Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

naona hi habari haijakamilika , Jana Maalim Seif alikuwa anaongea kwenye kituo radio Clouds kwenye habari ya saa 12 jioni anasema wao wanaiunga mkono TLP kwa sababu ndo ilikuwa na mgombea huko wameona waiachie, na si kweli kwamba wanaiunga mkono Chadema.

Ndiyo maana baada ya kuiona Nipashe nikaamua kuileta hapa kuu kwa sababu haku kosekani mtu anaye jua a little bet about something, na pia tuki put two and two togehter tuna weza kupata ukweli. Ngoja tuone post zingine zita semaje.
 
Umeleta habari kishabiki na ki unazi, aya za mwanzo unadai wamekubiliana "kuiachia" Chadema, wakati aya za mwisho habari hizo zinakanushwa na viongozi wa juu wa kitaifa wa vyama.

Punguza ushabiki jipange upya na lete habari kamili.

Birds of the same feathers, flock together!!
 
nani ni msemaji wa vyama?? Tamko lenye maamuzi kama hayo lazima litolewe na mtu mwenye dhamana hiyo
 
Hakuna aliekuliza source, the issue ni habari haijakamilika hao nipashe wako sio msahafu

Itakuwa vizuri ingalau siku moja na wewe ukatoa hoja yako na sio kila siku kupinga hoja za wenzio wewe ni nani humu?
 
Kama ni kweli ninaunga mkono hoja.
Nadhani wapinzani wamekubali sera za CHADEMA zinafaa kuongoza jimbo la Biharamulo. Na wafanye hivyo wakipeana katika nafasi nyenginezo pia. Ila kwa nafasi ya Urais wakubali kuvunja vyama na kuungana kisera ili wapate bonus kubwa ya kura au la watabaki kupiga porojo kama bongo fleva.

Tuombee muungano huu wabiharamulo udumishwe
 
Kama ni kweli ninaunga mkono hoja.
Nadhani wapinzani wamekubali sera za CHADEMA zinafaa kuongoza jimbo la Biharamulo. Na wafanye hivyo wakipeana katika nafasi nyenginezo pia. Ila kwa nafasi ya Urais wakubali kuvunja vyama na kuungana kisera ili wapate bonus kubwa ya kura au la watabaki kupiga porojo kama bongo fleva.

Tuombee muungano huu wabiharamulo udumishwe


Mrema huyu anaeaminia huruma za waTZ?
 
Hakuna aliekuliza source, the issue ni habari haijakamilika hao nipashe wako sio msahafu

We mtu una shangaza. post ya kwanza ume jibu kama mimi ndiyo muandishi, una pewa source una sema hauja uliza souce halafu una sema na nipashe yangu. Acha ushabiki wa ajabu. Thread iko hapo kama ina kasoro tuta jua na kama ina ukweli tutajua. Nia ya JF si habari ziwekwe na zijadiliwe. Kama una tatizo lingine sema usaidiwe.
 
naona hi habari haijakamilika , Jana Maalim Seif alikuwa anaongea kwenye kituo radio Clouds kwenye habari ya saa 12 jioni anasema wao wanaiunga mkono TLP kwa sababu ndo ilikuwa na mgombea huko wameona waiachie, na si kweli kwamba wanaiunga mkono Chadema.
Na kwa jinsi mahusiano baina ya Chadema na CUF yalivyo hivi sasa, ni vigumu sana kwa CUF kuisapoti Chadema
 
Jamani Chadema hata bila muungano wa vyama iko juu. Aiyekataa anyamaze tu lakini hata vyama vingine visipokiunga mkono bado ninaamini kinakubalika kama chama imara katika upinzani. Na kwa sababu ni vyama huru kila chama kina haki ya kuweka mgombea wake na waone nani ataonekana kukubalika sana upande wa upinzani. Bila ajuza atakuwa Chadema.
 
Ndugu zangu heshima mbele sana,

- Kamati kuu ya CCM, CC jana usiku imempitisha rasmi Bwana Oscar Rwegasira kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Biharamulo, hii ni kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo hili Mh. Kabuye.

- Uchaguzi huu unaonekana kuwakuna sana wananchi wengi, hasa kutokana na ushindani mkubwa ulioonyeshwa na Chadema, katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni kule Busanda, ambako CCM ililiinukia kidedea.

Tunawaombea heri kwanza wagombea wote watakaopitishwa na vyama vyao, kuwania jimbo hilo, na pia ni matumaini yetu wananchi kwamba sheria na utaratibu wa haki utafanyika na kufuatiliwa na wote watakaohusika na uchaguzi huu, na hasa wale wenye mamlaka kikatiba ya jamhuri yetu, pia ni mategemeo yetu wananchi tulio wengi, kuona masuala muhimu ya taifa, yakipewa nafasi kubwa katika majukwaa ya kampeni huko Biharamulo.

Na nina ushauri mmoja mdogo kwa wapinzani, tafadhalini simamisheni mgombea mmoja huko Biharamulo, kama itawezekana ikiwa ni kwa masilahi ya taifa letu.

Mungu Aibariki Tanzania.

Respect.

Field Marshall Es (Emergency System!).
 
CCM yamteua Rwegasira kuwania ubunge Biharamulo Habari Nyingin
NA JOSEPH BURRA

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Oscar Rwegasira, kuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa Biharamulo Magharibi, mkoani Kagera. Rwegasira aliteuliwa katika kikao cha kamati kilichofanyika juzi mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa ameteuliwa na mkutano huo kuzindua kampeni za uchaguzi huo, zitakazofanyika Juni 13, mwaka huu. Zitafungwa Julai 4, na Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Kamati ilikutana na wagombea sita walioomba kuteuliwa na Chama kuwania uongozi katika jimbo hilo.

Alisema lengo la kukutana nao ni kuweka mshikamano ili kukipatia Chama ushindi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Julai 5, mwaka huu. Rwegasira aliongoza katika kura ya maoni kwa kupata kura 309. Wengine walioomba kuteuliwa kuwania kiti hicho na kura zao kwenye mabano ni Magoha Agricola (120), Balagama Mwajemi (23), Rwabudongo Hassan (14), Matata Mussa (10) na Burchard Ntibihora (5).

Kupitia taarifa hiyo, Kamati Kuu imewaomba wana-CCM, wapenzi na wananchi wa Biharamulo kumuunga mkono Rwegasira ili ushindi upatikane. Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Phares Kabuye (TLP), aliyefariki dunia Aprili, mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Morogoro. Wakati huo huo, Angela Sebastian anaripoti kutoka Biharamulo kuwa, vijana wa wilaya ya Biharamulo wamepokea kwa furaha uteuzi wa Rwegasira.

Kutokana na uteuzi huo, vijana hao walifanya maandamano makubwa wakiimba nyimbo za kumpongeza. Vijana hao walisema uteuzi huo ‘umewakuna' na kilichobaki ni kumuunga mkono mteuliwa huyo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, ili aweze kuwa mbunge. Walisema wananchi wa Biharamulo wanahitaji mabadiliko, kwani wamekuwa na wabunge ambao kazi yao ni kwenda bungeni na kupokea posho bila ya kuangalia maslahi ya vijana.

Kwa upande wake, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Wilaya ya Ngara, Pantaleon Rumanyika, aliye Biharamulo kwa shughuli za Chama, alisema amepokea kwa furaha uteuzi huo na kwamba, wamejipanga kuhakikisha Chama kinaibuka na ushindi.
 
Ruzuku inayotolewa kwa vyama vyenye wabunge ndiyo inachowafanya wapinzani wasisimamishe mgombea mmoja. Wabunge wengi = Ruzuku kubwa.
 
Watz kwenye uchaguzi wa ubunge huko Busanda wameshuhudia utovu mkubwa wa nidhamu kisiasa pengine toka tz ipate huru,ufisadi huo wa kisiasa uliasisiwa na kuenziwa na mawaziri waandamizi wawili askari George Mkuchika na waziri kijana William Ngeleja.
Akiwa Busanda,katika kata ya Katondo,sehemu inayochukuliwa kama ndiyo ngome kuu ya wapinzani hasa Chadema,askari Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa "hata kama mnaishabikia Chadema,lkn CCM itashinda hasa kwa kura za vijijini kwani huko wakazi hawasomi magazeti na wala hawaoni TV kwani huko hamna umeme",alisema haya huku waziri wa nishati na madini kijana Ngeleja akiwa amekwisha ingia kwenye jimbo hilo kuipigia kampeni CCM,na ndiyo maana kwenye makala hii nitamchambua zaidi kijana Ngeleja zaidi kuliko propagandalist askari Mkuchika.
Willima Ngeleja,mbunge wa Sengerema hakuwepo kwenye baraza la kwanza la mawaziri ktk serikali ya kwanza ya mzee JK.Kabla ya kuja kwake kwenye siasa kijana Ngeleja alikuwa akijishughulisha na kazi yake aliyosomea ya utaalam wa sheria baadae akaibukia siasa kwa kutumia mkono" wa fisadi papa",lakini bado kwangu Kuteuliwa kwake kuwa waziri kamili mara baada ya mabadiliko makubwa ya serikali ya TZ kufuatia kashfa ya Richmond kulinifurahisha sana mimi kwani nilidhani kwa ujana wake atakuwa na mawazo mapana zaidi ya kuwatumikia watz kinidhamu na kujituma;kumbe nilikuwa najidanganya !
Madudu yote aliyoyafanya kijana Ngeleja kwenye wizara yake kwa miaka si zaidi ya 2 toka awe waziri wa Nishati na madini yanafahamika,toka zile kashfa za kutaka kununua mitambo chakavu ya Richmond wakijaribu hata kuvunja katibu inyokataza serikali kuu kununua vifaa vilivyokwisha tumika,songombingo la songas,baadhi ya wilaya kutokuwa na umeme hadi leo kwa sababu ya sera mbovu za wizara husika,kushindwa kuuondoa Umungu-mtu wa Dr Rashid na wenzake kwenye shirika la Tanesco,umeme usio na uhakika kwa mikoa mingi ya tz na kikubwa zaidi kutofaidika kwa sisi watz na mali asili zetu zitokanazo na madini kutokana na mikataba ya "carl peters'iliyosainiwa na vigogo ktk wizara ya Ngeleja.Kwa ufupi kama kuna waziri anatakiwa asibanduke hata dakika moja kwenye ofisi yake makao makuu kwa sababu yupo nyuma sana kwenye kufanikisha malengo yake kwa watz ni waziri wa nishati na madini Wiam Ngeleja,kinyume chake anakwenda hadi Busanda tena kuongea "pumba"tupu kwa niaba ya wizara yake!
Waziri Ngelaja akiwakilisha wizara ya Nishati na madini,akawasili Busanda kumnadi mgombea wa CCM mama Lorensia Bukwimba kwa kuwaambia wananchi hasa wachimbaji wadogowadogo kuwa"CCM ndiyo yenye nchi na kati yenu yeyote atakayebainika hajatupa kura yake tutaituma TRA kuja kuangalia rekodi yake ya ulipaji kodi".Kinachonishtua hapo,je kulipa kodi si ni wajibu wa kila mtz anayeingiza mapato ili kuinua uchumi wa nchi yake?kumbe ukiwa mwana CCM usipo lipa kodi hufuatiliwi sana na vyombo husika?uwezo mdogo wa kijana Ngeleja kwenye uongozi ulianza kudhihirika hapo!
Kijana Ngeleja hakuishia hapo,alizidi kuongeza kuwa"serikali ya CCM imetenga mirahaba mingi kuwapatia wana Busanda waendeleze uchimbaji wa madini",pia kwa kutumia wizara yake ya Nishati wafanyakazi wa Tanesco wakaanza kutandaza nguzo eti sasa baada ya miaka zaidi 40 ya kuwepo wilaya ya Geita duniani ndipo watapeleka umeme,huo ni utapeli mwingine mkubwa wa kisiasa ulioasisiwa na kuongozwa na kijana Ngeleja!
Wizara ya Nishati na madini ya TZ ina mambo mengi sana yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi,pia ni wizara hii yenye deni kubwa sana la maelezo kwa watz hasa kuhusu kugawana kwa watz faida ya madini yanavunwa kila siku na makampuni ya nje na ndani kutoka kwenye ardhi yetu.Ngeleja kaenda Busanda kupiga kampeni za kashfa na vitisho,lkn hajawaambia hadi leo watz mustakabali wa nchi yao juu ya uwizi mkubwa wa maliasili yetu ya madini unaofanywa kwa wazi hasa kama ujangili wa mgodi wetu wa kiwira ambapo kuna tuhuma dhahiri zinamuandama bwana mkubwa Mkapa na mwenzake Yona walipojiuzia mgodi huo kwa bei poa.Hapo najiuliza tena na tena na maswali, kibao,lipi lingekuwa jambo la kutusaidia sisi walalahoi kati ya kwenda kudanganya wananchi wa Busanda au kutusaidia kuturudishia mgodi wetu wa kiwira?
Ngelaja,dhambi uliyoichuma kule Busanda itakutafuna wewe milele!Geita ni wilaya tajiri sana tz iliyofunikwa na dhahabu lukuki,lkn ni wilaya masikini sana tz labda ikiizidi Bunda tu kwa utajiri.Na Ngelaja unajua kabisa kuwa ahadi zako Busanda hazitekelezeki kwani ni miaka zaidi ya 40 sasa mmeshindwa kufanya hivyo.Tulitegemea waziri husika ungesimama pamoja na wana Busanda kujaribu kuwaondoa kwenye lindo hili la umaskini hasa kwa kuwatetea kuwa nao angalau wafaidike na dhahabu waliyonayo,kinyume chake wewe unazidi kuwaibia kisiasa!CCM ipo pale toka enzi za mbunge Donald Max lkn huduma muhimu za binadamu kama vile umeme,maji na shule hamna!leo hii unakuja Ngeleja kuwatapeli kwa kusimikia nguzo?
Sio tu Busanda au Kyela au Hanang,matatizo ya huduma za jamii kwa watz ni yaleyale na wala CCM haipiganii kwa vyovyote vile kuyaondoa.Wakija kwenye uchaguzi mkuu wanaleta tu makarandinga kuwatapeli wananchi,uchaguzi ukiisha wanaondka zao na tambo nyingi huku eti mzee Malecela akipokewa kwao Mtera kama shujaa wa wa siasa za ulaghai ndani ya CCM.Busanda hawana umeme,maji,shule,zahanati na pia tija kwa wafanyakazi hata wa serikali ipo chini sana;sawa tu na Biharamulo labda kama wamebahatika Biharamulo ni kupata umeme wa kubangaiza,lkn kwa vyevyote vile huduma za maji,shule na huduma za kiusalama hawapo pazuri kama tu walivyo Busanda!
Kwa mtaji huo basi,sisi tunamtegema tena Ngeleja aende Biharamulo kuokoa jahazi ili CCM ichaguliwe tena!lkn akumbuke pia Biharamulo sio Busanda na kule watu wanaangalia TV na kusoma magazeti kwa hiyo basi askari Mkuchika hawezi kwenda huko!
Naam Ngelaja nenda tena kaambie wakazi kule kuwa umeme wao sasa utakuja kwa kutumia vinu vya nyuklia na ikiwezekana nunua hata kinu kimoja kwa bei yeyote ile kiwe cha mfano kawaonyeshe,na uchaguzi ukiisha ondoka zako na kinu hicho rudisha uliponunua wakurudishie hela zirudi tena wizarani,hii itakuwa sawa tu kwako kisiasa,sisi watz hatuna noma,kama tu ambapo sasa hutaki hata kusikia habari za Busanda.
Kwa vyovyote vile huenda CCM ikampeleka Biharamulo waziri mwingine "Mkuu wa Vitambulisho"ambaye pia waziri kijana Lawrence Masha ambaye kila siku alidamkia kule Busanda eti kuangalia usalama wa raia.Hakika kweli serikali hii ina vituko,je waziri Masha na hali ya usalama kwa raia wa tz ilivyo hivi sasa mbapo albino wanakatwa mapanga,majambazi yanapora mar kwa mara hadi mchana,anastahili kuacha ofisi yake hata kwa dakika moja na kuja kupiga soga za kisiasa Busanda?Masha sio polisi na wala hajawahi kuwa polisi, Mwanza kiulinzi chini ya kamanda Kapinga walikuwa imara mno na wala haikuripotiwa kuwa wanataka msaada wa wakuu wa wizara,ilikuwaje basi Masha kila siku yupo Busanda?kama Masha alikuwepo Busanda akiacha nchi kwenye usalama tete atashindwa vipi kujikongoja hadi Biharamulo kuhaidi wakazi kule kama mkiichagua CCM mtaletewa kombania nzima ya polisi kila kijiji?hawa ndiyo mawazir wetu vijana!
Imeniingia imani kwa Rais JK kuwa endapo atashinda 2010 ni bora awachague wazee akina Kingunge kuongoza wizara,ingawaje wamechoka lkn wanachagua la kusema!Ilikuwa kauli mbiu yetu zamani kuwa vijana na sisi tupewa nafasi kuonyesha uwezo wetu kuongoza,lkn kumbe kama tukipewa nafasi tija ya kazi ndiyo hii kama ya akina Ngelaja?ni heri mzee Kisumo,Shija na wengineo wengi mrudi kuongoza wizara!
Liwalo na liwe,lzm tutashuhudia kauli zisizo za kistaarabu kutoka kwa wanasiasa wa tz kwenye uchaguzi wa Biharamulo hasa hawa vijana;nikisikia tena kauli kama hizo toka kwa vijana wetu akina Ngelaja sitashangaa kwani hamna mzee wa chama hata mmoja aliyewakemea,badala yake wazee akina Ndejembi wanawaita waandishi wa habari pale Maelezo kutuambia nahau zile zile za kila mwaka"ndani ya CCM hamna fisadi,na kama fisadi yupo ni yeye na sio chama" huwa nacheka sana nikisikia habari za akina Ndejembi,je kuna Chama bila watu?Na ndiyo kusema labda wazee hawa wamebariki yale waliyoyasema akina Ngeleja kule Busanda?mbona hawawakemei vijana wao?
lkn Ngelaja kumbuka kuwa Busanda sio Biharamulo na muulize kilichompata mbunge aliyeangushwa Anatory Chonya kwa mbunge aliyeshinda hayati Phares Kabuye,nasisitiza tena Ngeleja usome alama za nyakati yasije yakakukuta kama ya Makamba Tarime.
 
Ruzuku inayotolewa kwa vyama vyenye wabunge ndiyo inachowafanya wapinzani wasisimamishe mgombea mmoja. Wabunge wengi = Ruzuku kubwa.
Inakuwa vigumu kuachiana kwa sababu baadhi ya vyama mnavyojaribu kuvishawishi kuungana vipo pale kulinda maslahi binafsi ya viongozi.Mchukulie Mrema akuambie ana ajenda gani kisiasa kwa sasa hivi,jibu atakalokupa ni kulinda nafasi yake ya uenyekiti ili aendelee kuishi kwenye nyumba ya chama Sinza.Je nyie wenye mapenzi mema na ujenzi wa Demokrasia mnakubaliana kweli na msimamo wa aina hiyo?Inawezekana kweli ufanye makubaliano na Kiongozi wa aina hiyo?
 
CCM watashinda wameweka mgombea strong sana anayekubalika sana Biharamulo...Mukasa alianza kampeni muda mrefu sana. Pamoja na mapungufu machache aliyonayo kama wengine wote, sioni upinzani utasimamisha nani kule.... Kijana analijua sana jimbo lake na amejiweka karibu sana na wapiga kura sioni sababu ya kushindwa ukizingatia Kabuye hakuwahi fanya la maana jimboni, wapiga kura watakuwa wanaresentment na wapinzani...

Mas
 
Demokrasia mnakubaliana kweli na msimamo wa aina hiyo?Inawezekana kweli ufanye makubaliano na Kiongozi wa aina hiyo?


Mkulu Nsaji heshima mbele,

- Sizijui siasa za Upnzani, lakini hakuna ubaya kujaribu labda akiwa confronted na hard political facts kwamba upinzani wana nafasi kubwa ya kushinda under one candidate anaweza kukubali ukweli, na depending nani wa kumu-approach au na yeye ana siri fulani anazijua on others upinzani's big ndio maana anakuwa mgumu kukubali? Maana na yeye sio mjinga!

Respect.

FMEs!
 
Je tz kweli tunahitaji uchaguzi mdogo na umaskini wetu??

Hivi gharama za uchaguzi mdogo ni kiasi gani???
 
Kwa ninavowajua waru wa Biharamulo, du wanabimulo huwa hawachagui chama ila tu mtu wnayemkubali ukiona Rwega kapitishwa na mtu ambaye siku zote wanabimulo wanataka hapo basi. Inabidi upinzani watengeneze jina huo tu kwani vyama vya upinzani vina influence jidogo huko Biharamulo
 
Mkulu Nsaji heshima mbele,

- Sizijui siasa za Upnzani, lakini hakuna ubaya kujaribu labda akiwa confronted na hard political facts kwamba upinzani wana nafasi kubwa ya kushinda under one candidate anaweza kukubali ukweli, na depending nani wa kumu-approach au na yeye ana siri fulani anazijua on others upinzani's big ndio maana anakuwa mgumu kukubali? Maana na yeye sio mjinga!

Respect.

FMEs!
Ni vigumu sana Mrema kukubaliana na mtu mwingine,kumbukumbu za uchaguzi uliofanyika hivi majuzi ndani ya chama chake ni ushahidi wa wazi kuwa si rahisi kumshauri akubali wazo la mtu mwingine.Watanzania tulishuhudia jinsi alivyolazimisha matakwa yake dhidi ya wanachama wenzake.
 
Last edited:
Back
Top Bottom