Biden-Trump 2020 Confusion Matrix

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
US President in 2021False Fraud AllegationsTrue Fraud Allegations Remarks
President BidenJamii itawaona chama cha Republican na Rais Trump ni ving'ang'anizi tu wa madaraka. Watu wasiokubali kushindwa. Wanaotumia mbinu mbalimbali kutaka kung'ang'ania madaraka. Rais Biden atafuta mengi aliyoagiza Trump yafanyike, na kuweka ya kwake. Idadi ya majaji mahakama kuu inaweza kuongezwa, na Biden kuchagua majaji wapya. Maamuzi ya mahakama kuu yakawa ya mrengo wa kushoto. Jimbo la Kalifonia linaweza kugawanywa mara tatu na hivyo kuongeza viti vya ushindi kwa Democrat kwenye chaguzi za Rais. Washington DC ikageuzwa kuwa jimbo, jambo litakaloongeza uwezekano wa Democrats kushinda chaguzi zijazo karibu zote.Chama cha Republican na hasa washabiki wa Trump watakuwa na ghadhab. Wengi watakosa kabisa imani na mfumo wa uchaguzi Marekani. Hapatakuwa na mshikamano na umoja wa kitaifa.Kushinda baada ya korti kufanya maamuzi au kura zote kuhesabiwa.
President TrumpChama cha Democrat na hasa washabiki wa Biden watakuwa na ghadhab. Wengi watakosa kabisa imani na mfumo wa uchaguzi Marekani. Hapatakuwa na mshikamano na umoja wa kitaifa. Panaweza kuzuka vurugu kama za zama za BLM.Jamii itawaona chama cha Democrat na VP Biden ni wenye uchu tu wa madaraka. Watu wasiokubali kushindwa. Wanaotumia wizi wa kura kutaka kunyakua madaraka. Rais Trump atafuta mengi yaliyoasisiwa na chama cha Democrat, kwa vile ni muhula wake wa mwisho kuwa Rais. Haki ya wananchi kumiliki bunduki itaimarishwa. Anaweza kuwashukia Twitter, Facebook na wenzao kuwaweka fungu moja la wachapishaji.Kushinda kupitia kortini au kwa kura zote kuhesabiwa au kwa kutangaza hali ya hatari.
RemarksSifa ya Marekani kama kinara wa demokrasia duniani itakuwa imeingia mashakani isivyostahili.Sifa ya Marekani kama kinara wa demokrasia duniani itakuwa imeingia mashakani kihalali.Patakuwa na kazi kubwa kuunganisha taifa baada ya uchaguzi na kuimarisha misingi ya kidemokrasia
References

Biden-Trump 2020 Confusion Matrix

Siye wengine ni wapenzi watazamaji tu tunaosubiri kuona sinema hii itaishaje.

Edit 1: Watazamaji wengine

EDIT 2: Barua ya Mkurugenzi wa Intelijensia ya Marekani Kwenda Seneti Januari 07 2021

EDIT 3: The Marekani 2020 Movie Plot

1. John Glubb published his famous The Fate of Empires and Search for Survival book in 1976. He claims empires last for 250 years, give or take.

2. The United States of America (USA) declared independence in the year 1776. The 250 years time-period is almost gone. What will be the fate of USA?

3. The USA 2020 elections are peak in terms of what is at stake: Democrats think that four more years of Trump will truly mean the end of USA as we know it. The Republicans think that four years of Biden (Harris / Clinton) will surely be the end of the republic. That is why this question is posed: Who is this movie's Hero ("stelingi")? Who is the main Villain ("Kubwa la Maadui")?

4. Each
side accuses the other of being the stooges of foreign bad guys. The left accuses Trump of being the stooge of Russians (Putin), while the Right accuses Biden to be the stooge of China (CCP). Which is which?

5. The Left blamed Russia for election losses in 2016. The Right blames China, Italy and others for the 2020 election loss. Was there election interference in the year 2016? What about year 2020? If there was, what does it mean to the republic?

6. What will happen to the American Republic? If USA falls as a republic, what chances of survival for newer, less stronger republics? Will USA fall?
7. A republic, if you can keep it ~ Benjamin Franklin (1787). Will the USA survive, and get new lease of life as a republic, for the next 250 years?

Edit 4: January 21 2021. Congratulations to President Biden. This discussion have reached its EOL.
 
Attachments

  • DNI_Letter_analysts_copy.pdf
    6 MB · Views: 5
Marekani ni pasua kichwa! Anatoka nafuu anaingia afadhali!
Nafuu mwenyewe hataki kutoka.

Hata hivyo, kwa uchaguzi huu, inawezekana kabisa sasa tukapata vyama vya siasa halisi vya Marekani. Kwani kwa sasa hapo US kuna chama kimoja tu cha REPU-DEMO! Ajenda yake moja.
===
Kuhusu hiyo matrix, ni kweli katika hali ya sasa itakuwa vigumu kuwaunganisha wamarekani! Labda wapigwe wote chini Biden na Trump na nchi ichukuliwe na Pentagoni!
 
Nadhani si vema kwa Rais wa Marekani kuwa madarakani huku akituhumiwa wizi wa kura. Kama kura hazikuibiwa, itakuwa ni ushindi maridhawa kwa Team Biden. Kama kura ziliibiwa, basi Trump arudi madarakani. Wazikague kura, wahesabu upya, na wachakate upya. Vyovyote vile kujiridhisha. Maana sasa hivi dunia inaangalia.

Baada ya hayo waweke utaratibu ambao itakuwa ni vigumu kwa mtu yoyote kudai kaibiwa kura.
 
===
Nadhani hii habari ya uchaguzi wa US haijafika tamati.
 
Nadhani si vema kwa Rais wa Marekani kuwa madarakani huku akituhumiwa wizi wa kura. Kama kura hazikuibiwa, itakuwa ni ushindi maridhawa kwa Team Biden. Kama kura ziliibiwa, basi Trump arudi madarakani. Wazikague kura, wahesabu upya, na wachakate upya. Vyovyote vile kujiridhisha. Maana sasa hivi dunia inaangalia.

Baada ya hayo waweke utaratibu ambao itakuwa ni vigumu kwa mtu yoyote kudai kaibiwa kura.

hata kama kweli zillibiwa, jambo ambalo siyo kweli hasa kwa vile state anazolalamikia zinangozwa na republican. Lakini kwa muda tujifanye kukubaliana na theory hiyo ya kura kuibiwa, hilo likitokea basi uchaguzi unakuwa nullified, halafu Spika Pelosi ndiye anachukua madaraka ya uraisi na kumteua mtu mwingine yeyote kuwa makamu wake. Ndivyo katiba ilivyo; Trumpians wanalalamika kitoto kwa kudhani kuwa kupinga uchaguzi kunampa mwanya Trump kuendelea kutawala kumbe mambo yako complicated zaidi.
 
Sifa ya Marekani kama kinara wa demokrasia duniani itakuwa imeingia mashakani isivyostahili
Ni kweli na yanayotokea leo 06.01.2021 huko DC ni kielelezo cha maelezo yako.

Donald Trump kwa kutumia mtandao wa tweeter pamoja na Insta kama sikosei aliweza kuwahamasisha wafuasi wake wafanye uchafuzi (4 people died). USA wamevuliwa nguo mchana kweupe, je wana cha kusema kuhusu mataifa mengine ulimwenguni? Turkey wamewaonya raia wake walioko USA wasivinjari nje kwa sababu USA sio salama.
 
Siku hizi tatu zitatoa picha muvi la Marekani litaishaje!

View attachment 1669153
1610143821838.png
TUJITEGEMEE na Mlenge, ni heri mngejikita tu katika siasa za dunia ya tatu kama Tanzania ambako Rais ni mungumtu. Nawashauri kama mnampenda Trump kiasi hicho, mkanywe naye chai ikiwezekana huko atakakojikuta siku si nyingi kutoka sasa. Misingi imara ya demokrasia na taasisi zilizojitosheleza haziruhusu hayo mnayotamani yatokee nchini Marekani...labda Urusi na China.
 
Misingi imara ya demokrasia na taasisi zilizojitosheleza haziruhusu hayo mnayotamani yatokee nchini Marekani.
Ha ha haaa! Tukanywe naye chai tena !
====
Turudi kwenye uhalisia.

Mkuu, wewe ni miongoni mwa wale mara zote unasema US ni bingwa wa demokrasia, na haki za binadamu ikiwemo ile haki ya kujieleza! Na mnainukuu mara nyingi kauli hii. Sasa, walichofanyiwa, waandamanaji raia wa US hiyo tarehe 06/01/2021 ndiyo demokrasia, ndiyo haki hiyo ya kujieleza, ?

Polisi wa US wameua waandamanaji!! Haya yana tofauti gani na yatokeayo kwenye nchi unazoziita za ulimwengu wa tatu?

Rais mteule (Biden) anawaita jina baya wananchi wa nchi yake ili 'wapigwe mawe' kwa sababu tu wanapinga mchakato wa kutia mashaka makubwa wa uchaguzi uliomuweka madarakani...eti ni terrorists waandamanaji wale...!! Hii inatofauti gani na yale yafanywayo na baadhi ya watawala wa nchi zile unazoziita za ulimwengu wa tatu ya kubambikia kesi eti za ugaidi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha nakadhalika?

Mkuu, mwasema kuwa US kila kitu ni 'liberty'. Kwamba huko ndiko 'dissidents' wanaweza kupokelewa wakafaidi 'liberty'. Sasa, hivi visa na vitimbwi anavyofanyiwa Trump kisa kawatikisa 'deep state' au 1% US population au US elites ni sahihi!? Hawa elites wanatumia vyombo vyao vya habari kumnyima liberty yake Trump aliyopewa na katiba ya US, yaani liberty ya kujieleza. Hakuna liberty US ni viini macho tu! Liberty inayotolewa US ni ya mambo ya kuwafanya elites wazidi kuneemeka, tena ni mambo ya hovyo kabisa..! Kuyaorodhesha hapa mambo hayo ya ovyo, ni kunajisi uzi huu (siyaandiki)! Trump kanyang'anywa liberty yake! Soma ushahidi hapa chini!

Wakati wa kampeni za kumuweka Trump madarakani, nilisema H.R.Clinton akiwa rais wa US, US itaporomoka kwa kasi sana; lakini, Trump ataiporomosha polepole. Kwa kiasi fulani Trump katimiza utabiri wangu kwa baadhi ya maeneo. Hata hivyo, kafanya kitu kikubwa kuusaidia ulimwengu kujua 'fitina' na unafiki ufanywao na US kwa ghiliba za demokrasia na eti haki za binadamu na kujieleza. Hii nampa heko.
---
Mkuu, kusema sisi twatakiwa tujadili masuala ya nchi unazoita za ulimwengu wa tatu badala ya US ni jambo la kushangaza haswa. Kwa sababu, suala la demokrasia, haki za binadamu mambo ya haki za kujieleza nayohimizwa na US yafanywe kwenye baadhi ya nchi uziitazo za ulimwengu wa tatu, kwa kiasi kikubwa sana hayafanywi na hiyo hiyo US . Hivyo, nakushauri, upitie upya ushauri wako wa masuala gani tujadili na kisha 'u-package' vema huo ushauri na uulete tena hapa, nitaupokea kwa mikono miwili. :):):)

Mchana mwema.
 
Siku hizi tatu zitatoa picha muvi la Marekani litaishaje!

View attachment 1669153

You know the game is over. Finito. Koniec.
Zakumi,

Ukiangalia time-stamp ya post yangu niliyojinukuu, niliiposti tarehe 05 January 2021. Matukio ya tarehe 06, 07 na 08 ndio yamezidi kulinogesha muvi. Hili muvi stelingi na kubwa la maadui wote bado wapo, linaishaje kwa mfano? Muvi lina sub-plots lukuki; unasemaje limeisha?
 
Ha ha haaa! Tukanywe naye chai tena !
Ndugu yangu, sidhani kama hata unafuatilia na kuelewa kile kinachoendelea ndani ya US na kujaribu kukuelewesha nadhani ni heri hata kujaribu kuielewesha meza sebuleni.

Hii inaitwa A history in the making na visa vyote unavyovishuhudia kwenye vyombo vya habari viko wazi na hata watoto wa shule wanakatizwa masomo waweze kufuatilia yanayojiri.

Nakuomba uendelee kufuatilia yanayojiri na ujizuie kutoa maoni yasiyo na maana...watu kama wewe ndio mnawawezesha watawala wa kiimla. Heri mwenzako aliyeamua kununua popcorn!
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽
View attachment 1672247
TUJITEGEMEE na Mlenge, ni heri mngejikita tu katika siasa za dunia ya tatu kama Tanzania ambako Rais ni mungumtu. Nawashauri kama mnampenda Trump kiasi hicho, mkanywe naye chai ikiwezekana huko atakakojikuta siku si nyingi kutoka sasa. Misingi imara ya demokrasia na taasisi zilizojitosheleza haziruhusu hayo mnayotamani yatokee nchini Marekani...labda Urusi na China.
 
Watu wasio na exposure kubwa ndiyo walivyo Mkuu huropoka ropoka ujinga wakidhani demokrasi ya USA inaweza kuchezewa chezewa hovyo na wahuni.
Ndugu yangu, sidhani kama hata unafuatilia na kuelewa kile kinachoendelea ndani ya US na kujaribu kukuelewesha nadhani ni heri hata kujaribu kuielewesha meza sebuleni.

Hii inaitwa A history in the making na visa vyote unavyovishuhudia kwenye vyombo vya habari viko wazi na hata watoto wa shule wanakatizwa masomo waweze kufuatilia yanayojiri.

Nakuomba uendelee kufuatilia yanayojiri na ujizuie kutoa maoni yasiyo na maana...watu kama wewe ndio mnawawezesha watawala wa kiimla. Heri mwenzako aliyeamua kununua popcorn!
 
Watu wasio na exposure kubwa ndiyo walivyo Mkuu huropoka ropoka ujinga wakidhani demokrasi ya USA inaweza kuchezewa chezewa hovyo na wahuni.
Ndugu yangu, Pro-Trump insurrection imeitwa the darkest day in democracy! Katika kutafuta kujiokoa Trump ameyanajisi mabaraza ya wawakilishi wa Wamarekani (Congress) na amenajisi idara nzima ya mahakama. Halafu wapo wapumbavu wanaotumia neno eti Deep State bila kujua wanaongelea nini!
 
Mimi Mkuu nimefurahi sana kuona demokrasi ya Marekani ilivyokuwa imara kutokana na kuwa na very strong institutions. Trump aliamini kwamba uongo wake wa kuwepo na kura fake na pia kura zake kutohesabiwa ungeweza kumrudisha WH kwa mlango wa nyuma kupitia SCOTUS kwa kuwa kule GOP wana majority ya 6 to 3 lakini kule wakasimama imara kuilinda constitution yao kwamba maamuzi ya Wamarekani wanataka nani awaongoze hayawezi kuchezewa hovyo hovyo kwa ushahidi FAKE.
Na hii ya jana ya Twitter kumpa ban permanently imewafurahisha watu wengi sana kwani sasa hana ukumbi tena wa kuandika ujinga wake.
Ndugu yangu, Pro-Trump insurrection imeitwa the darkest day in democracy! Katika kutafuta kujiokoa Trump ameyanajisi mabaraza ya wawakilishi wa Wamarekani (Congress) na amenajisi idara nzima ya mahakama. Halafu wapo wapumbavu wanaotumia neno eti Deep State bila kujua wanaongelea nini!
 
Ili tuwe pamoja, baadhi ya ploti kwenye muvi hili ni kama ifuatavyo:

1. Nani ndiye stelingi wa muvi -- Trump au Biden?
2. Nani ndiye 'Kubwa la Maadui' -- Trump au Biden?
3. Palikuwa na wizi kweli wa kura au la?
4. Kama ulikuwapo wizi, ulikuwa mkubwa wa kutosha kubadili matokeo au la?
5. Na iwapo ulikuwapo wizi, nani alikuwa ni mnufaika wa wizi huo?
6. Majimbo mengine yasiyoridhishwa na mchakato wa uchaguzi, yatafanya nini?
7. Nini mustakabala wa Marekani kama Jamhuri au kama Demokrasia?
 
Mkuu watu wanapojadili mambo ya maana ambayo watu wamefariki usilete utani wa kipuuzi. Kuna jukwaa la vichekesho huu upuuzi wako peleka kule utapata wachangiaji.

Asante kwa kuchangia. Upi unaona ni utani katika ninayoyazungumzia?
 
Back
Top Bottom