Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,190
- 34,526
SEHEMU YA 1.
Ndege kubwa toka shirika la ndege duniani Qutar ilionekana ikitafuta uelekeo mzuri wa kutua ndani ya uwanja wa kimataifa wa Hamid karzai international airport ndani ya mji wa kabul Afghanistan, kabla ya kutua taratibu ilishusha matairi ya mbele na kisha ya nyuma huku teyari abiria wote ndani ya ndege hiyo wakiwa wamefunga mikanda na kutulia katika viti vyao ,huku wengine wakiomba taratibu mioyoni mwao kumsihi mungu wao awasimamie katika nafasi hiyo iliyokuwa imesalia katika safari yao.
"Tunapenda kuwatakia mapumziko mema na shughuri njema ndani ya nchi ya Afghanistan "
Sauti nyororo ya msichana aliyekadriwa kuwa chini ya miaka ishirini na tano ilisikika ikipenya taratibu ndani ya kila ngoma za masikio ya kila abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo. Lugha hiyo ilizungumzwa kwa kiarabu lakini ilitafasiliwa kwa lugha zaidi ya nne kiswahili, kingereza, kifarasa, na, kichina hali hiyo ilisaidia baadhi ya abilia waliokuwa wangeni na lugha ya kiarabu kuelewa kilichozungumzwa .
Taratibu ilianza kushuka chini kwa Kasi huku tairi zote zikiwa nje teyari kuikanyanga aridhi ya nchi hiyo na kabla ya kusimama ilianza kuseleleka kwa kasi huku ikiendelea kupungunza kasi hiyo kisha ilisimama ,mlango ulifunguliwa huku ngazi ikiwa teyari .
"so tutaonana lini Ema?"
"aaaah!! sijui... "
"stop Ema ndo unataka sema hatutaonana tena ?"
Juliet aliongea kwa madeko sana kana kwamba walikuwa wanafahamiana kwa muda mrefu, yale mazoea mafupi na kufahamiana kwa muda mfupi ndani ya ndege hiyo yalimfanya Juliet kuwa karibu sana na Bwana Emanuel
"tutaongea"alijibu kwa ufupi huku akinyanyuka kitini hapo
"basi nipe contact zako "Safari hii Juliet aliongea kwa madeko zaidi macho akiwa ameyarembua akiyapa hali ya usingizi usingizi ili tu kumkoleza Emanuel, sura yake yenye umbo la yai ikiwa imezawadiwa mashavu meupe na makubwa kiasi yakiwa na vishimo pindi alipocheka ilimfanya azidi kuvutia zaidi.
"+25575620228.."
"ahsante sana "
"usijali"
"Mhhhh! samahani ulisema utakuwa hoteli gani?
"intercontinetal"
"waooo! kumbe upo hapa hapa Kabul, mie naelekea Ghazni"
"vyema zaidi"
Kadri muda ulivyozidi ndivyo maongezi na mazoea yalizidi kuongezeka hali hiyo ilimfanya kila mtu kumuamini mwenzake, kwakuwa ulikuwa wakati wa kutoka ndani ya ndege hiyo ilibidi wakatishe mazungumzo na kufuata taratibu zote zikiwemo za ugongewaji wa passport
"kimepotelea wapi hiki? Emanuel alijiuuliza peke yake akiwa anasukuma kitoroli kilichokuwa na begi Lake dogo pamoja na kifuko kidogo, shingo yake aliipa kazi ya kuzunguka huku na huko kumtafuta Juliet akiwa na lengo la kumuaga kabla ya kuondoka ndani ya uwanja huo
"samahani kaka tunaweza tukachunguza begi lako? "aliongea mmoja wa askari waliokuwa eneo la lango kubwa, kwa lugha ya kingereza
"hakuna shaka angalieni tu! "
Kwa kuwa hakuwa na wasiwasi wowote juu ya mizingo yake aliwapa begi lake huku akiwasaidia kufungua, macho yake yalishituka kidogo baada ya kukutana na nguo tofauti na iliyokuwa imewekwa juu na mkewe
"nini hiki? "
"s... si... jui"
Alijikuta akipata mshituko wa hali ya juu baada ya kutolewa mfuko mkubwa wa rambo rangi nyeusi ukiwa umefungashiwa vitu mithili ya unga
"drugs abuse(madawa ya kulevya) "
Askari aliekuwa akiufungua mfuko huo alijikuta akishituka Sana
"hapana begi hili silo langu! "
"kiaje wakati umekamatwa nalo wewe? " ilibidi askari asimame huku akimsogelea Emmanuel aliekuwa bado akilikagua kagua begi hilo ambalo lilikuwa lake kwa kila kitu kuanzia kimdori kidogo kilichokuwa pembeni alama iliyokuwa ubavuni lakini alichanganyikiwa na mzigo uliokuwemo ndani yake ,kwa macho yake mawili alishuhudia mkewe akipanga nguo moja baada ya nyingine huku yeye akiwa amejilaza pembeni akimtania,
"sasa madawa yameingiaje? "alizidi kuumiza kichwa chake bila kupata jawabu sahihi.
"kuanzia muda huu upo chini ya ulinzi? "alinzungumza askari aliekuwa akifahamika kwa jina la Nurdin , papo hapo alifungwa pingu mikononi na kutolewa nje ya uwanja huo akiwa chini ya ulinzi mkali sana
"lakini sihusiki na mzigo huu "
"hayo hatujui sie wewe subili ukifika pahali sahihi utaongea"
Emanuel alipakizwa ndani ya gari la polisi akiwa haamini tukio hilo ambalo aliliona kama ndoto ya mchana muda mfupi angeshituka, kutoka uwanjani hapo hadi kituo cha polisi hakukuwa na umbali mrefu walijikuta wakitumia dakika saba tu
"shuka"
Taratibu alishuka na kuanza kuelekea ndani ya kituo hicho kilichokuwa kikifahamika kwa jina la muhazrat police station.
"inakuaje raia wa Tanzania unaingia na madawa ya kulevya hapa ili hali nchi yako inasifika kwa amani, utulivu na kila kitu chema? " Asikari polisi aliekuwa amesimama nyuma ya meza kubwa aliongea huku akimtazama machoni, japo alikuwa amevaa miwani lakini macho yake makubwa na mekundu yalionekana dhahili
"si.. hu.. siki... na... tukio hili! "
"acha kudanganya kaka hapa si Tanzania ,tambua uko Afghanistan hatuna tamaa ya rushwa kama asksri wenu wasiotekeleza kazi zao,hebu lete na hiyo passport yako yawezekana umegushi "
Emanuel alimpatia huku akianza kuingiwa na woga, aliijua vyema nchi hiyo, teyari alianza kujihesabu mfungwa mpya nje ya nchi yake hakika aliumia sana, maneno matamu aliyoyapata toka kwa mkewe Janiphar pamoja na kijana wake Mdogo Poul wakiwa uwanja wa ndenge wa mwanza yalimuumiza sana
"Baba utaniletea baskeli ?"
"ndioo baba, tena niache aaaah! masihara hayo ".Alijikuta akikumbuka na kumfanya atoe machozi namna ushahidi ulivyokuwa wazi dhahili gereza lilikuwa halali yake.
Baada ya mahojiano hayo aliamriwa kuvua kila kitu kisha alipelekwa mahabusu.
******
"haloo "
"ndio niambie umefanikisha? "
"aaaah! mie tena ,andaaa pesa yangu tu "
"poa "
Simu ilikatwa huku kila mtu akiwa na furaha ndani ya moyo wake, kiasi cha milioni kumi kwa kazi ndogo kama hiyo kilimfanya dada huyo kucheka na kufurahi, teyari alikuwa tajiri mtoto
"kwanza nanua gari, nguo za kufa mtu watanikoma mwanza hahaha "
Aliongea peke yake akiwa kitandani ndani ya hoteli ya Intercontinetal ghorofa ya kumi na mbili chumba na 231 ,kwa furaha aliyokuwa nayo ilimrazimu kuanza fakamia vinywaji vilivyokuwa ndani ya jokovu ndogo. Ghafla alisikia mlango ukingongwa taratibu alinyanyuka huku mkononi akiwa na chupa ya kileo ,mwili wake mweupe akiufunga taulo lililoishia katikati ya mapaja
"nani? "
"mhudumu "
Jibu hilo lilimfanya afungue haraka bila kuwa na wasiwasi wowote
"shiii! kaa kimya "
Alijikuta akiamriwa baada ya kukutana na watu wawili wakiwa wamevaa mavazi yaliyowaficha sura zao, walimsukumia ndani ya chumba bila kuongea chochote huku mwingine akiwa ameshikilia bastola aina ya m-32
"sikia binti wewe ni mzuri sana kama hutaki kufa tupe penzi "Homayoun aliongea huku akumsogelea karibu kisha alilivuta taulo hali iliyopelekea wote kutoa macho na udenda baada ya kukutana na mwili mweupe ukiwa na ngozi nyororo
"naanza mimi "
"wapi acha nianze mie "
Walianza kubishana kwa lugha ya kiarabu ambayo ilikuwa ngeni masikioni mwa binti huyo aliekuwa akitetemeka Sana
"basi tukose wote paaaaaa! "
Murtaza aliongea huku akiyasindikiza maneno hayo na risasi moja iliyokifyatua vyema kichwa cha binti huyo.
"sasa nini? "
"kazi yetu ilikuwa kuua si vingine tuondoke "
Walitoka kwa tahadhari wakipitia mlango wa nyuma bila kuinewa na mtu yeyote.
"Juliet unatakiwa usafiri hadi Afghanistan na Emanuel hakikisha unakuwa nae karibu sana ili asije shituka kwa lolote sawa? "
"sawa boss vipi malipo yangu lakini tambua kazi ya kwanza hujanipatia " Juliet aliongea huku akinyanyua glass ya bia iliyokuwa mezani ndani ya mwanza hoteli na kuipeleka mdomoni alikunywa fundo moja kisha aliirudisha glass hiyo pahali pake na kumtazama David usoni
"pole Juliet malipo yote nitayaunganisha nitakupa milioni kumi keshi "
David alizungumza huku akimtazama machoni akisindikiza na tabasamu bashasha ili kumteka Juliet alikuwa ameshamjulia udhaifu wake
"sawa so lini ataondoka? "
"kesho na ndege ya saa mbili asubhi na nzuri zaidi nimekukatia kiti kimoja na yeye unatakiwa umchangamkie maana namjua hana tabia ya kuongea ongea "
"hilo niachie mie mmakonde halisi natema checheka kama sijielewi hahaha! "
Juliet aliongea huku akikitikisa kifua chake kilichojaliwa chuchu kubwa kiasi kulingana na mwili wake ,maneno hayo yalizidi kumpa faraja ya ushindi bwana David. Waliongea mengi sana na jambo kubwa kuliko yote lilikuwa ni kumkamata bwana Emanuel msukuma toka wilaya ya Simiyu mkoani shinyanga tajiri kupindukia akiwa chini ya miaka thelathini na tano ,alikuwa akiishi jijini mwanza wilaya ya nyamagana maeneo ya Bugando karibu kabisa na chuo cha udaktari Bugando.
Japo alikuwa tajiri sana hakuwa na moyo wa kichoyo kuanzia nyumbani kwao alikowajengea wazazi wake nyumba ya kisasa kabisa huku wadogo zake wawili mmoja wa kiume aliekuwa hajaoa alimshirikisha katika biashara zake, Dada yake alikuwa bado mwanafunzi ndani ya chuo cha udaktari Bugando.
Katika umri huo alikuwa teyari na familia mke na mtoto mmoja aliefahamika kwa jina la Poul, mkewe aliitwa Janiphar mwenyeji wa mkoa wa Moshi wilaya ya Rombo kijiji cha mashati, kutokana na upendo na uchapakazi kati ya wanandoa hao walijikuta wakifanikiwa sana kila iitwapo leo, utajiri wao haukuishia kuwasaidia wazazi na ndugu pekee bali kila iitwapo jumapili hawakusita kutoa misaada kwa wafungwa ndani ya gereza la Butimba na baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima pia jumamosi hawakusita kusambaza misaada kwa wazee na watoto waliokuwa wakiishi maisha ya mtaani arimarufu kama ombaomba vitendo vyote hivyo vilimfanya apendwe na kila mtu si mkubwa ama mdogo pia jina lake lilikuwa mswaki ndani ya vinywa vya wakazi wa mwanza na mkoani shinyanga.
*****