Bilioni 100 za Makamba zitumiwe kufunga mifumo ya gesi kwenye usafiri wa Umma!

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,361
5,879
Bilioni 100 za Makamba zitumiwe kufunga mifumo ya gesi kwenye usafiri wa Umma!

Nimekadiria jiji la Dar tu kuwa na dala dala si chini ya elfu hamsini ambazo zinatumia mafuta ya zaidi ya Bilioni 150 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya trilioni moja kwa mwaka.

Kuliko kuzipeleka fedha hizo kwenye kutoa ruzuku ambayo sio sustainable ni bora hela hizo zielekezwe kwenye kufunga gesi dala dala kwa kuanza na mkoa wa Dar Es Salaam.

Gari moja inaweza kufungwa mfumo kwa wastani wa Tsh milioni mbili hivyo fedha hizo kukidhi kufunga gesi kwenye dala dala elf 50.

Mkandarasi anayefunga gesi pale DIT au yule aliyefunga gesi malori ya Dangote anaweza kuifanya kazi hii huku eneo la kiwanda cha nyama cha Kawe kikitumika kama kara kana.

Serikali pia itumie mobile gas station kama iliyowekwa pale Tazara karibu na Heslab kusambazwa kwa vituo vya mafuta ambao watakuwa wanauza gas kama mawakala.

Dala dala hizi zitafungiwa mifumo kwa mkopo ambapo kila mwezi mwenye gari atatakiwa kurejesha sh laki mbili kwa mfumo ambao unatumika kulipa faini za magari (trafic fines). Kwa hiyo kila mwezi ile laki mbili itakuwa inasoma kwenye mfumo na hakuna gari iliyoko bara barani itakwepa kulipa fine.

Kwa kufanya hivi hizi bil 100 zitarudi (revolving fund)hivyo kutumika kufadhili ufungaji wa gesi kwenye dala dala za majiji makubwa mengine mpaka nchi nzima itakapofikiwa yote.

Kwa kufanya hivi tutakuwa tumetatua tatizo la kupanda kwa bei za mafuta zisiwaathiri wananchi wa kawaida moja kwa moja na kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagizia mafuta.
 
Umeamka usingizini? Gesi tulipigwa kitambo awamu ya nne! Jiulize vituo vya kujaza CNG(compressed natural gas) vipo vingapi hapo Dar?
 
Daladala 50 kwa watu milioni 5. Zipo jumla ya daladala elf 6 Dar pekee.
 
Athari za bei za mafuta ni nchi nzima.

Wewe unaleta solution za dar peke yake.

Na watu binafsi, mabasi ya mikoani, malorry nao wanaathirika sana tu.
 
Rekebisha heading hizo ni pesa za wananchi sio za waziri wala mwingine yeyote.
 
Athari za bei za mafuta ni nchi nzima.

Wewe unaleta solution za dar peke yake.

Na watu binafsi, mabasi ya mikoani, malorry nao wanaathirika sana tu.
Mkuu. Najua. Lakini mwenye gari binafsi akizidiwa anaweza kupanda dala dala.
Mikoani kama ambavyo umeona kwenye proposal yangu, mradi utafika but we need to have a starting point.
So far hakuna one solution that fits all.
Hayo malori na mabasi ya mikoani nayo tunaendelea kuyatafutia suluhu.
Wazungu wanasema, every crisis is an opportunity for a reset!
 
Umeamka usingizini? Gesi tulipigwa kitambo awamu ya nne! Jiulize vituo vya kujaza CNG(compressed natural gas) vipo vingapi hapo Dar?
Nimesema vituo hivi vya kuuza Petroli vitafungiwa matenki ambayo hayataunganishwa moja kwa moja na bomba la gesi, bali yatakuwa yanajazwa gesi na malori ya kusambaza gesi kama ilivyo sasa kwenye usambazaji wa mafuta. So hii itafanya gesi ipatikane maeneo yote muhimu.
 
Back
Top Bottom