Blackberry award 2,000,000 pound | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Blackberry award 2,000,000 pound

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Milindi, Aug 21, 2011.

 1. M

  Milindi JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,213
  Likes Received: 374
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana jamii nimetumiwa sms ifuatayo"RIM-Blackberry has awarded you 2,000,000 Pounds.Email NAME,COUNTRY to:ukblackberry@live.co.uk". from +4915159916575. Ninachokiona hapa ni utapeli.Kama kuna mtu ambaye anaweza kutoa habari na kushauri kuhusu hawa jamaa naomba msaada kama ni matapeli basi jamii nzima ipewe taarifa namna ya kuepukana nao.[SUP][/SUP]
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao ni matapeli na ni wengi sana, ukitaka kuwa report, google Nigeria scam reporting utapata pa kuwa report.
   
 3. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu hapo umekutana na maprofesa(matapeli). Binafsi nina experience na hawa matapeli. Mwaka juzi 2009 ilinitokea kwa kutumiwa email kutoka UK. Niliijibu kwa kutoa details walizohitaji,baada ya siku chache nikapata email kuwa mimi ni mshindi na nimepata euro 950,000.

  Nikapewa maelekezo ya namna ya kuipata zawadi ambapo nilitakiwa kwenda kulipia dola 450 au 350 au 250 kupata zawadi haraka itategemea umetoa dola ngapi. Walitaka nitumie moneywire au moneygram au westernuniun.

  Wakasema malipo ni kwa ajili ya firmchamber law kuwalipa wanasheria. Nikawaambia kateni kwenye zawadi wakagoma! Nikawaambia mie sinashida na zawadi yenye masharti,kama hivyo wampe mwingine. Walikuwa wananisumbua sana kwa kunipigia simu, baada ya hapo nilikuwa nakata kila wakipiga.

  Baada ya kuona response ni negative waliniacha hata email zikawa haziji. Walijidai wanatoka LG electronics. Niliamua kusachi kama kampuni hiyo inashindano la hivyo, nikakuta hakuna nikajua hawa ni mtapeli wa kimataifa. Kwa kuwa umeshajua, nakushauli jaza hizo details ila usiwape account yoyote wala namba ya simu.

  Wakikujibu tujuze kila hatua.
   
 4. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mimi nimepata the same message kutoka namba +60103365897. Kazi kwako.

  Huu ujumbe umekuja kwenye simu nyengine lakini hii line hapo awali ilikuwa kwenye blackberry.
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  hata zama hizi tena poleni.
   
 6. M

  Milindi JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,213
  Likes Received: 374
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana mpaka leo wamenitumia massage hiyo mara nne kwenye namba yangu ya Airtel,Nilichofanya sitajibu na line nimeitoa kwenye simu kwa vile siitumii sana nitaiweka baada ya mwezi mmoja natumaini watakuwa wamekata tamaa.
   
 7. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  jamaa yangu alinifuata jana usiku ananiuliza jinsi ya kufanya malipo na visa card, nikauliza k2 gani wanunua na visa akasema ameshinda £ ml 2 kutoka blackbery nikamuuliza ulishiriki shindano akasema no nikamuliza sasa umeshindaje km hujashiriki akashtuka
   
 8. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  They are ****ing sick con men with cheap minds.
   
 9. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Matapeli hao,hata mie ilinikuta wakijifanya ni kampuni ya microsoft,window live,ili nipate hela yangu pound laki mbili walinitaka nilipe ada euro 500, nitume oceanic bank,nilipogoogle nikagundua bank iko nigeria,duh! Kuona ni nigeria sikujisumba,hao ni matapeli mkuu,umesahau ile ya bongo kuwa umeshinda kenya shngs laki 2 kutoka kenya brwries?
   
Loading...