Biden atashinda, Trump is done

Biden atashinda, Trump is done

Kura za maoni ( Opinion polls) & kura za wengi ( Popular vote) hazina maana yeyote kwenye kuamua nani awe Rais zaidi ya kuonyesha maoni ya wapiga kura!

Uamuzi wa nani awe Rais wa Marekani unafanywa na Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi ( Electrol College) na si vinginevyo.

Kusema Trump atashindwa eti kwa sababu ya maoni ya Wamarekani ni kichekesho kikubwa.

Mfumo huo uliwekwa mahsusi kubalance Matokeo ya Uchaguzi ili Kuzuia baadhi ya majimbo yenye wapiga kura wengi au Jamii ya Watu walio wengi au Chama chenye wafuasi wengi kuamua nani awe Rais! Pia unazuia kura za MIHEMUKO Kwenye kuamua nani awe Rais wa Taifa hilo kubwa Duniani.

Wajumbe wa Baraza ndiyo wamepewa majukumu Kisheria na kwa mujibu wa Katiba kuchagua Rais wa Marekani kwa niaba ya Wamarekani Wote!

Kuna Kampeni zimeshika Kasi kufuta Mfumo huo wa kuchagua Rais kwa kutumia Baraza la Uchaguzi ila utahitaji upitishwe na Baraza la Wawakilishi, Seneti na Kupigiwa kura na Wamarekani Wote
 
Sijui uko wapi. Lakini kama uko Marekani, basi utagundua kuwa watu wengi wanaomuunga mkono Trump huwa hawapendi kusema sema hadharani kuwa wanamuunga mkono.

Na hiyo ni moja ya sababu inayoweza ku skew hizo opinion polls...
The silent majority.
 
Imebaki wiki tatu lakini naamini
Biden keshashinda na Trump keshashindwa.

Nimeangalia factors tofauti

1. pesa ..siku zote mgombea anaeweza changisha hela nyingi anashinda
Biden kamzidi Trump Kwa mbali

2. swing states..
Ohio na Florida kote Biden ana lead

3. Pandemic.
Hili mradi ni main news Trump hawezi shinda..

Naona Biden atakuwa new President
Trump is done..
Wote ni wa hovyo tu, vizee visivyo na maana yoyote

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa. Mwalimu wetu wa Civics O level alitudanganya kwamna hii electoral college ni Wamarekani wachache ambao wamesoma na wana hela ndo wanapiga kura na kuamua hatima ya urais wa Marekani. Nilivyokuja kugundua kuwa alitutia changa la macho nilicheka sana
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kura za maoni ( Opinion polls) & kura za wengi ( Popular vote) hazina maana yeyote kwenye kuamua nani awe Rais zaidi ya kuonyesha maoni ya wapiga kura!

Uamuzi wa nani awe Rais wa Marekani unafanywa na Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi ( Electrol College) na si vinginevyo.

Kusema Trump atashindwa eti kwa sababu ya maoni ya Wamarekani ni kichekesho kikubwa.

Mfumo huo uliwekwa mahsusi kubalance Matokeo ya Uchaguzi ili Kuzuia baadhi ya majimbo yenye wapiga kura wengi au Jamii ya Watu walio wengi au Chama chenye wafuasi wengi kuamua nani awe Rais! Pia unazuia kura za MIHEMUKO Kwenye kuamua nani awe Rais wa Taifa hilo kubwa Duniani.

Wajumbe wa Baraza ndiyo wamepewa majukumu Kisheria na kwa mujibu wa Katiba kuchagua Rais wa Marekani kwa niaba ya Wamarekani Wote!

Kuna Kampeni zimeshika Kasi kufuta Mfumo huo wa kuchagua Rais kwa kutumia Baraza la Uchaguzi ila utahitaji upitishwe na Baraza la Wawakilishi, Seneti na Kupigiwa kura na Wamarekani Wote
Huu pia ni uongo mwingine uliozagaa kwa Watanzania wengi kuhusiana na "electoral college votes", kwamba ni kura ambazo zinapigwa na Wajumbe wa baraza la uchaguzi...!! Mkuu Nyani Ngabu hebu tolea ufafanuzi kinaga ubaga juu ys mfumo wa electoral college votes. Naona huyu nae ni mhanga wa uongo kama ambavyo mimi nilidanganywa na mwalimu wa Civics O level. Uzalendo Wa Kitanzania
 
Hii ni 2020. Sioni Trump akishinda. I trust Americans and their sense of good judgement. Ila ikitokea Trump akashinda basi imani yangu kwa marekani na wamarekani itapungua sana
 
Huu pia ni uongo mwingine uliozagaa kwa Watanzania wengi kuhusiana na "electoral college votes", kwamba ni kura ambazo zinapigwa na Wajumbe wa baraza la uchaguzi...!! Mkuu Nyani Ngabu hebu tolea ufafanuzi kinaga ubaga juu ys mfumo wa electoral college votes. Naona huyu nae ni mhanga wa uongo kama ambavyo mimi nilidanganywa na mwalimu wa Civics O level. Uzalendo Wa Kitanzania
[/QUOTE]

Soma nyaraka rasmi zinazohusu Baraza la Uchaguzi Marekani na uache kutegemea kupewa hadithi na mtu MWINGINE!
 
Leta hizo nyaraka rasmi hapa tuzisome mkuu
 
Shadow government ndio iliyomweka pale trump kipind ameshindwa na hilary..na ndo kitakachotokea hata kwa biden..trump yupo kimkakat pale marekan...waalikua wanahitaj rais chiz ambae kwa macho ya dunia lawama zote atatupiwa trump kwa yanayofanywa na marekan..na sio marekan..so decisions znazofanywa na marekan now ambazo znaonekana ni mwiba znawanufaisha marekan zaid ya lawama....wazungu ni racists..wazungu watemi.etc..ndo wanachotaka hko so trump anawaafaa zaid
 
Kura za maoni ( Opinion polls) & kura za wengi ( Popular vote) hazina maana yeyote kwenye kuamua nani awe Rais zaidi ya kuonyesha maoni ya wapiga kura!

Uamuzi wa nani awe Rais wa Marekani unafanywa na Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi ( Electrol College) na si vinginevyo.

Kusema Trump atashindwa eti kwa sababu ya maoni ya Wamarekani ni kichekesho kikubwa.

Mfumo huo uliwekwa mahsusi kubalance Matokeo ya Uchaguzi ili Kuzuia baadhi ya majimbo yenye wapiga kura wengi au Jamii ya Watu walio wengi au Chama chenye wafuasi wengi kuamua nani awe Rais! Pia unazuia kura za MIHEMUKO Kwenye kuamua nani awe Rais wa Taifa hilo kubwa Duniani.

Wajumbe wa Baraza ndiyo wamepewa majukumu Kisheria na kwa mujibu wa Katiba kuchagua Rais wa Marekani kwa niaba ya Wamarekani Wote!

Kuna Kampeni zimeshika Kasi kufuta Mfumo huo wa kuchagua Rais kwa kutumia Baraza la Uchaguzi ila utahitaji upitishwe na Baraza la Wawakilishi, Seneti na Kupigiwa kura na Wamarekani Wote
Wananchi ndo wanaochagua ndio maana wanaenda kupiga kura. Hao wajumbe unaowasemea wao wanapiga kura mshindi akiwa ameshajulikana Ni Nani, na ndio maana wanapiga kura wiki kadhaa baada ya Uchaguzi na Ni vigumu kubadilisha matokeo kwani huenda Kama kumuidhinisha Rais mteule.

Unachopaswa kufahamu Ni kwamba hao wawakilishi wanatoka kila Jimbo na kila Jimbo Lina idadi ya wawakilishi. Iko hivi; mgombea anayeongoza kwa kupata Kura nyingi kutoka za wananchi katika Jimbo Fulani Basi ndiye anayechukua zile kura za wawakilishi. Mfano New York ina wawakilishi/ electral colleges 20 Basi Biden akiongoza kwa kupata kura nyingi za wananchi anazawadiwa 20 na hizo ndo kura zake. Utaratibu huu utaendelea hivo kwa majimbo yote. Baada ya hapo kinachojumlisha Ni idadi ya namba za wawakilishi ulizojikusanyia kutoka kila Jimbo ambalo umeongoza kwa kupata kura nyingi A wananchi.
 
Mtoa maada na kenge waliounga msafara wake imeonesha ya kwamba wengi humu wanamezaga takataka za cnn bila hata kuzichambua,

Hizo kura zwnyewe za maoni wamarekani walishastukia mchezo zilikuwa na lengo la voter suppression kwamba mfano mtu akitaka kumpigia kura A akaona mpinzani wake B yupo juu kura za maoni anakata tamaa, Cnn ndio vinara wa michezo hii na wamarekani walishawastukiaga ndio maana hata 2016 licha ya voter suppresion Trump ali win.

Trump kafanya mambo mengi sana aisee na kuvunja rekodi nyingi sana za kiuchumi ila tusiende mbali, Kwa muhula wa kwanza pekee trump kafanya kuwe na Waafrika wamarekani wachache zaidi kuwahi kutokea kukosa ajira, hii ni rekodi kubwa na hutakuja kuzisikia cnn, Obama aliishia kupiga picha na kina jay z,

Trump Minne Tena inamuhusu bila pingamizi
 
Shadow government ndio iliyomweka pale trump kipind ameshindwa na hilary..na ndo kitakachotokea hata kwa biden..trump yupo kimkakat pale marekan...waalikua wanahitaj rais chiz ambae kwa macho ya dunia lawama zote atatupiwa trump kwa yanayofanywa na marekan..na sio marekan..so decisions znazofanywa na marekan now ambazo znaonekana ni mwiba znawanufaisha marekan zaid ya lawama....wazungu ni racists..wazungu watemi.etc..ndo wanachotaka hko so trump anawaafaa zaid
Mkuu hivi mnajikutaga kisa mnajua vimaneno maneno vya english ndo mnajikuta mnajua siasa au?? Yani unalopoka tu shadow governent utafkiri aliiunda babu yako.
 
Unahis shadow government hazipo?au unaelewaje maana ya shadow government..mbona hata bongo ipo...watu wanaoamua mustakabal wa nchi hata kama wanavunja democrasia.umoja etc...

Watu ambao hawako kwenye serikal au wapo ..wenye kufanya maamuz mazito...

Kwa tanzania weng wanakuaga ni marais wastaafu.ma jaji.mawazir wakuu wastaaf na wafanya biashara wakubwa....hao huwa wanaitwa na system na kuulizwa wazee mnaonaje hapa.tunafanyaje situation kama hii....maamuz yanayotoka hapo hata kama wananch wamepiga kura.hao wazee wakiamua ndo imepita hyo...kama hutak kuamin.bas leo ndo nakwambia haya mambo yapo....soma sana vitabu mkuu
 
Sababu ya kwanza haina uhalisia. Hillary Clinton alikusanya pesa nyingi sana zaidi ya Trump ila hakushinda. Sababu nyingine sijui
 
Simple!

Ni kwa sababu ya blowback wanayoweza kupata.

Liberals/ Democrats wanapenda sana shari. Kwa mfano tu, hizi ghasia za mwaka huu huko Marekani unadhani ni washabiki wa nani wale waliokuwa wakizifanya? Republicans or Democrats?

Mtu hata kwa mfano ukivaa MAGA hat hadharani, uwezekano wa wewe kuwa harassased ni mkubwa sana.

Ndo maana baadhi ya watu wanaomuunga mkono wanaona kunyamaza ni bora zaidi kuliko blowback watayoipata lakini ikija siku ya kupiga kura, kwa sababu kura ni siri ya mtu, wanampigia kura mgombea wao.

NB: hiyo haimaanishi kwamba Trump atashinda au la...but it is the case.
Kumbe ndio The silent majority yenyewe inayosemwa. Nimekuelewa sana hapa
 
Back
Top Bottom