Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Nimenunua mijibundi mikubwa kwa midogo kwa mbwembwe nyingi sana. Kwa mikogo na mwendo wa madaha nilijigamba kila kona huku nikiwatambia wapinzani wangu kuwa naenda kuwa juu kama Pierre Liquid Konki Fayaaaaa.
Matarajio yangu ilikuwa niipeleke mibundi yangu nchi jirani na za mbali, hasa Bollywood na Uchinani.
Nimeshindwa, wamesema hawataki uchawi kwenye nchi yangu.
Mibundi mikubwa imelala tu inapigwa na vumbi na kuzeeka, vibundi vidogo navituma mikoani lakini navilisha kwa gharama kubwa na havinipi faida, watu hawana hela nashindwa kuwapiga chuma ulete.
Bora ningekuwa msikivu ningechimba visima wanangu wapate maji kuliko biashara hii kichaa ya uchawi wa mabundi.
Mapovu ruksa
Vipi ile biashara ya majongoo wa sgr?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni mafumbo....mambo ya kiswahili hayo....wanaume wanatoa strategy sio kulaumu na kunun'gunika kama watoto wa kike.....
 
Hah haha haaaa Watanzania MNA huzuni sana, endelea kuhuzunika mkuu, maana kwako Kila kitu kwako kinakuletea huzuni. Karibu kwenye ulimwengu wa ngonjera
Acheni mafumbo....mambo ya kiswahili hayo....wanaume wanatoa strategy sio kulaumu na kunun'gunika kama watoto wa kike.....
 
Ktk zama hizi za sasa ambazo biashara hiyo imehodhiwa na waarabu ambao wanayatikisa hata mashirika makubwa makongwe ya ulaya, ni chizi tu ndie alieamini kuwa tunaweza kutoboa na hivi videge vyetu vya kizamani.We angalia hapo kwa jirani pamoja na uzoefu wake wote tokea siku zile ilipovunjika EAA bado wanasuasua itakuwa sisi ambao ndio kama tunaanza?
Mi naona itafutwe kiki nyingine hii ishabuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimenunua mijibundi mikubwa kwa midogo kwa mbwembwe nyingi sana. Kwa mikogo na mwendo wa madaha nilijigamba kila kona huku nikiwatambia wapinzani wangu kuwa naenda kuwa juu kama Pierre Liquid Konki Fayaaaaa.
Matarajio yangu ilikuwa niipeleke mibundi yangu nchi jirani na za mbali, hasa Bollywood na Uchinani.
Nimeshindwa, wamesema hawataki uchawi kwenye nchi yangu.
Mibundi mikubwa imelala tu inapigwa na vumbi na kuzeeka, vibundi vidogo navituma mikoani lakini navilisha kwa gharama kubwa na havinipi faida, watu hawana hela nashindwa kuwapiga chuma ulete.
Bora ningekuwa msikivu ningechimba visima wanangu wapate maji kuliko biashara hii kichaa ya uchawi wa mabundi.
Mapovu ruksa

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Na hii coronavirus hii....! Bundi wako sijui utawafanyaje jamaa yangu.
 
Masikini walishaonywa sana kuhusu hii biashara ya bundi.

Kwamba ni ngumu na ghali kuiendesha, haitabiriki na kwa ujumla haina faida zaidi ya misifa isiyo na tija kwao.

Kwamba hatujawa na uchawi wa kutosha kuwarusha bundi, au ukwasi wa kuwalisha na kuwatibu sawasawa.

Ila kama ilivyo ada, sikio la kufa halisikii dawa na kusikia kwa kenge ni mpaka damu imtoke masikioni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom