Ila Lema ni mpambanaji haswa, hili balaa la kukwepa kodi itakuwa bahati mbaya tu au wahasibu wake ndio wanahusika sana na wao wamelamba hela nyingi kuliko yeye maana jamaa ni darasa la saba tu elimu ndogo, mwaka juzi alifukuza kazi karibu robo tatu ya wafanyakazi wake maana walikuwa wanamuibia sana, alikuwa na muhasibu anaitwa Ta....mo jamaa alikuwa mwizi sana, ameweza kuwa na yeye na vitega uchumi kadhaa, na alikuwa mchawi kweli dili likishtukiwa watu wanasubiri tu afukuzwe ila jamaa akisafikiri akirudi tu anaitwa ofisini kwa bosi na kupewa kazi ya kuhakiki mradi mpya watu wakawa wamechoka kabisa kumweleza bosi madhaifu ya jamaa. Ila mwisho alitimuliwa tu. Sasa hivi maskini ameajiri wazungu kwenye idara nyeti ili wasimzunguke, na balaa ni balaa tu yamemfika.