Nimependa hiyo ya senate kuhesabu na kuhakiki kura zote.Inapunguza vote rigging.
Iwapo electoral college vote ndio muhimu basi kuna haja gani ya kuwa na popular votes
Ili mgombea aweze kushinda electoral college votes za jimbo, ni lazima ashinde popular votes za hilo jimbo [statewide popular votes].
Kwa hiyo, mwisho wa siku national popular votes hazitumiki kuamua nani ndo mshindi.
Majimbo 48/50 yana utaratibu wa winner-take-all.
Yaani, mgombea anayeshinda popular votes za jimbo, anapewa electoral college votes zote za hilo jimbo.
Hizo electoral college votes zinakuwa allocated kwa jimbo kwa kuchukua idadi ya wawakilishi lilinao hilo jimbo kwenye bunge la Marekani [House of Representatives] na kuongeza wengine wawili kuwawakilisha ma seneta wa jimbo.
Kwa mfano, kama jimbo la Tennessee lina idadi ya wawakilishi 8 kwenye bunge, basi litakuwa na idadi ya hizo electoral college votes 10.
8 za kuwakilisha hao wabunge na mbili za kuwakilisha maseneta.
Kila jimbo Marekani huwa lina maseneta wawili.
Majimbo mawili, Nebraska na Maine, hayana huo mfumo wa winner-take-all.
Yanatumia mfumo wa congressional district [method].