TANZIA Mzee David Makerege (80) Afariki Dunia Akiwa Chumbani Kwenye Hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
152,934
2,000
AFANDE RPC (R)RCO(R)STAFF OFFICER (R)OPP OFFICER (R)OCD MABWEPANDE


YAH: TUKIO LA KIFO CHA MASHAKA
GBA/IR/142/2021

MLAL: O.A.MSHANGAMA - ASP

Mlalamikaji anaeleza kuwa mnamo tarehe 16/1/2021 majira ya saa 18:00hrs akiwa kituo cha polisi Mabwepande alipokea taarifa toka kwa incharge CID Goba A/Insp. Gwake kuwa huko Mbezi Makonde katika hoteli ya Mbezi Garden kuna mteja amefariki chumbani(x)

Taarifa kamili ni

Kwamba mnamo tarehe 16/01/2021 majira ya saa 17:55hrs huko goba kituo cha polisi(x) a/insp.gwake mwakapande alipokea taarifa toka kwa meneja wa hoteli ya mbezi garden aitwaye Newton s/o Simkonda, Mnyiha, 44yrs, Mkristo, Meneja, mkazi wa Ukonga Majohe(x)kuwa huko Mbezi Garden hotelini kwake katika wlaya ya kipolisi Mabwapande na mkoa wa Kinondoni kuna mteja amefariki dunia chumbani alipokodi akiwa na mwanamke wake(x)baada ya taarifa hiyo kupokelewa Mkuu wa Upelelezi Mabwepande pamoja na I/C CID Goba walifika eneo la tukio na kumkuta mwanamke aitwaye Neema d/o Kibaya, Mpare, 33yrs, biashara, Mkristo, mkazi wa Goba Marobo aliyekuwa na marehemu na (x) kueleza kuwa alifika hotelini hapo leo tarehe 16/01/2021majira ya saa 15:00hrs walipokuwa wamekubaliana wakutane na kumkuta marehemu ameshachukua chumba namba 22 akiwa na maji na juice(x)

Baada ya kufika aliweza kuagiziwa chips na mishikaki mitatu na marehemu(x) akiwa anasubiria chips hizo huku wakiwa wanaendelea maandalizi ya tendo la ngono(x) ghafla alimwona marehemu akipumua kwa shida ndipo akatoka kwenda mapokezi kuomba msaada(x)baada ya taarifa wahudumu waliongozana na uongozi wa hoteli walifika na kumkuta marehemu haongei na hafanyi chochote huku akiwa ametoa macho ambapo uongozi wa hoteli ulibaini kuwa mteja wao amefariki dunia (x) ndipo meneja akachukua jukumu la kuwajulisha polisi ambapo walifika eneo la tukio.

Katika uchunguzi wa awali uliofanyika mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha lolote (x). Katika upekuzi marehemu alikutwa na simu aina ya tecno na pesa Sh. 37,000/=na kitambulisho cha mpiga kura na kuweza kumtambua kwa jina la Davis Makerege Mabeba, Mluli, 80yrs, Mkristo, mkazi wa Goba kwa Ndambi(x)mwanamke aliyekuwa na marehemu chumbani anashikiliwa kituo cha polisi goba kwa mahojiano(x)tukio limekaguliwa na OC CID Mabwepande O. A Mshangama ASP akisaidiana na Incharge CID Goba A/Insp. Gwake pamoja na timu ya makachero (x)

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi (x) taarifa kituoni na Newton S/O Simkonda na kupokelewa na J 92 PC Inocent leo 16/01/2021 saa18:44hrs(x) fcr maendeleo zitafuata(x)

-Mwisho-

Toka Crime Mabwepande

====

David Makerege (80) Mkazi wa Goba Dar es Salaam amefariki Dunia akiwa kwenye Hotel ya Mbezi Garden (chumba No.22), January 16, 2021, Polisi Kinondoni wamethibitisha.

“Kwenye chumba hicho tulimkuta pia Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Kibaya (33) ambaye ameeleza kuwa Marehemu alikuwa ni Mpenzi wake”- POLISI

“Uchunguzi wa awali umeonesha mwili hauna jeraha lolote, baadaye mwili ulipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hifadhi” -POLISI

mzee.JPG
 

7ve

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
976
1,000
Yaani unaona kabisa umri umeenda unaenda kuchukua toto kama hiyo wakati una presha una kisukari unashushia na viagra unataka nini wewe kama sio kufia gesti.

Tumuombe Mungu atupe mwisho mwema wa maisha yetu.
 

Deo Castory

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
222
1,000
Mzee wa miaka 80 alienda kupiga kazi ya miaka 33 huku akiwa na 37,000 mfukoni baada ya chipsi na mishkaki 3.

Inasemwa kwamba daktari ndiye anaweza declare mtu kufariki, hivyo huu uongozi wa gesti kudai uligundua mteja wao amefariki na kuamua kutaarifu polisi ni move sahihi kweli?

As walitumia kipimo gani? Achana na muvi ule mtindo wa kusikiliza kifua... Mimi naona na mtu aliyetoa taarifa ya kifo angehojiwa pia.
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,511
2,000
Huwenda alikua ametumia dawa za kuongeza nguvu zikamzidi nguvu akapoteza uhai.

Siwezi kucheka huyo mzee kwa maana hata Mimi Sina nguvu za kustahimili matamanio ya ngono isipokuwa kwa uweza wa Mungu.

Lakini ni fedheha Sana mzee Kama huyo kumalizia maisha yake katika situation ya namna hio.

Lakini ninachojifunza katika tukio hili sitababaika tena na msichana mwenye uzuri wakati huu maana atakaezaliwa 2025 bado anaweza kuja kutumika na mtu Alie na umri Kama wangu kwa kipindi hicho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom