Birthday ya CCM Mwanza, Malori yaanza kumiminika

Birthday ya CCM Mwanza, Malori yaanza kumiminika

Habari za uhakika kabisa kutoka kwa kada mbalimbali ndani ya CCM Mwanza zinasema sherehe hizi zilipangwa kufanyika Mza kwa sababu kuu zifuatazo:KWANZA taarifa za ndani kabisa zinadai wenyeviti wale wa mashina walitakiwa kujieleza ni kwanini chama kilipoteza majimbo,kulikuwa na taarifa kuwa nao WAVUE MAGAMBA,baadae waliona chama kitakufa kabisa,hali hii iliongeza mpasuko,sasa kwa "Chakula hiki cha CCM Kirumba"tuwe pamoja na Wanachama.PILI:Kuzindua harakati za kupata kiti cha udiwani cha kata ya Kirumba ambacho diwani wake(CHADEMA) alifariki dunia.Ni moja kati ya kata muhimu sana kwa CCM.TATU:Makovu makubwa yanayotokana na uchaguzi uliopita,wanachama,viongozi na wangineo......UTANI KIDUCHU,Ni kwamba Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wanasema CCM imekuja kujifanyia"HITMA" na kwamba wamekuja kuwapumbaza watu kwa nyama,kuwafanya "Mazuzu"
Source:MWANACCM Aliyeasi-Kirumba

Wanaweka malengo bila kufikiria au wamechoka kufikiria. Inakuwaje wana lengo hilo halafu wanajaza watu kutoka sehemu za mbali ambao si wapiga kura wa kata hiyo?!!!!!!.
 
Kweli CCM hawana chao mwanza,hadi wameamua kwenda vijijini kusomba watu vijijini toka jana mpaka leo nimeshuhudia malori km 200 na vigari vidogo vidogo kibao,kweli hali ni mbaya sana,nimesikia gunia 100 za mchele zimeletwa na lifuso,na ng'ombe km 70 zitachinjwa. My take kwanini hawa watu wameamua kutumia gharama kubwa hiv kwa mambo ya kipuuzi wakati madaktari,walimu kila siku wanagoma na watu wanakufa mahospitalini je haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania?
 
Nashukuru kwa taarifa nitakuwa makini na hawa vibaraka wa ccm kila ninapokuwa kwenye tukio

Hata hivyo hawana lolote kumbe,yaani mimi nina siku tatu nawaendesha na hawajanigundua,nagida tu castle lager zao,jamaa wana mawe aisee yaani mnapiga misele weeeee halafu mnapumzikia bar.ccm oyeeeeeh
 
Hapa Mwanza leo magari ya serikali yamejaa kila sekunde unapishana na maV8 STK inaelekea sherehe za chama zimegeuka kuwa ya serikali gharama inaonekana kubwa sana kwani madc,wakurugenzi,maRC wote wapo wanatanua per diem na madereva wao, wakati madaktari na wagonjwa hoi hii ndio ccm inapotupeleka....
Wanawahi posho hao kusingekuwa na posho wasingeenda magamba ndo walivyo.
 
Nipo eneo la Kiseke PPF,limepita basi la ALLYS likitokea Busweru limepambwa na bendela ya CCM kwa mbele,ndani wamo watu kama 7 hivi. Kila wakiona mtu wanamuuliza kama anaenda CCM kirumba.
 
nipo uwanjani ni peupe cjawai ona! jamaa akiingia ataweza kuanguka kwa presha! wamejaa wasukuma katikati ya uwanja wamesombwa na malori, yasingekuwa malori cjui ingekuwaje! majukwaa yapo waziii, mwanza si petu tena!
 
Nipo eneo la Kiseke PPF,limepita basi la ALLYS likitokea Busweru limepambwa na bendela ya CCM kwa mbele,ndani wamo watu kama 7 hivi. Kila wakiona mtu wanamuuliza kama anaenda CCM kirumba.

na mimi limenipita wakati naelekea uwanjani, peupe jamani uwanjani! hakuna cha chai wala ubwabwa wala nyama!
 
Hapa Mwanza leo magari ya serikali yamejaa kila sekunde unapishana na maV8 STK inaelekea sherehe za chama zimegeuka kuwa ya serikali gharama inaonekana kubwa sana kwani madc,wakurugenzi,maRC wote wapo wanatanua per diem na madereva wao, wakati madaktari na wagonjwa hoi hii ndio ccm inapotupeleka....

sasa ndiyo tuone kama angalau wananchi wa tz wanaweza kuamka hata kidogo
 
Naona kibao kimebadilika tena badala ya Makhilikhili na ubwabwa kuwepo gari linatangaza saa hizi kuwa kwaya ya Ambassadors of Christ toka Kigali watakuwepo:Kwetu pazuuuuuri....
 
Naona kibao kimebadilika tena badala ya Makhilikhili na ubwabwa kuwepo gari linatangaza saa hizi kuwa kwaya ya Ambassadors of Christ toka Kigali watakuwepo:Kwetu pazuuuuuri....

Hahahaha.....CCM kumbe ina dini, wasije wakamkwaza my friend FF na Barubaru, wangeweka ToT plus kwakweli....
 
Wadanganyika sasa tumechoka kilichobaki ni kuwapopoa tu labda masikio yanaweza kufunguka wakasikia vilio vyetu
 
Huenda hata gharama nzima ya besidei ni kodi zetu. Yuck fou CCM.
Kuna kila dalili kuwa hizi ni kodi zetu kwa sababu hawana chanzo chochote cha kiuchumi zaidi ya ruzuku na lijisherehe lenyewe wamelifanya kuwa kubwa mno. Wakajifunze Rwanda waone chama tawala na vitega uchumi vyao. Wao walikula mtaji wote wa lile shirika la chama/ mradi wa SUKITA. Kufika tunapotaka na kuepukana na haya yote yahitaji fikra pevu za maono ya mbali yetu sisi wapiga kura.
 
nina sgh-780 samsung, nimepiga picha lakin kuatach ndo sijui nielekezeni niwape mambo, ila malori yanitaidi kinoma! mpaka sasa sherehe haijaanza! tunasubili pajae
 
Bwana yahya hii taarab ya kila kikicha lawama inayoenda na matangazo ya star tv mbona haiendani na tukio husika?
 
Hivi madaktari bado wanaendelea na mgomo?
madaktari bado wanaendelea na mgomo mkuu, muhimbili,kcmc,bugando,mbeya kote huko hali ni mbaya sana kwa kweli lakini serikali imezishikilia media zisitoe habari za huo mgomo, na kuna taarifa kuwa j3 madaktari bingwa nao wanaweka tools chini coz wameelemewa sana na kazi
 
Back
Top Bottom