Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297
Black-Mamba.jpg

MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).

Kuna aina mbili za mambas :
1. GREEN MAMBAS.
2. BLACK MAMBAS.

Green mamba wanasumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.

BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.

Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'ooki wakti wakigonga kitu. Meno yanayong'ooka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.

Iwapo nyoka huwa wata kung'ata utaweza kuishi kati dakika 20.
maxresdefault.jpg


=========

@Ipycalypse,

Habari wanaJF,

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.

1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.

3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.

PIA Unaweza SOMA: Ni kwanini nyoka aina ya Koboko anaogopeka kuliko Simba na Chui maeneo ya porini? - JamiiForums
 
Hakuna nyoka namwogopa kama black mamba ... Niliwahi shuhudia aking'ata daktari mmoja na kumuua chini ya nusu saa... Usiombe kukutana nae

Ilitokea wapi hiyo na ni lini? Ebu funguka ilikuwaje Dr. akang'atwa na Black mamba? Ilikuwa porini au mazingira ya namna gani?
 
Mmmmhhh aiseee hawa nyoka wanapatikana wapi hasa kwa hapa tz,makazi yao wanaopenda maana ni zaidi ya hatari,tiba ya haraka ya bite?

Kanda ya ziwa na mikoa ya kusini, kwa mikoa ya kusini anaitwa NKOLOWONJI. Ni noma sana huyu jamaa matukio yake nahisi ana IQ kubwa sana hasa timing zake. Ngoja niende google kumjua zaidi
 
Green mambas wanapatikana sana huku kwetu!!!!wqnapenda sana kuishi karibu na maji hasa mito!!mara nyingi sana hupendelea kukaa kwenye miti ya kijani kwa ajili ya mawindo sanasana hupenda kukamata ndege!!!ni vigumu sana kumwona kulingana na rangi yake!!!Usipokuwa makini anaweza hata kukunga 'ata kichwa/shingo!!!!na hukawii kufa!!!!
 
Green mambas wanapatikana sana huku kwetu!!!!wqnapenda sana kuishi karibu na maji hasa mito!!mara nyingi sana hupendelea kukaa kwenye miti ya kijani kwa ajili ya mawindo sanasana hupenda kukamata ndege!!!ni vigumu sana kumwona kulingana na rangi yake!!!Usipokuwa makini anaweza hata kukunga 'ata kichwa/shingo!!!!na hukawii kufa!!!!

Kwenu wap mkuu..?
 
Bucho acha fiksi mwanangu hiyo chai kawauzie simba wa msimbazi labda wataielewa maana hakuna mambas wa hivyo duh...
 
Wakati flani huko Zimbabwe Black Mamba alikua amekaa barabarani , huku akiwa ameachama mdomo, mdomo ulioanzia upana kutoka upande mmoja wa barabara hadi upande wa pili , gari Land-rover 110 likiwa safarini lilipofika hapo alipo nyoka , dreva alidhani kafika kwenye Tunel (njia ya chini kwa chini)
Akailengesha gari domoni mwa nyoka !
Na ndy gari ikawa imemezwa na wasafiri wake wa 5 (watu) haijawahi patikana gari wala watu!
Mwaka wa 10 sasa!

Mwongo mkubwa wewe, black mamba huyu hapa chini anakuangalia na kukushangaa kwa kumsingizia ukubwa asiokuwa nao, yeye ni mdogo tu, urefu wasitani futi 9; uzito wasitani kilo 2, ila ni mmoja kati ya nyoka wenye sumu kali namba 6 duniani, anapandisha hasira sana mara akishachokozwa au kitishiwa, na ni nyoka aendaye spidi kubwa kuliko wote duniani (20 km kwa saa). Huku kwetu mkoani Katavi wanaonekana mara kwa mara, na hawafugiki !!!

black-mamba_767_600x450.jpg
 
koboko ndiyo huyo black mamba .
ana akiri sana
ana kula mti wa bhangi
ana ngata kichwa na shingo tuu
ana sumu kali
ana wika kama jogoo
aja wahi kutembeea kichwA chini yaani siku zote kichwa chake kipo juu kama kasimama vile
ana kwepa mawe
ana ruka kama panzi nk
 
Ilitokea wapi hiyo na ni lini? Ebu funguka ilikuwaje Dr. akang'atwa na Black mamba? Ilikuwa porini au mazingira ya namna gani?


Ilitoke mwaka 2004 sehemu inaitwa gilai karibu na lake natron . Huyu docta alikuwa anaenda kutibu kwenye maboma ya wamasai bahati mbaya gari likaharibika ikabidi ashuke kurekebisha ndio kwa bahati mbaya akakutwa na huyu nyoka... Hawa nyoka wanapenda sehemu zenye joto.
 
Kuna kipindi mtandaoni niliona kua storry ya nyoka mubwa alokuwa akipatikana hukoisr chini ya habar ile ile story ilikaa kama imagneationa flan ivi naombawenye kujua lolote anipe ufham
 
Wakati flani huko Zimbabwe Black Mamba alikua amekaa barabarani , huku akiwa ameachama mdomo, mdomo ulioanzia upana kutoka upande mmoja wa barabara hadi upande wa pili , gari Land-rover 110 likiwa safarini lilipofika hapo alipo nyoka , dreva alidhani kafika kwenye Tunel (njia ya chini kwa chini)
Akailengesha gari domoni mwa nyoka !
Na ndy gari ikawa imemezwa na wasafiri wake wa 5 (watu) haijawahi patikana gari wala watu!
Mwaka wa 10 sasa!

acha we hadithi hii inatufunza nini
 
The feared Black Mamba is found throughout many parts of the African continent. They are known to be highly aggressive, and strike with deadly precision. They are also the fastest land snake in the world, capable of reaching speeds of up to 20km/h. These fearsome snakes can strike up to 12 times in a row. A single bite is capable of killing anywhere from 10-25 adults. The venom is a fast acting neurotoxin. Its bite delivers about 100–120 mg of venom, on average; however, it can deliver up to 400 mg.

If the venom reaches a vein, 0.25 mg/kg is sufficient to kill a human in 50% of cases. The initial symptom of the bite is local pain in the bite area, although not as severe as snakes with hemotoxins. The victim then experiences a tingling sensation in the mouth and extremities, double vision, tunnel vision, severe confusion, fever, excessive salivation (including foaming of the mouth and nose) and pronounced ataxia (lack of muscle control).

If the victim does not receive medical attention, symptoms rapidly progress to severe abdominal pain, nausea and vomiting, pallor, shock, nephrotoxicity, cardio toxicity and paralysis. Eventually, the victim experiences convulsions, respiratory arrest, coma and then death. Without antivenin, the mortality rate is nearly 100%, among the highest of all venomous snakes. Depending on the nature of the bite, death can result at any time between 15 minutes and 3 hours.
 
Back
Top Bottom