Black Mamba(Koboko): Nyoka hatari zaidi duniani

G_real

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2019
Messages
684
Points
1,000

G_real

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2019
684 1,000
Watu wengi hufikiri chatu ndio kila kitu kwa kuwa anameza watu; hapana kuna nyoka aitwae koboko huyu ni nyoka mshenzi na mjeuri mno.

Mara nyingi ana rangi ya kijivu na kichwa kidogo, ana uwezo wa kurefuka hata kukupita kimo chako. Ni nyoka mwenye sumu kali ambayo haichukui dakika kumi ndani ya mwili wako inakuwa ishaozesha ini, moyo kushindwa kufanya kazi, inapasua mishipa ya damu na kupelekea kifo ndani ya muda mfupi tu mara baada ya kukugonga.

Inasadikika nyoka huyu ana uwezo wa kugonga ng'ombe sabini kwa wakati mmoja na wale watatu wa mwisho ndio hulewa na sumu hiyo waliobaki wote watakufa.

Nyoka hawa hupatikana sana Tabora vijijini na hupenda kuishi kwenye vichuguu na muda wa usiku wa manane wanawika kama jogoo. Sasa wewe jua kumekucha utoke nje uone kasheshe yake.

Huwa ana tabia ya kuruka hewani na anaspidi ya ajabu ya kukimbia ambayo huwezi kukimbizana nae.

Ikitokea umekutana nae ukiwa na baiskeli ni kheri uitupe na ubaki umesima tu. Uzuri wa koboko huwa hapendi usumbufu, ukimsumbua aiseee atakugonga zaidi ya mara kumi na usithubutu kumshikia fimbo huwezi kumuua kabisa kwani ni mwepesi wa kukwepa na kuruka.

Ukikutana naye wewe simama kama gogo usijitikise kivyovyote vile koboko atakusimamia mbele yako usawa wa kimo chako ina maana wote mtakuwa sawa kiurefu. Mtaangaliana hapo kwa muda na akikuona umetulia tu ataanza kushuka taratiibu huku akikutazama hadi kwenye miguu yako na kuishia zake porini. Hakikisha amepotea kabisa ndio nawe uanze kwenda.

Ikitokea amekugonga sekunde hizo awepo mtaalamu wa kukutibia ipo dawa ya asili ukitibiwa unapona ila kwa sekude hizohizo maana ukipitisha dakika kumi tu wewe ni marehemu na unatakiwa utibiwe eneo hilo hilo usibebwe kupelekwa sehemu nyingine.

Ajabu ni kuwa nyoka huyu pamoja na ukali wote huo anamuogopa sana bundi. Bundi kitoweo anachopendelea kula ni nyoka aina ya koboko ambapo humkamata na kumla bila shida yoyote na ndio maana koboko hupenda kuishi kwenye vichuguu ili kujificha na ndege aina ya bundi yaani akisikia mlio wa bundi hatoki kwenye kichuguu.

Pambana na nyoka wote ila usiombe ukutane na koboko

69474668_2353246001602582_1355027877984206848_n.jpeg
69552731_2369709976621420_2950139368343339008_o.jpeg
 

HFOOO

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Messages
687
Points
1,000

HFOOO

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2018
687 1,000
Hakuna Nyoka anayewika,usidanganye
Mkuu mimi nimezaliwa porini asilimia kubwa ya maisha yangu ni porin hivyo usibishe kuwa nyoka huyo hawiki anawika kama jogoo, ila anaanza kuwika akikomaa na sumu ipo nyingi ndio anaanza kuwika hapo bhana ambiwa jambo jingine ila sio huyo mdudu hafai yaan kitendo cha kumuona tu unaweza kujinyea hafai huyo mdudu
 

lusekelo ephraim

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2014
Messages
263
Points
250

lusekelo ephraim

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2014
263 250
niwajulishe nyoka hatari sana, watu wengi hufikiri chatu ndio kila kitu kwa kuwa anameza watu ni hapana kuna nyoka aitwae koboko huyu ni nyoka mshenzi na mjeuri mno, mala nyingi ana rangi ya kijivu na kichwa kidogo, ana uwezo wa kurefuka hata kukupita kimo chako, ni nyoka mwenye sumu Kali ambayo haichukui dakika kumi ndani ya mwili wako inakuwa ishaozesha ini, moyo kushindwa kufanya kazi, inapasua mishipa ya damu na kupelekea kifo ndani ya muda mfupi tu mala baada ya kukugonga, inasadikika nyoka huyu ana uwezo wa kugonga ng'ombe sabini kwa wakati mmoja na wale watatu wa mwisho ndio hulewa na sumu hiyo waliobaki wote watakufa, nyoka hawa hupatikana sana Tabora vijijini na hupenda kuishi kwenye vichuguu na muda wa usiku wa manane wanawika kama jogoo sasa wewe jua kumekucha utoke nje uone kasheshe yake ,huwa anatabia ya kuruka hewani na anaspidi ya ajabu ya kukimbia kiufupi huwezi kukimbizana nae ikatokea umekutana nae ukiwa na baiskeli ni kheri uitupe na ubaki umesima tu, uzuri wa koboko huwa hapendi usumbufu, ukimsumbua aiseee atakugonga zaidi ya mala kumi na usithubutu kumshikia fimbo huwezi kumuua kabisa kwani ni mwepesi wa kukwepa na kuruka, ukikutana nae we simama kama gogo usijitikise kivyovyote vile koboko atakusimamia mbele yako usawa wa kimo chako ina maana wote mtakuwa sawa kiulefu, mtaangaliana hapo kwa muda akikuona umetulia tu ataanza kushuka taratiibu uku akikutazama hadi kwenye miguu yako na kuishia zake porini hakikisha amepotea kabisa ndio nawe uanze kwenda, ikatokea amekugonga sekunde hizo awepo mtaalamu wa kukutibia ipo dawa ya asili ukitibiwa unapona ila kwa sekude hizohizo maana ukipitisha dakika kumi tu wewe ni marehemu na unatakiwa utibiwe eneo hilo hilo usibebwe kupelekwa sehemu nyingine, ajabu ya nyoka huyu pamoja na ukali wote huo anamuogopa sana bundi nafikiri wote mnamjua ndege aina ya bundi, Bundi kitoweo anachopendelea kula ni nyoka aina ya koboko humkamata na kumla bila shida yoyote na ndio maana koboko hupenda kuishi kwenye vichuguu ili kujificha na ndege aina ya bundi yaani akisikia mlio wa bundi hatoki kwenye kichuguu,
Pambana na nyoka wote ila usiombe ukutane na koboko

View attachment 1198783View attachment 1198784
Huyoapo
 

Forum statistics

Threads 1,367,030
Members 521,607
Posts 33,384,927
Top