Bilioni 14 kuhamisha Gereza la Kilimo Mbeya kupisha uchimbaji wa madini ya Niobium

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Gereza la kilimo la songwe lililoko mjini Mbeya litahamishwa ili kupisha uchimbaji wa madini ya Niobium yaliyopo eneo hilo.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa jana na mwakilishi wa kampuni ya panda hill, inayotarajia kuchimba madini hayo Bw. Emmanuel Kisasi.

Kisasi alisema kwamba watahamisha pia nyumba za wafanyakazi wa gereza hilo, alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Kwa kuwa eneo lilipo gereza hilo kuna madini kampuni yetu ya Panda Hill imetenga shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kuhamisha gereza hilo,ikiwa na pamoja na nyumba za wafanyakazi kwa umbali wa kilometa tano.

Sambamba na hilo zaidi ya wananchi 467 waliopo maeneo ya mgodi wanatarajia kunufaika kwa kupata ajira mara tu uchimbaji utakapoanza mwaka 2017

Madini hayo tunatarajia kuyachimba yatatumika kutengeneza vitu chuma, kulainisha chuma na kuwa imara zaidi pia yatatumika kwenye ujenzi wa nyumba.

Pia yatatumika vifaa vya ndege, mabomba ya mafuta, mabomba ya gesi lensi za kamera pamoja na vifaa vya kompyuta, kwahivyo tafiti tumegundua tani milioni 96.3 za madini hayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 30 alisema Kisasi.
6a44ceda44a9614da43d828920fb902b.jpg


Chanzo : Mtanzania
 
Tanzania imebarikiwa kila mahali,JPM anazo resources za kutosha kuhakikisha kila anachokusudia kinafanyika.

hii Niobium bei yake ni nzuri sana katika soko la dunia na inapatikana Brazili na Canada tu.
kilo moja ya Niobium (FeNb) inauzwa $40

hizo tani millioni 96.3 tulizopata zina average grade of 0.52% Nb2O5. kwa hiyo ni kama tani million 0.5 za pure Nb2O5 ni sawa na kilo billion 0.5 kwa hiyo thamani ya madini hayo huko Mbeya ni sawa na $20bn!
 
Angalizo: Makengeza na yule advocates aliedakwa na tra juzi & Co wasipewe consultant ktk maandalizi ya mkataba huo. Tutalia!
 
Tanzania imebarikiwa kila mahali,JPM anazo resources za kutosha kuhakikisha kila anachokusudia kinafanyika.

hii Niobium bei yake ni nzuri sana katika soko la dunia na inapatikana Brazili na Canada tu.
kilo moja ya Niobium (FeNb) inauzwa $40

hizo tani millioni 96.3 tulizopata zina average grade of 0.52% Nb2O5. kwa hiyo ni kama tani million 0.5 za pure Nb2O5 ni sawa na kilo billion 0.5 kwa hiyo thamani ya madini hayo huko Mbeya ni sawa na $20bn!

....good analysis!, though i doubt kama yatawanufaisha wakazi wa eneo la mgodi!.
 
Nimeanza kuamini maneno ya mdau mmoja kuwa nyerere kipindi cha ukoloni sehemu zilizokuwa na madini jamaa aliweka makambi ya majeshi, magereza, ofisi za serikali pana shaka hata pale magogoni kuna vitu wanavyopendaga wadhungu
 
Achana na mkataba.. angalia manufaa ya mradi huu kwa wanaTZ
Mkuu kuuliza ivyo nataka kujua kwasababu kuna baadhi ya watu wametuingiza kwenye mikataba ovyo uko nyuma na isije ikatokea kwenye huu mgodi na kuna mchangiaji kasema haya madini adimu sana yapo brazil na canada
 
Back
Top Bottom