Bila kufuta kesi ya Mbowe, Siri za Serikali na Mambo ya ulinzi yanatufikia Raia hata tusiojua kusoma alama za nyakati

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Ni vyema kesi ya Mbowe ikafutwa, Kuna mambo ya ulinzi mazito na siri yanaongelewa mahakamani ambayo wengi hatukufahamu

Ushahidi unaonyesha maisha ya Askari wetu na haki zao zilivyo, Mambo ya dhuluma, Mateso na Sera za kustaafu au kufukuzwa kwa haki au kutokufuata haki zinatufikia hata mangumbalu kama sisi tusiojua kusoma

Unaweza ona jambo dogo, Lakini kwa upande wa pili linaharibu morali kwa wale Askari waliopo eneo la mapambano,

Wakianza kusikiliza kesi kamili kwa staili hii na maneno yanayozunguka kuwa mashahidi wengi wa utetezi watakuwa Askari wa kulinda mipaka na Amani Itakuwa aibu sana

Tulizoea siri za ulinzi zinabaki kwenye vyombo vyao husika vya kimamlaka na sio kutuhabarishi kila kitu sisi tusiojua kusoma kwenye vijiwe vya kahawa

Bila kesi hii kufutwa, Kuna majina yanatajwa sana sana hadi sisi mangumbalu tunahisi ndio wale wasiojulikana na sasa wanajulikana, Kuna Polisi wanahusishwa na utesaji mikoa tofauti na kauli za kupotezana

Siku yaja wale waliopotelewa na ndugu enzi zile za giza kuja kuwadai Polisi hawa ndugu Zao

Tunaishukuru Mahakama kwa kuweka siri ya mambo ambayo tusingeyajua Pengine mpaka tunaondoka

Wengi hii kesi ndio habari kuu, Details nyingi mimi binafsi sikufahamu, Sikufahamu kabisa kuwa kuna shida ya Brain mapema pale ndugu yako atokapo Kongo, Sudani au Somalia, Nimeyasikia kwenye kesi hii, Ingawa Marekani niliyasikia lakini kwa muundo tofauti na wa kwetu Mahakamani
 
Bila kesi hii kufutwa, Kuna majina yanatajwa sana sana hadi sisi mangumbalu tunahisi ndio wale wasiojulikana na sasa wanajulikana, Kuna Polisi wanahusishwa na utesaji mikoa tofauti na kauli za kupotezana
Mtani habari yako
 
Wacheni sheria ifuate mkondo wake

Acheni kuingilia mchakato wa Haki

Vyombo vya kutoa Haki havipo kwaajili ya kesi ya Mbowe peke yake bali vipo kwaajili y Watanzania wote hivyo tuviheshimu.
Mlijifunika shuka kumbe mmeacha miguu iko wazi
 
Mengi mazuri yaliyofanywa na utawaule uliopita yanawezwa kufunikwa na kutupwa mbali na mabaya machache yaliotokea.

Mfano kesi hii, vile ilivyoandaliwa tokea kipindi hiko mpaka leo gharama zilizotumika na zinazoendelea kutumika hali haina faida yoyote.

kwa ufupi ni kesi ya kisiasa na faida ilikua ni kwa walioiandaa na kwa sasa hawapo tena sijui hawa waliopo leo wanafaidika na nini au watafaidika na nini wanapoendelea kuing'ang'ania.

Ngoja tuone mwishowe. Sisi wananchi hatutakosa la kujifunza.
 
Labda sirikali imeamua kutumia njia hii kuwafichua wasio julikana na kutuonesha baadhi ya changamoto zinazo kabili taasisi zingine sirikalini. Tuiache inyeshe tuone panapovuja.
 
Sawa tu, ugaidi ndio hatari zaidi ya hizo siri. Ngoja tushughulike kwanza na ugaidi.
 
Hii kesi inatufundisha mambo mengi na ya kutisha sana ILA kubwa kuliko yote ni kuwa polisi sio walinzi wetu kama tunavyodqanganywa! polisi ni walinzi wa kikundi cha watu kwa maslahi ya kikundi hicho! tuwe makini sana tunapoongea au kuwa na ukaribu nao kwani kesi za kubambikiza ni asili yao!
 
Back
Top Bottom