Binti yake Raila Odinga aiomba msamaha Tanzania

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,288
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.

''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).

''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.

''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado
Jaguar : Nisemeje,nawaombeni radhi Watanzania.

Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya

'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.

Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo
Jaguar : cha ubinadamu'' alisema bi Odinga

Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)

Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.

Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.

Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.

====================
Good evening! I have just been reminded of an incident which occurred while attending the IYLA conference in New York, 7 months ago. There was a Freudian slip. Apparently, our brothers and sisters from Tanzania are alarmed that I have grabbed their Olduvai Gorge. In Kenya, we equally have a beautiful prehistoric site named Olorgesailie along the way to Magadi. So, poleni sana my Tanzanian brothers and sisters, your Olduvai Gorge is safe. That being said, I would like to share the entire speech. It highlighted my efforts, which mainly focus on bringing people together. Have a fabulous evening and stay blessed


My take: Binafsi naamini bado kuna watanzania wenyewe wanaamini mlima Kilimanjaro Olduvai gorge ziko kenya kwakuwa Serikali ya Tanzania haikuwahi kufanya juhudi zozote kutangaza vivutio vyake ,unlike kenya tunaona matangazo ya kenya airways na jiji la mombasa BBC na CNN, Kenya inatumia uzembe wa Tanzania kujinufaisha na sidhani kama ni kosa kwani kuna mtu yuko tayari afe na njaa ilhali chakula anakiona?

Nguvu inayotumiwa na Watanzania kutangaza vivutio vyenu ni ndogo mnooo ukilinganisha na kenya,soon tutasema mikumi iko kenya, halafu tutaappologize kimyakimya huku tayari ulimwengu ukiamini mikumi iko Kenya.

Nisieleweke vibaya jamani ila soon tukipata platform ya kuaddres kimataifa hatutakata tamaa kusema Mikumi iko Kenya manake najua hizi nafasi Watanzania hawazipatagi sijui kwanini tunazipataga sie tuu

Thank u

falcon mombasa
 
Kuomba msamaha kwenye instagram bado anatudhalilisha sana. Haiwezekani ametamtamka officially alafu anakuja kuomba msamaha rejareja. Alitakiwa kwenye moja ya mikutano kama hii ya east africa aombe msamaha huku baadhi ya hao waandishi wa habari walio kuwepo kwenye mkutano huo wakiwepo
 
Anaomba radhi huku anadhihaki? Arudi kwenye hadhira yake pale aliposemea akanushe siyo kukanusha kwenye mtandao. Makusidi ya wakenya
hadi lini?

Umeona yaani ukisoma kiingereza cha ameongea kinafiki wala hajaomba msamaha. Wakenya wanatuchukulia poa sana hakuna cha brother wala sisters hapa wanafiki wakubwa na siwapendi.


kwa ujumla ni kwamba tamko lake limewekwa kwenye kumbukumnu muhimu za hao wazungu kwamba Oldivai ipo kenya sasa kazi kwetu kikanusha.
 
Umeongea point sana mkuu,badala ya kufanya ya maana ,ccm wako bize kuafuta kalamu za ukawa
Mkuu hiki chama cha mazombie kina deni kubwa mno kwa Mungu, kwanza kabisa kudumaza akili za watu hata wasijielewe Na kuelewa nn kinajiri kibaya ama kizuri, badala yake kila wafanyiwacho kwao ni sawa tu, mapfrofesa, ma injinia, madokta hawajui nafasi zao kazi yao ni kugonga meza tu ili mradi wakuze matumbo yao, wajipendekeze wapate vyeo, Naichukia serikali ya CCM
 
Haya yote yanatokana Na uongozi mbovu wa serikali ya CCM, badala ya kufanya vya maana wako bize Na upinzani, chama na serikali vya ovyo sana kuwahi tokea duniani

Serikali ya CCM sijui imekukosea nini, ameongea bint wa Raila wewe unahamishia ugomvi kwa serikali kwanini usijitwishe mabomu ukamvaa wewe katika platform zingine. Halafu mwenzio ameomba msamaha kwamba alikosea sasa wewe bado unataka kugeuza kichaka kwa stress zako.
 
Umeona yaani ukisoma kiingereza cha ameongea kinafiki wala hajaomba msamaha. Wakenya wanatuchukulia poa sana hakuna cha brother wala sisters hapa wanafiki wakubwa na siwapendi.


kwa ujumla ni kwamba tamko lake limewekwa kwenye kumbukumnu muhimu za hao wazungu kwamba Oldivai ipo kenya sasa kazi kwetu kikanusha.
Yeah Kazi kwetu Na serikali yetu tukufu kuifanya dunia ijue ukweli kuhusu mengi walokwisha jitangazia, ndio tutumie polisi Na jeshi Na pesa pia kujingazia Mali zetu
 
Nadhani TZ tungetayarisha conference nyingine pale New York ya huyu Rose ODINGA aje aombe msamaha kwamba alikosea, au aje ajieleze alifundishwa na na nani kwamba Oldupai Gorge iko Kenya au aeleze kama alitumwa na nchi yake kuitangaza huko nje.

Hii SI mara ya kwanza kwa Wakenya kufanya kitu kama hiki.
Mt. Kilimanjaro wamesema sana kwamba iko Kenya.

Tanzanite gemstone wamepiga mdomo sana kwamba inatoka Kenya na wamepewa award kwa hilo.

Ni sehemu nyingi tu huwa wakipata upenyo wanajitangaza especially kwa TZ na hii ni kwa sababu tumekuwa loose and careless kuhusu chochote kinachotuhusu.

Kwa upande mmoja wako sawa kwa sababu tumekuwa careless na waetumia nafasi.
Ni ushindani wa Kibiashara, sidhani kama tuna hati miliki ya hiyo Oldupai Gorge kiasi kwamba mtu asitaje au haruhusiwi kusema iko wapi.

LA msingi tujitangazee vizuri ili tutambulike na tueleweke so mwisho Wa siku tutafaidika na radilimali zetu.

NB: Watanzania especially Viongozi wa juu muwe makini sana na Wakenya, hawa watu wanatumia akili kama resource yao hawana kingine so ukizubaa wamekupiga.

Kwenye ubinafsishaji Wa mashirika ya uma walifurahi sana wametupiga haswa na wanaendelea kutupiga and they're so happy kwamba hatuna viwanda.
Sisi tumekuwa ndiyo walaji wao wakubwa, so wako tayari kuja kununua kiwanda hapa na kukifanya godown ili kile kiwanda chao kule Kenya kiendelee kusurvive.
Hawana madini ya kuokota, hawana tanzanite ya kuchimba, hawana mlima, hawana gas(labda kama wamegundua juzi) hawana Chuma, hawana ngorongoro crater so wanachofanya ni kuzalisha na kuuza ndani na nje ili kuongeza kipato cha ndani na vilevile kuiba huko nje ili kuingiza pato la ndani.

Viongozi Wa TZ, u have to be smart kidogo mko lazy sana kama watoto kula kulala kwa sababu mmekuta urithi wa kila kitu mezani so hamtaki kufanya kazi
 
Bullshit! She based her next statement on the supposed "Freudian slip". If in fact she had made an honest mistake, when she went onto finish her statement about how all those in the audience were by default Kenyan because supposedly that is where you find the cradle of civilization, she would have realized that she had made a mistake. This was clearly a prepared speech and she would have practiced it prior to delivering it. So either she was grossly misinformed or she unashamedly chose to ignore facts so that she can serve up a cliche.
 
Back
Top Bottom