zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,239
- 39,816
- Thread starter
-
- #101
Duuh dunia ina mengi sikuwahi isikia hii mkuuNa kuna other schools of thoughts kuwa Noah aliingiliwa kimwili na kuhasiwa na mwanawe ili asipate mtoto wa nne ndio hasira zake kumlaani mtoto wa nne.
Google.com.Catholic dictionary.
Mkuu nilifikiri pia hata waislam huwa wanaquote hadeeth kadha wa kadha ili kupanua uelewa wa masuala fulani ya imani yaoNdio maana Mungu aliona Bible haijakamilika akaleta Qur'an, yote ya nini kuangaika na mavitabu lukuki wakati Quran ime summarize
Ndio wanaquote lakini ni tofauti na Bible ambayo km ulivyonukuu inakuambia uende kwenye kitabu fulani, Qur'an yenyewe ina conclude yenyewe haiitaji msaada wa nyongeza kwenye vitabu vyengine .Mkuu nilifikiri pia hata waislam huwa wanaquote hadeeth kadha wa kadha ili kupanua uelewa wa masuala fulani ya imani yao
Yes kwamba havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu na havikuandikwa na manabii wanaotambulika na vingine viliitwa forgery kabisa..... Ndio maana hata kwenye Biblia ya ya Vulgate apokrifa vilitengwa kabisa havikupewa hadhi ya Vitabu vile 66 vya Biblia!!kwani kwenye huo mkutano wa Nicea walitaja sababu ya kuviita hivyo vitabu kuwa ni apokrifa??
Kungezea kidogo hapa, mtoa mada au mtu mwingine yyte anatakiwa afahamu kuwa kuwa biblia inajitosheleza ktk kumpeleka mtu mbinguni ambapo ndiyo lengo na msingi wa ukristo. Inawezekana vitabu vikawepo sawa lakini ktk kujenga msingi wa safari yetu vitabu hivi vinatosha na ilishatambulika kadhia kama hizi zitatokea na hivyo kukawa na stance ktk bible kuwa usiongeze hata nukta moja. Siyo usisome, unaweza kusoma lakini usii distort bible iache kama ilivyo ipo ktk msingi sahihi.1:Kwa maoni yangu, hakuna anayezuiwa kucopy chochote popote ikiwa kitaboresha ukweli mkuu unaofundishwa na bibilia.
Ndio maana bibilia inasema '' Neno la manabii huwatii manabii''. Ikimaanisha Alichokisema Isaya hawezi kuibuka Yohana akakipinga. Na kwa bibilia hiyo kesi haipo,
Hivyo Kuquote au kuchukua maneno kutoka katika vyanzo vingine haivihalalishi isipokuwa '' niñi kilichoquotiwa na kwa madhumuni yapi, na Je! kinakinzana na ukweli mkuu wa bibilia''.
Nimekupa mfano, pale mlimani mars, Paulo aliquote maandishi ya kipagani huko athene '' tunamwabudu Mungu tusiyemfahamu'' na akatumia hiyo quote kuwaelekeza kwa Mungu anayejulikana. Haimaanishi sasa, Kuanzia hapo vitabu vya kichawi vya kigiriki viingizwe kwenye bibilia. La hasha.
2: Siamini kuwa akiibuka mtu akasema kuna kitabu cha bibilia kimepotea basi hiyo kauli yake ni kweli. hayo ni maoni tu yasiyo na uthibitisho wowote labda kama unaweza kujikita zaidi. Kitabu kuzungumziwa haikifanyi kuwa ulikuwa mpango kiwe sehemu ya bibilia. Lkn pia mkuu Bibilia inasema mfano stori zote za Yesu tu, zingeandikwa dunia ingebidi iwe karatasi na miti kalamu.
Kuna mambo mengi yqmeachwa yasiwe sehemu ya ujumbe kwa mwanadamu. Ndio maana huoni hata kama Yesu alienda haja ndogo mahala popote, haimaanishi alikuwa haendi. na ni lazima uandikiwe. Yaliyoandikwa yanatosha kabisa kuhekimisha, kuadilisha,kuonya na kumfanya mtu wa Mungu awe mkamilifu katika Yesu.
3: Hii nadhani nimekusia huko juu. Lakini ninaamini kuna mavitabu mengi fake ambayo yamekuwa backdated na kuhusianishwa na bibilia lkn ni hadithi za kutunga. Mfano Injili ya Barnaba yenye aya zaidi ya 100.
Lkni pia siamini kama Yuda amemquote huyo Enock, Kitabu cha enock hakina uthibitisho wa kushiba kama ni kweli ndiye enock yule au la. Na mambo yake mengi kwa kidogo nilivyopitia yanakinzana wazi na bibilia na ni stori nyingi tena nyingine za ajabu kabisa. Cha ajabu hata hollywood wanavitumia kutunga movie badala ya bibilia.
Mwisho
Hata mimi nasoma kila kitabu, mfano hapa ninakitabu kinahusu uchawi wa Misri, kuna morals and dogma, Kuna mengine mengi nikipata mambo ya kuwaimarishia watu nitaquote haimaanishi mavitabu hayo yatakuwa sehemu ya bibilia kwa sababu tu nimequote.
Pia hakuna ushahidi wa kushiba kuwa hivyo unavyodai ni vitabu vilivyotupiliwa mbali kwenye bibilia au kuwa quoted au reference na hivi vinavyodaiwa ndio vyenyewe leo, mara sijui vimefichwa vya siri ndio hivyo orginal. Maana historia ya ukristo inaonyesha hapo alexandria wasomi wa kale waliandika mambo na mavitabu mengi ambayo yalikuwa na mchanganyiko wa ukweli na uongo na philosophy za kidunia ili kuhalalisha mambo yao.
maoni mkuu unaweza kuwa na changamoto nikiwa siwezi ntasema. Ila Bibilia kwangu mimi ni Final authority nje ya bibilia ni maoni tu ambayo ikiwa yatakinzana na bibilia nayaweka dustbin.
Mkuu labda hoja yangu haikueleweka ni hivi Yuda alimquote Book of Enoch sura ya 6 ili kujengea hoja kuhusu kurudi kwa Yesu na pia Joshua alijengea hoja kutumia reference ya kitabu cha YashariKungezea kidogo hapa, mtoa mada au mtu mwingine yyte anatakiwa afahamu kuwa kuwa biblia inajitosheleza ktk kumpeleka mtu mbinguni ambapo ndiyo lengo na msingi wa ukristo. Inawezekana vitabu vikawepo sawa lakini ktk kujenga msingi wa safari yetu vitabu hivi vinatosha na ilishatambulika kadhia kama hizi zitatokea na hivyo kukawa na stance ktk bible kuwa usiongeze hata nukta moja. Siyo usisome, unaweza kusoma lakini usii distort bible iache kama ilivyo ipo ktk msingi sahihi.
Mkuu nimeelewa hoja yako sana tuu bosi na Mimi pia nielewe. Mfano biblia haijatoa taatifa ya vifo vya mitume wengi wa Kanisa la kwanza aliloacha Yesu lakini Mimi na wewe tunajua kwa wakati ulivyokuwa ingewezekana kila ntume wa baada ya Yesu kujulikana vifo vyao na vingewekwa ktk bible lakini hilo halukufanyika. Vifo vyao vipo ktk historia za machapisho mbali mbali na yameweza kuthibitika kbsa. Point yangu hapa ni hii mengi yalioandikwa ktk bible yanalenga kumshape mtu aelekee ktk njia ya kwenda mbinguni. Pia kuna mengi y ukweli yameachwa, yale yaliyowekwa yanakidhi na kujitoshelza kikamilifu ky serve the purpose ya Ukristo. Sikatai uwepo.Mkuu labda hoja yangu haikueleweka ni hivi Yuda alimquote Book of Enoch sura ya 6 ili kujengea hoja kuhusu kurudi kwa Yesu na pia Joshua alijengea hoja kutumia reference ya kitabu cha Yashari
Sasa mimi zitto junior nauliza je nikiquote let's say Book of Enoch kuhusu malaika kuzaa na wanadamu.... Au kitabu cha Yashari kuwa Kaini aliuawa na mwanae ntakuwa nafanya makosa
Hapa ndipo napouliza
doh!Yes kwamba havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu na havikuandikwa na manabii wanaotambulika na vingine viliitwa forgery kabisa..... Ndio maana hata kwenye Biblia ya ya Vulgate apokrifa vilitengwa kabisa havikupewa hadhi ya Vitabu vile 66 vya Biblia!!
Matope ya wapi hayo mkuu na hadi leo hayo matope hayajakauka?quran inasema jua linazama kwenye bwawa la maji
hatuhitaji kitabu kingine hapa!!!!
Hapa Mkuu umezalisha maswali mengi kuliko majibu,kwa sababu sio lengo la Uzi huu kujadili Quran na uandishi wake! Basi Inshallah! upo wakti wake.Allah anasema hichi ni kitabu kisicho na shaka ndani yake
Na pia akasema "wanasema hii Quran umeindika wewe muhammad basi walete mfano wa kitabu hichi watafute na wasaidizi
Pia akasema walete mfano wa sura moja kama wanasema kweli
Pia akaseama hata tungelishusha Kitabu hichi kwa mfumo karatasi bado wasingesadiki
Na akasisitiza "hich ni kitabu chetu na tutakilinda kwa na aina upotofu"
Mtume Muhhamad aliteua waandish 12 akiwemo Uthuman na Zeyd ambae ndio anatajwa kuwa hafidh mkubwa wa Quran...wakati mtume yupo Quran ilikiwa imeandikwa kwenye magome ya miti na majani na na nyingine imehifadhiwa kwenye maktaba ya kiislam, wakati Umary ndio khalifa alimua kuiweka Quran katika mpangilio wake sababu wakati wa Umar tecnolijia ya kuandika kwenye ngozi ngumu ilikuwa imenza so akaamua kuipangilia kwa mfumo wa kitabu baada ya umary kuondoka akachukua madaraka Uthuman ambae alikiwa msomo na mmoja wa waandish wa Quran wakati wa mtume, alipoluwa safarin oman alikuta Watu wanasoma Quran amabayo imekosewa baashi ya matamshi kwa sababu wakati Muhhamad amewateua wale 12 hakuzuia wengine wanaoweza kuandika waandike wengine walikuwa wapita njia na walikuta muhhamad anateremsha aya nao waliziandika ila mtu ali double check tu kwa wale aliowateua so sababu kubwa ya hao watu kuwa na Quran yenye mapungufu ya kimtamsh ambayo yangebadili maana....
Ndipo Uthaman akarud Makka na akawaita wale waandishi by that time walikuwa wamebaki sita wakaandika Quran Upya kwenye ngozi kwa kipindi hicho teknolojia ilikuwa ime advance na kaagiza watu wote kwa kipindi hicho waende waka copy Quran ile walioyoiandika wao na kila mtu achome moto copy yoyote ambayo yupo nayo iwe ina mapungufu au haina mapungufu...na Quran ile aliyoiandika Uthaman ipo had leo maktaba ya Uturuki na ipo sawa sawa had leo ukilinganisha na Quran tuliyonayo leo..
Uthaman amendika Quran hiyo miaka 10 tu baada ya kufariki muhammad so watu wengi walihifadh Quran walikuwa bado wapo ndio maana hakujatokea utata qa copy za Quran na ukiitazama Quran kwa structure utagundua hakuna mwanadamu anaweza kuindika hata Uthaman angejaribu kuhujumu bado angeshindwa...kasome kitu kinairwa Quran in Numbers utaona miujiza ya kimoangilio na ndio maana Mungu kajitapa anaeweza alete japo mfano wa kitabu hiki,baadae akasema alete mfano sura moja baadae akasema alete mfano wa aya kumi baadae akasema alete japo mfano wa aya moja...hii yote ni kwa sababu ya structure yake na mahesabu ukiacha ujumbe uliyoibeba humu ndani...ndio maana inaitwa LIVING MIRACLE..!
Ujinga ujinga mwingi unaandikwa juu ya Quran na watu wengi tu ila ukiamua kufata vyanzo sahihi utaupata ukweli Quran ni moja tu duniani
Habari za jioni wana JF natumaini wote humu ni wazima.
View attachment 885770
Nlipokuwa naipitia uzi huu Mjue Yoabu - Jenerali Mkuu wa Mfalme Daudi, Katili na asiyeogopa chochote! - JamiiForums
Mkuu Elungata aliibua hoja kuhusu Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja na nathan ila muanzisha uzi alipotaka ushahidi aliuwekea condition hii.
Baada ya kusoma hii comment nilisikitika sana na nilijiuliza sana kwamba inakuaje kila story ya watu waliotajwa kwenye bible watu wanataka reference kutoka ndani ya Biblia pekee as if Biblia imeandika kila kitu?? Kwanini tunapenda kujifunga akili kiasi hicho?
Baada ya kuona mentality hiyo imeanza kukua humu JF intelligence nikaona nilete mada jinsi Biblia yenyewe imetutuma tukasome vitabu vingine nje ya Biblia ili tuongeze ufahamu kuhusu baadhi ya watu na matukio ambayo Bibila yenyewe haikuandika yote kwa upana wake, hivyo nia ya uzi huu ni kwa wale waliojifunga kwenye kusoma maandiko pekee wabadilike na kuwa na fikra huru na kuruhusu maarifa kutoka kona zote kwa mithiri ya kujifunza zaidi na kupanua uelewa wa mambo.
View attachment 885772
Kwa kuanzia tu labda nitumie nafasi hii kumjibu mkuu wangu maishapopote kuwa hata biblia yenyewe inakiri kuwa maisha yote ya Daudi yameelezewa vizuri zaidi nje ya Biblia hivyo imetutuma tukasome vitabu hivyo mnavyoita vya kipagani ili tujifunze kwa ufanisi zaidi
1 NYAKATI 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.
Vitabu vilivyotajwa hapa ni Book of Gad the seer,Book of Nathan the prophet, Book of Samuel the seer (Sio samuel 1&2) ambavyo kwenye biblia havikuwekwa . Sasa kama Biblia inakiri kuwa sio kila story yake imeongelewa kwa upana wake katika biblia je kwanini siku hizi watu wakijengea hoja kuhusu personality za biblia mnalazimisha reference iwe ndani ya bible pekee??? Ina maana waandishi wa Biblia ni wajinga hadi watutume tukasome hivyo vitabu vingine ambavyo mnaviita vya kipagani??
MAANDIKO
Hapa chini nimeambatanisha vifungu vya Biblia hivyo ningeomba tuisome kwa makini kabla ya kuchangia hoja. Neno Tarehe kwenye maandiko haya kwa kiswahili rahisi inamaanisha Nyaraka/rekodi/kitabu au kwa kizungu book/journal/Annal.
View attachment 885773
1. Kitabu cha Yehu
2 Nyakati 20:34
34 Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.
2. Kitabu cha Nabii Gadi muonaji/ Kitabu cha shemaya
2 Nyakati 13:22
22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.
2 Nyakati 12:15
15 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.
1 Nyakati 29:29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji.
3. Kitabu cha mfalme Ahasuero
Nehemiah 12:23
23 Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu
Pia kinatajwa Esther 10:2, 2:23, 6:1
4. Matendo ya Mfalme suleiman
1 wafalme 11:41
41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani (Book of Acts of Solomon)
5. Nyakati za wafalme wa Israel & Yuda
1 wafalme 14:19
19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.(chronichles of the kings of israel/Judah)
6. Kitabu cha Hozai
2 Nyakati 33:19
19 Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.
Hivi ni kwa uchache tu ila kuna vitabu vingine zaidi ya 20 vinatajwa kama reference point kwenye biblia ilihali havipo kwenye Biblia na wala havitambuliki na kanisa lakini leo hii akijengea mtu hoja anaonekana shetani!!
View attachment 885774
HITIMISHO
Baada ya uzi huu nisingetegemea tena kusikia wana JF wakitaka reference kutoka kwenye biblia pekee ilihali Biblia yenyewe inataka tukarefer kwenye vitabu vingine ambavyo vingi ni vya kipagani tu ili tupate uelewa zaidi ya watu muhimu kwenye bible.
However ningependa tujiulize maswali haya ili kupanua fikra zaidi
1. Kwanini vitabu hivi ambavyo Biblia inaturefer tukasome ili kuelewa baadhi ya matukio havikuwekwa kwenye biblia??
2. Na kama havikuwekwa kwa sababu yeyote ile je ina maana ni vya kipagani??
3. Na kama ni vya kipagani ni kwanini vimekuwa referred kwenye bible?
4. Kuna vitabu vingine ambavyo vimenakiliwa hapa ni halali kabisa katika kanisa la kale lakini kwa sasa viko categorized kama vitabu vilivyopotea.... Je nini hatma ya Biblia kama maneno ya Mungu ilihali yanaweza kupotea??
5. Na kama yamepotea je ina maana biblia haijakamilika sababu sehemu ya stori yake imepotea??
Naomba kuwasilisha
Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler
Mkuu nafikiri bado kuna kitu tunakiacha.... Unaposema biblia ilitaka tufaham hicho tu ila mafundisho mengine yana walakini hapo unaniacha njiapanda mfanoMkuu nimeelewa hoja yako sana tuu bosi na Mimi pia nielewe. Mfano biblia haijatoa taatifa ya vifo vya mitume wengi wa Kanisa la kwanza aliloacha Yesu lakini Mimi na wewe tunajua kwa wakati ulivyokuwa ingewezekana kila ntume wa baada ya Yesu kujulikana vifo vyao na vingewekwa ktk bible lakini hilo halukufanyika. Vifo vyao vipo ktk historia za machapisho mbali mbali na yameweza kuthibitika kbsa. Point yangu hapa ni hii mengi yalioandikwa ktk bible yanalenga kumshape mtu aelekee ktk njia ya kwenda mbinguni. Pia kuna mengi y ukweli yameachwa, yale yaliyowekwa yanakidhi na kujitoshelza kikamilifu ky serve the purpose ya Ukristo. Sikatai uwepo.
Kukwoti hivyo vitabu??
Hapa inahitajika uthibisho sana kuhakiki kuwa kweli kitabu cha Gadi ni kile kile au kitabu cha fulani alichokiandika ni kilekile. Pia kumbuka vitabu vya kifalme si kazima viwe vinafaa kwa fundisho la neno la Mungu. Ndiyo maana kwa maneno yako ktk bandiko lako umekwoti yakihusisha habari za vizazi nafkiri biblia ilitaka ktk msingi wake tufahamu hicho tu ktk hicho kitabu labda mengine yanawalakini au hizo rekodi nyingine hazijafaa kwa fundisho
unaamini maandishi ya quran?Matope ya wapi hayo mkuu na hadi leo hayo matope hayajakauka?
inachekesha sanMatope ya wapi hayo mkuu na hadi leo hayo matope hayajakauka?
Mie nimetaka kujua tu kuhusu hayo matope ni ya wapi na hayajakauka hadi leo?unaamini maandishi ya quran?
matope? ni maandishi ya biblia yako unayosema ni maneno ya mungu wa israelMie nimetaka kujua tu kuhusu hayo matope ni ya wapi na hayajakauka hadi leo?
Ndiyo nauliza mkuu maana wewe ndio umesoma na kuelewa,hayo matope ni ya wapi na hayajakauka hadi leo?matope? ni maandishi ya biblia yako unayosema ni maneno ya mungu wa israel
..ahahahaaaa[emoji125]matope? ni maandishi ya biblia yako unayosema ni maneno ya mungu wa israel