Binti yake Raila Odinga aiomba msamaha Tanzania

Binti yake Raila Odinga aiomba msamaha Tanzania

Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.

''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).

''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.

''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado
Jaguar : Nisemeje,nawaombeni radhi Watanzania.

Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya

'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.

Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo
Jaguar : cha ubinadamu'' alisema bi Odinga

Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)

Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.

Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.

Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.

====================
Good evening! I have just been reminded of an incident which occurred while attending the IYLA conference in New York, 7 months ago. There was a Freudian slip. Apparently, our brothers and sisters from Tanzania are alarmed that I have grabbed their Olduvai Gorge. In Kenya, we equally have a beautiful prehistoric site named Olorgesailie along the way to Magadi. So, poleni sana my Tanzanian brothers and sisters, your Olduvai Gorge is safe. That being said, I would like to share the entire speech. It highlighted my efforts, which mainly focus on bringing people together. Have a fabulous evening and stay blessed


My take: Binafsi naamini bado kuna watanzania wenyewe wanaamini mlima Kilimanjaro Olduvai gorge ziko kenya kwakuwa Serikali ya Tanzania haikuwahi kufanya juhudi zozote kutangaza vivutio vyake ,unlike kenya tunaona matangazo ya kenya airways na jiji la mombasa BBC na CNN, Kenya inatumia uzembe wa Tanzania kujinufaisha na sidhani kama ni kosa kwani kuna mtu yuko tayari afe na njaa ilhali chakula anakiona?

Nguvu inayotumiwa na Watanzania kutangaza vivutio vyenu ni ndogo mnooo ukilinganisha na kenya,soon tutasema mikumi iko kenya, halafu tutaappologize kimyakimya huku tayari ulimwengu ukiamini mikumi iko Kenya.

Nisieleweke vibaya jamani ila soon tukipata platform ya kuaddres kimataifa hatutakata tamaa kusema Mikumi iko Kenya manake najua hizi nafasi Watanzania hawazipatagi sijui kwanini tunazipataga sie tuu

Thank u

falcon mombasa

Uhuru Kenyatta alijieleza vizuri sana majuzi akiwa Israel; Wakenya ni wataalamu wa wizi! Kenya is bandit economy by CJ Mutunga; Kenya is a man eat man society by JK Nyerere; kwa hiyo wakenya ndivyo mlivyo; manyag'au na majambazi; mnafanya hivyo kwa makusudi kwa sababu ndio hulka yenu; Unyang'anyi.!!
 
We nawe umeongea pumba kabisa,kweli znz hampendi shule nimeamini
Ni kweli nakubali kuwa ZNZ hatupendi shule, ikiwa kufanya hivyo ndio kupata leseni ya kuua wazee na vikongwe wenye macho mekundu, kuua Albino na kuchuna ngozi za binadamu. Kweli na mimi nimeamini kuwa nyie mnapenda shule, hongera !
 
Uhuru Kenyatta alijieleza vizuri sana majuzi akiwa Israel; Wakenya ni wataalamu wa wizi! Kenya is bandit economy by CJ Mutunga; Kenya is a man eat man society by JK Nyerere; kwa hiyo wakenya ndivyo mlivyo; manyag'au na majambazi; mnafanya hivyo kwa makusudi kwa sababu ndio hulka yenu; Unyang'anyi.!!
Ni kweli, kama sisi tunavyotaka kuwanyan'ganya Malawi ziwa Nyasa.
 
Ni kweli, kama sisi tunavyotaka kuwanyan'ganya Malawi ziwa Nyasa.

Malawi waliponzwa na mkataba wa Berlin 1881; The partitioning of Africa; kama tanganyika tumerithi mipaka kama tulivyoikuta; tukianza kuichora upya kutazuka vita vya hatari sana kutokana na haja ya kutetea raslimali kama mito; madini na mbuga nyeti; imagine leo Kenya waseme mlima Kilimanjaro ni wa kwao unategemea nini! Kama watu wako tayari kumsulubu Rosemary Odinga; raia wa kawaida asiye na madaraka ya kiserikali kuhusu Oldupai gorge; unategemea nini; let us leave pi a pi!
 
Ni kweli, kama sisi tunavyotaka kuwanyan'ganya Malawi ziwa Nyasa.
Kuhusu ziwa nyasa unaongea usichokijua, kama ambavyo Fatuma Karume alivyokudanganyeni, Ziwa lile ni haki ya nusu kwa nusu na Tanzania, kazi kubwa imefanywa na wanasheria mpaka kuweza kurejesha usawa, kaka epuka kukariri vitu usivyovijua.
 
Kuhusu ziwa nyasa unaongea usichokijua, kama ambavyo Fatuma Karume alivyokudanganyeni, Ziwa lile ni haki ya nusu kwa nusu na Tanzania, kazi kubwa imefanywa na wanasheria mpaka kuweza kurejesha usawa, kaka epuka kukariri vitu usivyovijua.

That makes two of us; kipofu na kiziwi hakuna wa kumcheka mwenzie! Hata wewe hapa umeonyesha kutokujua chochote kuhusu swala hilo! What can one read katika rejoinder yako hiyo? Umekariri ukasummarize
 
That makes two of us; kipofu na kiziwi hakuna wa kumcheka mwenzie! Hata wewe hapa umeonyesha kutokujua chochote kuhusu swala hilo! What can one read katika rejoinder yako hiyo? Umekariri ukasummarize
Mwanasheria aliyepewa kazi ya kuhakikisha Tanzania inapata haki katika matumizi ya ziwa nyasa ni my best friend. Aliyependekezwa na Benard Membe akiwa waziri wa mambo ya nje. Jamaa kafanya kazi nzuri mpaka sasa hivi Tanzania imefikia hatua nzuri. Huyo jamaa kwa sasa ndiye mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya anga, ni mwanasheria wa kimataifa, anaitwa Hamza Johari, ni mwanasheria na pia ni mtaalam wa masuala ya anga. Kwa hiyo nilichokiandika sio story ya mtaani. Jamaa aliwezeshwa na Kikwete, akapewa kila kilichotakiwa, na report ilishakabidhiwa kwa Kikwete kabla hajaondoka madarakani.
 
Back
Top Bottom