Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,253
Ni Binti mdogo mwenye umri wa miaka 23,na mwenye mtoto mmoja Familia hii haina Baba kwani baba yao alishafariki Miaka mingi iliyopita na kijana aliyempa mimba binti alimtelekeza tangu mtoto akiwa ana miezi 6.
Mama wa huyu binti ana umri wa miaka 63 alikuwa mzima kabisa tangu kuzaliwa huku akifanya vibarua vya hapa na pale lakini miaka sita iliyopita ghafla alipata tatizo hili la kupooza viungo vya mwili, ulimi kuwa mzito na hivyo kushindwa kuongea vizuri, pamoja na kuzimia mara kadhaa kila wiki tatizo linalooendelea hadi sasa.
Kutokana na uwezo duni wa hii familia walishindwa kumpeleka Hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi
Binti huyu amepangisha chumba kimoja kidogo akiwa yeye, mtoto wake wa kiume na mama yake huyo huku pembeni kukiwa na Ndoo yenye mfuniko wake ambae mama huyo hutumia kama choo usiku na mchana.
Alfajiri binti hujihimu kuandaa chai kwa ajili ya mama na mtoto wake ambae nae huenda shule na kumfungia mama yake ndani huku ufunguo akiacha kwa jirani hadi mwanae huyo ambae yuko la kwanza atakaporudi mchana na kumpa bibi yake chakula kilichopikwa usiku wa jana yake kwa ajili ya mlo wa mchana, hapo watajifungia ndani wote hadi binti atakaporudi saa moja usiku toka kibaruani.
Mara kadhaa bibi huyo amekuwa akizimia humo ndani na mjukuu huyo humwacha hivyo hivyo hadi fahamu zitakaporejea. Binti hiyo nilipata nafasi ya kumuuliza anagunduaje kama mama yake alizimia mchana na kunijibu kuwa hugundua hilo kutokana na kinyesi kutapakaa kitandani au chini au majeraha atakayomkuta nayo pindi arudipo jioni..
Kama kuna Umuhimu wa kuweka picha ya huyo Bibi mgonjwa basi ntaweka hapa.
Na hata kama kitapatikana wheelchair ♿ kwa ajili ya kumtoa nje wakati wa kuota jua pia itakuwa msaada mkubwa kwenye familia hii.
Wito wangu kwa Serikali iangalie Namna ya kusaidia aina hii ya wagonjwa kwani wapo wengi wanaopitia tabu na inatesa sana familia kwa kuwaletea umaskini na usongo mkubwa wa Mawazo.
Update :
Wengi naona wametaka namba ya binti na kabla sijafanya hivyo niliomba ridhaa ya binti kwanza na Amekubali.
Namba yake hii pia ipo whatsapp unaweza piga video call au picha kwa ajili ya kumuona mamake na huyo binti. 0685 52 86 30