Bill Clinton atembelea tena Tanzania

Bill Clinton atembelea tena Tanzania

Kama jangili kuu Kinana ni sehemu ya serikali hatuna ujanja wa kupambana nalo. Acha Clintoni atusaidie maana akina Kinana wakiguswa nchi itayumba
 
Bila shaka ziara hizi viongozi wa US zina salamu maalumu kwa China.Ngoja kwanza wamweke sawa JK.
 
Utawala wa JK utaingia katika historia ya kutembelewa na Marais wawili wa Marekani walioko madarakani na Marais wawili wastaafu wa Marekani. Na pia ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja Tanzania kutembelewa na rais wa Marekani aliyepo madarakani na Marais wawili wastaafu! Hata kama ni gas mbona hawajaenda Msumbiji ambako nako kuna gesi?
 
Utawala wa JK utaingia katika historia ya kutembelewa na Marais wawili wa Marekani walioko madarakani na Marais wawili wastaafu wa Marekani. Na pia ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja Tanzania kutembelewa na rais wa Marekani aliyepo madarakani na Marais wawili wastaafu! Hata kama ni gas mbona hawajaenda Msumbiji ambako nako kuna gesi?

Jiulize why more deeply.
 
hayati mwl nyerere aliwahi kunena hivi: hakuna ukoloni mbaya kama ukoloni mamboleo, ndo huu unaotokea hvi sasa. huwezi kupambana na aina hii ya ukoloni. tukubali matokeo mkuu.....
 
Una akili za Bavicha...


Una Akili za Hao Hapo chini
attachment.php


 
nitajie nchi iliyoendelea kuizidi tanzania hapa africa chini ya jangwa la sahara (ukiondoa south africa). Nitajie ambayo ina siasa nzuri kuliko tanzania (africa nzima) mpaka useme tuna siasa za ovyo!, pinda kusema wapigwe ndio unadhani tumekua ovyo sana? Tembelea nchi zinazokuzunguka halafu fikiria tulikua vipi mwaka 1995 wakati mwinyi anaondoka ndio utajua tunapiga hatua kwa kasi ya ajabu! Fikiria secta zote za elimu, kilimo, afya, barabara, biashara (makampuni yameongezeka je) na usisahau kuhesabu ni watu wangapi wamepanda daraja kutoka kwenye level ya kumiliki baiskeli mpaka kumiliki pikipiki, bajaji na gari. Usifikiri mpaka kuwa kati ya '7 fastest growing economies in the world' ni kubahatisha au kupendelewa. Tulia 2015 usifanye makosa tu, chagua atakae kemea rushwa, atakaeondoa tatizo sugu la umeme (kama litakuwepo bado maana juhudi zilizopo ni kubwa sana) na kuondoa tatizo la maji (safi na taka)

tanzania iko imara, iko vizuri na inaenda pazuri zaidi, ndio maana viongozi weeengi wa nje ya africa wanalala waiota huku watoto wa africa wakitamani wangezaliwa tanzania!

Go my dear tanzania!

umenena vyema mkuu.
 
CLINTON ATUA NCHINI,

Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton yuko nchini kukagua miradi inayofadhiliwa na Plan International, pia kuzungumza na akina mama Vikoba.

IMG_1700.jpg

Rais Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton ambaye yuko nchini kwa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na taasisi yake ya Clinton Foundation katika nchi kadhaa za Afrika

================
Akiwa Vingunguti:
================

RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI BILL CLINTON AFANYA ZIARA YA KUKITEMBELEA KIKUNDI CHA UPENDO HISA GROUP CHA JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akizungumza na wanachama wa Upendo Hisa Group alipotembelea kikundi hicho kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Miradi wa Shirika la kimataifa la Plan International Bw Paul Lusato na Catherine French Mkuu wa wafanyakazi ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Barclays.
Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton pia alitembelea moja ya saluni ya kutengenezea nywele ya Bi Zainabu Rashidi (kulia) ambaye ni mmoja wa wanakikundi cha Upendo Hisa Group cha Vingunguti Mtambani, DSM.
Baadhi ya wakazi wa Vingunguti Mtambani wakimsubili Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton (hayupo pichani).

Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akitembelea baadhi ya mitaa ya Vingunguti kwa Mtambani jijini Dar es Salaam.



Karibu nyumbani
 
Back
Top Bottom