Bilionea mwingine Arusha akutwa kafa chumbani

Bilionea mwingine Arusha akutwa kafa chumbani

calculator

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
279
Reaction score
137
Habari wakuu,

Naona a town wameandamwa sana na mtoa roho. Mmiliki wa Merimont Hotels & Lodges kakutwa amefariki jioni hii ndani ya chumba cha hotel ya City Plaza, iliyopokatikati ya jiji la Arusha.

Inasemekana alikuwa na mke wa rafiki yake aitwaye Chedi na mama huyo ametoweka na mamilioni ya fedha na gari aina ya Lincoln Navigator.
 
Habari wakuu, Naona a town wameandamwa sana na mtoa roho. Mmiliki wa Merimont Hotels & Lodges kakutwa amefariki jioni hii ndani ya chumba cha hotel ya City Plaza, iliyopokatikati ya jiji la arusha. inasemekana alikuwa na mke wa rafik yake aitwaye Chedi na mama huyo ametoweka na mamilioni ya fedha na gari aina ya Lincoln Navigator.

Kunani A town...??
 
Alikuwa na mke wa mtu? Kapigwa risasi au kafa kifo cha kawaida?
 
As-taagha-firuLaah majangaa hivi:-
Dawa za kulevya..
Mihadarati
Risasi za moto
Mauaji
Uzinzi
Ujambazi
TindiKali
.....................Mungu tokoe na mabalaa...............
 
mapenzi yanangao zake kazi inaendelea,

yeye kamuona mke wa rafiki yake ndiye mtamu kuliko wanawake wote,

kafa kijinga kwa ujinga shetani ampokee.
 
Hivi Arusha kuna mabilionea wangapi?

Kila mtu analalamika maisha magumu, lakini kila siku tunasikia kuna mabilionea. Hawa mabilionea pesa zao ziko wapi? au wanaweka chini ya uvungu?

Arusha bana kila mtu akiwa na hotel ni bilionea. Halafu wanawake Arusha wapo wengi sana tena wazuri kupindukia sasa inakuwaje wake za watu tu!!!

Mimi naamini hao watakuwa na imani ya Freemason na sasa masharti yamewashinda kisha wanakufa vifo vya ajabu ajabu.

RIP Bilionea mwingine.
 
bilionea
kafa
mke wa mtu
pesa
madawa ya kulevya
polisi
mabbomu
risasi
...... kwakweli kuna changes zimetokea Tanzania; tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Hivi Arusha kuna mabilionea wangapi?

Kila mtu analalamika maisha magumu, lakini kila siku tunasikia kuna mabilionea. Hawa mabilionea pesa zao ziko wapi? au wanaweka chini ya uvungu?

Watu wa Arusha wanajua sana kuwachanganya waTanzania yaani kila mkazi wa Arusha ni bilionea ipo siku hata mbuzi na ngo'ombe wa Arusha nao watakuwa mabilionea.Yaani du hata nashinwa la kusema kwa jinsi mji wa Arusha ulivojaa mabilionea inaonekana kila mtaa kuna bilionea kumi
 
Arusha mabilioni wanapukutika sana, na wote inaonekana visa vya kufa vinafanana.
 
Watu wa Arusha wanajua sana kuwachanganya waTanzania yaani kila mkazi wa Arusha ni bilionea ipo siku hata mbuzi na ngo'ombe wa Arusha nao watakuwa mabilionea.Yaani du hata nashinwa la kusema kwa jinsi mji wa Arusha ulivojaa mabilionea inaonekana kila mtaa kuna bilionea kumi

Inawezekana wenzetu hawa wanawatambua mabilionea kutokana na lugha wanazoongea!
 
Back
Top Bottom