Bilioni 14 kuhamisha Gereza la Kilimo Mbeya kupisha uchimbaji wa madini ya Niobium

Tumpe Lowassa na Mbowe wasimamie !
Ili kuwawezesha hao wapate nafasi ya kuzisimamia mali za watanzania ni kuwapa kura za kutosha wapinzani ili washike dola na ccm iwe sasa ni mkosoaji
 
Nchi hii tatizo wala sio ccm tatizo ni IQ ndogo, kwa mfano kila mwananchi/mwanasiasa utasukia anasema nchi hii ni tajiri sana huku akiorothesha utajiri tulionao, hakuna anayesema atatumia strategy gani kumaximize returns kutoka kwenye huo utajiri ghafi. PPP strategy kwenye natural resources ingesaidia sana, badala ya tax strategy ambayo multinationals walishajenga mikakati ya kuikwepa from day one.
Nchi hii ni tajiri sanaaaaaaa
 
Tanzania imebarikiwa kila mahali,JPM anazo resources za kutosha kuhakikisha kila anachokusudia kinafanyika.

hii Niobium bei yake ni nzuri sana katika soko la dunia na inapatikana Brazili na Canada tu.
kilo moja ya Niobium (FeNb) inauzwa $40

hizo tani millioni 96.3 tulizopata zina average grade of 0.52% Nb2O5. kwa hiyo ni kama tani million 0.5 za pure Nb2O5 ni sawa na kilo billion 0.5 kwa hiyo thamani ya madini hayo huko Mbeya ni sawa na $20bn!
USD $20,000,000,000 x TZS 2180 = TZS 43,600,000,000,000

Trillioni 43.6 za kitanzania.
 
kwanini haikuhama mpaka leo kila kitu kina maslahi yake ukute kwanza tyr kuna underground ways
Kama wajenzi(waashi) walikuwa Wajerumani, na Wajerumani ni watu wa kuficha sana mambo yao, huenda kukawa na underground ways(sina huakika).Na maeneo iliyopo ni ya kimkakati (Strategic) ili kuwapa wepesi wakati wa dharura.
 
Hii nchi sijui tumelogwa, hivi kama tutaruhusu kila madini yachimbwe bila ku engage bongo zetu sawa sawa mwisho si ndio tutakuwa hatuna chochote kabisa? Sasa rasilimali zilizokuwa explored zote zinauzwa halafu tunadai Tanzania iwe ya viwanda kweli? Hivyo viwanda vitatumia raw materials gani si ndio mwanzo wa kuanza kuagiza raw materials Australia ili tuzalishie mali hapa nchini?
Nasubiri kumsikia bw.Sospass mliar akifunguka kuwa tuna asilimia 0.5% katika hizo usd20 billion kama faida ya kuuza madini hayo
 
Nchi hii ni tajiri sana tatizo ni CCM.
Utajiri wa Tanzania

1. mbuga za wanyama
2. Bahari na maziwa m
Makuu matatu. (bandari na uvuvi)
3. Madini ya Tanzanite.
4. Madini ya dhahabu.
5. Madini ya almasi.
6. Madini ya uranium.
7. Gesi
8. Madini ya helium
9. Madini ya niobium.
10. Madini ya vito (gemstones)
11. Raslimali watu(human resources)
12. Ardhi yenye rutuba.

Matatizo ya Tanzania

1. Siasa chafu (siasa uchwara)
2. Uongozi mbovu
3. Rushwa
4. Ufisadi
5. Unafiki
6. Woga.
7. Elimu
8. Maradhi
9.umaskini.
 
Utajiri wa Tanzania

1. mbuga za wanyama
2. Bahari na maziwa m
Makuu matatu. (bandari na uvuvi)
3. Madini ya Tanzanite.
4. Madini ya dhahabu.
5. Madini ya almasi.
6. Madini ya uranium.
7. Gesi
8. Madini ya helium
9. Madini ya niobium.
10. Madini ya vito (gemstones)
11. Raslimali watu(human resources)
12. Ardhi yenye rutuba.

Matatizo ya Tanzania

1. Siasa chafu (siasa uchwara)
2. Uongozi mbovu
3. Rushwa
4. Ufisadi
5. Unafiki
6. Woga.
7. Elimu
8. Maradhi
9.umaskini.
Na kikubwa hapa ni kuongzwa na ccm kwa kipindi kirefu
 
nchii hii tajir sana bado yale ya bonde la ufa.tatizo ni viongozi tuu kusimamia hizo rasilimali utakuta hapo tunafaidika na %5 tuu
 
Back
Top Bottom