James Kasonda
Member
- Apr 2, 2012
- 84
- 49
Zamani sana kabla teknolojia haijasonga kama ilivyo leo, kumtumia mtu salamu ilikuwa kazi kweli kweli. Aidha uandike barua (ambayo itachukua wiki nzima kumfikia mlengwa), au utume salamu kwa njia ya simu ya mezani (wenye nazo walikuwa wachache kweli kweli) au utume salamu kwa njia ya Redio na wakati huo kulikuwa na kituo kimoja tu cha Redio.
Sasa hivi kumtumia mtu salamu hata dakika haipiti. Ninachoshangaa ni kwamba bado kuna watu wanapata tabu sana kutuma sms au kupiga simu kwenye vituo vya Redio eti kutumia salamu rafiki zao. Swali ni kwamba wanataka kutuma salamu kweli au wanataka wasikike tu hewani? Mtu anahangaika saa nzima kutafuta line!! Kwa nini asipige tu simu moja kwa moja kwa hao rafiki zake? Naomba kutoa hoja.