Nadharia isiyokuwa na mashiko.
Mtu akifa mwili wake unabaki hapa duniani na kuoza na Roho yake inakwenda katika kaburi la roho linaloitwa Barzakh, katika kaburi hilo Roho inalala "usingizi" ikisubiri kufufuliwa katika ZAMA (siku) ya akhera, katika siku/zama za akhera roho inafufuliwa kutoka Barzakh kuingia katika ulimwengu wa akhera kama jinsi mtoto anapozaliwa kuingia duniani, huko akhera ni ulimwengu wa Roho ambapo roho zitaachwa zipevuke kabla ya kusimamishwa KIAMA/hukumu kwa ajili ya kuingizwa peponi au motoni au kusamehewa kulingana na matendo ya mtu alipokuwa hapa duniani, pepo ni ya milele na moto ni wa muda fulani kwa ajili ya kuwaadhibu wakosefu na baada ya adhabu kali na ya muda mrefu wakosefu wataingizwa peponi.
Kwa kifupi hiyo ndio falsafa ya kifo na ufufuko.