Binti usilie ndo ukubwa huo

Binti usilie ndo ukubwa huo

intro

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
308
Reaction score
328
1.Ni zaidi ya miaka 50 tangu huyu binti avunje ungo.Ulikuwa shamrashamra kwa wazazi sababu binti hao amekua.

2.Ni utamaduni wake kubadili mume kila baada ya miaka 5.Ni utaratibu aliouweka yeye mwenyewe.

3.Binti ana uzuri wa kila namna...Rangi ya dhahabu,maziwa mazuri,milima yake ndo usiseme.

4.Mabwana wakichina na mmarekani walimtaka kwa mda tofauti ili kuutumia uzuri wa mwili wake,cha kusikitishs sasa analiwa mtungo na hao mabwana kwa idhini ya waume zake(wa sasa na waliopita)Huku mabwana wengine(wafaransa,wahindi,waarabu nk) nao wakimmezea mate huyu binti asiyejua kukataa.(neno SITAKI halipo kwenye kamusi yake)

5.Binti kwa sasa ana stress inayotokana na mumewe kugombana na mabwana kutoka kijiji cha pili wanaomuhitaji binti huyu kwa udi na uvumba toka mwaka 1992 tangu itangazwe kuwa mtu toka kijiji chochote unaweza kumuoa binti huyu mrembo.Ila kutokana na ukali wa mume wake wa sasa inaonekana harakati za hao mabwana kumpata huyu binti zinakuwa ngumu.Hao mabwana wataka kufanya maandamano kuonyesha jinsi gani mume wa sasa wa binti anavyowakandamiza katika harakati zao za kumuopoa binti,ndipo binti awaonee huruma na kuwapa mzigo.Ikumbukwe kila mwanaume anaruhusiwa kufanya harakati zake ili kumshawishi huyu binti kwa sharti la kufuata utaratibu uliopo.

Pole sana binti,nitazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akuepesha na mabaya yote.Amen
 
Lugha ya picha mkuu tufafanulie usizue ugomvi na mama zetu
 
Nahisi sio wanawake wanaozungumziwa hapo Ila ni nchi ya Tanzania na maandamano ya ukawa/ ukuta na 1992 ndo mfumo wa vyama vingi ulianzishwa nisaidie intro nipo sahihi ama?
Swadata
 
Tuendelee kumuombea huyu binti.
 
1.Ni zaidi ya miaka 50 tangu huyu binti avunje ungo.Ulikuwa shamrashamra kwa wazazi sababu binti hao amekua.

2.Ni utamaduni wake kubadili mume kila baada ya miaka 5.Ni utaratibu aliouweka yeye mwenyewe.

3.Binti ana uzuri wa kila namna...Rangi ya dhahabu,maziwa mazuri,milima yake ndo usiseme.

4.Mabwana wakichina na mmarekani walimtaka kwa mda tofauti ili kuutumia uzuri wa mwili wake,cha kusikitishs sasa analiwa mtungo na hao mabwana kwa idhini ya waume zake(wa sasa na waliopita)Huku mabwana wengine(wafaransa,wahindi,waarabu nk) nao wakimmezea mate huyu binti asiyejua kukataa.(neno SITAKI halipo kwenye kamusi yake)

5.Binti kwa sasa ana stress inayotokana na mumewe kugombana na mabwana kutoka kijiji cha pili wanaomuhitaji binti huyu kwa udi na uvumba toka mwaka 1992 tangu itangazwe kuwa mtu toka kijiji chochote unaweza kumuoa binti huyu mrembo.Ila kutokana na ukali wa mume wake wa sasa inaonekana harakati za hao mabwana kumpata huyu binti zinakuwa ngumu.Hao mabwana wataka kufanya maandamano kuonyesha jinsi gani mume wa sasa wa binti anavyowakandamiza katika harakati zao za kumuopoa binti,ndipo binti awaonee huruma na kuwapa mzigo.Ikumbukwe kila mwanaume anaruhusiwa kufanya harakati zake ili kumshawishi huyu binti kwa sharti la kufuata utaratibu uliopo.

Pole sana binti,nitazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akuepesha na mabaya yote.Amen
Utaratibu na Sheria ipi iko kwenye maandishi, au tofauti ya hizi lahaja ni ni nini?
 
Miss Tanzania by Solo thang ..... was good song .
 
Wanaume wanamchanganya huyu binti
 
Binti kawa mama na ana mtoto mmoja tu wakike huku akikaribia menopouse. Pole sana binti
 
Back
Top Bottom