Blandina Nyoni aula TRA!

Blandina Nyoni aula TRA!

Mnashangaa nini, mbona kwa Tanzania inawezekana kabisa
Kwani huyu ni wa kwanza? mbona wapo wengi tu anafanya madudu huku anapelekwa kwingine,Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo jamani
 
Ndugu unajua usemacho? Unataka tuurudishe mjadala hapa uone?
Mimi utafiti wangu usio rasmi ni kuwa pale kuna "system" ya ulaji ambayo ni ya hatari. Wapo tayari kupokea hata sumu wakidai kuwa ni madawa ili tu wapate pesa. Hivyo akija mtu ambaye anataka kuondoa genge hilo basi wanajiunga kumfanyia cha kumfanyia. Mambo ambayo huyo mama anatuhumiwa nayo yawezekana kabisa ni ya kuchonga ili tu kumpaka matope. mfano hivi sasa ulizia kitu chochote kipya kizuri ni cha nani jibu utalipata haraka sana RITZ1. Hivyo bila uchunguzi na kuwa na system ambayo ni transparent tutaendelea kukupiga ramli tu.

Kuna miungu watu pale ukigusa maslahi yao wanakula nawe sahani moja
 
Nchi hii ina mambo ya ajabu sana,ata ile jamaa iliyochangisha fedha pale nishati na madini kufanikisha bajeti ya Ngereja bado ina swing na government vehicle with a driver! Tusipoing'oa ccm hii nchi itakuwa zaidi ya congo-DRC.
They said 12M sir not 10M, si you know she was not fired? she still enjoys a Governement Car, a Driver, and all that goes with such callings am not sure if she is alone... Someone said 'dhaifu'
 
Mkuu hapo hamna kitu ni mbwembwe tu za magazeti,huyu mama kabla ya kuwa mhasibu mkuu wa Serikali alikuwa mmoja wa makamishna wa TRA.Kilichofanyika ni kumrudisha tu alikotokea,hakuna jipya hapo!

Dah fisi kakabidhiwa bucha kwa awamu nyingine
 
Aliyekuwa Katibu mkuu wizara ya Afya na ustawi wa jamii ambaye alisimamishwa kwa kashfa ya ukiukaji maadili ya viongozi wa umma anadaiwa kulipwa mshahara wa zaidi ya Shilingi Milioni 12 kwa mwezi na Mamlaka ya Mapato Tanzania kama Kamishna.
 
Kwani hapo Afya alifanya nini zaidi ya majungu na mapambano na MAFISADI, yeye akiwa upande wa wananchi. huyu ni kama yule Dr. Masau walipigwa vita kwa sababu alitaka kuiweka wizara ktk right direction basi. Take it from ME.
Tafadhali sana usimkashifu Dr.Masau(RIP) kwa kum-compare na huyo mama
 
Aliyekuwa Katibu mkuu wizara ya Afya na ustawi wa jamii ambaye alisimamishwa kwa kashfa ya ukiukaji maadili ya viongozi wa umma anadaiwa kulipwa mshahara wa zaidi ya Shilingi Milioni 12 kwa mwezi na Mamlaka ya Mapato Tanzania kama Kamishna.

Umepindisha ukweli kidogo........ni kuwa alipotoka TRA alihama na mshahara wake (scale) kwenda nao serikalini......ni kweli bado analipwa(na serikali na sio TRA) kwa mujibu wa sheria kwa kuwa "amesimamishwa" kazi
 
hili jambo kama ni la kweli ni hatari! watu ambao sio waadilifu wanakuwepo kwenye sekta nyeti!!!
nchi hii inahitaji kukombolewa.
 
YES! But i guess aliletwa Afya baada ya kuonekana she's ok! Is she still ok hata baada ya kufanya vibaya Wizara ya Afya? Kama ingekuwa ametoka Afya ktk mazingira ya kawaida, then nisingekuwa na tatizo!
Ubabe ndiyo ulimuondoa wizara ya afya.
Ila anachapa kazi.
 
Aaaa! mwacheni shemegi yangu, Mdogo angu ataendelea kuponda maraha, ndo uzuri wa ma-sugarmummy.
 
Hii ndo ccm bana, wanapofisadi ni mpango wa wengi ni lazima apelekwe kwingine akaendeleze Ufisadi
 
ndio system ya nchi yetu inavyo operate, wateule wachache wataendelea kuwa wateule
 
Kwani hapo Afya alifanya nini zaidi ya majungu na mapambano na MAFISADI, yeye akiwa upande wa wananchi. huyu ni kama yule Dr. Masau walipigwa vita kwa sababu alitaka kuiweka wizara ktk right direction basi. Take it from ME.

Kuna dalili za ukweli hapa mkuu.Kuna mtandao mchafu sana wa kimafia miongoni mwa madaktari bingwa wanaopigana vita kwa akili sana kulinda maslahi yao haramu!Mtandao huu hutumia wanasiasa na wanasiasa huwaamini kwa vile ni wataalam,na hukubali kuidhinisha bila kujua athari za maamuzi yanayolenga maslahi ya kikundi cha hao wachache mf.ni suala la vikwazo vingi kwa THI.Blandina alijaribu kubana fedha nyingi zinazoenda kwenye miradi kama ya malaria ambayo haina tija zaidi ya kufanikiwa kupika takwimu za uongo kuonesha eti malaria imepungua Tanzania wakati kusema kweli kinachoonekana sasa ni usugu wa vimelea vya malaria kwa dawa nyingi zinazotumika hususani dawa mseto!Ni kwa vile yeye Blandina Nyoni hawezi kujilipua hapa na kusema ukweli ulivyo kwa kuwa anazingatia maadili ya uongozi.Suala la yeye kujipa tenda za nguo nk ni sehemu ya ujasilia mali ambao umeruhusiwa baada ya Azimio la Arusha kuwekwa kando!Kama fursa ipo hata ingekuwa mtu mwingine angeweza tu kuitumia.I stand to be corrected!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwani hapo Afya alifanya nini zaidi ya majungu na mapambano na MAFISADI, yeye akiwa upande wa wananchi. huyu ni kama yule Dr. Masau walipigwa vita kwa sababu alitaka kuiweka wizara ktk right direction basi. Take it from ME.

Kuwatetea viongozi wa Tanzania hata kama unawaamini namna gani ni sawa na kuvaa mabomu. Mapungufu aliyoyaonesha akiwa wizara ya afya ni Mengi sana, haki yake ataipata kwa Mungu tuu, sababu ndio anaweza kusaheme na kuanza kukuhesabia haki hapo hapo, kwa sisi wanaadamu, Brandina is another rotten government official.
 
Ina maana hiyo nafasi mpya ilikuwa wazi?
Huyu Mama ni mchapakazi sana,na sio mbaya kama inavyozushwa na watu yote hayo ilikuwa ni kwa wale wavivu na wasiotaka kufuata taratibu,ila kikweli mama ni mfuatiliaji na mweledi mkwa kwa kazi kama afisa masuhuli(Accounting officer)wizara ya Afya haikuwahi kuwa bora na imara kama alipokuwepo.mimi Dakitari palepale wizarani,namfahamu vizuri huyu mama,na kabla ya hapo nilikuwa wizara ya mambo ya ndani!nilimfahamu vizuri akiwa Mhasibu Mkuu wa serikali!Mama ni mweledi kila anapokuwa amekabidhiwa majukumu,nilitamani sana angerejeshwa palepale wizara ya afya kama katibu mkuu,au wizara nyingine kama katibu mkuu.tukiwa na akina mama kama huyu kwa nafasi za kiutendaji hakika nchi ingesonga mbele,chapa kazi mama kazi yako wenye haki wanaiona na Mungu atakujalia.
 
Back
Top Bottom