Biashara za mtaji mdogo ukiwa chuo. Anza kujifunza kuhusu biashara mapema

Aug 24, 2021
27
16
Wewe kama mwanafunzi wa chuo, una nafasi nzuri ya kufanya biashara. Kutokana na wingi wa watu waliokuzunguka na kuwa na uwezo wa kujua mahitaji yao. Kwanza inakubidi kutambua mahitaji ya kila siku ya wanafunzi wenzako. Nikimaanisha kuwa mara nyingi mahitaji yako ya kilasiku, ndio mahitaji ya wenzako chuoni. Pia na matatizo yako ya kilasiku ndio matatizo ya wenzako chuoni. Tukianza na jinsi ambavyo chuo ni mahali pazuri sana pa kujijenga kama mfanyabiashara.

Hapa tunaanza na kile unachojifunza wewe kama mwanafunzi. Kwanza unatakiwa kutumia kile unachojifunza kulasiku ili kiweze kukuingizia kipato. Maana ni mambo mengi sana wanafunzi wa chuo ni tunajifunza. Lakini ili tuweze kupata maendeleo inabidi tufike mahali ambapo tunaweza kutumia vizuri kitu tulichokisoma.

Kwanza kabla hatujaingia kwenye kujua biashara hizi za mtaji mdogo kabisa za kufanya chuoni.

Tukirudi tena kwenye kujua biashara izi za mtaji mdogo za kufanya ata ukiwa chuo. Kwanza tufahamu kuwa kila biashara inakuja na changamoto zake. Yawezekana tayari ukawa umeona wanafunzi wenzako wanafanya biashara ndani ya chuo. Lakini kikubwa ni kwamba kuna changamoto zake nyingi sana. Ila wewe kama mfanyabiashara unatakiwa kuwa na Imani kwenye biashara unayo anza. Kwanza tukianza kuongelea biashara ambazo kila siku unaziona wanachuo wenzako wanafanya.

Mfano kuuza chips.

Kuuza chapati.

Biashara ya chai.

Mtori.

Mayai ya kuchemsha.

Nguo za mtumba za kike na kiume.

Mpesa au biashara ya kifedha kwa mitandao yote ya simu.

Kuna Wale wanaouza vitabu.

Biashara ya vifaa vya kielectroniki kama simu una laptop
.

Izo zote ni biashara ambazo wanafunzi hupenda kuzifanya wakiwa chuoni. Lakini kwa upande wetu hapa tunaenda kuangalia biashara nyinginezo kabisa. Ambazo wewe kama mwanafunzi unaweza ukachagua inayokufaa ili ufurahie biashara yako ata kama kutakuwa na changamoto.

Biashara ya kuandika
Nikimaanisha kuwa kama unaweza kuchukua mda wako masaa kadhaa. kuwasaidia kuandika, wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Ikiwemo kuwaandikia ripoti zao au kuwapangilia kazi zao kwa kiwango kidogo tu cha pesa. Utapata faida nzuri sana katika biashara yako hiyo ya mtaji mdogo.

Kikubwa unaweza ukawa na laptop au usiwe nayo ukatumia za wale wale wanaokuletea kazi.

Hapo unahitajika pia uwe na printer na scanner ya kuwavutia Zaidi wateja wako. Maana baada ya kuwaandikia uweze pia na kuwachapishia kazi zao.

Kuandika hakuishii hapo tu: lakini kuna wale wenye uwezo mzuri wa kuandika barua za maombi wakati wa field. Au wale wenye uwezo wa kuandikia vizuri cv, wanafunzi wanaomaliza mwaka wa mwisho. Hizi zote ni biashara nzuri sana za kufanya hata ukiwa na mtaji mdogo.

Biashara ya kupika keki na vitafunwa vya muundo mbali mbali
Kwanza tujiulize ni wangapi wanasherekea siku zao za kuzaliwa wakati wapo chuo?. Maana huo ndio wakati mzuri sana wa kufanya biashara yako hapo. Tukianza na wale wataalamu wa kupika keki. Kama unajua njia yeyote ya kujitangaza ambayo itapokelewa vizuri na wanafunzi wenzako.Utakuwa moja kwa moja umeshajiwekea uhakika wa kufanya biashara yako vizuri.

Kupika hakuiishii tu kwenye keki, bali ata kwenye vitafunwa vidogo vidogo. Vyenye bei ndogo ata kama ni shilingi 100 ukiweza kuona faida kwenye shilingi 100 moja kwa moja utapata ela nyingi sana ukiwa chuo.
 
Hivi buying power ya wana-Chuo ipoje ? Tusije tukawa tunaongelea premium products (cake) wakati uwezo wa wanafunzi ni vitumbua vya Tshs 100/= tena kwa mkopo wa bill ya kulipa siku Boom likija...

All in all hii nchi wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara.., biashara sio kujua tu au elimu ni attitude ya mtu na discipline ya pesa bila kukata tamaa (jambo ambalo wengi hawana)
 
Sawa mie nilikuwaga mpiga picha aina zoooteee!........kabla ya selfie kuwa nyingi....niliishi kwa raha sana...sasa naenda tena hili wazo ntalifanyia kazi faster!
 
Wewe kama mwanafunzi wa chuo, una nafasi nzuri ya kufanya biashara. Kutokana na wingi wa watu waliokuzunguka na kuwa na uwezo wa kujua mahitaji yao. Kwanza inakubidi kutambua mahitaji ya kila siku ya wanafunzi wenzako. Nikimaanisha kuwa mara nyingi mahitaji yako ya kilasiku, ndio mahitaji ya wenzako chuoni. Pia na matatizo yako ya kilasiku ndio matatizo ya wenzako chuoni. Tukianza na jinsi ambavyo chuo ni mahali pazuri sana pa kujijenga kama mfanyabiashara.

Hapa tunaanza na kile unachojifunza wewe kama mwanafunzi. Kwanza unatakiwa kutumia kile unachojifunza kulasiku ili kiweze kukuingizia kipato. Maana ni mambo mengi sana wanafunzi wa chuo ni tunajifunza. Lakini ili tuweze kupata maendeleo inabidi tufike mahali ambapo tunaweza kutumia vizuri kitu tulichokisoma.

Kwanza kabla hatujaingia kwenye kujua biashara hizi za mtaji mdogo kabisa za kufanya chuoni.

Tukirudi tena kwenye kujua biashara izi za mtaji mdogo za kufanya ata ukiwa chuo. Kwanza tufahamu kuwa kila biashara inakuja na changamoto zake. Yawezekana tayari ukawa umeona wanafunzi wenzako wanafanya biashara ndani ya chuo. Lakini kikubwa ni kwamba kuna changamoto zake nyingi sana. Ila wewe kama mfanyabiashara unatakiwa kuwa na Imani kwenye biashara unayo anza. Kwanza tukianza kuongelea biashara ambazo kila siku unaziona wanachuo wenzako wanafanya.

Mfano kuuza chips.

Kuuza chapati.

Biashara ya chai.

Mtori.

Mayai ya kuchemsha.

Nguo za mtumba za kike na kiume.

Mpesa au biashara ya kifedha kwa mitandao yote ya simu.

Kuna Wale wanaouza vitabu.

Biashara ya vifaa vya kielectroniki kama simu una laptop
.

Izo zote ni biashara ambazo wanafunzi hupenda kuzifanya wakiwa chuoni. Lakini kwa upande wetu hapa tunaenda kuangalia biashara nyinginezo kabisa. Ambazo wewe kama mwanafunzi unaweza ukachagua inayokufaa ili ufurahie biashara yako ata kama kutakuwa na changamoto.

Biashara ya kuandika
Nikimaanisha kuwa kama unaweza kuchukua mda wako masaa kadhaa. kuwasaidia kuandika, wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Ikiwemo kuwaandikia ripoti zao au kuwapangilia kazi zao kwa kiwango kidogo tu cha pesa. Utapata faida nzuri sana katika biashara yako hiyo ya mtaji mdogo.

Kikubwa unaweza ukawa na laptop au usiwe nayo ukatumia za wale wale wanaokuletea kazi.

Hapo unahitajika pia uwe na printer na scanner ya kuwavutia Zaidi wateja wako. Maana baada ya kuwaandikia uweze pia na kuwachapishia kazi zao.

Kuandika hakuishii hapo tu: lakini kuna wale wenye uwezo mzuri wa kuandika barua za maombi wakati wa field. Au wale wenye uwezo wa kuandikia vizuri cv, wanafunzi wanaomaliza mwaka wa mwisho. Hizi zote ni biashara nzuri sana za kufanya hata ukiwa na mtaji mdogo.

Biashara ya kupika keki na vitafunwa vya muundo mbali mbali
Kwanza tujiulize ni wangapi wanasherekea siku zao za kuzaliwa wakati wapo chuo?. Maana huo ndio wakati mzuri sana wa kufanya biashara yako hapo. Tukianza na wale wataalamu wa kupika keki. Kama unajua njia yeyote ya kujitangaza ambayo itapokelewa vizuri na wanafunzi wenzako.Utakuwa moja kwa moja umeshajiwekea uhakika wa kufanya biashara yako vizuri.

Kupika hakuiishii tu kwenye keki, bali ata kwenye vitafunwa vidogo vidogo. Vyenye bei ndogo ata kama ni shilingi 100 ukiweza kuona faida kwenye shilingi 100 moja kwa moja utapata ela nyingi sana ukiwa chuo.
Chuoni kunataka biashara ambayo si stationary bali ni mobile na inabebeka kwenywe kabegi simple,uza karanga za mia mia tu funga kwenye vipakti,hii unaweza kuuza hata darasani leckcha inaendelea,Kg 1 ya karanga za kukaanga inaweza kukulazia minimum buk 5 faida. na zinauzika hasaa......achana na mambo ya machapati sijui mtori,yatakupotezea muda tu.
 
Back
Top Bottom