavuta Dk. Eddyson. Hatua chache walisikia nyayo za watu, walitulia na kuangaza huku na huko, ndipo walipoona vijana watatu wa kichina
"tunaelekea Yi ,ila usafiri wetu umeharibika "aliongea MacDonald baada ya kuwafuata wale vijana ,
"aaah! Hata sie, njooni twende "
MacDonald aliwafuata wenzake kisha Safari Ya kuelekea Yi ikaanza.
****
ITAENDELEA
 
BLOOD DEAL
Author: Teddy
Cont:0655 202 285.
Whatsapp :0756 202 284
KWA MWENYE UHITAJI WA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MWANDISHI KWA NAMBA HIZO JUU.

SEHEMU YA 17

Wangyan kilikuwa ni kipori kidogo ila kilisifika uwepo wa wanyama wakali, lakini MacDonald hakujali hilo, mita saba walishuka na kulitelekeza gari hilo kisha walianza kutembea kuingia ndani ya kipori hicho, huku Hassan akiwa amembeba begani Poul, na snake Run akiwa anavuta Dk. Eddyson. Hatua chache walisikia nyayo za watu, walitulia na kuangaza huku na huko, ndipo walipoona vijana watatu wa kichina
"tunaelekea Yi ,ila usafiri wetu umeharibika "aliongea MacDonald baada ya kuwafuata wale vijana ,
"aaah! Hata sie, njooni twende "
MacDonald aliwafuata wenzake kisha Safari Ya kuelekea Yi ikaanza.
****
"Haiwezekani mzidiwe kiasi kile na watu watatu "
Hamayoun aliongea kwa jazba kupita maelezo, hakuamini kama kweli walikuwa wameshindwa, picha ya tukio zima alikuwa akiifuatilia kupitia mitambo yake, muda mwingine alipiga ngumu kali juu ya meza, achilia mbali kuuma meno yake kwa hasira, hakujua ni maneno yapi angemweleza Boss wake David zaidi ya miaka nane alikuwa mtiifu na mkamilifu, hata kifo cha Emanuel na Juliet ndani ya intercontinental hotel mjini Kabul Afghanistan alihusika, miaka kadhaa iliyopita, ufanisi mzuri wa kazi hiyo alijikuta akitunukiwa heshima ya uongozi ndani ya kundi lao la kimafia, kwa nchi tatu China, Iran na Afghanistan,akishirikiana na rafik yake mkubwa Murtaza .
Yale maneno ya ushindi akiyokuwa amemtamkia David masaa mawili yaliyopita angeyageuzaje ,
"inatakiwa muende Anhui haraka iwezekanavyo, mtu huyu yupo chini ya handaki "
"lakini h.. "
"hakuna cha lakini, just do "
Hawakutaka kupoteza muda safari ya kuelekea kambini kwa MacDonald ilianza,.

MacDonald alizidi kuchanganyikiwa hakujua ni kisa kipi kilipelekea kijana Poul kuendelea kuteswa kwa muda mrefu kiasi hicho ,roho wa huruma alikuwa hamtoki toka siku ya kwanza kumfaham Poul , japo hakumfahamu , wala hakuwahi kuonana nae ana kwa ana ,kwa muda mrefu sana , ,lakini alikuwa akimchukulia zaidi ya rafiki yake .kumteka Dk.Eddyson ilikuwa njia moja wapo ya kumfahamu mbaya wa kijan huyo.
“mleteni huku”
aliongea huku akipandisha ngazi ya nyumba yake , miguu yake ilikoma pindi alipokifikia kiti chake cha kuzunguka ,aliketi huku akiendelea kutweta kwa maumivu ya kupigwa risasi, yaliyochangnyikana na hasira,
“naomba uwe mkweli , kabla sijakipasua kichwa chako , haraka iwezekanavyo”
alizungumza huku macho yake makali yakiutazama uso wa Dk.Eddyson bila kuyapepesa macho, alichokiongea kilikuwa hakina utani kabisa ,
“ni..ni..same…he”
“nini ?”
Aliuliza huku akimugeukia vizuri hakutaka kuongea zaidi ya kumtwanga teke la kichwa lililompeleka chini mara moja , kabla hajaamka alipingwa ngumi ya kichwa ,nayo ilizidi kumpeleka chini zaidi ,kisha alimvuta na kumkalisha huku akimuegemeza nyuma ya meza .
“Boss kijana ameshtuka “ Hassan aliongea akiwa amesima kikakamavu mithili ya mwanajeshi vitani , “ kamlete” bila kuchelewa Hassan aligeuka na kuanza kuondoka kuelekea usawa alikokuwa Poul dakika tatu alilejea akiwa na Poul , alieonekana mnyonge kupita maelezo,
“ mototo mwema keti pale “ MacDonald alisema huku akinyosha kidole chake cha shahada ,kumuonesha Poul sehemu ya kuketi , kwa woga sana Poul aliketi , huku macho yake yakimtazama MacDonald pamoja na Dk.Eddyson , macho yake yalianza kumueleza kitu japo hakufahamu ni kipi hicho ,
“pole sana mwanangu nakupenda “ aliongea huku akimtazama kwa macho yenye huruma sana , kiasi flani Poul alihisi amani ndani ya moyo wake ,macho yake aliyapeleka tena kwa Dk.Eddyson kama dakika mbili alitumia kumtazama , akawa kama kakumbuka kitu
“unamfahamu huyu?”
“hapana !”Poul alijibu huku macho yake yakiendelea kumtazama Dk.Eddyson , bila kuyapepesa “alitumwa kukuua !”
“Nini?”
“Kweli Poul “
DK .Eddyson alijibu kwa haraka sana utazani aliulizwa yeye , aliona bora awe mkweli kuliko kuendelea kupata mateso kiasi hicho “nani alikutuma?"
Ilibidi MacDonald aulize kwa hasira mithili ya simba majeruhi
“Dav…i…..d “,
alijibu kwa wasiwasi baada ya kukutanisha macho na Poul
“ Daavid yu..yupi ?”
“Baba mdogo wakoooooooooo!” Dk. Eddyson alijibu kwa maumivu makali baada ya kuhisi kitu kikali kikiuchoma ubavu wake , tayari Poul alikuwa amepandwa na hasira , hakujali kisu kilichokuepo pahali hapo ,alikitumia kumchania mbavu zake za kushoto , hali iliyopelekea makelele ya maumivu hayo
“kwanini ?, na…….na…………” alishindwa kuongea vizur kutokana na hasira,kadiri alivyozidi kumtazama Dk.Eddyson ndipo hasira yake ilivyozidi kuongezeka , hata MacDonald alimuogopa
“naomba uelezee kisa cha wewe kutaka kuniua !”
“ni…n…nitaku……….eleza …ila nia…hidi hu..toniua taf..adhali “ aliongea kwa taabu sana kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia , ilibidi wampe ahadi hiyo , hivyo Dk.Eddyson alianza kueleza kila kitu alichokifahamu hususiana na David , kila neno alilokuwa akilitoa mdomoni mwake lilikuwa la maumivu moyoni mwa Poul , machozi na kamasi nyepesi nyepesi vyote viliupamba uso wake , hakusita kueleza na chanzo cha kifo cha mama yake , hakika Poul alikuwa katika wakati mugumu sana , alilia kama mt0to mdogo , picha na taswira ya mama yake ilikuwa bado kichwani mwake .
“Nakuua walaa…………….”hakuweza kumalizia sentensi yake baada ya macho yake kunganda mbele ya runinga ndogo iliyokuwa ukutani hapo .
“Hahahaha !” MacDonald aliachia cheko la dharau , pindi alipowaona vijana wa David wakikaribia eneo la kijiji hicho cha Anhui , hakuwa na wasiwasi aliendelea kumsikiliza Dk.Eddyson bila hofu.
Dakika saba alinyanyuka na kuelekea ofisini kwake , huko alitegesha mabomu kila sehemu na kurejea tena kwa Poul aliyekuwa bado akiendelea kulia sana , kilio chake kilizidi pindi alipomtazama Dk.Eddyson ,
“lest in peace (pumzika kwa amani)” maneno hayo yalitoka mdomoni kwa MacDonald huku yakisindikizwa na risasi tatu za kichwa , Dk.Eddyson akawa amefariki, “tuondoke “ papo hapa walinyanyuka na kuanza kukimbia kutoka ndani ya ngome hiyo na kuelekea ngome nyigine,japo Poul alikuwa mvuvi sana kukimbia lakini siku hiyo alijikuta akipata nguvu za kukimbia , hiyo ilisababishwa na hasira dhidi ya baba yake mdogo , roho ya kisasi ilianza kuikambili akili yake .
“panatosha hapa “
“hawawezi fika huku ?” Poul aliuliza kwa wasiwasi sana , hali iliyopelekea MacDonald kuachia tabasamu hafifu na kusema “ nina zaidi ya hekali elfu tatu , ninazomiliki uwezekano wa kunifikia haupo na nakupa dakika kumi utaona kilinachotoke .”
“kweli ?”
“ondoa wasiwasi “ wote wanne waliendelea kubaki eneo hilo huku MacDonald akiendelea kutazama kila kitu kilichokuwa kikiendelea , mkononi alishika rimoti yake ndogo ya kufyatulia mitego yake kilahisi sana ,
“angalia hapa” aliongea huku akimsogezea Poul kiona mbali na kuona kila kitu , kilichokuwa kikiendelea
“sasa nawamaliza kwa sitaili hii” alishika kirimoti hichio na kuifyatua mitego yote vijana wote wa David waliteketea kwa moto , ndani ya kambi yake .
*****
Hali ya Joan ilibadilika ghafla , alihisi moyo wake ukimuuma bila kufahamu chanzo cha yote hayo , ile furaha na raha iliyokuwa imeutanda moyo wake sasa iligeuka na kuwa karaha , hakutaka tena kuendelea kukaa eneo hilo , akili yake ilimtuma kwenda kuongea na Poul ,
“Chunchang Poul yuko wapi “ aliuliza huku akiwa amemkazia macho kijana huyo wa kichina aliekuwa rafiki mkubwa wa Poul toka wakiwa wadogo ,
“hata sijui “
“kweli ?”
“ndio “
Hakutaka kuyaamini maneno ya kijana huyo kirahisi rahisi hivyo , alianza kuzunguka huku na huko , huku akiwauliza watu lakini jibu lilikuwa ni hilo hilo Poul hafahamiki alikokwenda , akiwa katika hali ya kukata tamaa , ghafla shule yao ilivamiwa na askari waliowaamru walimu wote , kufunga kikao hicho mara moja pamoja na kuwaruhusu wanafunzi wote kurejea majumbani , pia tarifa ya kupotea na kutekwa kwa mmoja wa mwanafunzi nayo ilitolewa .Hapo ndipo huzuni kwa Joan ilizidi kuongezeka
“nitamtafuta kwa akili zangu acha nikazungumze na baba nadhani atanisaidi “ Joan aliwaza ndani ya kichwa chake ,akiwa ndani ya ndege ndogo akielekea Iran , masaa kadhaa alishuka ndani ya uwanja mdogo wa nchi hiyo na kuchukuwa tax zilizokuwa zimepaki nje ya uwanja huo , safari ya kuelekea nyumabani ikaanza , huku kichwani akiwa na mzingo wa mawazo .
“mama nahitaji msaada wako ?” Joan alisema mara baada ya kufika nyumani kwao
“siku hizi unavuta bangi ama ?”
“Bangi !Hapana kwani vipi?”
“Kwanza umeingia kwa kasi kama unafukuzwa ,pili salamu hakuna ,na tatu kwanini umetoka shule bila taarifa “ maama yake aliongea kwa jazba sana , huku akiwa amesimama katikati ya subulehiyo ,
“ kunatatizo “
“lipi?”
“Shule imefungwa kwa muda mfupi ,mara baada ya kutokea kwa mapingano kando ya shule , na mwanfunzi mmoja kapotea “ Joan aliongea kwa unyonge sana , pindi alipomkumbuka rafiki yake Poul alihisi kuumwa
“Nasra kapotea ?”
“Bora angepotea yeye “
“kumbe nani?" Mama yake aliuliza kwa hamasa kubwa , maneno ya binti yake yalikuwa yanaendelea kumchanganya zaidi ,
“Poul"
Mzazi huyo hakutaka kuogea chochote ,zaidi ya kumkata jicho la hasira na kuondoka sebuleni hapo , akiwa chumbani alianza kuwasiliana na mume wake , naye alishtuka sana kusikia habari ya kupotea kwa Poul , moja kwa moja aliwasiliana na rafiki yake kipenzi David aliyeyapokea maneno hayo kwa furaha sana .
“Nitaondoka , siwezi ishi bila Poul “ Joan aliwaza peke yake ndani ya chumba chake ,usiku wa siku hiyo ,hadi kunapambazuka hakuwa amepata hata lepe la usingizi.

Homayoun alizidi kuchangnyikiwa zaidi , kila alichokifanya kilionekana kigumu , picha na matukio aliyokuwa akiyaona kupitia kompyuta ndongo ya mezani yalimtisha , alitamani kuwazuia ila alishindwa , kila alipojaribu kupiga simu ilikuwa haitoki kabisa, muda mwingine iliandika, emergency call , hivyo akawa wa kuzunguka zunguka ,huku na huko ndani ya ofisi hiyo kubwa na ya kisasa ,mara arudishe nywele zake ndefu shingoni , achilia mbali kutoa misonyo ya hasira , muda mwingine akidiriki kuiziba komyuta hiyo kwa viganja vyake vya mikono ili tu asiendelee kuliona tukio hilo ,jinsi mitambo ya MacDonald ilivyokuwa imara na bora zaidi uwezekano wa vijana hao kupona uliwa mdogo sana , na mbaya zaidi mitambo hiyo ilikuwa na uwezo wa kukata mawasiliano pindi uingiaapo ndani ya ngome ya MacDonald , hivyo ndivyo ilivyokuwa , baada ya vijana hao saba kuikanyanga ngome hiyo mawasiliano kati yao na Hamoyoun yalipotea .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom