Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Biashara yangu ya Bundi imenidodea

Bundi wako ulitumia janja janja sana kuwaingiza sokoni. Mara wawameze KASUKU wa kijivu, mara wajinyakulie Nyama ya mbuzi ya CHOBBO INVESTMENT, vurugu tupu...!!!
Pambana na bundi wako...
karma inanimaliza mzee...... bora ningemwacha yule kasuku ningekuwa sasa nina kisingizio kuwa ananihujumu
 
Ila mkuu hapa mtaani kwetu unaheshimika sana kwa kuwa na hiyo mijibundi. Sifa zako zimeenea kila mahali kwa jinsi ambavyo umeweza kuendesha kilimo cha bundi kilichowashinda watangulizi wako hapo kabla. Sasa hivi wewe na wanao mnatembea kifua mbele kwa kumiki mijibundi yenye afya tele hata kama kwenye uchawi hai pafomu kiviile sio haba 😀😀
mibundi haina afya ni tumbo la kwashakoo...
 
GuDume sio Kila kiumbe kinafundishika, hebu jaribu kumfundisha bata uone
Waswahili walisema "MCHUMA JANGA HULA NA WAKWAO" tafuta namna ambayo unaweza tumia hao bundi wako. Unaweza tumia hata kusafirisha tu vitu tudogo tudogo nakumbuka zamani njiwa walitumika kupeleka taarifa kwa watu. Refer hata wimbo wa "ewe njia ewe njiwa peleka habari..."
Sasa wa train hao bundi wako wabadilishiwe
Shughuli za kufanya... Lakini pia haiwezekani hata ukaanza tangaza kwa watu kuwa nyama ya bundi inaongeza nguvu za kiume,inaponya ukimwi,inazuia cancer,inaleta mvuto wa mapenzi,inaleta utajiri n.k? Fanya hivyo....tengeneza uhitaji halafu uza hiyo mijibundi yako na vikinda vyake.
Siku nyingine Ukitaka Kukimbia Agana na nyonga. Usikurupuke tu.
 
Nimenunua mijibundi mikubwa kwa midogo kwa mbwembwe nyingi sana. Kwa mikogo na mwendo wa madaha nilijigamba kila kona huku nikiwatambia wapinzani wangu kuwa naenda kuwa juu kama Pierre Liquid Konki Fayaaaaa.
Matarajio yangu ilikuwa niipeleke mibundi yangu nchi jirani na za mbali, hasa Bollywood na Uchinani.
Nimeshindwa, wamesema hawataki uchawi kwenye nchi yangu.
Mibundi mikubwa imelala tu inapigwa na vumbi na kuzeeka, vibundi vidogo navituma mikoani lakini navilisha kwa gharama kubwa na havinipi faida, watu hawana hela nashindwa kuwapiga chuma ulete.
Bora ningekuwa msikivu ningechimba visima wanangu wapate maji kuliko biashara hii kichaa ya uchawi wa mabundi.
Mapovu ruksa
Lakini kule Njombe kulifanyika sala ya toba kuombea na kutubu makosa kama hayo ya manunuzi wa bundi wasio na tija.
 
Na maparachichi kutoka Mbeya na Moshi
Hivi bundi wengine wanakuja lini? Nimemiss water cannon salute...!! Halafu Mumbai hawaendi tena ilihali uliwaleta wateke soko la akina Ndugu ai kwenda Kliniki Apollo India
 
Mkuu acha tu niungame. Nilikurupuka. Sina business plan wala strategies za kufanya biashara za bundi niziendeshe kwa faida na weledi, naendeshwa na kiki tu ili nimfunike baba na kaka zangu wakubwa walionitangulia
Hapa nimekuelewa sana maana mda wote nilikuwa nimetoa macho najiuliza mijibundi ndo vitu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom