Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,463
- 113,532
- Thread starter
- #501
Kwa sasa vituo ni tupu na hakuna kinachoendelea. Wakati tukiisubiri hiyo saa 10 ifike zoezi la kuhesabu kura lianze, sio vibaya nikawamwagia data chache kuhusu Biharamulo.
Ina eneo la kilomita za mraba zaidi ya elfu 5 na wakazi wanaokadiriwa kufikia zaidi ya laki 2. Kati yao Wasubi ndio wengi zaidi ya 35%, Waha 25%, Sukuma 20% na Wahaya 10%.
Profile ya Biharamulo inaonyesha wana utajiri mkubwa wa kilimo, mifugo na uvuvi mpaka wameweka data za mavuno, cha ajabu wametaja tuu kuhusu mgodi wa dhahabu wa Tulawaka lakini hakuna data zozote zinazoonyesha kunapatikana nini, inawezekana hata mrahaba unaishia kwenye matumbo ya watu.
Pia kunaonekana kuna shule 16 za sekondari ila haijaelezwa kama zinafika form six au zote zinaishia form four.
Yaani Biharamulo ina kila dalili za neema, ardhi nzuri yenye rutuba, madini, maeneo ya malisho, bado sipati picha huu umasikini wa Biharamulo unaletwa na nini!?.