Binadamu ana tabia ya kugeuza matumizi ya vitu, sio ajabu Chupi akavaa kichwani, Bunduki haikuwa na lengo la kuonea

Binadamu ana tabia ya kugeuza matumizi ya vitu, sio ajabu Chupi akavaa kichwani, Bunduki haikuwa na lengo la kuonea

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,541
Reaction score
916
Binadamu ana tabia ya kugeuza matumizi ya vitu na sijajua hii tabia inatokana na nini

Anaweza hata akavaa chupi kichwani au akajipaka mafuta ya kulainisha break ilimradi tu ageuze matumizi ndipo aridhike

Lengo la kuundwa kwa bunduki halikua kuonea watu bali lilikuwa kujilinda na maadui lakini wale maadui wanaoweza kutoa uhai sio kila adui ni wakupigwa risasi wengine wanachapwa tu fimbo na kurushwa kichura

Nadhani aliko mgunduzi wa bunduki anajuta sana kwasababu ugunduzi wake umeleta madhara makubwa zaidi ya faida

Habari kubwa tuliyonayo duniani ni binadamu kutoana uhai kwa risasi kwenye makosa ambayo yalihitaji tu fimbo na kurushwa kichura
Tukitazama tasnia ya Hip Hop Marekani tunaona idadi kubwa ya Wasanii kupoteza maisha kwa njia ya risasi na mambo mengi chungu nzima tusiyoweza hata kumaliza kutaja endapo tutaanza

Imekuwa ni kawaida ya binadamu kugeuza matumizi anaweza hata kuweka sukari kwenye supu ilimradi aharibu maana ya vitu

Ifike mahali tuache kugeuza matumizi ya vitu kwasababu kama tukiendelea hivi ipo siku tutaweka Petrol kwenye chakula itutoe uhai
 
Silaha ni kitu hatari sana, ukishakuwa nayo kuna kaujeri unakuwa nako haswa kwa mtu ambae hana akili vizuri ndio balaa zaidi.
 
Silaha ni kitu hatari sana, ukishakuwa nayo kuna kaujeri unakuwa nako haswa kwa mtu ambae hana akili vizuri ndio balaa zaidi.
Ewaa hapo ndipo kwenye tatizo
 
Back
Top Bottom