Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 364,964
- 842,610
Mahakama ya Rufani imeamua kuwa baadhi ya mali zilizokuwa zikihusishwa na marehemu Getrude Rwakatare si sehemu ya urithi wake, bali zinamilikiwa kisheria na kampuni ya St Mary’s International Academy Limited.
Katika hukumu iliyotolewa Mei 18, 2026 jijini Dar es Salaam, Mahakama ya Rufani ilibatilisha sehemu ya uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu uliokuwa umejumuisha mali hizo kwenye mgawanyo wa urithi wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto.
Kesi hiyo ilifunguliwa na binti wa marehemu, Kellen Rwakatare, kwa kushirikiana na shule hiyo, wakipinga hatua ya kuingiza mali zinazomilikiwa na kampuni katika mchakato wa urithi.
Majaji wa Mahakama ya Rufani walieleza kuwa kwa mujibu wa sheria za kampuni, warithi wanaweza kurithi hisa za marehemu ndani ya kampuni, lakini hawawezi kurithi moja kwa moja mali zilizosajiliwa kwa jina la kampuni husika.
Mahakama pia ilibaini kuwa mali nyingi zilizokuwa zikibishaniwa zilisajiliwa kihalali chini ya St Mary’s International Academy Limited, hivyo haziwezi kuhesabiwa kama mali binafsi za marehemu.
Hata hivyo, Mahakama imeamua kuwa Kiwanja Na. 701, Block 46, Kijitonyama, kitaendelea kubaki sehemu ya urithi kutokana na kuwepo kwa sintofahamu kuhusu umiliki wake.