Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Nipo late kuona Hio thread.
Lakini argument yako kuhusu thread ya jamaa ambayo Elungata alileta nadharia zake kuhusu Daud kujihusisha na homosexual habits. Hazikujengwa na kutoka kwenye kitabu chochote credible Bali aliyoa kwenye site ambayo inajaribu kutetea ushoga kwa kufanya false interpretation ya vi verse Fulani vya bible. Hata ukisoma maelezo yake. I hisia za yule mwandishi tu hamna evidence wala hoja yoyote ya msingi.






2.pili thread yako inahoji kuhusu biblia kutoa baadhi ya reference ambqzo hazipo kwenye modern canon
Answer.
Hivo unavotaja ni historical books na vipo vingi sana ulitaka vyote viwekwe kwenye bible kwa lengo gani?? Kwani biblia ni chuo cha history ?? Machache ya MUHIMU yameandikwa kwenye some historical books within the bible na wakaweka references kama utaitaji more information kuhusu maswala husika iende uko ukapate more knowledge.


Hii haiwezi Kutumika kama hoja ya kuvalidate matumizi ya tungo dhahania zisizo hata na credible information kutumika kama reference yako kuelewa jambo Fulani katika bible.


Na kama unavyo hivo vitabu na una uhakika navyo asilimia 100% (vilivotajwa kama reference) vitumie tu maadam ulipewa reference so ndokazi ya reference hio mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama Lutu aliweza kulala na binti yake kwanini unaamini daudi hawezi fanya uhuni?? Mbona alimlala mke wa mwanajeshi wake na baadae akamuua kabisa?? Who is David mpaka asifanye huo uhuni??
Uzuri biblia matukio kama hayo inayaandika haiyafichi ndomana mmeyaona waandishi wangeweza pia kufuta usione !!!


Ishu ya lutu kasome vizuri mabinti zake walimlevya hakufanya kwa hiyari yake hivo hatuwezi kumuhukumu

Mfano wewe zitto Jr vidume vilivoshiba kama kumi vikakumata na kukufanyia ulawiti utataka tuje kukulaumu kwanini umefanya uchafu wa jinsia moja ilihali tunajua ulifanywa bila hiyari yako kwanguvu na ulichukia tendo hilo ??


Pili binti zake walidhani ulimwengu mzima wamebaki watu watatu tu baada ya sodoma kuangamizwa!! Waliona it is the only way Ku restart human generation lasivyo human species ingetoweka,na kwakutumia precedence ya awali ya uumbaji kipindi cha adamu ndugu walioana ili waongezeke so yeah they were right in their stupidity hawakuwa ma taarifa kuhusu other peoples existence.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nabii gadi kitabu chake kinakuwaje apocrypha ,correct me if I'm wrong lakini nijuavyo apocrypha age ilikuwa bado sana maana ipo mbele huku nyakati za makabayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa alitumia reference ya gay site unataka tuichukulie serious???

Yaani unafananisha reference ya gay site ( site ya kuteteta ushoga ) na kitabu kilichoandikwa na gadi na Samwel ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N
NaZani wewe ni MTU uliyejibu hoja wengine hawakutaka Hata kuvisikia hivyo vitabu vya reference

Nikuulize aliecombine bible alitumia vigezo gani kuweka vitabu na kutoa?
 
Nadhani hoja yako ni weak haina basis yoyote ya kusimamia

Hata kama kuna baadhi ya vitabu kadhaa vilikuwa referenced ( of which I told you earlier kama ur 100% sure you have that book una haki kabisa ya kusoma na kuongeza maarifa ) but tatizo hivi vitabu vingi vya kihistoria preservation zake haziaminiki maana vingi hata wayahudi hawakutumia kwenye canon yao kwahio ulinzi wa material content ni wa mashaka sana

Na vingi ukivisoma ( kwa vile vilivyopo available) vina information nyingi sana za ukweli hasa za kihistoria lakini bado haviwezi kutika kama spiritual books (in level with canonical) vinakosa authority kutokana na mashaka mengi mnoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko Hapo unapodai mabinti walidhani ulimwengu mzima umeteketea,lutu aliishi sodoma lakini nduguye Abraham aliishi SI mbali na hapo,
Sawa na tuchukue umbali toka kariakoo Hadi pugu ama ubungo,Hapa nakisia,lakini hata kwa Leo ukipima um
Jamaa alitumia reference ya gay site unataka tuichukulie serious???

Yaani unafananisha reference ya gay site ( site ya kuteteta ushoga ) na kitabu kilichoandikwa na gadi na Samwel ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui ulitaka bible iandike waziwazi,kitendo Cha bible kudai mwana wa Saul alimpenda Daud Ni redflag,
Kitendo Cha sauli kumgombeza mwanae kuwa ameitia aibu family kwa urafiki wake na Daud pia Ni gunsmoke
 
Mkuu hoja yako ni contradictory kabisa.

Nachosema ni kwanini mfano Joshua achukue simulizi za Book of Jasher kuwaeleza issue ya jua kusimama alafu mimi nikichukua simulizi za kitabu hiko hiko nionekane sipo credible?

Kama ina mashaka kwanini Joshua alitumia

Unaweza ukatuweka sawa hapo
 
Jamaa alitumia reference ya gay site unataka tuichukulie serious???

Yaani unafananisha reference ya gay site ( site ya kuteteta ushoga ) na kitabu kilichoandikwa na gadi na Samwel ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu toka mwanzo nilisema hoja hapa sio daudi kuwa shoga au lah ila concern yangu ni kwanini source outside the bible imekatazwa na huyo mchangiaji?.

Sasa ndio nauliza kama Bible yenyewe imeturefer kwa outside sources ili kuweza kuongeza maarifa ya historia husika kwanini basi tukijengea hoja kutumia hizo historia iwe nongwa??

Kama hizo source sio credible kwanini basi hao manabii wa Biblia wazitumie kujengea hoja?? Mfano Yudah kujengea hoja zake kutumia Kitabu cha Enock
 
Nabii gadi kitabu chake kinakuwaje apocrypha ,correct me if I'm wrong lakini nijuavyo apocrypha age ilikuwa bado sana maana ipo mbele huku nyakati za makabayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Padre jerome wakati ana tafsiri Bible aliigawa hivyo yaani NT,OT na vile alivyohisi havina uvuvio vikawekwa kipengele cha Apocrypha whether kiliandikwa kabla au wakati wa silent period!!

Otherwise vinaitwa pseudepigraphi kwamba ni vitabu halali kabisa ila vina utata mahali fulani ndio maana vikaachwa

Lakini cha kujiuliza Song of songs na Hebrews ni pseudepigrapha ila havijatolewa kwa bible? Unaweza kutupa maoni yako
 
Mkuu najaribu kujenga picha kwa muktadha wa Nabii wa Mungu kazaa na mabinti zake!! Yaani hata uleweshwe kweli ubakwe tu na mabinti zako kirahisi hivyo?? Kwanini isingetokea radi iwamalize hao watoto??

Nachosema ni hiki..... Kila binadamu yuko prone kwa dhambi bila kujali status yake kwenye Biblia

Mfalme suleiman tunaambiwa ndio mwenye hekima zaidi ila ndio mfalme aliyepelekea anguko la Israel, Samson cjui daudi wote walipotea kabisa kisa ngono ndio sembuse nani??

Yaani nini cha ajabu hadi Daudi ashindwe kutenda dhambi?
 
Jamaa anashangaa Daud kuwa gay,Samson mwenyewe kwa mujibu wa Bible alikua muuaji mkubwa,anaua watu 1000 ili awakate magovi ya kulipa betting,Moses alikuwa muuaji,abrahamu alikuwa tapeli akimtumia mke wake kutega ugoni alipwe mifugo,Solomon alikua womaniser,etc
 
Yote hii kwasababu wao pia walikuwa ni binadamu kama sisi tu hivyo kwa kuwa nao pia walizaliwa, wakaishi katika jamii yao kuna mazuri watafanya na yapo mabalaa kama hivyo. Sasa jamaa huwa wanawatazama kama watu waliokuwa clean sana wakati inaelezewa kabisa Hata Petro alikuwa Mvuvi mwenye silika ya ukorofi sana ukitazama uhalisia wa maisha ukiwa kiongozi hutapendwa na jamii nzima unadhani hao wanaokupinga nini kitawapata mbona ipo wazi. Hao nao walikuwa binadamu sasa watu wanawachukulia kama malaika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada vitabu vilivyokataliwa kwanza vingine vilijaa uongo Wa wazi kabisa ambao mfano hauendani na mafundisho ya Yesu

Mfano kitabu cha Henoko kinatamka wazi kuwa gharika ilikuja sababu malaika walioa na kuzaa na wanadamu .Wakati Yesu alitamka wazi kuwa malaika Hawaoi wala kuolewa na hawazai

Kuhusu agano la kale kanisa halikupata shida kubwa kusema vitabu vipi likubali na vipi likatae sababu waisrael wana Biblia yao tayari.Na ndio agano la kale linawahusu na walitunza kumbukumbu zake vizuri sana .Kuanzia vitabu vya Musa kiongozi wao.
.Wana Biblia yao inaitwa Biblia ya waebrania au Hebrews Bible .Kwa hiyo kanisa lilichukua yote kama ilivyo na kuiweka kama agano la kale.Bila kuongeza wala kupunguza maneno

kwa Agano jipya vilichukuliwa vitabu vile tu vilivyoandikwa na mitume Wa Yesu sio wengineo.Hivyo vingine vikatupwa nje

Kwa hiyo Agano la kale wanalo wayahudi na wanavitumia hadi Leo ndio walikabidhi kanisa.Vitabu ambavyo wayahudi hawavitumii na hawavitambui kanisa pia halivitambui

Kwa hiyo habari zako za vitabu vyote vya agano la kale vilivyokataliwa na wayahudi kanisa halivitambui.Kiwe kitabu cha Henoko sikui japher sijui Jehu na matapeli wengine

agano jipya pia nje ya walichoandika mitume Wa Yesu hakikubaliki.
 
Nabii gadi kitabu chake kinakuwaje apocrypha ,correct me if I'm wrong lakini nijuavyo apocrypha age ilikuwa bado sana maana ipo mbele huku nyakati za makabayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wayahudi wenye nabii wao walikikataa hicho kitabu .Hawakikubali.Na kanisa likakikataa
 
1. Mkuu unaweza kutuambia hiyo Hebrew Bible
(a) Ina vitabu vingapi?
(b) vitaje.
2. Umesema kanisa lilipokea biblia ya kale kutoka kwa Hebrews na wakaitunza Kama walivyopewa bila kubadilisha chochote. Iweje leo zinatofautiana idadi ya vitabu?

3. Umesema hivi vitabu nje ya Bible Ni vya kitapeli mfano jasher, gadi,etc. Mbona biblia imevifanya reference?
Sent using LEAGOO M12
 
Hebrew Bible ina vitabu 39 viko kama vya agano la kale la Biblia yenye vitabu 66 .sio kama ile ya Catholic yenye vitabu 72

Catholic walichakachua agano la kale waligoma kupokea vitabu vya Biblia ya wayahudi .Wakaongeza vyao ambavyo havimo kwenye Biblia agano la kale la wayahudi

Agano la kale hasa wenye rekodi zao halisi ni wayahudi na rekodi wamezitunza vizuriHivyo vingine hawaviitambui
 
Hizo reference hata wayahudi hawana sababu kubwa ya kukosekana mojawapo ni kuwa hivyo vilikuwa havitumiki hekaluni.Na haviko maktaba yoyote ya wayahudi .Kuna wahuni ndio walikuja kuandika kama Novel za enzi hizo wasio wayahudi wakaamua kuvitambua sio kama Novel Bali kama vitabu halali vya kidini

Reliance kubwa ya agano la kale ni biblia ya wayahudi .Hebrew Bible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…