Kuwatetea viongozi wa Tanzania hata kama unawaamini namna gani ni sawa na kuvaa mabomu. Mapungufu aliyoyaonesha akiwa wizara ya afya ni Mengi sana, haki yake ataipata kwa Mungu tuu, sababu ndio anaweza kusaheme na kuanza kukuhesabia haki hapo hapo, kwa sisi wanaadamu, Brandina is another rotten government official.
Mkuu acha majungu. Ni Blandina aliyefanya hiyo Wizara ijulikane kama Wizara ya Afya ya wananchi wote, kabla ya Blandina ilikuwa Wizara ya watu wateule wachache sana, ata wengi wa madaktari walikuwa hawatii mguu Wizarani, Wizara ilikuwa inatawaliwa na AMO ambao walikuwa na inferiority complex ya hali ya juu. Hawakutaka mtu yeyote aingie kwenye anga zao, walikuwa wamejiundia mirija na safari nyingi ambazo zilikuwa hazina tija wa impact kwa jamii. Ni Blandina Nyoni aliyefanya mabadiriko makubwa mpaka ata wewe sasa unajua kuna kitu kinaitwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Nitakupa mfano amabao utakuwa umekugusa kwa namna moja au nyingine, ni Blandina Nyoni aliyeanzisha utaratibu wa raia yeyote wa nchi hii ata kama akiwa maskini aende nje ya nchi akapatiwe matibabu hapo zamani ilikuwa ndoto leo hii watoto maskini makundi kwa makundi wamepelekwa nje ya nchi kwa matibabu hii ushuuda ninao. Ni Blandina alileta mabadiriko mpaka Muhimbili National Hospital ikawa kama ilivyo sasa (Emergency medicine dept ni mfano mmoja wapo).
Ni blandina aliyethubutu kuwatawanya Madaktari Bingwa waliomaliza masomo yao kwenda Mikoani ili wakatoe huduma za kibingwa katika hospitali za Rufaa Mikoani ili watanzania maskini walioko huko nao wapate huduma. Alidiriki ata kuwachimba mkwara kwamba atayekaidi atamtimua. Hii ndo chanzo na kisa hasa cha matatizo yote yalipoanzia (Migomo), sababu ata Viongozi wa MAT walikubwa na kimbunga hiki cha Blandina.
Mengi yaliosemwa kuhusu Blandina ni majungu tu na yameshajulikana kama ni majungu ya kupikwa tu. Waliopika majungu yale hawana tofauti yeyote na wale walioneza uvumi wa dawa ya Babu wa Loliondo na kudakwa na watu wavivu wa kufikiri hadi kupelekea maelfu ya watu kupoteza maisha. Ata Mhe. Rais alishawahi kusema kuwa "watanzania wana viwanda vya uongo"