Bilioni 44.8 kujenga chuo cha kimataifa cha reli mkoani Tabora

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Serikali ya Tanzania imesema imetenga Shilingi Bilion 44.8, kwa ajili ya kuanza Ujenzi Chuo kikubwa cha Reli mkoani Tabora chenye kiwango cha Kimataifa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Kupitia kipande cha Tabora-Isaka.

Taarifa hiyo imetolewa mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Bi, Amina Lumuli ambapo ameeleza chuo hicho kinatarajia kujengwa katika eneo la Malabi lenye ukubwa wa ekari 183.1. Kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora.
 
Chuo cha reli Moro kina 'shared facilities' na chuo cha ualimu Kigurunyembe kama vile viwanja vya michezo. Pia kuna karakana kubwa ya reli ambapo wanafunzi wangeweza kupata mafunzo kwa vitendo.
Siungi mkono hoja ya kujenga chuo kipya Tabora.
 
Kwamba kwa sababu kina-share facility ndio maana huungi mkono, hebu fikiri vizuri zaidi impact yake kwa mkoa wa Tabora na Taifa, usiwe selfish kiasi hicho
 
Serikali ya Tanzania imesema imetenga Shilingi Bilion 44.8, kwa ajili ya kuanza Ujenzi Chuo kikubwa cha Reli mkoani Tabora chenye kiwango cha Kimataifa kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Kupitia kipande cha Tabora-Isaka.

Taarifa hiyo imetolewa mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Bi, Amina Lumuli ambapo ameeleza chuo hicgo kinatarajia kujengwa katika eneo la Malabi lenye ukubwa wa ekari 183.1. Kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora
Hapa ndipo akili zetu sisi waafrika tunapoamua kuziweka mahala.

Chuo kipo Morogoro kwanini kisiboreshwe na kupanuliwa ili kiwe cha kimataifa?
 
Hapo haijakaa poa. Hapo ingekuwa ni upanuzi wa chuo cha usafirishaji. Hapo pawe ni tawi la Tabora. Linaloshighulika na usafiri wa reli na taaluma zake.
 
Sasa naelewa kuwa kumbe umefunikwa fikra na zama za kimapokeo, basi sasa UDOM tutahamishia Moro, UDSM na SAUT tutahamishia Moro, au unasemaje?
The statement is simple and clear. Morogoro is railway and railway is Morogoro. atakayetenganfanisha Morogoro na reli, azikwe kama mzoga (bila heshima)... Nimemaliza sitaki kibishana... Moro is rail and rail is Moro.
 
Back
Top Bottom