=*=*=....BIG UP Faiza Foxy....=*=*=

Hongera FaizaFox na Gozi kwa pamoja.

Kama alivyokuvusha salama kwenye hii miaka 30 ya ndoa, Mungu akuvushe na mengine kama hiyo

Na hapa JF, mwendo uwe ni ule ule tu ili uwe role model kwa wanawake wengine katika kutetea wanavyoviamini

Ahsante Gaijin, ntafutie moja basi ya mnasaba, ya Mohamed Eliyas hivi...
 
30 years in marriage!!
yaani hongera sana manake siku hizi ndoa zimekuwa ndoana, harusi leo baada ya miaka 3 or within 5 years unasikia divorce after divorce. Yaani kuoa/kuolewa imekuwa kama fashion ya kutoa nuksi, utasikia aaah bora kaoa. Kuna ndoa na ndoano, mashehe na mashehena basi ili mradi dunia hii imekuwa na karaha tele
Sijapata jiko na naendelea kutafuta lakini kwa hiyo milestone yako, duuu!! hongera sana na Mola azidi kukujalia wewe na mzee. Kila la heri
 
Ahsante Gaijin, ntafutie moja basi ya mnasaba, ya Mohamed Eliyas hivi...

Nitakurushia special dedication baadae ila nakuachia hii mistari ya Mohamed Ilyas

"pendo lawasikitisha, lina wakata maini
Sisi tutalidumisha, hatujali limbukeni"

Hilo lenu sikitiko, mapenzi yetu kukua
Mmejipa maudhiko, moyoni mnaugua
Mmejiweka kitako, hamwishi kutuumbua
Wetu ndo kwanza mkoko, unaalika maua

Pendo letu linazidi, msemayo mnazua
Tumepeana miadi, kisha tukajizingua
Nyuma katu haturudi, ahadi tumeshatoa
Mtakoma mahasidi, sisi si wa kuchezewa

Mbinu tumezibaini, hakika mmepwelewa
Hatukhofu limbukeni, tuweni msojiiua
Tumepasi mitihani, na shahada tumepewa
Wakudodosa pembeni, irabu zawasumbua
 
<br />
<br />

FF hata hapa ndani wewe hupapasha moto hasa, kwa hiyo pakiwa kimya kunyummba yako JF panalipuka kama si JF (maana ukikosekana hapa kama siku mbili hizi) basi kwako huko mashallah familia inafurahia!

Hahaaaa lol jamani mbona unamkomoa Gozi lakini FF? (daah napenda unavotania juu ya G)

Inshallah natumai watoto walirudi salama!
 

Ahsante sana, hiyo kwenye red ni kweli kabisa, kuna baadhi ya wasichana (geti kali) huwa ni njia ya kufungulia (mageti). Nimeona, yanafanyika na nnaijua mifano hai ambapo mtoto wa kike wanaolewa kwa nia kabisa ya kuachwa baada ya muda si mrefu, ili atoke kwenye utoto na kuingia utu uzima!

Ahsante sana.
 

Duhhh, never knew that!

AlhamduliLlah, watoto wamerudi alfajir kuchukua ku "pack" day bag zao, wamerudi na rafiki zao kundi zima, they are on their way to Kilwa Beach for a trip out, I cant believe it, they spent the whole night out and within 15 minutes they are gone... wheeew. Bora I'll be in peace for the next 2 dayz, nikawachomekea "nchukueni na mimi basi", no one answered, wamejizungusha huku, kule, kama vile hawajanisikia mara "mama tuombee dua, see yah on Monday".
 


I knew it will be a Perfect choice. Thanks a million. Nimeitafuta kwenye collection yangu, nnaisikiliza sasa hivi.
 
Ofcoz you do....mi nilikusikia hata kabla sijarudi huku ndaani baada ya kujipa mapumziko....(u can imagine)

hahaaa FF wakuchukue wapi? Ukawawekee usiku? (i can imagine the way they couldnt even maintain eye contact with you..lol)

Wee kaa hapo nyumbani na Gozi lako, mjisikilizie dedication ya Gaijin na nyinginezo. Wamewap space mmalizie malizie kushereheka! (lol hapo sijui mnakumbusha mambo gani?)

Enjoy today tomorrow and forever!
 


Na mi si "nlichomeka tuu", I know I wouldn't fit in. Gozi lina visa hili jamani, limeondoka asubuhi mapema basi ujue harudi mpaka atafutwe kwa simu. Hana Jumamosi wala Jumapili.
 
FF siri ya mafanikio basi jamani....nakuonea donge sana ujue...

Ndo maana bado wamo huyo....hehee shughuli j3 hadi J3.
 
Chei Chei Faiza Foxy! Takupitia leo twende Upanga kwenye Sekela na Hajam
 
FF siri ya mafanikio basi jamani....nakuonea donge sana ujue...

Ndo maana bado wamo huyo....hehee shughuli j3 hadi J3.

Hakuna ujanja wala siri mama niliulizwa na nikajibu haya kwenye post #222:

 
Chei Chei Faiza Foxy! Takupitia leo twende Upanga kwenye Sekela na Hajam

Chei chei, mie favorite yangu bokoboko! duhh, ulipate kwa samli saafi ile ya Dodoma au Singida? hee he.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…