Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Pole sana mzee wa mijibundi, hapo ndo utakumbuka usemi usemao tamaa mbele mauti nyuma
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa pole isiyo na msaada.
Kwa kweli nilikurupuka sikufanya business survey na wala sikuwa hata na business plan, hata vibali vya kufuga bundi kutoka mamlaka ya IATA (INABIDI AJE TANZANIA ASHANGAE) sikuwa navyo na mpaka sasa sina
 
Usinicheke nisaidie mwenzenu naangamia. Nilisahau kuwa kila mchimba shimo huingia mwenyewe. Nimeharibu na kuroga biashara za wenzangu, kumbe wangefanikiwa kwenye biashara zao na kupata fedha wangeweza kutumia uchawi wangu wa bundi na mimi in return ningepata pesa
Mamaweee....hii midege aina ya mibundi nasikia inaletaga uchuro
 
Inabidi ukapimwe mkojo wewe
Nimenunua mijibundi mikubwa kwa midogo kwa mbwembwe nyingi sana. Kwa mikogo na mwendo wa madaha nilijigamba kila kona huku nikiwatambia wapinzani wangu kuwa naenda kuwa juu kama Pierre Liquid Konki Fayaaaaa.
Matarajio yangu ilikuwa niipeleke mibundi yangu nchi jirani na za mbali, hasa Bollywood na Uchinani.
Nimeshindwa, wamesema hawataki uchawi kwenye nchi yangu.
Mibundi mikubwa imelala tu inapigwa na vumbi na kuzeeka, vibundi vidogo navituma mikoani lakini navilisha kwa gharama kubwa na havinipi faida, watu hawana hela nashindwa kuwapiga chuma ulete.
Bora ningekuwa msikivu ningechimba visima wanangu wapate maji kuliko biashara hii kichaa ya uchawi wa mabundi.
Mapovu ruksa

Mti wenye matunda.
 
Hivi hii mibundi hatuwezi kuifanya chuma chakavu ..oh sorry hatuwezi kuifanya kitoweo?
 
Mkuu ndege wote hawa wanaofugwa umekosa hadi kufuga mabundi? Anyway lakini Tz ili utoboe lazima ufanye mambo ya ajabu ajabu kimtindo
 
"Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko, ukalisimamie hilo, kwa sababu nina matatizo sana na baadhi ya miradi ya maji, na ndio maana nimekuwa nikifanya mabadiliko kwenye miradi ya maji, kwa sababu haileti impact. Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa, mradi umetumika milioni 400, zilikuwa milioni 800 lakini maji hayapo, sasa nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavute bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta, ili ukienda kwenye mradi hawa mainjia wa maji wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.
 
Nimenunua mijibundi mikubwa kwa midogo kwa mbwembwe nyingi sana. Kwa mikogo na mwendo wa madaha nilijigamba kila kona huku nikiwatambia wapinzani wangu kuwa naenda kuwa juu kama Pierre Liquid Konki Fayaaaaa.
Matarajio yangu ilikuwa niipeleke mibundi yangu nchi jirani na za mbali, hasa Bollywood na Uchinani.
Nimeshindwa, wamesema hawataki uchawi kwenye nchi yangu.
Mibundi mikubwa imelala tu inapigwa na vumbi na kuzeeka, vibundi vidogo navituma mikoani lakini navilisha kwa gharama kubwa na havinipi faida, watu hawana hela nashindwa kuwapiga chuma ulete.
Bora ningekuwa msikivu ningechimba visima wanangu wapate maji kuliko biashara hii kichaa ya uchawi wa mabundi.
Mapovu ruksa
Kwa definition ya uchochezi ya awamu hii, huu ni uchochezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom