Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 13, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,589
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Hatimaye kile kitendawili cha kuwepo au kutokuwepo uchaguzi mdogo Jimbo la Biharamulo Magharibi, kimeteguliwa baada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Rajabu Kiravu, kukitegua.

  Uchaguzi huo unafanyika kesho Jumapili Julai 5.

  Uchaguzi huo unafuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo Hilo, Pheres Kabuye, kilichosababishwa na ajali ya gari mkoani Morogoro. Huu ni uchaguzi mwingine wa moto kati ya TLP kuthibitisha sio chama mfu kwa kutetea kwa nguvu zote, kiti pekee cha ubunge kilichoshikwa na chama hicho, Chadema lazima ifanye tena kipimo cha operesheni Sangara huku CUF iking'ang'ana na Ngangari yake wakati CCM watataka kumaliza usongo wa kulikosa jimbo hilo kwa kipindi kirefu.

  Je Matokeo yatakuwa yale yale kama tutakayoyashuhudia Busanda hivi karibuni, watagawana kura nyingi hivyo kumpa mwanya mgombea wa CCM kushinda kwa kura chache na mwisho wa yote, "The winner takes it all".

  Kwa wapinzani kutoungana na kumsimamisha mgombea mmoja, ni CCM Busanda, CCM Biharamulo na 2010 ni CCM kwa kwenda Mbele.
   
  Last edited by a moderator: Jul 4, 2009
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu, asante kwa taarifa, hayo mengine hapo,(underlined) yaache tu mkuu, tarehe 24 si mbali tutapata majibu ya kina kuliko haya ya hisia.
  asante mkuu.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hivi CCM wakilala ktk majimbo yote utasemaje mzee.
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Si ndo hapo mkuu?
  Unjaua hata mi mwanzo nilitamani sana muungano wa upinzani, lakini baadae nikaja stukia kwamba Chama cha mafisadi wanatumia huo Muungano kuvidhoofisha vyama wanavo viona vinakuwa tishio. Wanapandikiza mamluki humo ndaniii na migogoro.. na kuwa fanya wakae kuparulana badala ya kujenga vyama vyao!

  Kama wananchi wamechoka wamechoka, hata chama kikisimama peke yake kama mgombea wao anakubalika kitashinda tu, sana sana watumie ubinadamu na busara kuona wapi wengine wanakubalika zaidi bila hata kuingia kwenye Muungano waachiane.
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rai yangu kwa Wasubi na wakazi wote wa B'mulo kwa ujumla: wekeni kando tofauti za kikabila na mpeni kura Capt. G. Kaijage awe mbunge wenu.

  Capt. Namkubali kwa uchapakaza na kupenda maendeleo binafsi na ya jamii. Nilipokuwa B'mulo nilibahatika kufanya kazi na huyu Capt. Na Kila mara mimi na wenzangu tulipojikuta tumepangwa na Capt. Tulifahamu hakuna mchezo bali kazi na matokeo yaliyolengwa.
   
 6. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rai yangu kwa Wasubi na wakazi wote wa B’mulo kwa ujumla: wekeni kando tofauti za kikabila na mpeni kura Capt. G. Kaijage awe mbunge wenu.

  Capt. Namkubali kwa uchapakaza na kupenda maendeleo binafsi na ya jamii. Nilipokuwa B’mulo nilibahatika kufanya kazi na huyu Capt. Na Kila mara mimi na wenzangu tulipojikuta tumepangwa na Capt. Tulifahamu hakuna mchezo bali kazi na matokeo yaliyolengwa.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hivi vyama vyetu vya upinzani samtaim vina tukerrrrrrra. Kwanini havipeani adventeji kukubaliana kuwa chama kinachokubalika ktk eneo husika kiungwe mkono na vyama vyote, muhimu tuwe na wapinzani wengi na wamaana bungeni habari za kungeza viti kwa kutaka ruzuku tu ni ufisadi mwengine wa kiujanja hauwasaidii wananchi walioachoka na umasikini.
   
 8. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  jamani hayo mambo ya kuachiana majimbo yamepitwa na wakati, kila chama kinataka kikue na kichukue Dola. Hatua moja wapo ya kukua ndo hiyo ya kushiriki chaguzi. watanzania wanapoenda kupiga kura hawachagui kambi bali chama. Demokrasia safi ile ya watu kuwa na choice nyingi iwezekanavyo kisha kila mtu achague anayoikubali. Chama kitakachopata wengi ndo kinachokubalika. Wakienda kama kambi ushindi ukipatikana hatokuwa wa kambi bali wa chama kilichoshinda, hivyo haina mantiki hata kidogo. lazima watanzania tujue jinsi ya kuchambua ngano toka kwenye magugu mengi.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  tume hiyo imesema uchaguzi mdogo katika Jimbo la Bihalamuro Magharibi utafanyika Julai 5, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Phares Kabuye (TLP), aliyefariki dunia mwezi uliopita kwa ajali ya gari.
  -___________________________________________________-
  Hata malaika anaetoa roho anasaidia vipimo vya kuwap[ima wananchi kama kweli wamechoka na maisha haya ,jamani ndugu wananishi pelekeni ujumbe kuwa kweli mmechoka na utawala wa Sultani CCM kwa kuipiga na chini kila tunapoletewa maombi ya kuulizwa kama tumechoka na utawala huu usiofuata sheria.
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hizi changuzi ndogo waziangalie upya. Kuna umuhimu gani kufanya uchanguzi mwaka huu wakati kuna General Elections mwakani? Gharama zisizokuwa za lazima (na usumbufu vilevile).
   
 11. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  heheheh... ni kweli upo sahihi kabisa na mimi nakubaliana na wewe ila sasa kwenye hali ya ushindani hivi unaweza kumpa mwenzako nafasi ya kujitangaza huku wewe ukisubiria mwakani kwa sababu ya gharama? Haiwezekani ndio maana lazima iwe hivi.

  Mimi ninachohoji ni kujua kama ndugu wa marehemu wote utaratibu upoje wa kuhusu mafao yao ndugu zao waliotumikia muda wote maana najua wanachukua kama zaidi ya million 30 ama 60 kama sikosi kama wakimaliza muda wote wa miaka 5 sasa na wale ambao hawajamaliza sijui magao wao unakuwaje na ndugu wanafaidika vipi? Na hali kadhalika kwa hao ambao wameingia mgao wao unakuwaje kwa muda huu ambao wamekaa kwenye hizi nafasi? Isije tukaambiwa pesa zinakwenda kwenye vyama vyao
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wazo lako zuri. Mimi nadhani nina suluhisho mbili, sijui wenzangu mta fikiriaje?

  1.Chama kilicho poteza mbunge wake kichague mtu kutoka chama chao kujaza nafasi mpaka uchaguze utakapo fanyika tena. Kama tuna wabunge wa kuteuliwa sidhani kama hili litakua neno.

  2.Aliye chukua nafasi ya pili toka kwa aliye acha kiti wazi achukue nafasi. Rekodi za uchaguzi si zipo. Yule aliye kuja wa pili apewe nafasi hiyo nk huyo asipo weza basi apewe aliyemfuatia. Kama hamna waweza kurudi tena kwenye suluhisho la kwanza.
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =========

  Ukifuata hii logic yako itabidi wabunge wote walioshinda wawe na walinzi masaa 24 ili kuwakinga wasiawe maana aliyepata namba ya pili daima atatafuta aue ili awe mbunge. Chama kilichoshinda itabidi kiwalinde wagombea wake wasipate tamaa ya kuwa wabunge kwa kuwaua wenzao.

  Napendekeza tu kama muda umebaki chini ya miaka 2 uchaguzi usiitishwe.
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu, mkuu hiyo kweli yaweza kuwa hatari! Hata hivo kumbe hata saa hizi basi tu Mungu kaweka neema , bado watu wanweza uana ili zifanyike chaguzi nyingine wakiamini wanaweza bahatisha!
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ni haki ya msingi kila mwananchi kuwa na mmbunge sio wa kupewa bali wakuchagua wenyewe.....
  pili izi chaguzi ndogo zinasaidia kama watu walifanya makosa kusahihisha makosa yao
  eti hela zinapotea kutokana na uchaguzi, hela zinazoibiwa nyingi hamzioni wacheni kudumaza demokrasia TZ
  hao waTZ wenyewe ndio kwanza wanaanza kujifunza kupiga kura, kuwatoa majumbani kwenda kupiga kura ni shida, leo hii uchaguzi ukiwa kila baada ya miaka mitano watu siwatasahau kabisa
   
 16. n

  nat867 Member

  #16
  May 18, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya haya ndo hivyo tena, NEC imeshatangaza ratiba ya uchaguzi wa jimbo la Biharamulo baada ya kifo cha aliyepata kuwa mbunge wa jimbo hilo mh. Kabuye (RIP).

  ni wakati muafaka kwa vyama vya upinzani kuweka mkakati kuhakikisha vinalitwaa jimbo hilo. mojawapo ya mkakati ni kuhakikisha vinaenda katika grassroot level na kuongea na wananchi na kuweka sera nzuri... But sera tupu inaonekana hazitoshi, pia ni kuweka mbinu mpya mpya!!!!

  Je vyama vitakumbali kuungana au itakuwa kama Busanda!!
  yetu macho!!
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Vyama vya upinzani wilayani Biharamulo, vimekubali kumuunga mkono mgombea ubunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Anthony Mbassa.
  Hatua hiyo ilifikiwa jana katika kikao cha pamoja cha viongozi wa vyama vinne, TLP, CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema.
  Tayari vyama hivyo, vimepanga kuzindua kampeni ya pamoja leo kuutaarifu umma kuhusu ushirikiano huo.
  Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu jana, viongozi hao walisema hali ya kisiasa jimboni humo, inaashiria kukubalika zaidi kwa Chadema na mgombea wao.
  Katibu wa TLP wa Wilaya ya Biharamulo, George Kasaiza, alisema uamuzi wa kuiunga mkono Chadema, unatoa nafasi kubwa kwa jimbo hilo kurejea kwa wapinzani.
  “Tumeona tusipoteze muda, fedha na kura za wananchi wetu, kwa kuwa Chadema na mgombea wao wanakubalika, tumeazimia kuwaunga mkono na hivi sasa ndio tunatoka kikaoni,” alisema.
  Kasaiza, alisema ili kufanikisha kampeni hizo, vyama hivyo vitateua wanachama watakaoshiriki kwa namna tofauti, ikiwemo kuzunguka na timu ya mgombea wa Chadema.
  Naye Katibu wa NCCR-Mageuzi wilayani humo, Seif Abdulrahman, alisema kufikiwa kwa uamuzi huo kulitokana na kudhihirika kwa ishara za Chadema `kuimeza' TLP.
  Alisema wakati wa uhai wa Phares Kabuye, TLP ilikuwa na nguvu zilizotokana na hamasa na kukubalika kwake.
  Hata hivyo, alisema NCCR-Mageuzi inaandaa mapendekezo ya jinsi mgombea wa Chadema atakavyokiwezesha chama hicho, ikiwa atachaguliwa kuwa mbunge.
  Wakati viongozi hao wakiafikiana kuinga mkono Chadema, TLP na NCCR-Mageuzi (Taifa), viliwahi kutoa tamko la kusimamisha wagombea katika jimbo hilo, huku CUF ikikaririwa kutoa kusudio la kumuunga mkono mgombea wa TLP.
  Akizungumza na Nipashe wiki iliyopita, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alivitahadharisha vyama vingine kutosimamisha wagombea, kwa madai kuwa jimbo hilo `ni mali' ya TLP.
  Naye Mwenyekiti wa TLP mkoani Kagera, Joas Kahiula, alisisitiza kuhusu nia ya chama hicho kumsimamisha mgombea ambaye hakumtaja, kwa madai kuwa ni siri.
  Aliahidi kuwa TLP itawasilisha jina la mgombea wake katika kikao cha jana.
  Uchaguzi mdogo katika jimbo hilo utafanyika mwezi ujao kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wake, marehemu Kabuye.
  Kabla ya kifo chake, Kabuye alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Ziwa, kumvua ubunge wake ambayo hata hivyo, ilikuwa haijatolewa uamuzi wake.
  NIPASHE
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Umeleta habari kishabiki na ki unazi, aya za mwanzo unadai wamekubiliana "kuiachia" Chadema, wakati aya za mwisho habari hizo zinakanushwa na viongozi wa juu wa kitaifa wa vyama.

  Punguza ushabiki jipange upya na lete habari kamili.
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Angalia mwisho kume tajwa source which is Nipashe siyo una payuka payuka tu. kama una tatizo sema usaidiwe.
   
 20. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  naona hi habari haijakamilika , Jana Maalim Seif alikuwa anaongea kwenye kituo radio Clouds kwenye habari ya saa 12 jioni anasema wao wanaiunga mkono TLP kwa sababu ndo ilikuwa na mgombea huko wameona waiachie, na si kweli kwamba wanaiunga mkono Chadema.
   
Loading...