The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,576
- 17,697
Msingi wa dini uko kuanzia mwanzo 1 inayoelezea uumbaji wa Mungu wa binadamu wa Kwanza.
Baada ya Adamu kuubwa, alipewa mke wake akamuita Eva, wakazaa watoto 2, mmoja Abeli mwingine Kaini.
Hao watoto mmoja akawa mkulima (Kaini) na mwingine Abel mfungaji. Mmoja, Abel akapata kibali machoni pake Bwana baada ya kua anamtolea dhabihu ya mwana kondoo alienona( sijui kwa nini Mungu anapenda vitu vinono) na mwingine akawa anatoa dhabihu ya mazao, bwana hakuyapenda. Hata wewe ungekubali, mwingine anakuletea nyama iliyonona mwingine anakuletea mihogo sijui viazi, magimbi, utampenda nani?
Msingi wa hoja yangu uko Mwanzo 4:12- 14 ambapo baada ya Kaini kumuua kaka yake Abeli, Mungu akamtimua Kaini kwenye ardhi aliyokua amewaweka na akamuagiza atoke kwenye eneo lake na kwenda huko kutangatanga.
Kaini akaomba kwamba akitimuliwa kwenye ardhi ile ya kwao akaenda kwenye ardhi nyingine huko nje kutangatanga itakua ni rahisi mtu yoyote yule kumuona na kumuua ama kumdhuru.
Mwanzo 4:15 Mungu anamuahidi Kaini yoyote atakaemfanyia jambo baya Kaini ataadhibiwa mara 7 na Mungu akaahidi kumuwekea alama maalum Kaini ili watu wengine huko nje wamtambue na wasije kumdhuru ama kumuua.
Swali langu linakuja, kama Adam ndio alikua binadamu wa Kwanza, Abel na Kaini ndio walikua watoto wa Adam pekee, Kaini akamuua kaka yake Abel akabaki mwenyewe, hao watu ambao Kaini alikua anahofu watamuua walitoka wapi?
Kumbuka aliefukuzwa Eden ni kaini tu. Na kaini baada ya kufukuzwa Eden akaenda huko kwenye kutangatanga akapata mke, wakazaa mtoto Enoch na kuendelea.
Je biblia inadanganya kuhusu binadamu wa kwanza hapa Duniani ama inajichanganya?